Bado sijaona mantiki ya kuambiwa hizi teuzi hadharani. Ni upuuzi mtupu.
Hivi kuna haja ya kuutangazia umma uteuzi wa wasaidizi wako binafsi wa ofisini ukiwa kama Rais?
Hivi watangulizi wake walifanya hivi?
Maana ukianza kufanya haya, itabidi kila msaidizi wa Rais awekwe wazi.
Kwa mfano; msaidizi wa mambo ya afya, michezo, biashara, kilimo, uvuvi, walemavu, Daktari wa Rais, Dereva wa Rais, Dressing designer wa rais, Mpishi wa rais nk.
Na pia siku ukimbadilisha msaidizi itabidi uutangazie umma.
Yoyote kwa yote hao wasaidizi unawaweka katika mazingira ya kufuatwa fuatwa na watu ili wawasaidie kufikisha ujumbe kwa rais au kufanya lobbying. Na wakipata kashfa itahusishwa na ofisi ya rais.
Binafsi naona hili ni kama jambo la kishamba, kutokujiamini na udhaifu wa rais Samia ambao ameuweka hadharani. Sio kila kitu kinapaswa kuletwa hadharani.