Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,251
- 22,929
Mvomero sio Wilaya kongwe,na kwa hiyo kimaendeleo iko nyuma sana.Wilaya hii ina matatizo mengi, ya msingi yakiwa upatikanaji wa maji,migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imedumu kwa miaka mingi sasa.Awamu zote zinaonekana kushindwa kabisa kutatua tatizo hili,sababu kubwa ikiwa viongozi kuwa mgongano wa kimaslahi. Lipo pia tatizo la kilimo,hasa upande wa ugani na umeme.Lipo pia tatizo la miundombinu ya elimu, ambalo limefanya wananchi wengi wa Wilaya hii kukosa elimu na hivyo kuwafanya wawe nyuma sana kimaendeleo.
Lipo tatizo kubwa mama la uongozi katika Wilaya hii.Sina haja ya kusema awamu zilizopita uongozi ulikuwaje,itoshe tu kusema kwamba Wilaya hii tangu kuanzishwa kwake haijawahi kupata viongozi committed kwa maendeleo ya Wilaya hii,tangu ngazi za chini kabisa mpaka juu.Si ajabu kwa hiyo kwamba maendeleo ya Wilaya hii ni duni sana.
Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi,tena uchaguzi wa mhula wa pili awamu ya tano.Tulitegemea basi kwamba Wilaya yetu ingeangaliwa kwa jicho la pekee,ili ipate viongozi makini na wazuri ambao watasukuma mbele maendeleo yetu.Kilichotokea hata hivyo ni tofauti kabisa.Van Zealand ambaye ameteuliwa kugombea kwa tiketi ya CCM hawezi kutusaidia kabisa.
Huyu bwana amekuwa mwenyekiti wa Halmashauri kwa muda mrefu,na katika kipindi chake chote alichokuwepo hali ya Wilaya yetu haijaboreka na matatizo ya wananchi yapo pale pale, au hata kuzidi. Katika hali ya kawaida kabisa, hili lingetosha kumuengua. Na kwa nini ameteuliwa yeye kupeperusha bendera ya CCM wakati aliyepita kwenye kura za maoni ni Makala?
Niseme wazi, kwetu Makala angekuwa bora zaidi kuliko Zeland,ingawa of course naye ana matatizo yake.Van Zeland tunamjua, yuko kimaslahi zaidi na naamini ameingia huko kwa ajili ya maslahi yake binafsi,na wala sio kuwatumikia wananchi.
Ipo minong'ono mingi kuhusu michezo michafu,na inasemekana hata tambo zake mwenyewe zinaashiria hili. Katika hili naiomba TAKUKURU iingilie kati,huenda labda ikatunusuru.
Mwisho,binafsi najiuliza sana,hivi kwa nini CCM ilitangaza hadharani kwamba si lazima anayepita kwenye kura za maoni ateuliwe yeye kupeperusha bendera ya CCM?Hivi chama hakikuona kwamba mwanya huu ungeweza kutumiwa vibaya na watu wasio waaminifu kama ilivyotokea Mvomero, ingawa nia ilikuwa njema?