Uteuzi wa Paul Makonda kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa ni moto!

Huyo alikuwa anafata amri za boss wake hajajifanyia hata kimoja kwa mawazo yake.

CCM wanalifahamu hilo ndiyo maana hawakumuadhibu muda wote.
hivi sasa tutajua kama alikua ni yeye mwenyewa ama ni maelekezo kutoka juu
 
Huyo alikuwa anafata amri za boss wake hajajifanyia hata kimoja kwa mawazo yake.

CCM wanalifahamu hilo ndiyo maana hawakumuadhibu muda wote.
umeongea kinyonge sana bibi. inaonyesha hujafurahishwa na uamuzi wa ikulu kumrudisha makonda kwenye mfumo.

umepigwa na kitu kizito.pole sana bibi.
 
makonda na mama wanajuana mda mrefu, nadhani lilikuwa ni swala la when and which position tu, ila ilikuwa wazi kuwa makonda angerudi kwenye uongozi, ukizingatia pamoja na kuwanna kashfa nyingi kama sabaya ila hajaguswa kabisa.
 

Timu Za Wasaka Urais kama Yule Mvaa bendera , na lile kundi la Februari uteuzi huuu ni pigo kubwa sana ..

Kuna kundi jipya linaibuka la kumsaidia mama na 2025 watoe PM na Makamu Halafu Makonda naye atapata jimbo moja pale Mwanza…na uwaziri
 
makonda na mama wanajuana mda mrefu, nadhani lilikuwa ni swala la when and which position tu, ila ilikuwa wazi kuwa makonda angerudi kwenye uongozi, ukizingatia pamoja na kuwanna kashfa nyingi kama sabaya ila hajaguswa kabisa.

Bila mama Makonda angekua segereea Au angekua katunguliwa na maadui zake…..,

Amemsaidia kupata moja ya nyumba za TBA pale Oysterbay na akaaigiza auziwe.

Ameingizwa kwenye payroll na Pamoja na kuwa nje amekua anapokea mshahara

Biashara zake hazijabuguziwa….Maduka manne ya madawa miji ya DAR, MWANZA na Arusha .

Ana uangalizi au ulinzi wa aina fulani hata kama sio moja kwa moja kumekua na watu wa kumtizama asidhurike..

KESI zake zote zimekwamia kwa DPP kwenda mahakamani.

ILIKUA arudi toka mwaka Jana wakawa wanasubiri baadhi ya kesi alizofunguliwa ziishe … [ kina Kubenea wa kesi binafsi nao wamevuta ]


Tatizo pekee linaloenda kutokea ni mgawanyiko ndani ya ccm hasa kwa wafuaasi wa Mwenyekiti ambao hawaataki kabisa kumuona Makonda ……hivyo anaenda kukabiliwa na upinzani mkali ndani .

HUENDA Makonda akadumu Muda mfupi sana kwenye cheo hasa itategemea na siku zake 100 za mwanzo na maoni ya wanachama …na pengine uwezekano ni kurudishwa kuwa Mkuu wa Mkoa au kuingia kama msaidizi wa Rais hasa kuelekea uchaguzi Mkuu.
 
Tulizen mshono , makondonda kwenye siasa bado sana japo anabebwa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…