Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliofanyika Juni 2021 umeshusha hadhi ya nafasi hiyo

Yaani nakubaliana na wewe kabisa. Fikiria mtu hujawahi kuajirwa au kufanya kazi serikalini ulikuwa unajifanyia shughuli, biashara au unajiimbia na kufanya maigizo ghafla unateuliwa kuwa DC au RC kwenda kusimamia watumishi na maafisa waandamizi kama mkuu wa polisi wa walaya, RPC, wakuu wa idara, wakurugenzi na vibopa wengine waliofanya kazi serikalini na sehemu mbalimbali kwa zaidi ya miaka 15 mpaka 28 wewe hujui hata ABCs za utumishi wa umma kwakweli siajabu ukageuka Sabaya au Bashite.

Kwakweli mama hakushauriwa vizuri kabisa. Yaani kama mtu mwenye leseni ya bodaboda unamkabidhi kuendesha basi la abiria 65 au mwendo kasi la abiria 100 na wakati huo huo hajawahi kuwa ha konda au tandiboi kwenye vyombo hivyo
 
Wewe nani mpaka useme hivyo cha kushangaza wewe ni mateka wa Mbowe unataka Rais Samia, akufurahishe? Nyie kupinga ndiyo kazi mliotumwa na Mfalme Mbowe, Rais kawambia mpo huru kufanya mikutano yenu nchi nzima au nyie mnafanyie JF.
Hivi unatambua kwamba vyama vya upinzani viko kisheria, kuikosoa na kuipinga serikali? Eti wanapinga kila kitu, wewe ni nani uwapangie cha kukosoa?

Kuhusu nafasi za RC na DC, jinsi siku zinavyokwenda mbele, ndio tunatambua kwamba nafasi hizo ni kama peremende za kumgawia yeyote ambaye Rais anamtaka. Hatuhitaji tena kuwa na nafasi kama hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…