Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Bonde la Baraka,
naona unataka kupata wazo la biashara ili ijumaa ukakope 50 vicoba
Acheni kuwa na mawazo negative kwa kila kitu; Hivi ukitaka kumsaidia mtu usiyemfaham utatuaje kuwa yupo tayari ?
Lakini pia; wazo moja linaweza kufanyika sehemu tofauti tofauti Dar, Arusha, Tabora nk
Kwani watu wengine wakipata wazo hapa wakafanya mikoani kwao kuna shida gani? ndio maana halisi ya mtandao wa jamii/kusaidiana
Binafsi, mtoa mada hata akiweza kusaidia mtu mmoja tu ila amefungua watu akili kuwa kusaidia mtu sio lazima uwe Tajiri; Watu wengine wanahitaji mtaji wa kianzio tu 50,000 - 100,000shs wajiendeleze wenyewe
 
Huwa unanifurahisha lakini hapa umenifurahisha zaidi

I like you
Hiyo elfu 50 mchanganuo, wake kwa biashara ya mishikaki.

Naenda kwa Fundi kuchomelea aniandalie Jiko elfu 25,

Natafuta kijiwe kizuri sehemu wanayopita watu wengi,

--Sokoni nyama kg 2 steki tupu =16000,
--mkaa wa 1500
-Viungo vyake 5000(hiyo siyo vya siku moja ukinunua ni vingi mpaka viishe vitakaa kaa kidogo. )
-vijiti vile vistiki vyake 2000.

Naandaa mishikaki yangu ya wastani tu ya kuuza mia 2 mia 2 tu,

Kwenye kg 2 nina uhakika wa kupata faida ya 10K kila siku hapo baada ya kutoa matumizi ya mkaa, vijiti na Nyama.

Ndani ya wiki tayari nimekurudishia 50k yako.

NB:
Nilishawahi kufanya hii kazi hivyo nina uhakika nayo. Ndio kazi iliyonipa mtaji wa kibanda cha kuchakata viazi kuwa Chips.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Good
Habari Mkuu

Mimi nitaitumia 50000/= katika mchanganuo ufuatao kupitia biashara ya mahindi ya kuchoma

Naishi temeke stereo jirani na soko hapo wanauza mahindi mabichi nami ndiyo biashara niliyowah kuifanya Tandika sokoni

Mchanganuo
Mahindi 50@300= 15000
Usafiri = 500
Mkaa. = 1500
Chumvi. = 300
Ndimu. = 300
Ushuru. = 500
Pilipili. = 300

JUMLA. 18900

MAUZO

Nitauza mhindi 1 kwa shilingi 800 hiyo kwa mahindi 50 kwa siku n shilingi ( 50×800= 40000)

jiko ninalo hivyo sihitaji kununua

JUMLA YA MAUZO - JUMLA YA MCHANGANUO.

40000 - 18900= 21100

kwa hyo ninauhakika wa kurudi na elfu 21100 kila siku kumbuka situmii nauli kurudi nyumbani

Ninauwezo wa kuuza mahindi 50 kwa sababu Tandika n sehemu ambayo inawatu wengi ni soko kubwa hvyo mwingiliano wa watu ni Mkubwa

Baada ya siku 7 ninauwezo wa kuwa na shilingi 147700

Pia kumbuka katika elfu 50 ya mtaji baada ya matumizi ya siku ya kwanza ilibaki (50000-18900= 31100) itabaki shilingi 31100 nitaitumia kuongeza mtaji taratibu kwa siku zinazofuata maana biashara sio siku zote huwa nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awakopeshe mitaji ili badae waje wampiku??
Hongera mkuu. Huo ndio ubinadamu. Ingekuwa wale wenye mitaji mikubwa wangewafanyia hivi wengine Tanzania ingebadirika haraka sana. Huwa najiuliza sana mtu kama mo au bakhresa kwa nini asikopeshe wenye kutaka biashara lakini hawana mitaji?.

Kuliko kufadhiri litimu kama simba wanakula hela tu tena nyiiingi sana ukipiga hesabu kwa mwaka. Lakini hakuna faida yoyote wala muendelezo wa hizo timu,zote zinashindana kushindana zenyewe tu na kuishia hapa hapa.

Lakini kwa wazo kama hilo wangekuwa wanawakopesha watu hata kwa liba ndogo tu hata iwe 3% ya kuilinda tu ile hela. Hongera sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengine tujitolee kuwawezesha hao washindi walio bakia wakuu.Nipo tayari kumuwezesha mmoja wapo.

Unajitangaza una hela wewe sio bure!...unajifanya una hela eh😄..unajitangaza kusaidia eh😄...kidding!
 
I salute you
Biashara iliyokushinda wewe, haiwezi kuwa ndio msimamo wa LIGI

Biashara haifanywi kwasababu flani imemfanikisha au mtajirisha

na wala biashara haiachwi kufanywa kwasababu flani ilimfilisi

Halafu (mimi) nafanyaga Biashara NGUMU KUMEZA ambazo

watu kama wewe hamuwezi kuona faida ninayopata,zile biashara ukiiona "unabinua mdomo"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom