Uthibitisho wa Tiba ya Gumboro

Uthibitisho wa Tiba ya Gumboro

Habari wanajamii leo napenda kushare na Jamii pamoja na taasisi mbali mbali ili kuthibitisha na kufanya utafiti zaidi kuhusiana na Ugonjwa wa GUmboro kwa Kuku.


Nikiwa mgeni katika sekta ya ufugaji wa kuku wa kienyeji nimekumbana na ugonjwa wa Gumboro kutokana na kuchelewa kutoa Kinga na kupelekea ugonjwa kushambulia vifaranga na kuku wa kubwa.
Baada ya kuthibitisha ni ugonjwa wa gumboro unashambulia kuku wangu na kuripot vifo viwili vya vifaranga huku wengine wakiwa tayari na maambukizi.niliwapa kinga kujaribu kokoa hasara.
baada ya siku ya 3 kutoa kinga kuku wengi walinyong'onyea na kusinzia .siku hiyo majira ya saa 6 siku ya jumapili nikua nimenunua nanasi,mke wangu alilichonga alikuta sehemu kubwa ya nanasi imekua rangi ya udongo/kuharibika na nanasi lenyewe lilikua na sukari kali sana.
sehemu ile iliyokua imeharibika ilikatwa.. Baada ya muda yule kuku alizidiwa alifata harufu ya nanasi na kuanza kulidonodono na kula wengine nao walifata wakaligombania na kulimaliza
nilipoona vile na kuku wamepoteza hamu ya kula niliwaopa na vipande vingine wakaendelea kula baada ya kama dakika 30 yule kuku wa kwanza nilimwona akiwa anachangamka.kuku huyu nilimwona wakwanza kutokana yeye kupenda kukaa mahali nipo. niliwatafuta kuku wengine nao walikua wanacheza cheza na wengine wakila kile chakula kwa kasi.

Leo siku ya 6 sijaona kuku anaezubaa tena na kuharisha.

Huu ni Uthibitisho wangu wa Kuku wangu kupona Gumboro kwa Nanasi ?
Wanajamii na Taasisi za mifugo na kilimo naomba mufanye utafiti Katika Katika nanasi pamoja na jamii yake. huenda likawa ni suluhisho la maradhi mengi kwa KUKU.

ASANTE!
Asante nimejifunza kitu
Mkuu niPM namba yako. Nataka kuchi
0717209059 ila mayai yanachanganyika mkuuu kuku wote wapo pa1 kama uonavyo profl picha
HII NI RATIBA YA CHANJO NA DAWA
SIKU YA 7.

vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDELI).chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kasha kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga mbali na eneo ambalo kuku wengine

wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baada ya hapo vifaranga wapewe maji yenye vitamin

SIKU YA 14.
Wapewe chanjo ya GUMBORO(IBD).chanjo hii pia huchanganywa katika maji na kupewe vifaranga kwa muda wa masaa mawili tu.baada ya hapo vifaranga wepewe vitamin.
Siku ya 21.(wiki ya tatu)
Rudia chanjo ya Newcastle
SIKU 28(mwezi)
Rudia chanjo ya GUMBORO IBD
 
HII NI RATIBA YA CHANJO NA DAWA
SIKU YA 7.

vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDELI).chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kasha kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga mbali na eneo ambalo kuku wengine

wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baada ya hapo vifaranga wapewe maji yenye vitamin

SIKU YA 14.
Wapewe chanjo ya GUMBORO(IBD).chanjo hii pia huchanganywa katika maji na kupewe vifaranga kwa muda wa masaa mawili tu.baada ya hapo vifaranga wepewe vitamin.
Siku ya 21.(wiki ya tatu)
Rudia chanjo ya Newcastle
SIKU 28(mwezi)
Rudia chanjo ya GUMBORO IBD
one lv umetisha upo wap ww
 
Back
Top Bottom