Pre GE2025 Uteuzi na Utenguzi unaofanywa na Samia ni mbwembwe tu za Madaraka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tuwe na mfumo ambao unamlazimiasha Rais kuumiza kichwa sana wakati anaunda timu yake.

Ule mfumo walio nao Kenya na Marekani ambako mawaziri wateuliwa na Rais kisha wanakuwa approved na Bunge kabla ya kupewa madaraka ni mzuri sana.

Hii teua teua kila siku na kuhamisha kila kukicha haileti tija katika maendeleo ya taifa na pengine inatokana na Rais kukosa umakini.

Longevity ni aspect muhimu sana katika uongozi na maendeleo. Hauwezi kubadilisha watu kila siku ukategemea matokeo makubwa.
 
Mnadhani kwa nini Masauni bado yupo mambo ya ndani?
Sasa ukiangalia ni lipi la maana anafanya!! Au mama wa ngekewa(mhagama) huwa hata sielewi anafanya nini lakininpanga pangua yumo tu
 
Huyu ni Rais wa hovyo na mwoga kuwahi kutokea! Anakimbia kivuli chake mwenyewe!
 
Ndipo mwisho wako wa kufikiri ulipoishia?

Unajuwa maana ya R nne za Rais mama Samia Suluhu Hassan?
Huu ndiyo mwanzo wangu wa kufikiri ulipoanzia! Kwani maana ya R nne ni kuteua na kutengua kila kukicha. Kwamba uwezo wake wa kutambua watendaji wazuri wanaomfaa umeishia kama mama anachagua nyanya sokoni? Kwamba hana kazi zaidi ya kuteua na kutengua?

Samia hafai!
 
sio mbwembwe bro,kila aliyeteuliwa alipewa kpi ambazo alitakiwa kuzitimiza na muda,wanaposhindwa ndipo unatenguliwa
Boss "literature" yako nzuri ila ndani ya uwanja mambo hayako hivyo.
 
Huu uteuzi ni ili tuhame kumsakama na maaskari wake walio tumwa kuvuruga mkutano wa CHADEMA
 
Sasa ukiangalia ni lipi la maana anafanya!! Au mama wa ngekewa(mhagama) huwa hata sielewi anafanya nini lakininpanga pangua yumo tu
Huwa wanasema Mbowe kakaa sana Chadema apishe damu changa. Akina Kabudi na Lukuvi wa nini tangu TANU!
 
Katika mawaziri alioteua yeye ni kama wannę tu ndio waliodumu kwenye wizara zao mpaka muda huu.

Wengine ni kila siku panga pangua akijisikia tu.
Kama leo teua kesho pangua si wanaoteuliwa wakatae? Yaani wanakubali wao wanajiona Bora kuliko walioondolewa? Hatimaye wanaona bora wapige madili maana wanajua hawamalizi miezi 3. Urefu wa kamba.
 
Kama leo teua kesho pangua si wanaoteuliwa wakatae? Yaani wanakubali wao wanajiona Bora kuliko walioondolewa? Hatimaye wanaona bora wapige madili maana wanajua hawamalizi miezi 3. Urefu wa kamba.
Kabisa ‘chelewa chelewa, ukute mwana si wako’.

Mbaya zaidi serikali inakosa consistency.
 
Kwa kiingereza ana recycle watu wake bila kuwapa elimu wala semina elekezi.

Anachofanya Samia ni kuonyesha nguvu na madaraka aliyonayo kikatiba. Madaraka na nguvu za Rais ndicho anaonyesha.

Asomaye na aelewe...
 
Naunga mkono hoja!
 
Wala hakuna tija yoyote zaidi ya gharama kwa walipa kodi
 
Hamkumbuki Kuna kipindi alimteua marehemu?! Kazi yake ni kutengua , kuteua na kufanya utalii wa ndani kidogo na utalii wa nje kwa sana. Kuna watu walikuwa wanalalamika Serikali ya awamu ya 4 kuwa kikwete alikuwa anasafiri sana nje ya nchi lakini huyu mama kwa kusafiri ameishamfunika hata kikwete.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…