Uteuzi wa Paul Makonda kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa ni moto!

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ni moto, si, tu kwa Upinzani bali pia kwa waliolala na kujibweteka kwa kufanya kazi kwa mazoea ndani ya chama na ndani ya serikali iliyopo mamlakani.

Huyu kijana si tu mwanasiasa bali pia mwanaharakati mahiri nchini. Ana hulka za jino kwa jino, sina hakika kama kabadilika.

kwa maoni yangu uteuzi wake unalenga kujibu mapigo ya upinzani dhidi ya chama na serikali iliyopo Madarakani kwa hoja na vihoja.

Uteuzi huu pia unalenga kuudhibiti upinzani na kile kinachodaiwa ni upotoshaji dhidi ya mipango na hatua mbalimbali zinazo chukuliwa na serikali kuwaletea wananchi maendeleo.

Uteuzi huu ni amsha amsha dhidi ya walio lala na kujisahau ndani ya chama Tawala na ndani ya serikali sikivu, hii ni pamoja na mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi na wateule mbalimbali wa Rais.

Kwa kijana huyu ubunifu na uwajibikaji wenye matokeo yanayo jidhihirisha na kuonekana kwa umma ndio itakua pona ya wateule wengi.

Uteuzi wa Paul Christian Makonda kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa ni moto chini nchini.

swali linabaki ni je, uteuzi huu utaimarisha au utadhoofisha upinzani katika siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu 2025?
 
Kazi yake ni kupewa vya kusema na kusemea chama akizidi zaidi ya hapo wahafidhina wamefungua mlango nusu wana mlia mingo!
 
Mjini njoo na akili tu...
7a8bf818785d418f81c649cf8d99db82.jpg

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Nadhani CCM itadhoofu maana kuna vijana ndani yake hawajafurahia huu uteuzi.

Kikazi Makonda anaweza sana.

..kipindi cha Magufuli alionekana anaweza kwasababu alikuwa na vyombo vya dola nyuma yake.

..hili jukumu alilopewa linamlazimisha awe mjenga hoja zenye mantiki na ushawishi, na sio kutisha watu kama alivyozoeleka ktk awamu ya 5.
 
Ni moto, si, tu kwa Upinzani bali pia kwa waliolala na kujibweteka kwa kufanya kazi kwa mazoea ndani ya chama na ndani ya serikali iliyopo mamlakani.

Huyu kijana si tu mwanasiasa bali pia mwanaharakati mahiri nchini. Ana hulka za jino kwa jino, sina hakika kama kabadilika.

kwa maoni yangu uteuzi wake unalenga kujibu mapigo ya upinzani dhidi ya chama na serikali iliyopo Madarakani kwa hoja na vihoja.

Uteuzi huu pia unalenga kuudhibiti upinzani na kile kinachodaiwa ni upotoshaji dhidi ya mipango na hatua mbalimbali zinazo chukuliwa na serikali kuwaletea wananchi maendeleo.

Uteuzi huu ni amsha amsha dhidi ya walio lala na kujisahau ndani ya chama Tawala na ndani ya serikali sikivu, hii ni pamoja na mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi na wateule mbalimbali wa Rais.

Kwa kijana huyu ubunifu na uwajibikaji wenye matokeo yanayo jidhihirisha na kuonekana kwa umma ndio itakua pona ya wateule wengi.

Uteuzi wa Paul Christian Makonda kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa ni moto chini nchini.

swali linabaki ni je, uteuzi huu utaimarisha au utadhoofisha upinzani katika siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu 2025?
Ni Makonda au Bashite tuanzie hapo kwanza???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo alikuwa anafata amri za boss wake hajajifanyia hata kimoja kwa mawazo yake.

CCM wanalifahamu hilo ndiyo maana hawakumuadhibu muda wote.
 
Back
Top Bottom