Nakuelewa, ila kwa sasa ubalozi umekwishafunguliwa na tuna balozi wetu mjini Tel Aviv.
Sikuongelea kwa undani kuhusu mgogoro wa mfereji wa Suez kati ya Israel na mataifa ya kiarabu wakiongozwa na Misri chini ya marehemu Anwar Sadat.
Ila unafamu kwamba nyuma ya mgogoro wa mfereji wa Suez kulikuwa na Marekani na ilokuwa USSR?
Kwa wakti ule Tanzania ilikuwa inafuata siasa za kikomunisti na ilikuwa inawafuata USSR yaani "soviet sphere of influence".
Hiyo ni historia na kuna topic kabisa kuhusu mfereji wa Suez ambayo inajitosheleza.
Bila kwenda ndani sana kwenye suala la mafunzo ni kwamba kwa sasa teknolojia na nyenzo za kisasa zipo na zinatengezwa na Israel na nchi nyingi tu sasa hivi zinaiangalia Israel.
Katika ulimwengu wa leo wa tishio la ugaidi na kila aina ya uhalifu wa kiteknolojia na uhalifu ulosukwa yaani "organised crime" basi unahitaji msaada wa wale wajuzi ambao wapo "available" na Israel wanajaza namba.
Ukizungumza utekaji ndege, utekaji meli na shughuli zozote ambazo zinaleta madhara kiuchumi kwa nchi fulani basi kuna njia za kuweza kujifunza namna ya angalau kuzuia mambo hayo yasitokee hivyo Israel wapo karibu kabisa na eneo la tukio kusaidia.
Ukiingia katika tovuti ya Bloomberg kwenye "innovation index" utapata Data kwamba Israel ni nchi ya tano duniani kwa ubunifu yaani "innovation".
Israel ina wanasayansi na wahandisi 140 katika idadi ya waajiriwa 10,000 ikiwa ni sawa na asilimia 85 kwa idadi hiyohiyo nchini Japan na asilimia 83 nchini Marekani.
Hawa wanasayansi na wahandisi pia wameshiriki kuendeleza mambo mengi katika sayansi ya asili, sayansi ya kilimo kwenye umwagiliaji (drip irrigation), vifaa vya umeme, sayansi ya kompyuta, na hata kumuunda robot.
Kwa mfano leo hii nchii Israel wanakunywa maji ambayo awali yalikuwa ni maji ya bahari baada ya kufanya kitu kinatwa "water conversing" ambapo maji ya bahari yanavunwa na kuchujwa.
Ninaweza kujaza hii sehemu lakini hayo ni machache tu mkuu, jifunze zaidi kuhusu hawa jamaa.
Pia unapojadili hii mada, jaribu sana kuepusha suala la dini maana siko huko.
Mkuu,
Inawezekana kabisa ni kweli hao jamaa wana sifa ulizoorodhesha hapo juu na pengine kuzidi hizo,lakini,hivi tunawseza kunufaika nazo kweli kama ambavyo tumekuwa tukifikiria hapa na kwingineko?
Mleta uzi anaelezea jambo kama ulilolisema wewe,tatizo ambalo ninaliona hapa siyo hawa jamaa au sisi kuwa na ubal;ozi kokote maana tushakuwa na mabalozi kwenye nchi nyingi sana zenye maendeleo kwenye sekta mbali mbali lakini hapa ndipo tulipo....
Tatizo langu siyo wenzetu bali ni sisi,hapa tulipo na namna tunavyofikiria tunaweza kweli kunufaika na kwa sisi kuwa na mahusiano mazuri ya kibalozi na Israel au nchi nyingine yoyote yenye maendeleo yoyote?
Jibu la swali hili ni gumu kidogo kwasababu kama ingekuwa ni rahisi basi leo tungekuwa mbali sana....
Kuna mambo kadhaa ya kujiuliza,hivi ni kweli hawa jamaa wapo tayari kutukwamua hapa tulipo?
Ni kweli tupo kwenye mazingira rafiki ya kunufaika na hawa jamaa?
Ni kweli tumeshindwa kunufaika na maendeleo ya Japan,Marekani,China na nchi nyingine hadi iwe ni jambo la ajabu sana sisi kuwa na mahusiano ya kibalozi na nchi hii?
Ni kweli changamoto zetu zitaondolewa na watu wengine na siyo sisi wenyewe?
Hivi wakati wa changamoto hizi huko kwao walisaidiwa?
Mkuu hapa sijagusia suala la ugaidi ambalo umelitaja ambalo kwa maoni yangu sidhani hata kuna umuhimu wa sisi kulifikiria kwa sasa maana mazingira yetu ni tofauti kabisa na wao....