Uthibiti wa Matumizi ya Mapanga/Machetes Nchini Tanzania

Uthibiti wa Matumizi ya Mapanga/Machetes Nchini Tanzania

fundi radio

Member
Joined
Apr 2, 2023
Posts
61
Reaction score
104
ulinzi ni jukumu la kila raia , sasa tukiweka ulinzi tu kwa viongozi pekee tukawaachia raia mzigo mkubwa wa ulinzi wao. itakuja kuwa backfire vibaya sana. sio salama sana viongozi kuzungwa na watu wengi wa hovyo(wasio fuata taratibu na sheria/( kujichukulia sheria mkononi)).


ili jamii nzima iwe salama na amani, inabidi watu wa kawaida (local people) kuishi kwa amani na upendo ndipo na huku juu kwa viongozi nao watakuwa salama. Tuache kuweka taratibu na sheria zinazo tugawa.

kuna haja ya lazima ya kudhibiti matumizi ya mapanga/machetes. panga ni zana au silaha hatari inayotumika kufanya uhalifu kwa muda mrefu.

mauwaji ya albino ni (mapanga/machetes) ndio hutumika kufanya butcher,

wezi hutumia mapanga kuwaibia wananchi,( panya road, wezi wa kutumia boda).

migogoro ya jamii mfano jamii ya wafugaji na wakulima hutumia mapanga kufanya uhalifu,

unyanyasaji wa kijinsia pia mapanga yametumika kufanya uhalifu kwa jinsi Fulani.


sasa nini kifanyike ?


kuwepo na usimamizi wa utengenezaji wa ndani na vibali vya kununua kutoka nje ie(china).

maana sasa ivi karibia kila nyumba hapa mjini kuna mtu anamiliki panga , sasa hapa mjini panga la kazi gani ? ukiwauliza ooo kwa ajili shughuli kadhaa ikiwemo ya ulinzi.

na kuna wale wanatembeza barabarani na bar wanauza mapanga na visu , aloo ukiwatizama nyuso zao zinatia wasiwasi.

pia na ndugu zetu wafugaji wanao tembea na masime, jambia, malungu kiunoni , huku mjini hili jambo halikubaliki kwakweli. wafundishwe utaratibu wa kuishi wafikapo mjini.

okay kama panga, wananchi wanaitambua kama ni silaha ya kujilinda inabidi sasa kuwe na utaratibu wa kisheria wa umiliki. japo kwa sheria zilizopo panga haitambuliki rasmi kama ni zana ya kujilinda na adui.
na kwaambao hawana vibali iabidi wazisalimishe kwa polisi na kupewa zawadi kwa kuwa raia wema.

Tuendelee kuboresha mipango miji ya iwe ya kisasa , itawasaidia sana vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kufanya KAZI zao kwa weledi.

Pia kama jamii ina Amani na upendo , wananchi wanamiliki silaha za KAZI Gani?,
Wanajilinda na nini ?.

Je wananchi kuzidi kumiliki silaha ndio kutaleta Amani na upendo ? Jibu ni hapana.

Ili Amani, upendo na Haki zitawale kwenye jamii basi wananchi hawapaswi kumiliki silaha yoyote ile.

ujue tusichukulie Mambo POA POA.
 
Wanaume wa Daslamu bwana,
Yani kumiliki panga ndani nikiwa Dar unaona ajabu
 
Unapigia chapuo tusiwe na silaha za kawaida za kujihami halafu kukitokea dharura mnaanza kulialia na kutia huruma

Suluhisho la yote uliyoandika lipo kwenye ubongo zaidi na siyo kwenye misuli. Kama moyo wa mtu unawaza uharibifu hata umnyang'anye panga haitasaidia
 
Mi namiliki rungu hiyo hata uje na panga hutoboi nikikushushia moja tu watu wanaulizana "Mbona taarifa ni za ghafla alikua anaumwa au?"
 
Kwahiyo wakisha chukua mapanga miti na nyama machinjoni tutakatia nini? Nafikiri shida siyo mapanga, shida ni akiri za watumiaji, kama kweli wameamua wapambane na dawa za kulevya kwa nguvu zote, bangi, sigara, matumbaku na aina za upuuzi wowote ule, kama wanata jamii bora yenye afya ya akili, piga vita kila mihadalati uwe halali au si halali piga vitaaaaaaaaa...
 
Back
Top Bottom