seedfarm
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 260
- 2,655
Kwanini kama Taifa tunarudia makosa ya kuteua watu wenye makando kando kama Afande Ramadhani Kingai? Huyu mtu kwa sasa anafahamika na kila Raia kwa matendo yake yaliyojidhihirisha pale Mahakamani wakati wa kesi ya Mbowe
Je, tunasubiri afanye ukatili na unyama wa kiasi gani kwenye hili Taifa?
Tulishajifunza wakati wa JPM umuhimu wa vetting ya viongozi kwa yaliyotokea. Je, bado tunaendelea kujifunza.
Afande Kingai hakupaswa kupewa nafasi ya DCI hata kidogo, Imani ya Raia kwa huyu mtu ni ndogo sana, Wakati wa kesi ya Mbowe huyu alihusishwa na utesaji na utekaji, Na hata majibu yake mahakamani alijichanganya sana kuhusu kuwahamisha watuhumiwa tokea kituo kimoja cha polisi kwenda kingine na malengo yake kuhusu utesaji
Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa Mkurugenzi wa makosa ya jinai unaligawa Taifa ambalo Rais Samia alikuwa anafanya jitihada za kuliunganisha kwa maridhiano
Kwenye kesi ya Mbowe pale mahakamani, Afande Kingai alikuwa shahidi mkuu upande wa jamhuri na ushahidi wake alioutoa pale mahakamani wa kuwanunulia watuhumiwa Mo energy ikawa mwanzo wa watu kuamini huyu Bwana ameshiriki Katika kesi ya mchongo kuanzia kudraft mpaka kupeleka mahakamani.
Afande Kingai alishindwa kujibu maswali ya mawakili wa utetezi hata moja na hata maswali yaliyohusiana na kitendea kazi chake ya General Orders of police (PGO) alionekana haelewi pale Mahakama ya uhujumu Uchumi.
Ushahidi wa Afande Kingai ambaye alikuwa Shahidi mkuu ulileta mkanganyiko pale Mahakama ya Uhujumu Uchumi na ndio ukawa mwanzo wa watu kufahamu siri ya kesi ya akina Mbowe pamoja na Kikosi kazi maalum kilichojumuisha Afande Goodluck
Maswali ya kujiuliza sisi kama Raia wa nchi hii:
Unawezaje kumpa mtu nafasi ya DCI wakati umma wa Watanzania wanafahamu huyu mtu amechafuka?
Je, huu ndio mwanzo wa watu kubambikiwa kesi za mauaji hapa nchini?
Je, uteuzi huu Bwana Kingai sio ni mwanzo wa kufumua madonda ambayo Rais Samia alishaanza kuyaponya?
Moja ya watu kuzidi kudai Katiba Mpya ni kutokana na uteuzi wa watu aina ya Afande Kingai, Tungekuwa na tume maalum ya kuchuja na kuteua aina ya watu kama Afande Kingai kama Rasimu ya Jaji Warioba alivyopendekeza tusingekuwa na utata.