Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Biashara ya maziwa ,Kuna sehemu chalinze wanauza Lita 1 elfu moja
Mchanganua kwa elfu 50
Lita 40@1000=40000
Dumu la Lita 50=3000
Nauli =7000
Apo elfu hamsini inakua imekwisha
Maziwa kwa dar Lita moja 2000 mpaka 1500
Kwa kua Lita hamsini ni kidogo ,sio lazima kufikisha mzigo dar.unaweza uzia kibaha kwa Kila lita 1500
Faida 20000 kwa siku.ukiuza dar kwa 2000 kwa Lita ,faida 40000 kwa siku.
Nikiikosa 50000 hiyo ,kutakua na mkono wa mtu
 
10000 × 30 = 300000

hao wanafunz utawauzia chips mpaka jmosi na jumapili

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikisema kila siku 10k haimaanishi nitafanya biashara ya mauzo 10,000 kila siku

kuna siku biashara nitapata 15k kuna siku nitauza 20k na kuna siku nitarudi na 8k

kwenye 15k (lengo ni 10k so 5k ipo pembeni) kwenye 20k (lengo ni 10k so 10k ipo pembeni)

Jmosi na Jpili we fill the gaps kwa zile zilizokua zinazidi na tunaziweka pembeni kila siku.
 
Nikisema kila siku 10k haimaanishi nitafanya biashara ya mauzo 10,000 kila siku

kuna siku biashara nitapata 15k kuna siku nitauza 20k na kuna siku nitarudi na 8k

kwenye 15k (lengo ni 10k so 5k ipo pembeni) kwenye 20k (lengo ni 10k so 10k ipo pembeni)

Jmosi na Jpili we fill the gaps kwa zile zilizokua zinazidi na tunaziweka pembeni kila siku.
well noted

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bonge la shule hili mkuu
Hakuna tajiri mwenye dhamira ya kumkomboa masikini maana umasikini wetu ndiyo utajiri wao.
Ndiyo sababu wako tayari kutapanya pesa ovyo (kuwalipia viingilio uwanjani, kudhamini team mnazozipenda n.k) lakini si kuwekeza kwenye sekta zitakazowagusa moja kwa moja kiuchumi.
Kwa tajiri kumuwezesha masikini ni kujibomoa mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Respect sana kwako mkuu
Kwa kijana yoyote ambae ramani hazijakaa sawa namshauri afwate huu ushauri kwa moyo wote na akili zote na kama ataona aibu ahame mkoa akaifanye mkoa mwingine kwa uhuru.kwani ni biashara ya mtaji mdogo na yenye faida kubwa.

Mimi ni shuhuda wa hii biashara na sijaiacha hadi leo.nilipomaliza college na kielimu cha diploma ya pharmacy nimedispense dawa kwenye maduka makubwa ya wahindi kwa miezi 3 tu nikiwa nalipwa laki 5 na nusu.
Nkaacha kazi nkasepa chuga kuuza mishkaki! Wazaz,ndugu na jamaa wacha wanilaumu mno hakuna hata mmoja alienisupport ila sasa hivi wananipongeza!

Yani watanzania wengi sijui tukoje,mtu yupo radhi afanye kazi ya heshima ila haina maslahi makubwa kuliko kazi isiyo na hadhi yenye faida lukuki.ndani ya mwezi wa kwanza tu niliingiza faida ya m1.2!sasa ndugu zangu wana jf kipi kilikua bora kati ya kugawa dawa huku ukiwa na clinical coat ndani ya kiyoyozi mhindi anakupelekesha siku nzima kafunga na camera kabisa kila kona ukichat au ukisinzia ni msala,kazi unaingia saa 1.30 hadi saa 2-3 usiku kila siku huku upande wa mishkaki nilikua nadaamka saa10 kwenda machinjioni kununua nyama kwa bei chee narudi naandaa saa12 niko shule ya msingi naanza kuwachomea madogo saa 6 mchana nshamaliza naingia mtaani kuangalia mishe nyingine,jioni tena huyo maeneo ya stendi kuchoma mishkaki.

Najua ni ngumu sana kwa msomi ila toka mkoa uliopo wanakujua nenda sehemu ambayo hakuna hata anaejua kama ulifika hata la 7!

Nilianza hivyo taratibu hatimae nkaweka vijana waaminifu niliowatoa vijijini huko na hivi nnavyoandika,naingiza si chini ya laki mbili faida kila siku ya Mungu bila pua za TRA wala cha Halmashauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera mkuu. Huo ndio ubinadamu. Ingekuwa wale wenye mitaji mikubwa wangewafanyia hivi wengine Tanzania ingebadirika haraka sana. Huwa najiuliza sana mtu kama mo au bakhresa kwa nini asikopeshe wenye kutaka biashara lakini hawana mitaji?.

Kuliko kufadhiri litimu kama simba wanakula hela tu tena nyiiingi sana ukipiga hesabu kwa mwaka. Lakini hakuna faida yoyote wala muendelezo wa hizo timu,zote zinashindana kushindana zenyewe tu na kuishia hapa hapa.

Lakini kwa wazo kama hilo wangekuwa wanawakopesha watu hata kwa liba ndogo tu hata iwe 3% ya kuilinda tu ile hela. Hongera sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
serikali haiwezi kukubali mo na bakhresa waingilie sekta ya benki na kuvuruga uchumi kwa kukopesha kwa riba ndogo.....kumbuka wanaopanga viwango vya riba ni bot kwa niaba ya serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuuza Karanga za Kukaanga na Sigara

Mahitaji :

Jiko la mkaa : 3500
sufuria : 5000
pakti : 5000
Mkaa : 1000
Ungo : 2000
Ports : 3400
Embassy : 4300
SM : 3400
Karanga 1kg : 5000

JUMLA : 32,600 (katika 50,000 nitabaki na 17,400 kilinda mfuko)

Karanga nitafunga size 3 tofauti,za 200 za 300 na 500,nitauza mchanganyiko mbichi na za kukaanga mteja atachagua yeye anataka pakti gani.

Hii biashara nina uwezo wa income ya faida above 5000 per day x 30 = 150,000,hapo ni karanga tu,sijapiga hesabu ya sigara. Hiyo 50,000 yako nina uhakika ndani ya mwezi itakua imerudi mkuu.
Katanga kilo 5000 hautoboi kwa upande wa Arusha cz hamna faida yeyote nauzoefuu labda mteja umuzie punje 5 mia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karanga kilo inatoa vijiko 65 vya 100 kama unatembeza hapo unatafta 1500 kama unafunga unatafta 500 kama unauza jumla unatafta -1500
Kuuza Karanga za Kukaanga na Sigara

Mahitaji :

Jiko la mkaa : 3500
sufuria : 5000
pakti : 5000
Mkaa : 1000
Ungo : 2000
Ports : 3400
Embassy : 4300
SM : 3400
Karanga 1kg : 5000

JUMLA : 32,600 (katika 50,000 nitabaki na 17,400 kilinda mfuko)

Karanga nitafunga size 3 tofauti,za 200 za 300 na 500,nitauza mchanganyiko mbichi na za kukaanga mteja atachagua yeye anataka pakti gani.

Hii biashara nina uwezo wa income ya faida above 5000 per day x 30 = 150,000,hapo ni karanga tu,sijapiga hesabu ya sigara. Hiyo 50,000 yako nina uhakika ndani ya mwezi itakua imerudi mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katanga kilo 5000 hautoboi kwa upande wa Arusha cz hamna faida yeyote nauzoefuu labda mteja umuzie punje 5 mia

Sent using Jamii Forums mobile app
Biashara iliyokushinda wewe, haiwezi kuwa ndio msimamo wa LIGI

Biashara haifanywi kwasababu flani imemfanikisha au mtajirisha

na wala biashara haiachwi kufanywa kwasababu flani ilimfilisi

Halafu (mimi) nafanyaga Biashara NGUMU KUMEZA ambazo

watu kama wewe hamuwezi kuona faida ninayopata,zile biashara ukiiona "unabinua mdomo"
 
Back
Top Bottom