MREJESHO
Wakuu habari ya leo,
Tumshukuru mungu kwa wale tulio na afya njema, na kwa wale wenzetu wenye shida mbalimbali basi mungu awafanyie wepesi.
Kama nilivyoanza na kichwa cha habari hapo juu nimeleta mrejesho wangu wa kinyang'anyiro hiki kilichokuwa kinaendelea kwa siku kadhaa hapa jukwaani, na wengi wetu kutoa mawazo yetu mbalimbali.
Mleta mada jana usiku wa saa sita aliahidi kumleta mshindi wa hili shindano,ambalo miongoni mwa orodha ile nami nilikuwepo na kuibuka na ushindi mnamo saa sita na dakika mbili usiku.
Akanifuata pm tukawasiliana usiku ule na akaahidi leo akishatoka ibadani, basi atakamilisha lile dhumuni lake. Na ilipofika saa 11:42am alinitumia hiyo pesa ikiwa kamili na ya kutolea.
Shukrani zangu za dhati ni kwa mwenyezi mungu kwanza,halafu wale wote tulioshiriki kutoa mawazo yetu hapa, sababu yatanufaisha watu wengi.
Bwana
Bonde la Baraka mungu akuzidishie baraka zaidi kama unavyojiita, kwani umekuwa faraja kubwa sana kwetu,na naomba na wengine wenye uwezo mjitokeze zaidi ili kuweza kusogeza gurudumu hili la maendeleo hasa kwetu vijana.
Mungu awabariki sana.
NB:Si mwandishi mzuri kwa hiyo tuvumiliane kwa hili.
View attachment 1367006
Sent using
Jamii Forums mobile app