Utiaji saini Mikataba ya Miradi ya maji katika Miji 28, Kama Nchi tuna safari ndefu

Utiaji saini Mikataba ya Miradi ya maji katika Miji 28, Kama Nchi tuna safari ndefu

Econometrician

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2013
Posts
16,879
Reaction score
31,253
Nimeangalia wakandarasi waliopata zabuni za miradi ya maji, kwa kweli binafsi yangu sijamuona Mtanzania ngozi nyeusi aliye pata zabuni. Wote niliowaona mie, ni ngozi nyeupe (mabeberu), sasa nacho jiuliza ngozi nyeusi sisi tatizo ni nini?

Sote tunafahamu njia kuu ya Serikali kuongeza fedha kwenye mzunguko na kuzalisha ajira ni kupitia miradi kama hii-sasa Miradi yote wanapopata Wakandarasi Mabeberu-sijui kama Taifa tunaelekea wapi huku tuna engineers wengi wana graduates, tuna Wakandarasi wazawa wengi.tunachofanya ni kuhamisha pesa kwenda katika Nchi za hao Wakandarasi na kuongeza ajira zao.
 
Nitarudi kuchangia nikithibisha usemalo ni kweli.
 
Wote niliowaona mie,ni ngozi nyeupe (mabeberu),sasa nacho jiuliza ngozi nyeusi sisi tatizo ni nini??.

Bado tuna safari ndefu
  1. Upigaji mwingi kazi hakuna
  2. Siasa nyingi hata kwenye mambo yasiyo ya siasa
  3. Utaalamu hafifu umakini hakuna
  4. Maono ya mbali hakuna tunatazama kesho ya familia zetu tu
Jifunze toka mambo yanayoendelea bungeni kipindi hiki
 
Wakati mwingine Wabongo tunajiaribia wenyewe utakuta mkandarasi anakula hela na mradi unaenda mwendo wa kinyonga matokeo yake muda unakwisha na hela hana ya kumalizia mradi.
 
Wakati mwingine Wabongo tunajiaribia wenyewe utakuta mkandarasi anakula hela na mradi unaenda mwendo wa kinyonga matokeo yake muda unakwisha na hela hana ya kumalizia mradi.
Kwahiyo suluisho ni kuwapa wageni?
 
Wakandarasi wengi wa ndani mmefeli sana katika ubora, kudhibiti variations za vifaa vya bei na kumaliza kazi kwa wakati. Mifano iko kibao, hata barabara fupi fupi nyingi zilizojengwa na wakandarasi
wa ndani, hata bajaji au bodaboda zinabomoa baada ya mwaka au miaka 2.
 
Wabongo kuna muda mwingine akili zetu huwa hazimo,

Nimewahi Kufanya KAZI kampuni moja ya mtanzania alipata mradi mkubwa WA maji, kabla hata KAZI haijaanza akaanza kujenga nyumba zake Binafsi. Sitasahu Ile KAZI ikivyokuwa ngumu Kwa upungufu WA hela site.
 
fedha zenyewe tunaomba kutoka kwao usikute kwenye mukataba kuna kipengele cha kuwapa kipaumbele Contractors kutoka nchi wahisani
 
Wabongo tunajuana wenyewe jinsi tulivyo na makando kando
 
Back
Top Bottom