Uteuzi wa Job Masima kuwa Balozi Israel ni ishara ya Rais Magufuli kuinoa na kuiimarisha TISS

Uteuzi wa Job Masima kuwa Balozi Israel ni ishara ya Rais Magufuli kuinoa na kuiimarisha TISS

Tanzania Intelligence and Security Service, hawa ni wana usalama wa ndani ya nchi. Nje ya mipaka ya nchi wapo MI.
Lengo la awali lilikuwa ni usalama wa Taifa! Sasa hapo clouds TV sijui walikuwa wanashughulikia usalama wa Taifa au usalama Bashite wa Koromije!
 
Not at all, naamini hata siku upinzani ukijaaliwa kupata kukaa Ikulu watalindwa na haohao tiss.

Huo ndiyo utaratibu.
TISS hawapaswi kuangalia usalama wa mtu Bali usalama wa Taifa! Mtu atalindwa tu kama kulindwa kwake kuna maslahi ya Taifa!
Tunachokishuhudia bongo ni dhana potofu kabisa! Tunashuhudia TISS wakimlinda mtu kwa maslahi yasiyokuwa ya Kitaifa! Kumlinda Bashite na cheti chake fake si kwa usalama wa Taifa kinyume chake ni kwa kuangamiza Taifa Bashite analindwa! Dhana ya Tiss imepotoshwa!
 
Nimepata kusikia TISS ni kama jeshi la kulinda maslahi ya watawala, that is why matukio yao mengi yanahusiana na kuzuia wakosoaji wa serikali na kulinda viongozi na familia zao
 
Tanzania bado tuko imara sana barani africa katika ulinzi na usalama.Hilo halina shida.
Tatzio langu ni wanasiasa kutumia vyombo vya usalama nathani hilo linahitaji kukomeshwa.
Hawa watu ni wazalendo sio wanasiasa. Wako tayari kulinda nchi kwa gharama zozote zile lakini sio mwanasiasa bahati mbaya huku kwetu ni kitu tofauti.
Tuanze na katiba ambayo itawatoa wanasiasa kwenye professionalism? Magu unaweza kufanya hio?
 
TISS itaimarika kwa kuwa chombo huru...na siyo kuwa chini ya ofisi ya rais...kwa kuondoka kwenye majukumu ya ushauri tu, kwenda kwenye majukumu ya kutekeleza...

kuanza na hapo wanahitaji kupeleka bill bungeni then wafanye hivyo. Lakni nchi ya ccm hio haiwezekani maana wataogopa kuondelewa maana wanajua fika maamuzi yao mengi sio kwaajii ya usalama wa taifa na ustawi wake.
 
Mbona Trainers wao wengi huwa wanatokea huko huko Israel na mara nyingi Wajanja huwa tunagongana nao sana pale JNIA wakiwa wanakuja kuwafunza Vijana katika Vyuo vyao? Sasa unaposema kuwa Ubalozi umeanzishwa ili kuiimarisha hiyo idara unataka kutuambia nini labda ambacho hatukijui?

Nakumbuka mwaka juzi Trainer mmoja ( najua Vijana wa Idara mliokuwa zamu pale JNIA ) mtakumbuka baada ya huyu Trainer wa Kiyahudi kutoka Mossad alipokuwa anaingia aliambiwa akaguliwe vitu vyake lakini akakataa kata kata na Jamaa walipozidi kumlazimisha akatishia kugeuza na kurudi Kwao ndipo ikapigwa Simu Magogoni kwa Mkwere na Chuoni baada ya hapo ikatoka tu amri kuwa aruhusiwe kupita na asikaguliwe Jamaa akaingia nchini kweli na kutufundishia Vijana kwa wiki mbili tu lakini waliofunzwa wanasema mafunzo yake utadhani ni ya mwaka na baadae akaondoka zake.
sawa bhana mzee wa DATA...
 
mkuu katika vitengo imara Tanzania naweza kusema ni MI wa Tz. Wako kila pahala nje na ndani na wametulia sio wale madude wa bashite kujiita wao usalama wa taifa.

i love my country and i love the TPDF
Unajua hicho kitengo kinahusika na nini?...au ndio walewale mnaotoa ushauri wakati hamjui hata mfumo wa utendaji kazi wao.....hunatofauti na mtu anaetoa ushauri huku akirefer M15!!...hajui hata jinsi ya kuiandika halafu anatoa ushauri wa vyombo vya intelligence!.
 
Umeandika vyema sana.

Japo, nimesikitika sana kuona ama kusoma.kuwa pana mtu alikuja akapata shida ya kuingia japo JNIA yaani, sielewi kabisa sisi hapo Tanzania, unawezaje ukamuita mkufunzi toka nchi nyingine halafu ushindwe kumpokea hadi Simu ipigwe kutoka feri na chuoni?

Hii ni aibu kubwa na pia ni uratibu wa wageni wa kiwango cha zero brains kabisa.

Intelligence services, wanashindwaje kumpokea mtu kwa ajili yao?

Ni aibu kama hayo ni kweli , wanahiitaji kufanyiwa msasa.

Ila, nimuulize mwansishi wa thread hii, kwa nini wewe unaona ulinzi na usalama kwa Tanzania kushirikiana na Israel na siyo nyanja zingine za maendeleo maana naona ndiyo sekta umeipatia kipaumbele? Ni kwa nini?
Ahsante.
umeuliza swali zuri na la msingi sana
 
Unajua hicho kitengo kinahusika na nini?...au ndio walewale mnaotoa ushauri wakati hamjui hata mfumo wa utendaji kazi wao.....hunatofauti na mtu anaetoa ushauri huku akirefer M15!!...hajui hata jinsi ya kuiandika halafu anatoa ushauri wa vyombo vya intelligence!.
Mwandishi wa makala was just writing what he had in his mind na wala hakuna sehemu amesema yeye ni mtaalam wa masuala ya ujasusi
 
Mkuu umeleta uzi mzuri sana, Mkuu ana nia ya dhati kabisa ya kuumarisha taasisi yetu hii ya Usalama ambayo kiuhalisia imekuwa iko operate locally sana na haitakii kubadilika kwa mwavuli tu wa kuwa utendaji wao ni secret Mheshimiwa JPM alianza kuonesha nia ya ya dhati pale tu alipo mteua Modestus kipilimbi kama GD wa idara Kumuweka tu mtu ambae ni professional wa Computer science basi kutamfanya aipelekee idara Kisasa kabisa , Mbinu za Intelligence karibia katika agency zote ni Moja tunachozidiana Ni technology leo ukiangalia M15 ya uk au FBI utaona wanapopishana ni Tech tu, Uteuzi huo wa Job masima kama Balozi utaleta matokeo chanya katika kujifunza na kupata mapya juu ya usalama Huko.
Mkuu Infantry ...nilikua namzungumzia huyu...mfano unawezaje kushauri vipi ushauri wenye tija kwenye swala la kusafirisha mchanga wa madini wakati hamna unachojua kuhusu madini?.....vitu vingine sio lazima tukomenti!
 
Mkuu Infantry ...nilikua namzungumzia huyu...mfano unawezaje kushauri vipi ushauri wenye tija kwenye swala la kusafirisha mchanga wa madini wakati hamna unachojua kuhusu madini?.....vitu vingine sio lazima tukomenti!
Boss umechanganya ku quote;!
 
Boss umechanganya ku quote;!
Mkuu sijachanganya...nilikua namjibu infantry soldier kwa kurefer komenti yako....yani wewe unaandika M15 halafu unatoa ushauri?!!....ushauri wako hauwezi kuzingatiwa kwasababu mlengwa ataona hujui chochote kwenye hayo maswala!
 
Mkuu sijachanganya...nilikua namjibu infantry soldier kwa kurefer komenti yako....yani wewe unaandika M15 halafu unatoa ushauri?!!....ushauri wako hauwezi kuzingatiwa kwasababu mlengwa ataona hujui chochote kwenye hayo maswala!
Mkuu ushauri unapotolewa sio lazima uzingatiwe.
 
Back
Top Bottom