Uteuzi wa Mabalozi 23 leo, Hakuna aliepangiwa kituo cha kazi au mimi sijaelewa?

Uteuzi wa Mabalozi 23 leo, Hakuna aliepangiwa kituo cha kazi au mimi sijaelewa?

Leo kupitia page ya kurugenzi na mawasiliano Ikulu nimeona statement ya uteuzi wa wabarozi 23 uliofanywa na Mh Rais Samia, lakini sijaelewa mpaka sasa kuwa katika wote 23 hawajapingiwa vituo vya kazi? Kwanini? Anafanya alimradi abadili ama ye anateua wakati akisubiri wa kumtoa?
Ubalozi ni hadhi, ni cheo, si lazima mtu akiteuliwa kuwa balozi awe na kituo cha kazi kwa maana ya kuwa balozi wa Tanzania katika nchi nyingine.

Anaweza kuwa balozi ana kituo cha kazi Wizara ya Mambo ya Nje. Au balozi wa kazi maalum.

Kuna vyeo vingi unakuta mwenye cheo ni balozi, lakini hawakilishi Tanzania kwenye nchi nyingine.

Wakuu wa itifaki mara nyingi wanakuwa mabalozi hivyo.

Tumeona pia makatibu wakuu viongozi wakiwa mabalozi hivyo.
 
Kuwa BALOZI sio mpaka upangiwe nchi.
Rejea BALOZI dk bashiru ally

..huo sio mfano mzuri kwasababu Rais Magufuli alikuwa amefanya makosa ktk uteuzi ule.

..Balozi ndio ngazi ya juu kabisa ya watumishi [ foreign service officers] wa wizara ya mambo ya nje.

..Mara nyingi foreign service officer anapofikia ngazi ya ubalozi hupangiwa nchi ya kuwakilisha, au huteuliwa kuongoza idara mojawapo ktk wizara ya mambo ya nje.
 
Bashiru si alikuwa katibu mkuu KIONGOZI.
Na hicho CHEO si wanasema mpaka uwe balozi ndo uteuliwe
..huo sio mfano mzuri kwasababu Rais Magufuli alikuwa amefanya makosa ktk uteuzi ule.

..Balozi ndio ngazi ya juu kabisa ya watumishi [ foreign service officers] wa wizara ya mambo ya nje.

..Mara nyingi foreign service officer anapofikia ngazi ya ubalozi hupangiwa nchi ya kuwakilisha, au huteuliwa kuongoza idara mojawapo ktk wizara ya mambo ya nje.
 
Bashiru si alikuwa katibu mkuu KIONGOZI.
Na hicho CHEO si wanasema mpaka uwe balozi ndo uteuliwe

..mimi siamini kama Katibu Mkuu kiongozi lazima awe balozi.

..nasema hivyo kwasababu wako makatibu wakuu kiongozi ambao hawakuwa mabalozi.

..timothy apiyo alikuwa katibu mkuu kiongozi lakini hakuwa balozi.

..pia wako makatibu wakuu kiongozi ambao walikuwa mabalozi, lakini wao walitokea ktk utumishi wa wizara ya mambo ya nje.

..balozi paul rupia alikuwa balozi kutokana na utumishi wake wizara ya mambo ya nje, halafu baadae akateuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi.
 
Zama zimebadilika
..mimi siamini kama Katibu Mkuu kiongozi lazima awe balozi.

..nasema hivyo kwasababu wako makatibu wakuu kiongozi ambao hawakuwa mabalozi.

..timothy apiyo alikuwa katibu mkuu kiongozi lakini hakuwa balozi.

..pia wako makatibu wakuu kiongozi ambao walikuwa mabalozi, lakini wao walitokea ktk utumishi wa wizara ya mambo ya nje.

..balozi paul rupia alikuwa balozi kutokana na utumishi wake wizara ya mambo ya nje, halafu baadae akateuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi.
 
..wakurugenzi wote wa idara za wizara ya mambo ya nje, isipokuwa mkurugenzi wa fedha, na mkurugenzi wa utawala, huwa na hadhi / cheo cha ubalozi.
Si huyu wa "utawala" ndiye angekuwa BALOZI hasahasa! Au kuna masharti/sababu zinakataza!
 
Sijawahi kuona uteuzi wa Mabalozi wengi hivi bila kupangiwa vituo. Kama mama hakuwa tayari kuwapangia vituo si angesubiri? Kwanini alikurupuka kuwatangaza ilhali vituo vyao vya kazi havijapangwa?
Kwa mara ya kwanza umeongea pointi.
Kongolee 👊
 
Hatimaye angalizo la mbunge wa CHADEMA limeanza kutekelezwa katika awamu ya sita, mwezi May 2021

Toka maktaba :

30 May 2017

DIPLOMASIA YA UCHUMI: Alichokizungumza Mch Peter Msigwa

 
Si huyu wa "utawala" ndiye angekuwa BALOZI hasahasa! Au kuna masharti/sababu zinakataza!

..wakurugenzi wa utawala huwa wanatokea wizara ya utumishi.

..na wakurugenzi hao huweza kuhamishwa toka wizara moja kwenda nyingine.

..binafsi namfahamu bwana mmoja alikuwa mkurugenzi wa utawala wizara ya ujenzi halafu baadae akahamishiwa mambo ya nje.
 

Iko wapi Diplomasia katika “Diplomasia ya Uchumi”?

Iko wapi Diplomasia katika “Diplomasia ya Uchumi”?
Dastan Kweka
@KwekaKweka
Kiutaratibu, sera ya mambo ya nje ya nchi ni mwendelezo wa sera ya mambo ya ndani, na huainisha kanuni na misingi ambayo huongoza dola husika katika kujenga mahusiano na nchi nyingine, kukuza ushawishi, na kutetea maslahi yake. Pia, sera ya mambo ya nje, kama zilivyo sera nyinginezo, hupaswa kubadilika ili iendane na muktadha, kwa mfano; mabadiliko – ya ndani au ya nje - katika fikra, mienendo, au mitazamo.

Nchi yetu imeshuhudia mabadiliko makubwa ya kiutawala katika kipindi cha takribani miaka mitatu, tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani. Mabadiliko ambayo siyo tu yameathiri utekelezaji wa sera ya mambo ya nje ya Taifa letu, bali yanaashiria mwelekeo mpya kabisa wa kisera. Lengo la makala haya ni kuainisha nakisi iliyopo katika utekelezaji wa sera hiyo, kwa lengo la kuonesha wapi panahitaji maboresho.

Sera ya Taifa ya Mambo ya Nje, toleo la mwaka 2001, imesimikwa katika dhana ya “diplomasia ya uchumi” - dhana yenye lengo la kuhakikisha kuwa, mbali na malengo mengine, mfano ya kiulinzi, shughuli za kidiplomasia zinazoendeshwa na nchi yetu zinajikita katika kuujenga na kuuimarisha uchumi wetu. Utekelezaji wa sera hii, ambayo imekuwepo kwa karibia miongo miwili sasa, ulipaswa kuimarisha misingi muhimu ya “sera ya asili” ya mambo ya nje ya Tanzania, huku ukiongozwa na kanuni kadhaa, ikiwemo ya kulinda uhuru wa Taifa, haki za binadamu, na usawa na demokrasia (Ukurasa wa 11).
Sera ya asili ya Mambo ya Nje ilikuwa na misingi yake - “fundamental principles of Tanzania`s foreign policy” - ambayo ni ile iliyokuwa katika sera ya mambo ya nje ya serikali ya awamu ya kwanza, na ilihusisha kuunga mkono juhudi za kujikomboa za watu, na mataifa yanayoonewa. Usimamizi thabiti wa msingi au kanuni hii, na nyinginezo, hasa wakati wa harakati za uhuru, na vita vya ukombozi, uliipatia Tanzania heshima kubwa Afrika, na duniani. Hata hivyo, ni wazi kuwa ingawa sera ya sasa ya mambo ya nje imeainisha haja ya kuimarisha misingi hiyo ya asili, kuna ushahidi wa wazi kuwa imeshatelekezwa.

Kwa mfano, tumeona Tanzania ikianzishamahusiano ya kibalozi na Israeli, na kujivuniakupokea watalii kutoka nchi hiyo, huku mgogoro baina ya nchi hiyo na Mamlaka ya Palestina ukibaki kuwa kitendawili.


Pia, tumeona nchi yetu ikiimarishamahusiano na nchi ya Morocco, na kupokea misaada kadhaa, huku suala la Sahara Magharibi likibaki bila ufumbuzi. Tafsiri ya dhana ya diplomasia ya uchumi, katika muktadha wa mabadiliko haya, ni kuwa, yeyote mwenye fedha, teknolojia, au kingine chochote tunachokihitaji, hata akiwa dhalimu, ni swahiba wetu.

Hoja ya msingi kuhusu kubadilika kwa mahusiano baina ya nchi yetu na Israeli, au Morocco, siyo mabadiliko peke yake. Mabadiliko haya yangeweza kuwa muhimu, kwa mfano, kama yangejikita kwenye haja ya kubadili mbinu. Ajabu ni kuwa, tunaambiwa mabadiliko haya ni muhimu kwa sababu za kiuchumi, basi. Ni kama vile, kwa kuimarisha mahusiano na nchi hizi hali yetu kiuchumi itaboreka kabisa.

Ajabu!
Mwenendo wa utekelezaji wa sera yetu ya mambo ya nje unaonesha kuwa, watawala wanadhani inawezekana, na ni sawa, kwa dola kusukuma ajenda zake katika ngazi ya kimataifa, bila kulazimika, au kulazimishwa, kuheshimu misingi na kanuni muhimu, hata zile ambazo Taifa limejiwekea lenyewe katika sheria na sera zake. Kwa mfano, mojawapo ya kanuni ya msingi katika sera yetu ya mambo ya nje inahusu ulinzi wa uhuru, haki za binadamu, usawa na demokrasia. Bila shaka, kanuni hii ina msingi wake katika Katiba ya nchi yetu (1977). Kwa hiyo, tumeiambia dunia kuwa hii ndiyo misingi tunayoiheshimu na kuithamini.


Ajabu ni kuwa, serikali inatarajia jamii ya kimataifa ikae kimya pale inapoonekana kukiuka misingi hii, na kutowajibika kwa namna yoyote ile, hata pale baadhi ya miili ya raia wake inapoibuka baharini, kutekwa, au kunusurika kifo katika mashambulio mbalimbali. Sikitiko ni kuwa, nchi ambayo kwa miaka mingi ilifahamika kwa kukemea uovu, uonevu na ukandamizaji uliofanywa na mataifa ya Magharibi, hasa nyakati za ukoloni, sasa imegeuka ya kukemewa kupitia (ma)azimioyatolewayo na jamii ya kimataifa, ikiwemo Jumuiya ya Umoja wa Ulaya. Mkemeaji amegeuka mkemewaji.

Historia inaonesha kuwa, suala la haki za binadamu limetumiwa mara kadhaa na mataifa yenye nguvu duniani kuingilia uhuru wa nchi nyingine, hasa zinazoendelea, na kuleta dhahama kubwa. Mfano mzuri, na unaopendwa na “viongozi” wetu, ni Libya. Jumuiya ya Kimataifa imeweka misingi ya kuingilia uhuru wa nchi nyingine, hasa pale ambapo waliopewa mamlaka wameshindwa, au hawana motisha ya kusimamia haki za watu wanaowaongoza. Na, hatua za mwanzo za kuingilia uhuru huanza kwa maazimio, yakiwa na lengo la kujenga uhalali wa hatua zaidi. Madhara ya maazimio ni kumomonyoa heshima ya nchi, na ushawishi wake, ikiwemo katika nyanja za kiuchumi.


Wakati fulani katika historia, Tanzania ilikua Taifa masikini, lakini ambalo lilipata heshima kubwa kwa kusimamia utu na haki, na kupinga uonevu na udhalilishaji. Tulipaswa kuendelea kusimamia misingi hii, ndani na nje, huku tukiweka juhudi katika kujenga nguvu yetu ya kiuchumi. Kwa kukanyaga misingi hii, Taifa limefungua milango ya kuingiliwa, kubezwa ama kubagazwa, na kupuuzwa.


Mwanzoni mwa miaka ya sitini, Mwalimu Nyerere alitoa muongozo maarufu wa kisera juu ya namna ya kushughulika na sera ya mambo ya nje, uliokuwa na jina la kimombo, “Argue, Don’t Shout.” Tafsiri isiyo rasmi ni, “Jenga hoja, Usipayuke.” Katika utangulizi wa muongozo huo (ukurasa wa 11), yaliandikwa yafuatayo (nanukuu);
“Tunataka ama kushawishi watu, au kuwafanya waelewe ni kwa nini tumechagua mwelekeo fulani. Na kwa yoyote kati ya malengo haya, tunapaswa kujenga hoja, siyo kupayuka.” (Tafsiri yangu, ukurasa wa 11).


Kuna dalili za wazi kuwa, kama Taifa tumeanza “kupayuka”, badala ya kujenga hoja. Mfano mzuri ni namna ambavyo nchi imekabiliana na madukuduku ya jumuiya ya kimataifa juu ya hali ya haki za binadamu, uhuru wa kujieleza, kujumuika na kukusanyika. Hatua ya kumfukuza balozi wa Umoja wa Ulaya nchini ilifuatiwa na taarifa nyingi zenye mwenendo wa kubomoa jina, na hadhi ya nchi.
Majibu yetu yakawa duni, na yasiyojitosheleza. Kimsingi, ni hatua iliyoishia kudhoofisha mahusiano, na jina la nchi. Ni mgogoro wa kidiplomasia ulioanzishwa wakati ambao nafasi ya nchi kidiplomasia ni duni kabisa.


Tatizo kubwa katika utekelezaji wa sera ya mambo ya nje, kwa sasa, ni mkanganyiko (contradictions) kati ya hatua ambazo taifa linachukua, na malengo ambayo linataka kufikia. Kwa mfano, wakati tunadai hizi ni zama za diplomasia ya uchumi, ushiriki wa Taifa letu katika diplomasia ndani ya bara letu, na hata nje, unafanyika zaidi katika ngazi “za chini”, yaani waziri, na mabalozi. Kwa uwiano, ni mara chache unahusisha Rais, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais.


Athari ya aina hii ya utendaji imekua ni kutuma ujumbe, kwa jamii ya kimataifa, kuwa nchi yetu haioni umuhimu wa kuweka mkazo katika muhusiano, na kwamba siyo ya kutegemewa, kama ilivyokuwa zamani. Na ndivyo ilivyo; nchi yetu kwa sasa inaangalia ndani zaidi(inward looking), na imeacha ombwe la uongozi katika jamii ya kimataifa, ikiwemo katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Na, sababu ni kuwa kiitikadi (soma misingi, lugha isiyo na ukakasi), tumeyumba.


Mfano mwingine wa mkanganyiko unaonekana katika nia ya taifa letu kujiimarisha kama ushoroba wa biashara katika ukanda wa maziwa makuu, kwa upande mmoja, na namna ilivyokabiliana na mgogoro wa Burundi, kwa upande mwingine. Ushiriki, na juhudi za usuluhishi za Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, zimedunishwa sana na mwenendo wa mahusiano ya nchi yetu na Rwanda. Diplomasia ya uchumi, katika muktadha huu, ilipaswa kuhusisha taifa letu kujitanabahisha kuwa liko juu ya mgogoro husika.


Kuna changamoto za kimkakati pia. Kwa mfano, watawala walitangaza “vita ya kiuchumi” katika wakati ambao pia wanaonekana kuazimia kuweka mkazo katika diplomasia ya uchumi. Tatizo ni kuwa, vita ya kiuchumi inadunisha, au kufuta kabisa (negate) juhudi kiduchu za diplomasia ya uchumi. Haiwezekani kuendesha vita ya kiuchumi nyumbani, na diplomasia ya uchumi ugenini, na usitarajie madhara (hasi). Hili siyo suala la mapungufu kuhusu uzuri, au ukuu wa lengo, bali nakisi katika mbinu.


Tanzania, chini ya serikali ya awamu ya tano, ina malengo makubwa, na yenye kutia shauku. Changamoto kuu katika kufikia malengo hayo, hasa katika nyanja ya sera ya mambo ya nje, ni mkanganyiko katika utekelezaji wa sera hiyo. Mkanganyiko huu ni mkubwa kiasi kwamba sisi tunaotazama kutoka pembeni tunashindwa kuiona diplomasia katika inayoitwa diplomasia ya uchumi

Source : Iko wapi Diplomasia katika “Diplomasia ya Uchumi”?
 
Uteuzi huu unaonesha Mh. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anataka kushiriki moja kwa moja ktk masuala ya diplomasia kwa kuchukua cheo chake kama 'Balozi Namba Moja'.

Tofauti na mwendazake hayati Rais John Pombe Joseph Magufuli aliamua kujivua cheo chake cha ' Balozi Namba Moja" na kukikabidhi kwa 'Balozi Namba Mbili' Prof. Palamagamba Kabudi.

Hili la Prof. Palamagamba Kabudi kumuona 'Balozi Namba Moja' akijitoa umuhimu wake ktk kuelekeza diplomasia kulimpa wakati mgumu balozi namba mbili ambaye ni waziri wa mambo ya nje ambaye pia hakuwa na ushawishi au ujuzi wa diplomasia wala makuzi ndani ya wizara ya mambo ya nje kama kina Dr. Augustine Mahiga.

Sasa awamu ya sita kuna matumaini kuanzia balozi namba moja ambaye ni Mh. Rais, balozi namba 2 ambaye ni waziri wa mambo ya nje na wale mabalozi wengi wengine namba 3 wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje watakuwa wanasoma diplomasia ya uchumi ya kutoka ukurasa mmoja usio na maneno 'beberu, wanyonyaji, wezi, n.k' .
 
Na vyote hapo vinaweza kumtokea balozi kufuatana na recommendation za nchi alipo. Wao wanaweza kuomba aendelee kuwepo, wanaweza kuomba aondoke pindi muda ukiisha au kabla n.k.
 
Sijawahi kuona uteuzi wa Mabalozi wengi hivi bila kupangiwa vituo. Kama mama hakuwa tayari kuwapangia vituo si angesubiri? Kwanini alikurupuka kuwatangaza ilhali vituo vyao vya kazi havijapangwa?
Wazee wengi wamestaafu au muda wao umefika Mama anaona warudi wapumzike pia majina wateule lazima yapelekwe kwa nchi husika na kukubaliwa ndio hupangiwa vituo....sio shida ni protocol tu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Wakuu naomba tujuzane hapa hapa, Nowdays naona ubalozi imekuwa kama hisani au mapenzi ya mtu siyo taaluma au?

Although pale kurasini jirani na jkt mgulani kuna chuo cha diplomasia kinazalisha wasomi wenye fani na ustadi huo.

Now naona kila mtu popote alipo ananyofolewa kuwa balozi, so hao wasomi wanafanya kazi gani mpaka kupewa mtu kama mwanaharakati, mstaafu au mjeda?
.

NANI KATUROGA?
 
..kweli zama zimebadilika.

..lakini ukweli huwa haubadiliki.

NB:

..naamini kilichotokea ni Magufuli kujaribu kulazimisha uteuzi wa Dr.Bashiru.
Ila mpaka sasa Dr. Bashiru ni - Balozi Mheshimiwa Dr. Bashiru Ally. Cheo chake cha balozi bado anacho, cha ubunge (Mheshimiwa).
 
Sijawahi kuona uteuzi wa Mabalozi wengi hivi bila kupangiwa vituo. Kama mama hakuwa tayari kuwapangia vituo si angesubiri? Kwanini alikurupuka kuwatangaza ilhali vituo vyao vya kazi havijapangwa?
Nahisi ni kwasababu hana kazi nyingi za kufanya Ikulu anajikuta anaboreka. Hivyo anaamua kufanha vitu vya kum keep busy. Kumbuka hana ratiba ya kufanya ziaea yoyote kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom