Je, Roho Mtakatifu anazungumza na Wakristo wema na waovu vile vile? Je, Roho Mtakatifu yu pamoja nao wakati wote au wakati fulani tu? Je, ni wakati gani anaanza kumtembelea mtu atakaye kuwa Mkristo?
Utasemaje kuwa wewe ni Mkristo ikiwa Roho Mtakatifu yu ndani ya Mkristo mwingine? Inakuwaje Wakristo wengi wanawapumbaza watu kwa kudai kwamba Roho Mtakatifu yu ndani yao tu! Na baadaye wanabadilisha dini?
Je, Roho Mtakatifu anaamuru kile ambacho Wakristo wanapaswa kukifanya bila ya uhuru wa kuchagua hata kidogo au anawaongoza tu na wao wana uhuru wa kufuata au kuto fuata?
Ikiwa Roho Mtakatifu anaamuru kile Wakristo wanachopaswa kukifanya, kwa nini Wakristo wanafanya maovu na madhambi? Vipi unaweza kuuelezea ubadilishaji wa dini na kuingia dini na imani mbali mbali kunakofanywa na Wakristo wengi? Je, Wanaambiwa kufanya hayo na Roho Mtakatifu?
Ikiwa Roho Mtakatifu anawaongoza Wakristo tu, na wako huru kufanya wanavyotaka, sasa ni vipi tutajua kwamba waandishi wa Biblia hawakufanya makosa wakati walipoziandika?
Ikiwa Wakristo wanaamini kwamba Roho Mtakatifu huwajia na kuzungumza nao kila siku, kwanini hawamuulizi Roho Mtakatifu kuhusu chapisho lipi la Biblia wanalopaswa kulifuata kwa vile kuna machapisho mengi