Mkuu
kwanza elewa kwamba hata pale Mbingu na Nchi zilipoumbwa ambapo maji yaliujaza ulimwengu, Roho wa Mungu (Mtakatifu) alitulia juu ya vilindi vya maji.
Unapomtaja Mungu yaani YHWN ujue umemtaja katika ukamilifu wake yaani Utatu Mtakatifu.
Kinachotakiwa kufahamika hapa ni kwamba definition ya uhuru wa mtu anapokuwa ndani ya Roho Mtakatifu ni definition nyingine.
Nitajie wakristo waliojazwa Roho Mtakatifu pls
Ulitaja utatu Mtakatifu , lakini
Huku Biblia ikihubiriwa na kuaminika kuwa ni Neno la Mungu, haina imani ya Utatu inayotukuzwa sana.
Kama imani hii ya Utatu ilikuwa ni ya kweli, ilitakiwa iletwe kiwaziwazi kwenye Biblia kwa kuwa tunahitaji kumjua Mungu na njia ya Kumwabudu Yeye.
Hakuna yoyote miongoni mwa mitume ya Mungu, kuanzia Adam hadi kufikia Yesu (AS), mwenye ufahamisho wa Utatu au Mungu wa Utatu.
Na hakuna yoyote katika wajumbe wa Mungu aliyezungumza habari yoyote hata ya siri juu ya hilo au je, kuna rejeo lolote ima katika Agano la Kale au Agano Jipya la Biblia linalothibitisha imani hiyo.
Kwa hiyo, hilo ni geni ambalo si Yesu (AS) wala wanafunzi wake anayezungumzia Utatu katika Biblia.
Kinyume chake, Yesu (AS) anasema:
"Marko 12:29. "Yesu akamjibu, Ya kwanza ndio hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;"
Kwa mujibu wa Mt. Paulo: "Matendo 2:22 "Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;"
Aya za hapo juu zinajieleza zenyewe.
Kwa nini mtu ajisumbue katika imani iliyojaa machafuko wakati Wanazuoni wa Kikristo wa vyeo vya juu hawawezi kufasiri au kufafanua imani hiyo kisomi na kiakili?
Yesu kwa haki kabisa ameshatabiri aina ya tatizo hili katika (Mathayo 15:8-9)
"Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami, nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu."
Kwa kuongezea, hayo yalisemwa na Mt. Paulo katika (2 Timotheo 4:3-4) "Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo."
Pia tunasoma zaidi katika (Tito 1:16) "Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai."
Katikati ya mkanganyiko huu, akili kuu miongoni mwa Wakristo zimemaliza mantiki zote zinazojulikana ili kuazima uthibitisho wa imani ya Utatu lakini wameshindwa kinyonge na kisha wametangaza kuwa hilo ni fumbo.
Hata hivyo, kumwabudu Mungu Muweza hakuwezi kuwa kwa maafikiano.
Yeye anataka watu wa kumwabudu Yeye peke yake kwa mujibu wa Mwongozo wake Mtakatifu.
Kwa kuwa yeye ni mwadilifu, kinachofuata ni kuwa, Uadilifu wake unalazimu ujumbe wake uwe wa wazi na mwepesi katika mtindo wake.
Mafundisho yake, kiujumla, lazima yasiwe na makosa/dosari yoyote, ushirikina wala kuchanganya. Lazima uwe wa ukweli kabisa, ambao siku zote utaweza kuhimili changamoto za elimu ya aina yoyote zikiwemo za magunduzi ya wanadamu katika nyanja za kisayansi.
Kwa vile imani ya Utatu yenyewe ni "Fumbo", kwa hiyo, haiwezi kuzingatiwa kuwa ni neno takatifu.
Biblia inasema: (1 Wakorinto 14:33) "Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani..."
Ensaiklopidia ya dini inakiri kuwa:
"Wanatiolojia wa sasa wanakubaliana kuwa Biblia ya Kiyahudi haina imani ya Utatu". Na Isaiklopidia mpya ya Kikatoliki vilevile inasema: "Imani ya Utatu Mtakatifu haijafundishwa katika Agano la Kale."
Sawa sawa, katika kitabu chake "Mungu wa Utatu", Jesuit Edmund Fortman anakiri: "Agano la kale..... halituelezi chochote kwa uwazi au kwa kulazimisha kinachodokeza Mungu wa Utatu ambaye ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.... hakuna ushahidi wa kuwa mwandishi yoyote mnyofu aliyewahi kugusia kuwepo kwa (Utatu) ndani ya Uungu.
Hata ukitazama katika ("Agano la Kale"), mapendekezo, maashirio na alama za siri juu ya nafsi tatu, utaziona kuwa huko ni kwenda nje ya maneno na dhamira ya waandishi wanyofu." ( ibid, page 6)