Uteuzi mpya wa Rais Samia, leo Juni 8, 2023, Prof. Abel Makubi ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa MOI

Uteuzi mpya wa Rais Samia, leo Juni 8, 2023, Prof. Abel Makubi ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa MOI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewateua wafuatao:

1. Amemteua Bw. Omar Issa kuwa Mkuu (Chancellor) wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST)...
ivi huyu edwini mhede si ndio mtendaji mkuu wa wakala wa mabasi yaendayo haraka(DART) mbna watu wanapewa vyeo vingi vingi ivi sijui watu wengine wameisha

  • Huku mtendaji mkuu (DART)
  • Huku mwenyekiti wa bodi NMB

watoto wa maskini tutaendelea kulia njaa
 
Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee? Jeshi litagueka Wamakunduchi watupuuuu? Enzi zake SMZ yote iligueka watu wa huku kwao Kusini Unguja, mkabila khatari. Tanganyika itatulia inshallah.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa nafasi kadhaa, amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (#MOI) akichukua nafasi ya Dkt. Respicious Boniface ambaye amemaliza muda wake

Omar Issa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) akichukua nafasi ya Gharib Bilal (Makamu wa Rais Mstaafu) ambaye amemaliza muda wake

Amemteua Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee kuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) akichukua nafasi ya Balozi Dkt. Marten Lumbanga aliyemaliza muda wake

Dkt. Edwin Mhende ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB Plc kwa kipindi cha pili
View attachment 2649635
View attachment 2649639
Prof. Abel Makubi
View attachment 2649640
Dkt. Respicious Boniface
Sasa hawa watazima mjadala gani? Zena anatukosea sana watanzania
 
Inabidi tupate elimu ya URAIA vizuri.
  • Mambo ya Muungano na yapi?
  • Hao wa upande wa pili, wanawekwa kwenye sehemu sahihi zinazoruhusiwa kimuungano?
  • Nani ni mkaguzi na msimamizi wa hilo kwa huku Jamhuri?

Kule SMZ, ni strictly kwa wao tu!
Ukiongea mambo kama haya unaambiwa ni mbaguzi, kwamba utafute hotuba ya Nyerere ya mwaka 1995........sasa unajiuliza hiyo hotuba ya Nyerere ina msaada gani leo hii ambapo watawala kutoka upande mwingine wa nchi yenye watu chini ya milioni 2 wanakuwa na nguvu ya kufanya decisions kubwa zinazoathiri zaidi ya watu milioni 60 wa upande mwingine wa nchi.​
 
Mmeacha Uteuzi wa Bandari!
Kamata haoo, shikaaa haooo, wana ona haya haoooo


Wamasai
Bandari
....na 2025 kwishney. Sijui watarudisha nini kwa Waarabu. Haki ya ngai.
nafsi yangu inaumia sana!
naona kila kitu kilichokizuri cha watanganyika kinaondoka na wanaotengeneza hoja ya kuondoka hivi vitu ni watanganyika wenyewe wakimtumia mama kama muhuri tu na kumbebesha kila lawama huku wakisema hawana cha kufanya watapiga kelele kisha watanyamaza tu halafu watasahau kweli?
binafsi sijausoma lakini mpaka unafika hapa lazima nikubali kuwa tumepigwa na tutake tusitake tanganyika wanayoifaidi ni familia chache sana zenye hoja nzuri za ushawishi lakini wakiuza nchi kwa faida ya ubinafsi wao.
kuna muda unatamani viongozi wote wafe na tuanze upya labda kunaweza kuwa na unafuu.
waafrika bado tunasafari ndefu sana hapa ndipo naukumbuka wimbo wa utoto unaosema tumefika bado kisha mwitikiaji anasema bado achoki anauliza tutafika lini naye anabaki na jibu moja linalojirudia kuwa bado.
 
Na huku kuna Wazanzibari wanaongezwa wakati Makame Mbarawa hatujamalizana naye kwenye Bandari.
 
Back
Top Bottom