Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Wazo hilo hapo nimequito hapo mkuu
Naomba uniwekee wazo lake mkuu,niweze kulipitia..Maana uzi ndo nmeusoma leo..nmepitia juu juu saana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hes
Kwa heshima kubwa nikushauri ubadili ID name sasa.
 
Liko vyema mzee.Lakini umesema hilo ndo lilikuwezesha kupata mtaji wa chips..je unaeza elezea hiyo 50k nikikupatia utaiongezea kwenye chips? Maana sitegemei kama utaanza na mishikaki tena.
Mkuu kwa sasa nafikiria kupata fedha kiasi kadhaa niboreshe hilo wazo,

Kwanza nataka niuze mishikaki vizuri siyo local tena kama mwanzo,
Nataka nitafute sehemu nzuri niweke meza flani hivi nilishadizine,
Then kwa juu naweka katent flani hivi na bango kubwaa,

Hapo itakuwa ni mishikaki ya Nundu plus Nyama ,
Then pembeni kutakuwa na ndizi za kuchoma pamoja na kukaanga ,chachandu flani hivi ya kuvutia,

Mavazi ,nitakuwa na mavazi flani special Tshirt ya kuprint yenye logal mbele na maandishi Nyuma,chini laba flani hivi na jinsi Nyeusi ya kuchomekea(lengo kuwa Nadhifu muda wote wa kazi)

Nje ya meza kutakuwa na Viti vya kudizine vitakavyowezesha kukaa watu nane tu (kila upande watu wanne,)

Yaani nataka niifanye kiaina flani hivi ambayo ata wewe mwenye Suti yako usione Aibu kushuka kwenye gari yako kuja kununua mishikaki ,

hapo kwa haraka haraka mchanganuo wangu mpaka sasa ulikuwa hivi.

Hiyo meza niliyodizine nilishaongea na fundi inacost kama 300k (ni ya chuma alafu itakuwa na umbo kama L )

Carpet yake ya kutandika meza (vile ninavyotaka mimi)35.

Majiko mawili 80k (kubwa 45k, dogo la karahi 35k)

Karahi 1. 9k

Meza na viti vile navyotaka kudizine vitanicost 150k,


Chuma nne za kusimama 120k (kila moja 30k)
Za juu 40k ,turubahi la kuweka 30k (hapo tent ) fundi sijajua bado

So hapo kwa haraka haraka 800k - 900k inatosha Biashara itakuwa kama vile ninavyotaka mimi,

Nilishaweka kiasi kadhaa na bado nazidi kuweka Akiba, wazo langu halina haraka sana nategemea kuanza ikifika mwezi wa Sita hivi ,

Eneo ninalotegemea kuweka ni mapito ya watu wa aina tofauti

Biashara yenyewe.
Nitakapoanza biashara nategemea kuanza kwa bei ya kawaida tu ,
Kila mshikaki utauzwa shilingi 500,
Ndizi ya kuchoma shilingi 500,
Na ndizi ya kukaanga shilingi 400,

Pembeni ya jiko kutakuwa na mishikaki pia midogo ya shilingi mia 2, mia 2 kwa ajiri ya wanafunzi na watoto.

Ongezeko la bidhaa itaongezeka kulingana na ongezeko la wateja watakaokuwa wanakuja mfano.

Naweza kuweka mihogo,maziwa fresh kwa Jioni, maini na firigisi za kuku Nk.

ila tu sitaweka chipsi nataka nidili na hivyo Vitu tu na nitasimamia mwenyewe.

Nb.
Kwenye banda langu la kiepe kama kawa watu wapo wa kufanya kazi mimi binafsi nataka nigeukie huko kwanza


Cc Zero IQ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisoma hii post kwa mara ya kwanza extensively, naomba radhi kwanza kwa kutokupa unachostahili!!

Hakika unatakiwa kupongezwa mno tena mno kwa ubunifu huu, yaaani nimesoma kwa kina nikagundua kitu kikubwa sana katika nafsi yako, baadhi ya nilichobaini kwako kupitia hili andiko ni

#1 unamoyo wa kusaidia pasipo kujali kipato chako, umeonyesha nia yako ya kusaidia pasipo kujali uwezo wako

#2 una nia ya kusaidia wajasiriamali, hapa ndo uliponigusa yaaani hujataka mbwembwe bali umehitaji mjasiliamali mwenye kuonyesha ubunifu wake, kupitia hli wazo watu wengi na wasio wajasiriamali wamejaribu kuja na wazo ikiwa na lengo la kutwaa mkwanja kwa kufanya hivyo wamejikuta wamekuja na wazo akilini mwao ambapo umewapa mtihani mwingine ili waendelee kuchekecha AKILI hongera sana!

Hakika jamii ingekuwa hivi au watu wa namna yako tungekuwa mbali mno, unfeigned I eulogize this idea, Bravo! Am so proud of this speaking not in a clandestine situation, thanks and be blessed na MWENYEZI Mungu akubariki na kukuongezea kipato chako ndg!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
zero iq once again umetisha kinyama

cc October man njoo huku mkuu
 
Amina.
Asante sana kwa kunitia moyo, tarehe kumi na saba March nitauanzisha mchakato tena
 
Naomba na mimi lisinipite hili . .
Mimi idea yangu kuuza sambusa na kacholi mashuleni (msingi na secondari ) na mtaani.
Gharama .
kalai lipo tayari
Deli lipo tayari
Viazi 2@5k
Ngano 2@1300
mafuta 2@2000
Nyanya kwa siku , pilipili, chumvi rangi ya kacholi (2000) =2000+ 5000= 7k
Jumla ni 24k
Sales
sambusa 100@100 =10k
kacholi 100@100=10k
Mauzo Jumla 20k kwa siku
20×siku 6 = 120k
120k-22k=98k

Haha kama hauna Deli na Kalai (au ukaazima )bado kuna uwekan0 ukatengeneza pesa ya kutosha said ya 50 kwa wiki .
Hili ni wazo ninalo liishi
Asante
 
Naomba na mimi lisinipite hili . .
Mimi idea yangu kuuza sambusa na kacholi mashuleni (msingi na secondari ) na mtaani.
Gharama .
kalai lipo tayari
Deli lipo tayari
Viazi 2@5k
Ngano 2@1300
mafuta 2@2000
Nyanya kwa siku , pilipili, chumvi rangi ya kacholi (2000) =2000+ 5000= 7k
Jumla ni 24k
Sales
sambusa 100@100 =10k
kacholi 100@100=10k
Mauzo Jumla 20k kwa siku
20×siku 6 = 120k
120k-22k=98k

Haha kama hauna Deli na Kalai (au ukaazima )bado kuna uwekan0 ukatengeneza pesa ya kutosha said ya 50 kwa wiki .
Hili ni wazo ninalo liishi
Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…