Uteuzi wa mapema wa Prof. Kabudi, kama Waziri wa Mambo ya Nje ni kujiaandaa kwa ajili ya kesi iliyofunguliwa huko ICC?

Wameshakiri kupokea barua, kama bado huamini Hilo sio tatizo letu. Na pia kama uchaguzi ulikuwa WA haki walalamishi wataumbuka.
 
Unajilisha upepo na kuidanganya nafsi yako kwa kitu unachojua kabisa hakipo. Jitathmini
 
Mkishashindwa uchaguzi mnageuka wapiga ramli na wambea.
 
Katiba imesiginwa kwa nguvu zote. Baraza la mawaziri huteuliwa baada ya waziri mkuu kuapishwa.Baraza la Mawaziri mhimili wake ni waziri mkuu. Uteuzi wa baraza la Mawaziri sharti ufanywe na Rais wakisaidiana na waziri Mkuu ambaye hawi waziri mkuu hadi aapishwe na Rais. Kwa hiki kilichofanyika ni kwamba Waziri mkuu si kitutena, Katiba imevunjwa waziwazi. Waziri Mkuu akijiuzulu au kufutwa kazi maana yake Baraza la mawaziri linavunjika hapo hapo.

Kwetu sasa waziri mkuu si chochote. Ni kukiuka na kuvunja katiba waziwazi. Halafu huku ni kuweka madaraja miongoni mwa mawaziri. Inaonekana hawa wawili ndio muhimu na wa kipekee kuliko wengine.

Hii siyo picha nzuri. Mawaziri wote ni sawa mbele ya Katiba. Tunaoneka wote nchini ni wahovyo kabisa.
 
Nachopende ICC usiri na ukusanyaji ushahidi..... Yaan unatunzwa na kukusanya by any cost...
Pompeo alitonya kidogo pale alipo mbani kijana wa Kolomije na wenzake kukanyaga USA RIVA Hilo pia liangalieni kwa umakini hiyo Usariva aliyo baniwa siyo inayo ongozwa na J wa muro (take care)
 
Inabidi Waiziri wetu Kabudi awe makini asije akaenda huko kwa mabeberu wakamdaka kama walivyokuwa wanadaka ndege zetu
 
Uteuzi wamapema haujakaa vizuri kiprotoko kwa heshima ya Waziri Mkuu kwa rejea kisheria katiba inavyo tamka ataapishwa pm kwanza ndipo washauriane kuunda baraza la mawaziri.

Kama alivyofanya kwa kulipeleka jina la pm bungeni kupitishwa na bunge.

Akili kidogo imeshindikana nini? Subira huvuta heri
 
Huyu Jiwe ni kawaida yake kuisigina Katiba ya nchi waziwazi kabisa!

Kama alivyofanya katika hili la uteuzi wa mawaziri wawili pekee, kati ya mawaziri zaidi ya 20 wanaohitajika katika Baraza la mawaziri
 
Chandimu mnajitekenya bureee! Hafungwi mtu hapa, muda huu mngekuwa mnajipanga kujenga Chama nyie kaguu na njia kwa Wazungu, kuja kushituka 2025 tunawapiga spana tena
Nyinyi mnajivunia kwa kuwa mnatumia dola kubaki madarakani.

Hayo si maneno yangu, bali ni maneno ya Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally
 
Yani apo wale mawaziri waliobaki wajiandae kutorudi tena. Hawa wengine nafasi yao ilikuwa imeandaliwa hata kabla ya uchaguzi.

Kumbuka Philip Mpango na mwenzie waliingia kama viti maalumu. Maelekezo yakatoka wagombee majimbo na wakapita bila kupingwa. Na yeyote aliyejaribu kupinga anakiona cha moto hivi sasa.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Tukisema mmekunywa mnapaniki.
 
Yaani hapo ndiyo ujue kuwa huyu mtu hapendi kabisa kufuata sheria na kanuni za kazi

Katiba ya nchi anaisigina waziwazi

Badala yake anataka kutumia ubabe wake kwa kila kitu akifanyacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…