Uteuzi wa wabunge Ulenge wabunge walio na uchungu na nchi hii na wasomi

Uteuzi wa wabunge Ulenge wabunge walio na uchungu na nchi hii na wasomi

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,199
Kwenye kura za maoni asilimia kubwa RUSHWA ilitumika sana na hii haina mjadala kila mtu aliona. Wengi waliopita waliwanunua wapiga kura na kuwaacha wale walio na uwezo kwa kukosa fedha za kuwahonga wajumbe waliachwa.

Ninaishauri Chama changu. Chama kifanye utafiti wa kina na iwapendekeze wale wanaofaa hata kama alishika namba za mwisho. Msituteuliwe Wabunge wanaojua kusoma na kuandika. Achaneni na kuteua Wabunge waliomaliza darasa la saba.

Hawa ukiwapa kitabu cha bajeti ili wakitafsiri hawawezi . Tuko kwenye ulimwengu wa kidijitali achaneni na kuteua Wabunge wa darasa la saba. Tumieni haki. Mfano jana wananchi wa Vunjo wanashangaa kwa nini Mbunge wao aliyemaliza muda wake hakushika namba moja. Wote tunajua sababu ni nini.

Kushika namba moja kisiwe kigezo cha kuteuliwa. Fanyeni utafiti . Bunge lijalo tunawataka Wabunge walio na uchungu na nchi na wasomi. Wabunge ambao siyo rubber stamp.
 
Back
Top Bottom