Uteuzi wa Mabalozi 23 leo, Hakuna aliepangiwa kituo cha kazi au mimi sijaelewa?

Uteuzi wa Mabalozi 23 leo, Hakuna aliepangiwa kituo cha kazi au mimi sijaelewa?

Leo kupitia page ya kurugenzi na mawasiliano Ikulu nimeona statement ya uteuzi wa wabarozi 23 uliofanywa na Mh Rais Samia, lakini sijaelewa mpaka sasa kuwa katika wote 23 hawajapingiwa vituo vya kazi? Kwanini? Anafanya alimradi abadili ama ye anateua wakati akisubiri wa kumtoa?
Utaelewa tu ndani ya siku mbili tatu.
 
Kituo cha kazi ni mpaka nchi wanazotakiwa kwenda waridhie
Hiyo iko tayari list ni mchakato tu ila wameshapangiwa approval zikija na huku wameshaapa inakuwa tu taratibu za kutaarifu tu wewe huku wewe kule kwa maana hiyo wanaorudishwa majina tayari haya ni mambo ya kawaida ni kama unasajili team halafu kocha anapanga nani anacheza na bench nani.
 
Vuta subira kuna maBalozi wanarudishwa na wengine kustaafu...
 

1. Kwa Tanzania ubalozi huwa ni uteuzi wa miaka 4. Mabalozi wengi walioteuliwa na JPM wameshamaliza muda wao.


2. Kwenye orodha ile kuna watumishi wa wizara ya mambo ya nje wanaokaimu ukuu wa idara mbalimbali. Utaratibu ni watumishi hao kupandishwa ngazi kuwa mabalozi, na kuthibitishwa kuwa wakurugenzi ktk idara husika za wizara ya mambo ya nje.

3. Kwenye orodha ya walioteuliwa wako watumishi mbalimbali wa IKULU ambao walikuwa wasaidizi wa Rais aliyepita. Kama mpya amekuja na wasaidizi wake hivyo wale wa zamani inabidi wapangiwe majukumu mengine.

4. Nchi walizopangiwa kwenda kutuwakilisha bado hazijatuma taarifa za kuridhia uteuzi wao.
 
Zamani kama vile huwa wanateuliwa na nafasi zao tayari, siku hizi naona kama uteuzi then kupangiwa kunafuata au ni taratibu za diplomasia zimebadilika?
 
Serikali ya Bongo iliwahi kumkataa balozi wa Zambia sababu ya jina lake, ni mpaka nchi wanazokwenda waridhie, pia mabalozi wanaorudishwa wanahakikiwa mfano Slaa, Tossi ni lazima wanrudi
Lakini balozi wa Zambia alitisha,. Musenge Mukuma! Hata Mimi nisingempokea.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
..nimewahi kusikia tetesi kuwa nchi moja ya ulaya ilikataa kumthibitisha balozi wetu.

..pia nimewahi kusikia tetesi za jamaa mmoja aliteuliwa kuwa balozi akakataa uteuzi huo.

..wote wawili walikuwa na vyeo vya kijeshi.

cc MALCOM LUMUMBA
Tumainiel Kihwelu R.I.P (Nigeria) akapelekwa kuwa mkuu wa mkoa shinyanga.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
..pia kuna wateuliwa ambao wanakaimu kurugenzi mbalimbali ktk wizara ya mambo ya nje. Nadhani kuteuliwa kwao kuwa mabalozi ni KUWATHIBITISHA ktk nafasi hizo.

..wakurugenzi wote wa idara za wizara ya mambo ya nje, isipokuwa mkurugenzi wa fedha na mkurugenzi wa utawala, huwa na hadhi / cheo cha ubalozi.
Kwanini isipokuwa hao wakurugenzi wawili wa fedha na utawala ndio hukosa hadhi ya ubalozi?
 
Kwanini isipokuwa hao wakurugenzi wawili wa fedha na utawala ndio hukosa hadhi ya ubalozi?

..kwasababu hao wakurugenzi wawili sio watumishi specific wa wizara ya mambo ya nje.

..watumishi wa wizara ya mambo ya nje wana ngazi zao za utumishi, na cheo cha mwisho ni ambassador / balozi.
 
Back
Top Bottom