Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Yaani nakubaliana na wewe kabisa. Fikiria mtu hujawahi kuajirwa au kufanya kazi serikalini ulikuwa unajifanyia shughuli, biashara au unajiimbia na kufanya maigizo ghafla unateuliwa kuwa DC au RC kwenda kusimamia watumishi na maafisa waandamizi kama mkuu wa polisi wa walaya, RPC, wakuu wa idara, wakurugenzi na vibopa wengine waliofanya kazi serikalini na sehemu mbalimbali kwa zaidi ya miaka 15 mpaka 28 wewe hujui hata ABCs za utumishi wa umma kwakweli siajabu ukageuka Sabaya au Bashite.
Kwakweli mama hakushauriwa vizuri kabisa. Yaani kama mtu mwenye leseni ya bodaboda unamkabidhi kuendesha basi la abiria 65 au mwendo kasi la abiria 100 na wakati huo huo hajawahi kuwa ha konda au tandiboi kwenye vyombo hivyo
Kwakweli mama hakushauriwa vizuri kabisa. Yaani kama mtu mwenye leseni ya bodaboda unamkabidhi kuendesha basi la abiria 65 au mwendo kasi la abiria 100 na wakati huo huo hajawahi kuwa ha konda au tandiboi kwenye vyombo hivyo
Inasikitisha sana Tanzania sijui inaelekea wapi. DC ni nafasi nyeti ya kuunganisha watendaji na jamii inayowazunguka. Kusimamia mambo ya ulinzi na usalama.
Hii ni nafasi ya waandamizi kutoka katika utumishi au chama, wakiwa wamejaa utu uzima na busara za kumwagika. Leo unaenda kuokoteza wasanii na watu mitandaoni.
Naona Tanzania inapoteza uelekeo kabisa. Hawa jamaa wanatupa kazi sana kuirudisha Tanzania kwenye reli.
Mimi sijawahi kushuhudia uteuzi wa hovyo kama huu toka nizaliwe.
Kiufupi rais kaelemewa na majukumu