Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Kuna sehemu wale wakaanga ndizi kwenye mabanda ya chips huwa wanapata tabu kuzipata zile ndizi ndefu kubwa(mzuzu),,, sasa Kuna mahala zile zinapatikana kwa wingi, na huko zinanunuliwa sh 50 kila moja mara usafiri na vingine zinafika sokoni kwa sh 80 mpaka 90 kwa kila moja, na huwa zinachukuliwa kwa bei ya jumla 200 mpaka 250 kila moja.... Kwahiyo mtu hapo anaweza kutengeneza hiyo elfu 50 sio mwezi Bali tuchukulie wiki mbili tu maximum

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapi huko mdada?
 
Vumbi la Kongo!
Wanaume Wengi wana matatizo ya nguvu za kiume na wanahitaj sana huduma hiyo. Kwahyo hii ni biashara inayolipa sana mtu ukiifanya serious.

Mimi ni mwanaume wa mkoani na nimefanya tafiti nikagundua uhitaji ni mkubwa sana na hakuna supplier wa huku huku.

Sasa basi,

Kwa hiyo 50k nitaagiza mzigo kutoka Dar kwa bei ya jumla ambapo sasa kichupa kimoja nitanunua sh. 5000.

Chupa 10x5000=50k

Then nitatumiwa parcel kwa basi la shabiby na gharama yake ni 5000 (hii nitatoa mfukoni).

Hapo sasa nitaanza kusupply kwa wateja ambao nitakuwa nawauzia kwa 15k kwa chupa moja. Net profit hapo ni 10k.

Nikimaliza chupa Zote 10 nitakuwa na 150k huku net profit Ikiwa 100k.

Nitawapataje wateja sasa?
Mitandaoni!

Tayari Nina akaunti Instagram na Facebook na twita ambapo natangaza hii biashara ingawa bado sijaanza kuuza kutokana na changamoto ya mtaji.

Response ya wateja ni kubwa mno. Kwa siku wananitafuta watu sio Chini ya 10.

Naombeni mtaji ndugu zangu nijikomboe
Mkuu mkoa gani huo wananunua hiyo kwa bei hiyo?
 
Mkuu, Mimi hapa ukinipatia Mtaji wa TZS 50,000 nitairejesha baada ya Miezi mitatu na nitaiwekeza katika huduma/biashara ya hii hapa chini:
  1. Nitaanzisha taasisi ambayo italenga kutoa huduma kwa wenye nyumba na wapangaji ambayo sio real estate agent bali ni zaidi kwa ajili ya kuwasaidia wapangaji kufahamu ubora wa nyumba kwa kuzifanyia nyumba grading,mitaa grading kwa kutumia vigezo vya kitaalam.Na nitaanza kwa kutoa huduma hio kwa jiji la Dar es Salaa kwanza.Gharama ya huduma hio itakuwa ni nafuu ambapo mwenye nyumba atalipia kisha Mpangaji akitaka kufahamu iwapo nyumba au eneo husika limefanyiwa utafiti atapatiwa ripoti ya eneo husika.
  2. Ripoti hizo zitakuwa za kiswahili na zitaonesha,wastani wa gharama za maisha,ikiwamo kodi chakula,maji umeme.Uwepo wa huduma za elimu afya na burudani,vituo vya polisi,mawasiliano ya viongozi wa eneo husika,usalama na uhalifu.Fursa za ajira zilizopa maeneo ya karibu.Fursa za biashara zilizopo maeneo hayo.
  3. Vilevile mpangaji anaweza kuomba kufanyiwa utafiti huo kabla ya kuhamia eneo fulani.
  4. Kwa kupitia taarifa hio tunaweza kupima na kutoa taarifa juu ya maeneo mazuri kabisa kuishi na maeneo mabaya kabisa kuishi na pia taarifa yetu itakusaidia kufahamu fursa na changamoto za kila eneo bila kujali umbali wa eneo.
Kwa shilingi elfu 50 utakayonipatia nitawekeza TZS 25000 kwenye kusajili jina la biashara brela na TZS 25000 kwenye kusajili domain name ambamo taarifa hzio zitawekwa.Mimi binafsi nitachangia gharama za kufanya hosting pamoja na gharama za kupata leseni ya biashara,gharama za nauli na uendeshaji kwa kipindi cha mwanzo.Iwapo utapenda kuwekeza zaidi katika biashara hii ili tuweze kuwa wabia tunaweza kujadili zaidi kwani wazo hili linahitaji mtaji wa TZS milioni 75 na lina potential ya kuleta mapato ya hadi milioni 150 kupitia huduma,matangazo commision n.k.

NB.Unaweza kutekeleza wazo hili ila hakikisha unawasiliana na mimi kwanza

Gharama utakazoziongeza mwenyewe ni nyingi kuliko hiyo 50
 
Kuna sehemu wale wakaanga ndizi kwenye mabanda ya chips huwa wanapata tabu kuzipata zile ndizi ndefu kubwa(mzuzu),,, sasa Kuna mahala zile zinapatikana kwa wingi, na huko zinanunuliwa sh 50 kila moja mara usafiri na vingine zinafika sokoni kwa sh 80 mpaka 90 kwa kila moja, na huwa zinachukuliwa kwa bei ya jumla 200 mpaka 250 kila moja.... Kwahiyo mtu hapo anaweza kutengeneza hiyo elfu 50 sio mwezi Bali tuchukulie wiki mbili tu maximum

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni wapi huko mkuu,, naomba kuelekezwa kama hautojali
 
Ni wapi huko mkuu,, naomba kuelekezwa kama hautojali
Simjibii.
Ila Ifakara huko ndani ndani esp Mbingu mikungu Bei kama bure .2000-4000!Kuna dogo aliniomba June hii nimtaftie soko sijatulia sijamtafutia. Ana mashamba mikungu haina pa kwenda!
 
Tunasubiri Mrejesho Wakuu na sisi tutangaze nia ya kuazimwa.. 🤗

Tuko nje ya muda, Dirisha lilipaswa kuwa limeshafunguliwa..

Mkuu Bonde la Baraka umesitisha mpango wa kuzungusha mtaji?

Ilikua platform nzuri Sana...nataman atokee mtu a-base kwenye gender ya kike walah! Kumkomboa mtoto wa kike🤭!sema ndo hivyo wabongo hatuna userious huoo!
 
Ilikua platform nzuri Sana...nataman atokee mtu a-base kwenye gender ya kike walah! Kumkomboa mtoto wa kike🤭!sema ndo hivyo wabongo hatuna userious huoo!
Mange hemu anzisha yako hata ya 30,000 Tzs tu tupaje hata mada ya kuchangia changia angalau...anzisha watu watililike.

Nyuzi zimekuwa chache.
 
Mange hemu anzisha yako hata ya 30,000 Tzs tu tupaje hata mada ya kuchangia changia angalau...anzisha watu watililike.
Sina kipaji boss wangu... anzisha tu wewe... Bora iwe 500k!
Ila kwa jicho ambalo sio la kinafki wabongo wengi hatupo serious...!
Tuna ideas kibaooo...kuziimpliment Sasa🤸!
 
Sina kipaji boss wangu... anzisha tu wewe... Bora iwe 500k!
Ila kwa jicho ambalo sio la kinafki wabongo wengi hatupo serious...!
Tuna ideas kibaooo...kuziimpliment Sasa🤸!

Hee kipaji gani tena.

Haha uanzishe ya 500K sikutachafuka humu kama kule Twitter alivyochafua watu MO.
 
Hee kipaji gani tena.

Haha uanzishe ya 500K sikutachafuka humu kama kule Twitter alivyochafua watu MO.
Means mtu apewe laki 5 then atakuwa anafatiliwa anaendeleaje na biashara zake ..!asirudishe na riba...! Mo kafanyaje tena
 
Back
Top Bottom