Pre GE2025 Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa tenguzi hizi mbili, naona mwisho mbaya wa Mh. Samia 2025
Sasa hao wawili wans athari gani kwenye jamii?

Kwamba Nape ama January ndiyo wawe na ushawishi wa kumkwamisha Rais asishinde?

Nani atawasikiliza na kuwaamini hao wanaoleta mafarakano kwenye jamii kwa kuwaona wananchi mapunguani.

Samia bado yupo sana hadi 2030 atakapostaafu kwa mujibu wa katiba.

Hakuna mkubwa zaidi ya Chama kama unabisha hao wamewekwa benchi na hakuna kitakachokwama.
 
My Take
Cheo ni dhamana, maisha yaendelee 🙏🙏👇👇

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt, Moses Kasiluka, viongozi hao ni kama ifuatavyo;-

  1. Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Silaa alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anachukua nafasi ya Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  2. Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu);
  3. Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Kikwete alikuwa Naibu Waziri, Odisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  4. Balozi Mahmoud ThabitKombo ameteuliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy, anachukua nafasi ya Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
  5. Mhe. Cosato Dvid Chumi (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiki. Mhe. Chumi anachukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi;
  6. Mhe. Deus Clement Sangu (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  7. Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Mhe. Londo anachukua nafasi ya Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  8. Bw. Eliakim Chacha Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huu Bw. Maswi alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA);
  9. Bi Mary Gasper Makondo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Makondo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Bi. Makondo anachukua nafasi ya Bi. Rehema Sefu ambaye amestaafu.
  10. Bw. Kiseo Yusuph Nzowa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huu Bw. Nzowa alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikuli;
  11. Bw. Musa Haji Ali ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Ali alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;
  12. Bw. Louis Peter Bura ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Bw. Bura anachukua nafasi ya Bw. Said Juma Nkumba ambaye amepangiwa majukumu mengine;
  13. Bi. Kemirembe Rose Lwota amehamishwa kutoka Wilaya ya Manyoni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti;
  14. Dkt. Vincent Biyegela Mashinji amehamishwa kutoka Wilaya ya Serengeti kuwa Mkuu wa Wilaya Manyoni;
  15. Dkt. Maulid Sleiman Madeni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti;
  16. Bw. Afraha Nassoro Hassan amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Seringeti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Bw. Hassan anachukua nafasi ya Bw. William Anyitike Mwakalambile ambaye uteuzi wake umetenguliwa na;
  17. Bw. Dennis Kwame Simba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Kabla ya uteuzi huu Bw. Simba alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Pia soma DOKEZO - Nape, Makamba kuondolewa Baraza la Mawaziri
Wajinga mtashangilia. Ila hao Vijana wawili ndio wanajua mbinu za uchaguzi ukiondoa wakongwe akina kinana na Makamba senior. Wanarudishwa kwenye majukumu yao ya siri pale masaki hadi mama hashinde 2025 ndipo watarudishwa tena kwenye hizo kazi za kuzurula.

Kizimkazi sasa Hivi anawaza uchaguzi tu na lazima aipange safu yake vyems ili hata akipiga la mkono muone ni kisigino na goli la kideoni. Narudia tena wajinga shangilieni ile ilikuwa staged wenye Akili kubwa wanajua.
 
Mama alifikiro Mwendazake aliwaonea? Aliona ni makapi mambwa koko yaliyo jificha kwa migongo ya majina ya baba zao sasa huu si uzalendo wabaki na ubunge wao wa kuchaguliwa na wananchi tu tamaa mbele mauti nyuma
 
Mh.January Makamba na Mh.Nape Nauye, hongereni sana kwa utumishi uliyotukuka sana Serikali kuu ....

mmefanya mambo makubwa mno kwenye wizara mlizozitumikia,
na sasa kwa wakati muafaka ubunifu, ushawishi, maarifa na uchapakazi wenu ni muhimu na unahitajika sana ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM tunapoelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa na baadae mwaka ujao Uchaguzi mkuu....

Asanti na Hongera sanaMh.Rais Dr Samia Suluhu Hassan kuimarisha chama na Serikali yako sikivu kwa maslahi mapana ya waTanzania wote 🐒
Ndio mwanzo wa mwisho hivyo, haitasaidia chochote hata mjitulize vipi!
 
My Take
Cheo ni dhamana, maisha yaendelee 🙏🙏👇👇

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt, Moses Kasiluka, viongozi hao ni kama ifuatavyo;-

  1. Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Silaa alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anachukua nafasi ya Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  2. Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu);
  3. Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Kikwete alikuwa Naibu Waziri, Odisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  4. Balozi Mahmoud ThabitKombo ameteuliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy, anachukua nafasi ya Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
  5. Mhe. Cosato Dvid Chumi (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiki. Mhe. Chumi anachukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi;
  6. Mhe. Deus Clement Sangu (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  7. Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Mhe. Londo anachukua nafasi ya Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  8. Bw. Eliakim Chacha Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huu Bw. Maswi alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA);
  9. Bi Mary Gasper Makondo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Makondo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Bi. Makondo anachukua nafasi ya Bi. Rehema Sefu ambaye amestaafu.
  10. Bw. Kiseo Yusuph Nzowa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huu Bw. Nzowa alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikuli;
  11. Bw. Musa Haji Ali ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Ali alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;
  12. Bw. Louis Peter Bura ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Bw. Bura anachukua nafasi ya Bw. Said Juma Nkumba ambaye amepangiwa majukumu mengine;
  13. Bi. Kemirembe Rose Lwota amehamishwa kutoka Wilaya ya Manyoni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti;
  14. Dkt. Vincent Biyegela Mashinji amehamishwa kutoka Wilaya ya Serengeti kuwa Mkuu wa Wilaya Manyoni;
  15. Dkt. Maulid Sleiman Madeni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti;
  16. Bw. Afraha Nassoro Hassan amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Seringeti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Bw. Hassan anachukua nafasi ya Bw. William Anyitike Mwakalambile ambaye uteuzi wake umetenguliwa na;
  17. Bw. Dennis Kwame Simba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Kabla ya uteuzi huu Bw. Simba alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Pia soma DOKEZO - Nape, Makamba kuondolewa Baraza la Mawaziri
Magu aliyaona haya mapemaa, ye akawarudisha.
 
britanicca nakuaminia. Kuanzia leo hata ukiandika kuwa mende anatoa maziwa nitakuamini.

Uliandika wiki moja iliyopita kuwa mama akimaliza ziara ya Katavi Nape na Makamba wataondolewa. Na imetokea.

Kabla ya hapo ulitabiri uteuzi wa DGCI Mombo.
Yule Yuko jikoni na ndiye mhariri WA mikeka. Since enzi za jiwe mwamba katutonya mengi.
 
Duuuh

Wazee wa Goli la Mkono wamewekwa kando.

Najiuliza, kulikuwa na ulazima wowote wa kumstaafisha Mbunge ili kumteua mwingine?

Tunajua Waziri si mtendaji Mkuu wa wizara. Hivyo, ingelikuwa vema yule anayeonekana kufaa angepelekwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara husika.
Lakini KM baadhi ya maamuzi atahitaji Baraka za waziri.. waziri ana nafasi kubwa hata kama si mtendaji.
 
Ndio mwanzo wa mwisho hivyo,haitasaidia chochote hata mjitulize vipi!
Kwahiyo uteuzi na utenguzi ni kujituliza?

Sio kuimarisha utendaji wa Chama na Serikali Sikivu ya CCM katika kuwaletea wananchi na waTanzania wote Maendeleo 🐒
 
Back
Top Bottom