Utii wa wanawake wa kisasa

Zemanda

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
8,323
Reaction score
18,051
Kutokana na malezi ya kisasa na mifumo ya kisasa ya maisha ile kanuni ya mtii mwanaume wako kwa wanawake wa kisasa ni kitu ambacho hawakielewi kabisa wala kujua maana yake wakiwa katika umri wa usichana au umri wa kuchumbiwa na kuolewa.

Ila asili au nature ilivyo na power katika kufundisha kanuni zake za asili bila kupangiwa au kubembeleza mtu utashangaa sana binti akisha chezewa sana mwili wake akafikia ule umri wa utu uzima yaani 30,then mwili unaanza kupungua mvuto, anaanza kuwa na muonekano wa kimama, automatically utashangaa anaanza kuwa na adabu na yale mawenge, machepele, viburi, dharau ghafla hupotea anaanza kuwa na mwenendo wa utaratibu na anatengeneza haiba ya kukua kiakili.

Huwa najiuliza why huwa mnakwepa kitu ambacho mtakuja kukifanya siku za baadae tena kwa lazima?

Hapa tunaongea swala la utii na adabu kwa mwanaume ila mabinti kama akina Jadda watakaza fuvu kabisa na majibu ya kejeli ila subiri umri ufike. Kama kuna kamera za kuwamulika hamtaamini kuwa ndio wataufyata kuliko wale ambao ndio watii kwasasa.

Usiponyooka utanyooshwa, maisha hayajawahi na wala hatakuja kuwahi kubembeleza mtu, utakwenda vile yanavyotaka. Kanuni ya kutii mume na mke kupendwa ni ya miaka ya enzi na enzi. Wewe mtoto wa 1990's uje kuleta kanuni zako na kuamulia jamii iende kwa fikra zako utajua haujui, mtego utakapokufyatukia ndipo utaelewa maisha ni kama upepo, yapo ila hayashikiki.
 
Well said mkuu.
Me wanachonishangaza ni kitu kimoja, Kuwa na tabia njema ni sifa ya kuonyesha umelelewa vyema. Its like unawapa maua yao wazazi/walezi wako indirectly. Ila mabinti at their 20's wanashindana kuonekana hawana tabia nzuri kwa jamii as if ni jambo jema, which is very weird.
Ukikuta na hawa single mama at their late 30's nao wamevamia hoja za feminist bila kuchambua kwa ufasaha ndo utazidi kuchoka.
 
Acheni hizi porojo zenu msingi wa mwanamke kumtii mwanaume uko katika mwanaume kumhudumia mwanamke huwezi kukitawala kiumbe usichokihudumia, kinachofanya wanawake wengi wa dunia ya leo kutokuwatii wanaume wao ni kile kitendo cha wao nao kuanza kujitafutia pesa na mali zao bila kuwategemea wanaume, hata mimi huwa nasema humu kama mwanaume anamhudumia mwanamke basi shurti huyo mwanamke amtii hiyo siyo hiyari bali lazima, ila kama mwanaume hawajibiki kwa lolote kwa mwanamke wake halafu anataka utii basi mtaendelea kulalamika na kutukana hadi mwisho wa dahari, huku mkisubiri mwanamke awe 'reject' ndio awe na utii
 
Kama kuwa na tabia njema ni kuwapa maua wazazi au walezi wako, kwanini wanaume msiwe na hizo tabia njema, au ninyi hamtaki wazazi au walezi wenu wapate hayo maua
 
Uyo uliemtag sasa akija mtakesha hapa.
 
Huyo Jadda uliyemtaja nadhani ndo mwanamke jeuri JF nzima, ngoja nature ifanye kazi yake kisawasawa.
 
Kuna baadhi wanahudumiwa ila ni majeuri
 
Huyo Jadda uliyemtaja nadhani ndo mwanamke jeuri JF nzima, ngoja nature ifanye kazi yake kisawasawa.
Nature my foot ninyi endeleeni kujifariji na huo ujinga wenu mnaouita nature mkidhani eti wanawake watakuja kujirudi na kuwa kama bibi zetu, kadiri miaka inavyozidi kuenda ndivyo wanawake wanavyozidi kuujua uhalisia na kuachana na uwongo wa hizi kauli zenu, jiandaeni kisaikolojia tu maana alama za nyakati zinaonesha yajayo yatawavuruga zaidi mpaka muwe vichaa hapa mbona hamjaona kitu bado
Kuna baadhi wanahudumiwa ila ni majeuri
Basi ndio mdeal na hao na siyo wanawake wote, wanawake msiowahudumia waacheni kama walivyo, na pia siyo kila mwanaume anastahili kupewa utii kaa ukijua hilo
 
Utiiiai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…