Utii wa wanawake wa kisasa

Tatizo lako unalazimisha kila swali liwe na jibu la moja kwa moja (kama vile ndio au hapana) na mtu akikujibu tofauti na ulivyotarajia unaanza kusema ametoka nje ya mada, sasa hiyo siyo namna ya kujadili hoja bwamdogo usilazimishe watu wakujibu kile unachotaka kusikia wewe, kwa mfano hilo swali lako hapo halina jibu la moja kwa moja kwa sababu siku hizi kuna aina nyingi za mahusiano kwahiyo inategemea hao watu wapo kwenye mahusiano ya aina gani
 
Maelewano baina ya pande mbili , (kila mtu atambue nafasi yake)
Sasa maelewano yapi ikiwa mmoja anatakiwa kufuata na kutii tu amri za mwenzake, hapo kwenye kila mtu kutambua nafasi yake ndipo kwenye utata hapo, kwa sababu kuna mmoja hapo analazimishwa kutambua nafasi ambayo hajajipangia yeye na ni kinyume na utashi wake
 
Sawa basi ngoja nielezee izo aina ili unijibu. Aina ya kwanza wapenzi mnaishi sehemu tofauti yaani boyfriend and girlfriend na aina ya pili mnaishi pamoja kama mume na mke halafu mwanamke ana ajira inayomuingizia kipato. Je mwanaume atatakiwa kumuhudumia mwanamke?
 
Nafasi ya mwanamke inajulikana na wajibu wa mwanaume unajulikana kila mmoja akisimama kwenye nafasi yake ndoa ni amani.
Hakuna gari iendeshwayo na madereva wawili
 
Kwanza kabisa hujanitajia aina zote za mahusiano inaonesha hata huzijui hizo aina zenyewe, pili bado swali lako halina hilo jibu la moja kwa moja unalotaka kulisikia, mwisho hata kwa hizo aina ulizonitajia inategemea wenza mmekubalianaje kuhusu namna ya kuendesha hayo mahusiano yenu
 
Sidhani kama tumeshindwa na hainipunguzii kitu. ila ni vile tu wanawake siku hizi ham act like real women. Mna mentality ya kuona kama mnalingana na wanaume in terms of everything ambako hakutawahi kutokea milele wewe unaweza kuhisi ni sawa because system na sheria zinawabeba ila trust me kuna mda utakuja kulielewa hili, sisi sio kwamba tunataka mtunyenyekee kama mnavyodhani ila ni ile feminine quality ambayo wanawake wengi wameipoteza kwasababu ya utandawazi.
 
Kama mume hana kipato labda.
Utii uleta upendo.
Uliona wapi ndoa ya wababe wote ikaenda
Hayo mambo ya vipato umeyaleta wewe, hoja yangu ni kwamba kama mwanamke anamsaidia mwanaume majukumu yake basi anastahili kumsaidia na nafasi yake, ila kama mwanaume anapambana peke yake na majukumu yake bila kujali kipato chake wala kuhitaji msaada wa mke basi huyo anastahili utii
Nafasi ya mwanamke inajulikana na wajibu wa mwanaume unajulikana kila mmoja akisimama kwenye nafasi yake ndoa ni amani.
Hakuna gari iendeshwayo na madereva wawili
Sasa kama hakuna gari inayoendeshwa na madereva wawili kwanini kwenye upande wa majukumu mnataka kuwe na madereva wawili, unafahamu kwamba mkiwa kwenye gari jukumu la dereva ni tofauti na jukumu la abiria yeye abiria kazi yake ni kustarehe huku dereva ndiye akitakiwa kuwa makini kuanzia mwanzo hadi mwisho wa safari, sasa inapotokea dereva anataka abiria naye amsaidie baadhi ya mambo kama kumuangalizia alama za barabarani au vyombo vingine vya usafiri hapo hiyo gari inakuwa na madereva wangapi au wewe unadhani udereva ni kudeal na usukani gear na pedals pekee siyo
 
Sawa, tuachane na suala la aina za mahusiano, tujadiliane kwa mtazamo wako binafsi. Situation ya kwanza wewe na mpenzi wako mnaishi sehemu tofauti na situation ya pili mnaishi kama mume na mke halafu wewe una ajira inayokupa kipato. Sasa mmekaa chini mjadiliane kuhusu suala la nani anawajibika kutoa huduma wewe kama mwanamke utakuja na terms zipi mezani?
 
Elewa point yangu kwa malezi ya kiafrika dereva abakie kuwa dereva na konda abakie konda
 
Nta dislike mpaka nyue mashangazi na feminist mtakapopata akili nzuri na bado huu ni mwanzo tu!
ebu ntolee degedege lako apa,,ukikataliwa acha majungu mkaka ebu kua mtu mzima basi we dogo hujafunzwa kwenu nin.
 
Hivi hii ya wanaume kuona kwamba wanawake wanataka kuwa sawa na ninyi inatokana na nini, kwa sababu mimi sidhani kama mwanamke kushindwa kumtii mwanaume kunamaanisha kwamba wako sawa, na huo utofauti uliopo kati ya mwanaume na mwanamke sidhani kama ndio justification ya mmoja kulazimika kuwa chini ya mwenzake hata kama hayuko tayari
 
Singo maza punguza povu relax my dear 😝
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…