Uthubutu: Kiwanda cha JF members

Uthubutu: Kiwanda cha JF members

thomas300

Member
Joined
Jan 11, 2015
Posts
9
Reaction score
12
Katika jukwaa hili nimeona na kujifunza mengi..kitu ambacho naona na ambacho kipi kwa wengi sio hapa JF tu ni uthubutu. Nchi zilizoendelea zimefika huko kwa watu wao kuwa na uthubutu, uthubutu wa kufanya kitu tofauti ambacho anaamini kitamtoa lakini hajiamini. Vijana wengi wanaamini bila hela hawawezi kutoka. Ukweli ni huu, MTAJI PEKEE NI AKILI NA UBUNIFU WAKO. Hela ni matokeo ya ubunifu wako.

Baada ya kusema hayo nakuja na wazo ambalo naamini litasaidia kwa namna moja au nyingine kututoa hapa kwenda mbele ambapo wengine hawathubutu.

Uanzishwaji na umiliki wa manufacturing company/industry. Kutakuwa na shares zitakazomilikiwa na members wa jukwaa hili na inakuwa vizuri iwe kwa wale ambao hawako kwenye masomo, uwe umeajiriwa/jiajiri au huna kazi hii ni nafasi kwako.

Nafasi ya members hawa watakuwa si zaidi ya 45 na watamiliki 49% au 51% ya kampuni hii. Kwa kuwa wote hapa uwezo wetu kwa mradi kama huu ni mdogo kifedha na kirasimali, wazo hili baada ya kuundwa vizuri tutaliuza kwa government au private institution au individual mmoja au zaidi ya mmoja. Hawa watamiliki asilimia zitakazobaki japokuwa sisi tutakuwa na uwezo wa kuzinunua shares zao pale inapoitajika (buy back option).

Sisi members tuwe watanzania wanaoishi sehemu yoyote ndani au nje ya nchi. Wazo hili nimeona ni jambo linalowezekana pale panapokuwa na utayari na maelewano. Tanzania inaagiza vitu vingi toka nje wakati mali ghafi zinatoka hapa. Wale ambao wanakubaliana na hili na wapo teyari wani PM na namba zao tuungane kwenye whatsup group kuweza kuliongezea uhai wazo hili na namna ya kusonga mbele.

Criticks zinakubalika kwani zinatujenga.
 
Wazo zuri sana, naunga mkono hoja!! Kwa kuanza tuanze na kamati tendaji itakayokuwa ikiratibu hili suala!!
 
Tupo pamoja na wazo lako ni bora zaidi boss wetu,tuwasiliane hapa /inbox pia tena tuwe serious wakuu..tena udhubutu unahitajika zaidi hapa JF..
 
Wazo zuri, but fafanua zaidi vision, mission, objectives na goals kwa ufupi ili watu wasipime kina cha maji kwa miguu yote miwili.
 
Mkuu naona kwa stage hii ya kwanza tujadiliane haap5 wote kwa pamoja ili wataokuja kwenye group wawe na uelewa na maudhui ya kusudio zima la group
 
Wi_Fi na Everlenk jambo hili vision na the way foward haliwezi amuliwa na kupangwa na mtu mmoja, hao 45 ndio watakaopanga yote ili kuanzia siku ya kwanza inaitajika wote tuwe kwenye page moja..nimesema 45 kwakuwa limited company mwisho 50,jambo ambalo members wakitaka zaidi litafanyika
 
Sio mbaya kujadiliana hapa hapa na pale mtu anaeona ameridhika anachukua maamuzi ya kujiunga.
 
Hili jambo ni zuri sana, wenzetu kenya wanajua kutumia instituations vizuri katika kuuza mawazo yao, nitakuPM namba yangu
 
Tunapaswa kutambuana pia tupo waandaaji wa memorandum&legal document zinginezo pia kuwa shareholder&director sio kuuza sura bali ni utambuzi wa majukumu kiujumla zaidi...KARIBUNI WADAU WOTE.
 
Ni wazo zuri sana ila ktka social netwwork hizi nchi za wenzetu wengi wao wametapeliwa sana kupitia lugha za hapa
hofu yangu ni kwamba je pindi ikitokea tatizo hilo itakuwaje? au hatua gani zitachukuliwa kwani hata hapa kuna mtu anatapeli sana anakwambia anauza viwanja/nyumba halafu ukikontact naye anakulia kona kiaina hvyo mtoa mada inatakiwa iwe makini kwa upande wa kuwapata viongozi ambao wataendesha mchakato huu


kingine kinachotakiwa ni ni kuhusu ambao watakuwa watendaji wakuu ambao wataendesha gurudumu hili watatakiwa wawe wametoka mkoa, nchi moja au inakuwaje kwa hili?

Mtoa mada nimependa sana hii kitu na imenifanya nifurahie ila naomba unijibu hayo maswali yangu hapo juu pls.
 
Kuna wengi wana wasiwasi na utapeli..ila jambo la kutilia maanani ni kwamba members ndio tutakaokuwa na jukumu la kuzuia hili,kila mmoja atapewa jukumu. Haya yote yatatekelezwa baada ya kufahamiana na kukutana..hili jambo ni kubwa kukulikeleza kwa kutumia mitandao
 
Wazo zuri sana.Tatizo la watanzania wengi ni matapeli/wadanganyifu katika 45 sijui kama patakosekana angalau watatu watakaofikiria kunufaika kwa haraka kupitia wenzao thru utapeli/udanganyifu hii ni shida kubwa sana hapa Tanzania.
 
Wazo zuri sana.Tatizo la watanzania wengi ni matapeli/wadanganyifu katika 45 sijui kama patakosekana angalau watatu watakaofikiria kunufaika kwa haraka kupitia wenzao thru utapeli/udanganyifu hii ni shida kubwa sana hapa Tanzania.

Ni jukumu letu 45 kuhakikisha hakuna linalotokea kwa kuja na mbinu za kuzuia hilo lisitokee..kukiwa na nia ya kweli hakuna baya la kutokea
 
Back
Top Bottom