Utii wa wanawake wa kisasa

Umeona ulivyo mjinga?? Hapo nimesema shetani nyoka nikaweka mabano. Nyoka kwenye biblia katumika km kiwakilishi. Kwanza unanichosha ninachoona unajiongelesha vitu havieleweki
 
Sometimes shida sio mwanaume kushindwa kumhandle mwanamke, bali shida inakuwa ni mwanamke asiye na maadili na ambaye hajafundwa vizuri.
Shida ni kwa mwanamme, hata kama mwanamke hana maadili na hajafundwa vizuri.

Kwa sababu mwanamme makini anatakiwa kuwa na uwezo wa kumjua mwanamke asiye na maadiki au asiyefundwa vizuri, whatever that is, na kumuepuka mapema.
 
Dada angu kuna sehemu unakosea. Mtoa mada hajasema kwamba mwanaume asiwajibike, mfululizo wa hoja zako inaonekana wewe kiasili ni mjeuri sasa unachokifanya ni kutafuta justification ya ujeuri wako. Hakuna popote ambapo mtoa mada kasema mwanaume hatakiwi kuwajibika ni wewe ndio umekuja na masharti ambayo unataka utimiziwe ndio in-return uwe mtiifu na huo kiasili sio utiifu anaoongelea mtoa mada, hapo unaigiza tu lakini huo unaoita uwajibikaji wa mwanaume(bila shaka ni kukuhudumia) ukikosekana kwa sababu yoyote basi na utiifu unaishia hapo. Tunaongelea utiifu ambao upo ndani ya mtu na anau-practice naturally tu hatuongelei mdangaji aliejivisha vazi la uwife material ili ahudumiwe
 
Ujana usikupotoshe dada angu ukaja kushtuka muda ushaenda wapo wengi waliokua na mawazo kama yako wakati wakiwa 20's na sasa wapo kule kwenye jukwaa la love connect wanatafuta mume. Suala la kuwa na mwenzi wa maisha ni hitaji la kila mtu na bahati mbaya sana wanawake mnatakiwa kufukuzana na muda maana mkifika 30's tu hapo mshaingia kwenye decline stage kwenye suala la kupata mume na uzazi unaanza kusumbua.
 
Narudia tena, sio kila mwanaume wa kuolewa naye. Siwezi kupanga kuolewa na mwanaume mjinga, mvivu na mpumbavu eti kisa nionekane nina ndoa, nehi nehi my friend.
Kama hawa ndio aina ya wanaume unaokutana nao basi badilisha cycle yako au jitengenezee mazingira ya kuwavuta wanaume wa maana lakini sio kuchukulia wanaume wote ndio wapo ivyo au kama ushawahi kupita katika mahusiano na mwanaume mwenye tabia izo basi pptezea chukulia ulipotea tu njia kila mtu anafanya makosa lakini kuishi na trauma za mahusiano yako ya nyuma utaishia kujaza sumu tu dhidi ya wanaume na haitakusaidia chochote.
Kanuni ya asili inataka mwanaume ampende mkewe na mwanamke amtii mumewe, hauwezi kwenda nje ya hapo na mahusiano yakabaki imara. Hizi chokochoko za ferminism, 50/50, upinde n.k ni vulugu tu za binadamu.
 
Bi Jadda Wewe sio Muadilifu Kabisa Wewe Umesema Wanawake Wengi Nimekwambia Wengi Inamaanisha Sio Wote. Umeshindwa kuleta Hoja unaruka ruka Plus Malalamiko.
Mimi nimekuambia siyo wanawake wote wanazaliwa na msukumo, wa kukubaliana na kila fikira wanazomezeshwa, kama hiyo hoja imekushinda sema
Wapi Mimi nimesema Kipofu atawaliwe na Anaeona Mbona Unachanganya Mambo.

Maandiko Matukufu kwa Mujibu wa Nani?? Mbona Swali lako halieleweki. Anyways Kwa Mujibu Wa Mungu.
Ndio maana nikakuuliza kwa mujibu wa mungu gani, mimi sijakataa kwamba kuna miungu ila nakuuliza mungu gani, maana kuna miungu mingi kulingana na dini zilizopo duniani kwa sasa
Hoja Umekosa Umebaki kujigonga gonga. Nature Ndo Imeamua Mwanamke Awe Dhaifu (kwa maana no external force) Sasa Unaponiuliza Ni Nature Gani!! Nashindwa Kuelewa unataka nikutajie Jina La Nature hiyo?? (Bi Jadda Umefirisika Hoja)
Ni kwanini nature imeamua mwanamke awe dhaifu according to majukumu ya mwanaume tu, kwanini haijaweka into consideration majukumu ya mwanamke au mnayaona marahisi, okay tuseme mwanaume kushindwa kubeba mimba na kuzaa maana yake naye ni dhaifu
Na kwanini utolee mfano wa ng'ombe tu na ndicho nilichotoka kusema hapo sababu nilishajua utatolea mifano ya wanyama wafugwao tu, japo hata hao ng'ombe wenyewe kuna muda huwa wanawadhuru binadamu kwa kutumia pembe zao sasa kuna utii hapo, kwanini usitolee na mifano ya wanyama pori je na wenyewe unaweza ukawaamrisha na wakakutii si ndio
Bi Jadda Unafurahisha kwa kweli Hivi hujui Wanaoteseka Mitaani ni Single Mothers na Wale wa Mikopo kausha Damu hujui kuwa Wanawake wanaojiuza na Kudanga wanazidi kuwa wengi Inaonekana wewe Huijui Jamii.
Wanawake kinachowatesa siyo guilty consciousness bali ni gender stereotypes zilizopo kwenye jamii dhidi yao, laiti jamii ingeacha kuwasimanga wanawake kama ambavyo haiwasimangi wanaume basi wanawake wangekuwa wanafanya mambo yao bila pressure, ila pamoja na kwamba wanaume hamsimangwi kwenye jamii bado mnalalamika kwamba wanawake wanawatesa sasa mnateseka na nini
Acha kupindisha Hoja Mimi nimesema Sio kila Anaetawaliwa Anakuwa Hana Furaha. Hatujazungumzia Suala la Kufaidika au kutofaidika.
Je hiyo furaha anakuwa ameikiri yeye mwenyewe kwamba anayo au ni wewe ndiye unayemsemea, ni lini wanawake walikiri wenyewe kwamba wanafurahia kutawaliwa na wanaume, kwanini ninyi ndio mnawasemea kwanini msiwaache wajisemee wenyewe kinachowapa furaha
Nilishakwambia Kila Kitu kina vigezo Vyake Na Haviingiliana Utawala Umejengwa katika misingi ya Nguvu na Umadhubuti na Uwezo. Hili ni Muhimu ili uwe unaweza Kumuwajibisha Unaemtawala itapo bidi.
Vipi na mwanaume akifanya makosa ni nani anayemuwajibisha au mwanaume hakosei, kwani mliambiwa wanawake ni viumbe wasio na utashi kwamba hawajui kuwa wanachofanya ni kizuri au kibaya, kwahiyo wewe mama yako anatakiwa akutii kwa sababu tu wewe ni mwanaume una nguvu zaidi yake mbona hujibu hili
Sasa huo utawala umekuja automatically kivipi mbona wanawake wengi hawautaki huo utawala, kama hilo suala lingekuwa automatic basi wanawake wangejikuta tu wanalifurahia wala wasingehitaji kulazimishwa, kitendo cha kutumia nguvu kubwa kutaka kuwatawala maana yake hilo siyo natural bali ni man made
Siwezi kufungua mjadala mwingine wakati huo mfano niliotoa ni relevant unaendana kabisa na hii mada, jinsi wanaume mnavyoona sababu zenu zina mashiko ndivyo hata wazungu nao wanavyoona sababu zao zina mashiko, jinsi mnavyoona kwamba utawala wenu ni nature na ni scripted ndivyo hivyo hivyo nao wanavyoona
Uelewa wako Mdogo Ulitakiwa Uniulize Kuna Uhusiano gani kati ya Vitu Hivyo na Jee kivipi Vinatafsiri Feminism. Ila Sababu unapenda tuu kibisha bila hoja unaleta Mifano Irrelevant.
Wewe unanikataza mimi kufanya kile ambacho hata wewe unafanya mimi nimetolea mfano wa ukoloni jinsi unavyohusiana na mfumo dume, wewe ukasema mada ni mfumo dume kama nataka kuongelea ukoloni nianzishe mjadala mwingine, ila wewe hapa unataka kuleta habari za atheism na homosexuality je mada inahusu hivyo vitu kwanini na wewe usianzishe mjadala mwingine kuhusu hivyo vitu
Unataka kutuambia kuwa Uongozi katika Familia ni dynamic leo Baba anaongoza kesho Mama Kama baba akishindwa kuhudumia. Nadharia zako ni za ajabu mno.
Ndio kwani uongozi ni nini hadi usiwe dynamic uongozi ambao umejengwa katika misingi ya huduma za kiuchumi ni dynamic kwenye nyanja zote, hata leo hii Tanzania akifanikiwa kuwa superpower kisha Marekani akaanza kuitegemea kiuchumi basi hana budi kuitii, uongozi ni conditional huwezi kumtawala tu mtu hivi hivi kwa visingizio vya kipuuzi visivyoeleweka
Yeah kumbuka wote mwanaume na mwanamke ni viumbe wenye utashi wote wanajua mema na mabaya sasa ni kipi cha ziada alichonacho mwanaume ambacho kinampa advantage ya kumuamulia mwanamke juu ya maisha yake, yani mfano mwanamke anataka kufanya kitu fulani au kuenda mahali fulani halafu wewe kwa sababu zako binafsi tu zisizo na mashiko ukaamua kumkataza unadhani ni kwanini anatakiwa akutii, kumbuka wewe ukitaka kufanya kitu hiko hiko au kuenda mahali hapo hapo hakuna anayekukataza lakini kwanini unaona una mamlaka ya kumkataza mkeo na ukategemea akutii
Acha blah blah sasa si ndio uelezee hiyo namna ambayo waliitumia kuishi, pale ambapo mume kafukuzwa kazi halafu mke ni mama wa nyumbani, ili turudi sasa kwenye ile hoja ya mwanzo
Ndio maana nikakuuliza na nakuuliza tena, je ina maana mwanaume naye ni dhaifu kwa sababu hawezi kubeba mimba na kuzaa, naomba unijibu jibu lilinyooka tafadhali acha kona kona
Sasa wewe Huamini Maandiko Ya Mungu Utaamini Maneno Yangu mimi. Kazi ipo yaani Mtu Yupo Tayari akane imani ili tuu Kudhibitisha Kuwa Yeye ni Sawa na Mwanaume kuna Fikra ni hatari Mno.
Wewe una uhakika na imani yangu, kwani tangu tumeanza huu mjadala kuna mahali nimespecify kwamba mimi ni wa imani fulani, wewe jibu hoja achana na my personal issues
Ndio Maana Nilihusisha Feminism na Atheism Vyote ni Mipango ya Watu wenye Fikra za Kishetani. Na haya Maneno yako Yanathibitisha hilo.
Hebu thibitisha kwamba feminism na atheism ni mipango ya watu wenye fikira za shetani na onesha namna hizo concepts mbili zinavyohusiana
Acheni hizi propaganda zenu feminism ilianzishwa na wanawake kisha wakajitokeza na wanaume baada ya hapo serikali nazo ndio zikaanza kuunga mkono, sasa hapa nataka nione uelewa wako juu ya haya mambo kama kweli nyuma ya feminism kuna watu walikuwa wanasuka mipango yao hao watu ni kina nani na walikuwa wanasuka kwa faida ya nani, itapendeza kama utakuja na ushahidi wa kihistoria kama ambavyo wewe unanidai mimi ushahidi kuhusu haya ninayoyasema
Ni vitu viwili vinavyoenda sambamba na ndio maana mwanamke hawezi kumtii mwanaume yeyote yule anayekutana naye eti kwa sababu tu ni mwanaume na ana nguvu zaidi yake, bali anatakiwa amtii mume wake tu tena wa ndoa haya jiulize kama utii ungekuwa hautegemei huduma kwanini pale juu umesema mwenyewe kwamba, ni sawa kila mmoja ajitawale mwenyewe kama siyo wanandoa sasa jiulize kwanini utii lazima uwepo kwa wanandoa tu na si kwa mwanamke yeyote kuenda kwa mwanaume yeyote tu
Nashukuru umekubali kuwa Ndoa za Zamani zilikuwa na Furaha. Sasa ndio Ujue Walioleta Feminism hawakuitaka hii Furaha iendelee na Wamefanikiwa Now ndoa hazina Furaha.
Acha kulazimisha kuniwekea maneno hakuna sehemu nimekubali ila nilinukuu kile ulichosema wewe, zamani ndoa zilikuwa na furaha kwa mujibu wa nani na kwa kuzingatia vigezo gani, na sasa ndoa hazina furaha kwa mujibu wa nani na kwa kuzingatia vigezo gani jibu hapo
Sio kweli Wanawake Walikuwa wanaweza kushitaki kwa Wazee kama kuna Jambo baya anatendewa. Mind you serikali za kijadi zilikuwa zinatatua migogoro katika familia. Usitutengenezee Jamii ambayo haikuwepo.
Kama kweli wazee wa zamani walikuwa wanawasikiliza wanawake kwanini sasa ukeketaji na unyanyasaji wa aina nyingine uliendelea kuwepo hadi pale serikali zilipoanza kuingilia kati, kwani ukeketaji ulikuwa una faida gani kwa wanawake na je wanawake walikuwa wanaufurahia, ninyi ndio mnatengeneza jamii ambazo hazikuwepo yani wanaume ndio mmekuwa wasemaji wakubwa wa wanawake kuliko wao wenyewe yani eti ninyi ndio mnaamua ni kipi kinawapa furaha au huzuni wanawake
Nyinyi mmesoma ila badala muelimike Elimu yenu yote mnawekeza ku prove kuwa Mpo Sawa na Wanaume.
Sasa ndio uone kwamba utii wa mwanamke kwa mwanaume siyo natural bali ni man made, kwa sababu ungekuwa ni nature basi usingeathiriwa na elimu, ajira wala any other external forces yani mwanamke angekuwa mtii tu bila kujali amesoma, ana pesa au la, na ndio maana zamani babu zetu hawakutaka wanawake wasome, maana walijua wakiruhusu hilo basi mwanamke atafunguka akili na kutaka kutoka kwenye utumwa ambao mwanaume alimuweka katika kipindi kirefu, na hilo likitokea itakuwa ni hasara (maumivu ya kihisia) kwa mwanaume na ndio kinachoendelea sasa hivi kote vijiweni na mitandaoni wanaume ndio wanaongoza kulalamika kwenye ndoa kuhusu tabia za wanawake ilihali malalamiko ya wanawake kuhusu tabia za wanaume yanazidi kupungua
Kwa hapa umethibitisha kuwa utii au Utawala Upo based on Nguvu na Uwezo. Ila Mimi Nilisema Sio kila Anaetawaliwa Anakuwa Hana Furaha. Siku sema Wote.
Sasa kwanini ninyi ndio muamue kwamba huyu akitawaliwa anakuwa na furaha, ila huyu akitawaliwa anakuwa hana furaha mnatumia vigezo gani kuconclude hivyo, je ni hao watawaliwa wenyewe ndio huwa wanasema hivyo au ni mawazo yenu tu
Sasa Swala la Kukeketwa Linahusika Vipi hapa. Mbona unaongelea Mambo tofauti tofauti. (Umefirisika Hoja)
Ofcourse suala la kukeketwa linahusika kwa sababu wewe ulisema kwamba, kitendo cha bibi zetu kushindwa kuwapinga babu zetu maana yake walikuwa wanafurahia hayo maisha, ndio nikakuuliza je ina maana hata kukeketwa pia walikuwa wanafurahia kwa sababu tu walishindwa kulipinga hilo
Mimi Sijasema Kwamba wanawake waliifurahia kila Jambo. Mimi Nimesema Sio Kila Anaetawaliwa Anakua hana furaha. (Usinipeleke kujadili tamaduni zisizo faa katika jamii hatupo katika Mada hii).
Hili nimeshalifafanua tayari
Bi Jadda Upo wapi wewe!!! nani Kasema Mwanaume anatiiwa bila sababu ya Msingi?? Sisi tumeshataja Sababu kuwa ni Nguvu uwezo na Umadhubuti Sasa unaposema bila Sababu ya Msingi Mbona Unatusikitisha.
Hizo nguvu na umathubuti kwanini ziapply kwa mke wa ndoa tu kwanini zisiapply na kwa mama, shangazi, dada, au ndugu na jamaa wengine wa kike kwani hao siyo wanawake, au kwako mkeo wa ndoa tu ndio mwanamke
Sasa kama unajua nimeyakataa maandiko kwanini unaendelea kuniletea reference kutoka kwenye maandiko hata hivyo mimi hapa sijadili kulingana na imani yangu mimi, bali nakupeleka popote unapotaka tuende ili usilete visingizio ukitaka tujadili kidini tutajadili ukitaka tutoke nje ya dini pia tutajadili kwahiyo chagua moja, kama unataka tutoke nje ya dini basi tustick huko siyo ukiona hoja zimekuzidia unahama unarudi tena kwenye dini na kama unataka tujadili kutumia dini basi tustick ndani ya dini na siyo mimi nikikupa maandiko yanayohusiana uanze kusema eti ni nje ya mada

Sasa ni hivi kwenye biblia hilo andiko la mwanamke kumtii mumewe linaambatana na andiko la mwanaume kumpenda mkewe yani hauwezi kutengenisha hayo mawili maana yanaenda sambamba, kwahiyo kama mungu alimaanisha mwanamke anatakiwa kumtii mumewe regardless of what basi bila shaka pia alimaanisha mwanaume anatakiwa kumpenda mkewe regardless of what, kwahiyo tufanye utii wa mwanamke na upendo wa mwanaume vyote ni nature kwa sababu viliagizwa na mungu si ndio

Sasa ndio nakuuliza je kwa kuzingatia hayo maandiko ina maana hata kama mke yupo tu nyumbani, hatimizi majukumu yake kama kufanya kazi za nyumbani au kuzaa watoto muda mumewe anaotaka, bado huyo mumewe ataendelea tu kumpenda
Nani kakudanganya kwamba uzuri na upole ni masuala objective hivi hujawahi kusikia msemo usemao "uzuri upo machoni pa mtazamaji", uzuri na upole ni masuala subjective (mtambuka) hakuna fixed standards za uzuri na upole ambazo zimekuwa approved na watu wote dunia nzima, bali kila mtu hutoa mawazo yake kulingana na mitazamo yake
Mimi nilikuuliza na hukujibu UNA USHAHIDI WA KIHISTORIA KUWA WANAUME WAKI INSTALL UTAWALA WAO KIMABAVU??
Ushahidi wa kihistoria unaotaka ni upi wakati kila kitu kiko wazi, kitendo cha kuwepo wanawake walioanza kuupinga huo utawala ni uthibitisho tosha kuwa huo utawala ulikuwa ni wa kimabavu haukuridhiwa na watawaliwa wenyewe, ila wengi walikuwa wanakaa kimya kwa sababu tu hawakuwa na sauti wala nguvu ya kuupinga
Na ndio maana nikakutolea mfano wa kukeketwa hata kukeketwa nako wanawake walikuwa wanaona fahari kwa sababu walishaaminishwa kwamba mwanamke asiyekeketwa ni malaya na haolewi hivyo kukeketwa ni ufahari ila mioyoni mwao hawakuwa wakifurahia hilo jambo maana lilikuwa ni la maumivu tu, kwa mfano kuna article nilisoma kuna makabila huko ethiopia zamani mwanamke kabla ya kuingia kwenye ndoa ilikuwa ni lazima achapwe viboko hamsini na mumewe mtarajiwa kuashiria kipimo cha uvumilivu atakachokuwa nacho ndani ya ndoa na akishindwa kuvivumilia hivyo viboko basi haolewi lakini wanawake walikuwa wanavumilia ili tu wapate ndoa na walikuwa wanaona ufahari kabisa, sasa huo ni mfano mmoja tu nilikuwa najaribu kukuonesha kwamba mambo mengi wanawake wa zamani waliyokuwa wanayaona ni ufahari si kwamba walikuwa wanayapenda kwa utashi wao ila ni kwa sababu tu ya fikira walizomezeshwa na wanaume wao kwamba mwanamke asipoolewa anaonekana hafai katika jamii na ni wa kutengwa so wanawake wakawa tayari kuvumilia manyanyaso ya ndoa kuliko masimango ya jamii halafu wewe uko hapa unajadili haya mambo kwa kutumia mihemko na hisia zako
Umerudi kule kule Ndo maana nilikwambia Kwenye kila Utii kuna aina furani ya Uoga. Unachekesha Bi Jadda

Kulipa mshahara sio ndio uwezo tunaouzungumzia sisi au wewe unahisi tunaposema nguvu ni kwamba Ni Physical strength pekee??
Sasa mshahara si ndio huduma za kiuchumi, strength ni kile cheo alichonacho acha kupotosha, watu hawawatii maboss wao sababu tu ya vyeo bali kwa sababu za maslahi ya kiuchumi
Hili jambo halipo Hakuna Familia Hiyo Acha Maigizo Nasisitiza Hili Jambo Halipo acha kutufanya Sisi ote hatujui maisha ya familia kama wewe.
Hapa hatuzungumzii whether jambo fulani lipo au halipo, bali tunazungumzia whether uwepo wa hilo jambo ni nature au ni injected au engendered, ili tujue kwamba linastahili kuwepo au ni watu tu ndio wanalazimisha liwepo
Hapa bado nitasisitiza ile hoja yangu kuhusu mama na ndugu na jamaa wengine wa kike wa mwanaume
Kwanini Wanawake Hawakujipa utawala wao kwanza ndo Ujue Strong must rule weak.
Hawakujipa kwa sababu hawakuutaka utawala walitaka usawa in the first place, kiumbe chochote kinazaliwa na neutral feelings and thoughts hadi pale kitakapofunzwa otherwise, ila wanaume ndio mkalazimisha kujipa utawala kwa kuzingatia vigezo vyenu vinavyowafavour ninyi tu
Utawala wa wanaume haukulazimishwa kama unaushahidi wa kihistoria Juu ya installment ya Huo utawala nipe.
Hili nimeshafafanua tayari
Wewe ulishayakana maandiko sina la kukushawishi hapa.
Hapa tusijadiliane kulingana na imani yangu mimi
Utii ni Natural na Uoga ni Natural Lazima ujue hivyo. Leo wewe ukimuona Simba Hutalazimishwa kuogopa Na Pia ukiona Sungura Hata uweje Huwezi kuogopa hata ukilazimishwa Hiyo ndio maana ya Nature. Una kichwa kigumu sana.
Hapo ndio umezidi kudhihirisha jinsi gani una uwezo wa mdogo wa kufikiri na kuchanganua mambo, wewe kumuogopa au kutokumuogopa mnyama ni kwa sababu either una kumbukumbu ya kudhuriwa na mnyama fulani au umesikia sifa kuhusu huyo mnyama kwamba ni hatari au siyo hatari, na ndio maana mtoto ana uwezo wa kucheza na nyoka hamuogopi sababu bado hawajaumwa na nyoka au hajaambiwa na watu kwamba yule ni mnyama hatari ila siku akiumwa au akikuwa na kuja kuambiwa ataanza kumuogopa nyoka kwahiyo hadi hapo huo uoga unakuwa siyo nature bali ni injected au engendered
Sasa si ndio swali langu lilipo kwanini mwanamke yuko obligated kumtii mumewe wa ndoa tu na siyo mwanaume yeyote yule, unaniuliza tena mwanamke amtii mwanaume aliyekutana naye barabarani kwa lipi wakati umesema msingi wa mwanamke kumtii mwanaume ni nguvu na umadhubuti kwani hizo sifa anazo mumewe tu, ndio maana nikakuuliza kwa mfano mwanaume na mwanamke ni workmates ofisini na wote wana vyeo sawa halafu mwanaume akamtuma mwanamke afanye kitu fulani au akamkataza mwanamke asifanye kitu fulani je huyo mwanamke anapaswa kumtii kwa sababu tu ni mwanaume na ana nguvu zaidi yake
Leo Umezungumza Porojo tuu na Kupindisha pindisha Maneno.
Ukishazidiwa hoja lazima uone nimepindisha maneno tuende taratibu tu tutaelewana, we si umesema unataka kumwaga elimu unieleweshe basi acha kujilalamisha, tuende kazi mwisho zitajulikana tu mbivu na mbichi
 
Mimi nimekuambia siyo wanawake wote wanazaliwa na msukumo, wa kukubaliana na kila fikira wanazomezeshwa, kama hiyo hoja imekushinda sema
Unakichwa kigumu sana. Unaposema Sio wanawake Wote Inamaana Si Wapo Wachache Katika Hao. Ulikosea Kutumia Neno Wanawake Wengi ulitakiwa Useme wanawake wote Tangu kule Mwanzo. Tatizo umekaa kiubishi ubishi Tuu Mdada.
Ndio maana nikakuuliza kwa mujibu wa mungu gani, mimi sijakataa kwamba kuna miungu ila nakuuliza mungu gani, maana kuna miungu mingi kulingana na dini zilizopo duniani kwa sasa
Mungu Wa Mbinguni Kama na Hiyo Miungu Mengine ipo Mbinguni Jenga Hoja Nyengine.
Ni kwanini nature imeamua mwanamke awe dhaifu according to majukumu ya mwanaume tu, kwanini haijaweka into consideration majukumu ya mwanamke au mnayaona marahisi, okay tuseme mwanaume kushindwa kubeba mimba na kuzaa maana yake naye ni dhaifu
Naona Sasa Unataka Kukataa Tena Kuwa Nyie Sio Dhaifu Ukilinganisha na Wanaume. Naendelea Kukufundisha Majukumu ya Kimaumbile Ya Mwanamke Yanaambatana Na Udhaifu Na Kuhitaji Msaada Wa Njee Madhalani Kubeba Ujauzito kunaambata na Udhaifu Na Wanawake wanakuwa Dhaifu katika Kipindi hicho (Kama hujawahi Kubeba Mimba Kaa Kimya) Jukumu lengine la Kuzaa(Labor and Delivery) pia Ni Matukio yanayomfanya Mwanamke Awe Dhaifu au Katika kipindi hicho Mwanamke Anakuwa Anahitaji Sana Msaada Wa Njee. Sasa Sijajua Haya Majukumu ya Kimaumbile Yanamfanya Vipi Mwanamke Awe Strong au Japo Unipe Mahusiano Baina Ya Kuzaa na Kuwa Strong.
Na kwanini utolee mfano wa ng'ombe tu na ndicho nilichotoka kusema hapo sababu nilishajua utatolea mifano ya wanyama wafugwao tu, japo hata hao ng'ombe wenyewe kuna muda huwa wanawadhuru binadamu kwa kutumia pembe zao sasa kuna utii hapo,
Hapa umeandika Utoto Mtupu.
kwanini usitolee na mifano ya wanyama pori je na wenyewe unaweza ukawaamrisha na wakakutii si ndio
Nimezungumzia Kuwatawala in General Term Namaanisha Binadamu Wanaweza kufanya Lolote Kwa Wanyama Hata hao Simba Sijui na nini Bado Binadamu wanaingia Hifadhini na Wanafanya Utalii na Hakuna Kitu Wanyama Wanafanya Yote haya Ni kwa sababu ya Uwezo wetu mkubwa wa Akili. Sasa wewe unatafuta Kauchocholo (Rare Cases) unang'ang'ania Hapo hapo. Umefirisika hoja.
Wanawake kinachowatesa siyo guilty consciousness bali ni gender stereotypes zilizopo kwenye jamii dhidi yao, laiti jamii ingeacha kuwasimanga wanawake
Jamii iache kuwasimanga kivipi!!! wakati kila Kitu ni Wanawake siku Hizi Ajira wanawake Mikopo Wanawake Viongozi Wanawake Na Tawala zinawapa Kipaumbele na Sauti wanawake Sasa Jamii gani Inayowasimanga Wanawake washindwe Kufanya Mambo Yao??
kama ambavyo haiwasimangi wanaume basi wanawake wangekuwa wanafanya mambo yao bila pressure, ila pamoja na kwamba wanaume hamsimangwi kwenye jamii bado mnalalamika kwamba wanawake wanawatesa sasa mnateseka na nini
Nani Anamtesa Mwanaume katika Jamii?? Mbona Unatunga Mambo. Unachekesha mno . Eti Single Mothers ni kwa Sababu Wanawake wanasimangwa ,,, Mikopo kausha Damu Kisa wanasimangwa Wadangani na Makahaba Kisa wanasimangwa.( Unasikitisha)
Je hiyo furaha anakuwa ameikiri yeye mwenyewe kwamba anayo au ni wewe ndiye unayemsemea, ni lini wanawake walikiri wenyewe kwamba wanafurahia kutawaliwa na wanaume, kwanini ninyi ndio mnawasemea kwanini msiwaache wajisemee wenyewe kinachowapa furaha
Tumezaliwa Tuwewakuta Bibi zetu Wanaishi Maisha ya Furaha Na Babu Zetu hili linatosha Kusema Walikuwa na Furaha Au wewe Bibi yako ulikuta na Huzuni??? Na for your information. Mwanamke ambae ni pure Mwanamke Sio Manipulated kama wewe Huwa anajisikia Fahari kumuhudumia Mumewe na Kumtii.
Vipi na mwanaume akifanya makosa ni nani anayemuwajibisha au mwanaume hakosei, kwani mliambiwa wanawake ni viumbe wasio na utashi kwamba hawajui kuwa wanachofanya ni kizuri au kibaya,
Yaani Tatizo wewe ni Mwanafunzi Jeuri yaani Hujui Jamii ila Unakazana Kuizungumzia kana kwamba Labda ulishaishi Miaka hiyo zamani kumbe Unasikia sikia kwa Dada zako (Feminist wakongwe) Wanaume Waliwajibishwa pale ilipobidi Na Wazee wa Koo husika na Kama Ikishindikana basi Kwa Viongozi wa kimila (Jadi). Usidhani kuwa Wanawake walikuwa Wanafungiwa Ndani tuu Wahawezi kufanya lolote. Usitutengenezee Jamii ambayo haikuwepo.
kwahiyo wewe mama yako anatakiwa akutii kwa sababu tu wewe ni mwanaume una nguvu zaidi yake mbona hujibu hili
Mbona hili Jambo tumelizungumza Mara nyingi Hapa Tunazungumza Utii Wa Mwanamke Kwa Mwanaume Katika Taasisi Yao ya Ndoa(Familia). Tukasema Mke lazima Amtii Mume kwa Vigezo ambavyo Tulishavielezea. Hata kama tulikuwa tunatumia Mwanaume na mwanamke ilikuwa inatosha kutumia hivyo kwa sababu huu mjadala ulianzishwa kwa Ajili ya Utiii katika Ndoa Sio Utii kila Mahali.
Mtoto anatakiwa Amtii Mama yake sababu Amemzaa. Mke anatakiwa amtii mumewe sababu Ana Nguvu na Uwezo na Umadhubuti kuliko Yeye. (Unatuchanganyia Mambo.)
Sasa huo utawala umekuja automatically kivipi mbona wanawake wengi hawautaki huo utawala,
Hawautaki Baada ya Kumezeshwa Fikra Bibi Zetu Hawakuwahi Kupinga Utawala wa Mwanaume. Hili limekuja Baada ya Kuanzishwa Fikra Chafu na Wakamezeshwa Wanawake Waone Wanaonewa. Mind you Hata Mashoga Nao Wanaona Wapo Sahihi na Jamii inawaonea kuwasema vibaya. Sio kila fikra ni Sahihi Eti kwa Sababu imepata Wafuasi.
kama hilo suala lingekuwa automatic basi wanawake wangejikuta tu wanalifurahia wala wasingehitaji kulazimishwa, kitendo cha kutumia nguvu kubwa kutaka kuwatawala maana yake hilo siyo natural bali ni man made
Hakuna Utawala uliotambulishwa kimabavu Maisha Yalikuwa yanaenda Smoothly Zamani. Unachanganya kati ya Manipulated women (kama wewe) na Wale pure women (Bibi zetu)
Inabidi ujue Nature na Scriptures Ni vitu viwili tofauti. Ila vinaweza kutumika Kujengea hoja Moja Ila Haimaanishi Vinafanana Usichanganye vitu.
Historia inavielezea vitu hivyo hivyo vitatu katika paragraph moja. Ila sijui kama Historia inaelezea Utawala wa wanaume kwa wanawake na Ukoloni katika Paragraph moja. (UNARUKA RUKA MNO)
Huijui Familia wewe Binti Unaongea Nadharia na Pumba.
Yeah kumbuka wote mwanaume na mwanamke ni viumbe wenye utashi wote wanajua mema na mabaya sasa ni kipi cha ziada alichonacho mwanaume ambacho kinampa advantage ya kumuamulia mwanamke juu ya maisha yake,
Tumeshataja mbona ni ile Nguvu yake Uwezo wake na Umadhubuti wake Sasa unaposema kitu gani cha ziada Unamaanisha huoni kwamba Wanaume wana Nguvu kuliko Wanawake??. (Unafikiri kwa kutumia nini??)
yani mfano mwanamke anataka kufanya kitu fulani au kuenda mahali fulani halafu wewe kwa sababu zako binafsi tu zisizo na mashiko
Upo so negative always kwanini usingeegemea katika Sababu zenye Mashiko kama Kuangalia watoto. Kwanini Umerukia sababu zisizo na mashiko kujengea hoja. (Una Matatizo makubwa)
ukaamua kumkataza unadhani ni kwanini anatakiwa akutii, kumbuka wewe ukitaka kufanya kitu hiko hiko au kuenda mahali hapo hapo hakuna anayekukataza lakini kwanini unaona una mamlaka ya kumkataza mkeo na ukategemea akutii
Ndio Maana nikasema Maisha ya Kifamilia lazima Awepo kiongozi. Na Bibi Zetu waliwatii Babu zetu Na Hakukuwa na Kitu walipungukiwa kwa kuwatii. Ninyi mnaona Tabu Sababu Nyie sio pure women ni Manipulated Women.
Acha blah blah sasa si ndio uelezee hiyo namna ambayo waliitumia kuishi, pale ambapo mume kafukuzwa kazi halafu mke ni mama wa nyumbani, ili turudi sasa kwenye ile hoja ya mwanzo
Nasisitiza wewe ni mwanafunzi Jeuri.Haya Ngoja Nikufundishe Maisha.
Itokeapo Changamoto kwa Baba basi hupata Msaada katika namna nyingi mno.
Kutoka kwa wazazi wake (mume) kutoka kwa wazazi wa mke kutoka kwa ndugu wa Mume au Mke,, kutoka kwa Marafiki na watu wa karibu. Kupitia mikopo. Au kutoka kwa mkewe kama anaweza kufanya biashara ndogondogo kwa wakati huo na kadhalika(unatakiwa ujue Binti kuwa Jamii inaishi kwa kutegemeana na kusaidiana katika matatizo. Hoja yako ipo wapi??
Ndio maana nikakuuliza na nakuuliza tena, je ina maana mwanaume naye ni dhaifu kwa sababu hawezi kubeba mimba na kuzaa, naomba unijibu jibu lilinyooka tafadhali acha kona kona
Kuzaa na Kubeba Mimba nishafafanua Ni katika Vitu vinavyohusiana na Physical Weakness ya Mwanamke sasa vipi uvihusishe na Umadhubuti wa mwanaume??(Hoja kituko).
Wewe una uhakika na imani yangu, kwani tangu tumeanza huu mjadala kuna mahali nimespecify kwamba mimi ni wa imani fulani, wewe jibu hoja achana na my personal issues
Wewe Ulishapinga maandiko wazi wazi Sasa unalalamika nini?? Wewe umeshakana Imani kwa Mungu ili utete Feminism kama una Imani basi ni Huo u Feminism.
Hebu thibitisha kwamba feminism na atheism ni mipango ya watu wenye fikira za shetani na onesha namna hizo concepts mbili zinavyohusiana
In summary Feminism ipo against Maandiko Matukufu ya Dini kubwa Duniani (naamini unazijua) So ili Uwe Feminist na ufanikiwe kutetea na kujenga hoja Lazima kwanza Ukane Dini za Maandiko ,,, Uwe mpagani (huna Dini). Ukishayakubali Maandiko basi Mwanaume ni kiongozi Kwa mwanamke katika Familia na Jamii in large Jambo ambalo Hasira ya U Feminism imeegemea hapo. (Achalia mbali historical aspects)
Acheni hizi propaganda zenu feminism ilianzishwa na wanawake kisha wakajitokeza na wanaume
Hapa kwanza utuambie hao Wanaume ni kina nani na walikuwa na mchango gani ni lipi lilikuwa jukumu lao??
Sasa kumbe nilishakudai ushahidi Sasa mbona hujauleta bali umezua lengine. Niletee mimi kwanza ushahidi alafu kisha mimi nije nikufundishe.

Kama sio Wanandoa Namaanisha ninyi sio Taasisi moja Yaani Hamjaungana Kuwa Kitu kimoja Sasa Binti yupo kwa Wazazi wake Na Kijana Yupo na harakati zake Sasa binti anamtii katika jambo gani??. (Tunaposema utii inabidi ujue Vitu vinavyokusudiwa hapo tatizo wewe bado Binti unanipa kazi sana).
sasa jiulize kwanini utii lazima uwepo kwa wanandoa tu na si kwa mwanamke yeyote kuenda kwa mwanaume yeyote tu
Mwanaume wa Barabarani utamtii katika nini?? Tunaposema mume na mke tunamaanisha Mke atamtii muwe katika majambo ya mule ndani na ya kifamilia kwa ujumla Sasa mwanaume wa barabarani unamtii katika nini. (Unatengeneza scenario za ajabu)
Acha kulazimisha kuniwekea maneno hakuna sehemu nimekubali ila nilinukuu kile ulichosema wewe, zamani ndoa zilikuwa na furaha kwa mujibu wa nani na kwa kuzingatia vigezo gani,
Kwa mujibu Wetu sisi tuliozikuta Mimi nimeshuhudia ndoa za zamani nyingi zilikuwa na Furaha.
Vigezo ni kuwa hakukuwa na Mashindano na Magomvi Hakukuwa na Talaka mwendokasi hakukuwa na single mothers kama Hivi Sasa Hakukuwa na Mikopo kausha Damu.
na sasa ndoa hazina furaha kwa mujibu wa nani na kwa kuzingatia vigezo gani jibu hapo.
Sasaivi ndoa hazina Furaha kama tunavyoshuhudia Talaka mwendokasi,, Single Mom wa kutosha ,, Magomvi na kutunishiana misuli kuliko zidi. Au wewe unapinga haya??
Kama kweli wazee wa zamani walikuwa wanawasikiliza wanawake kwanini sasa ukeketaji na unyanyasaji wa aina nyingine uliendelea kuwepo hadi pale serikali zilipoanza kuingilia kati,
Wewe unachanganya Tamaduni za watu Mbali mbali na kuzihukumu kama kitu kimoja. Kitu ambacho Sio kizuri kwako kwa Mwengine ni kizuri. Mimi sisemi Kukeketwa ni Jambo zuri ila Jamii Zenye mila hizo zilishakubaliana Na Hakukuwa na aliepinga hilo na wote waliona Ni jambo la kitamaduni. Kama ilivyo Ushoga ulaya ni jambo la kawaida kwao lakini sisi waafrika hatulikubali.
Faida au hasara ni kwa Mujibu wa Jamii husika wewe unaona ina hasara kwa kuangalia upande wako lakini wao waliona una faida kwa kuangalia Vipengele vyao.
Sasa ndio uone kwamba utii wa mwanamke kwa mwanaume siyo natural bali ni man made, kwa sababu ungekuwa ni nature basi usingeathiriwa na elimu, ajira wala any other external forces yani mwanamke angekuwa mtii tu bila kujali amesoma, ana pesa au la,
Wanawake kama wewe mliomezeshwa fikra za Ajabu ajabu ndio Ma feminist kwani wapo Wanawake waliosoma na wanawatii waume zao wapo wenye Mamlaka makubwa lakini wanawatii waume zao usi generalize mambo.
Hapo mwanzo Hakukuwa na Elimu both kwa wanaume na wanawake ila Wanaume Waliwatawala Wanawake Ila unakuja hapa unatuambia ninyi akili zimefunguka baada ya kusoma Kwaiyo Wanaume wao akili zao zilishafunguka hata bila ya kusoma???
kwa mwanaume na ndio kinachoendelea sasa hivi kote vijiweni na mitandaoni wanaume ndio wanaongoza kulalamika kwenye ndoa kuhusu tabia za wanawake ilihali malalamiko ya wanawake kuhusu tabia za wanaume yanazidi kupungua
Unachekesha sisi tunaelezea kinachoendelea Haimaanishi kuna kitu Kinatozonga kichwani. Matatizo mengi mnayapata ninyi wanawake. Mwanaume ni Constant na Mwanamke ni dependent Variable utake usitake.
Sasa kwanini ninyi ndio muamue kwamba huyu akitawaliwa anakuwa na furaha, ila huyu akitawaliwa anakuwa hana furaha mnatumia vigezo gani kuconclude hivyo, je ni hao watawaliwa wenyewe ndio huwa wanasema hivyo au ni mawazo yenu tu
Bibi zetu walidhibitisha hili. Acha porojo.
Kukeketwa Kuna madhara ambayo yanayoweza kuulezewa kibailogia na Kitabibu naomba nipe madhara atakayoyapata mwanamke akiimtii Mumewe????
Hili nimeshalifafanua tayari

Hizo nguvu na umathubuti kwanini ziapply kwa mke wa ndoa tu kwanini zisiapply na kwa mama, shangazi, dada, au ndugu na jamaa wengine wa kike kwani hao siyo wanawake, au kwako mkeo wa ndoa tu ndio mwanamke
Kwa Sababu Mahusiano yaliyopo baina ya Mke na Mume Sio Sawa na mahusiano na hao watu uliowataja.
KIDINI Tunajadili nini wakati wewe ni Mpagani!!!
Tangu ulipoyakataa maandiko sikujengea Hoja tena Maandiko Kwaiyo Kuwa mpole. (Usilalamike)
Regardless of what ndo nini!!!! kwani VIGEZO tulivyovizungumza huvioni mbona unaturudisha nyuma kila mara.
bila shaka pia alimaanisha mwanaume anatakiwa kumpenda mkewe regardless of what, kwahiyo tufanye utii wa mwanamke na upendo wa mwanaume vyote ni nature kwa sababu viliagizwa na mungu si ndio.
Malalamiko.
Sasa ndio nakuuliza je kwa kuzingatia hayo maandiko ina maana hata kama mke yupo tu nyumbani, hatimizi majukumu yake kama kufanya kazi za nyumbani au kuzaa watoto muda mumewe anaotaka, bado huyo mumewe ataendelea tu kumpenda
Hakuna Hoja hapa.
Nikishakitaja kitu unakin'gan'gania hata kama mimi nilikuwa nakusudia General meaning wewe unakaza Kichwa. (Umefirisika)
Usitudanganye Binti. Leta ushahidi acha Porojo.
Na ndio maana nikakutolea mfano wa kukeketwa hata kukeketwa nako wanawake walikuwa wanaona fahari
Si ni wewe ulisema walikuwa hawapendi kukeketwa wewe huyo huyo unasema walikuwa wanaona Fahari kwaiyo Unaona Fahari huku hupendi??? (Umechanganyikiwa)
kwa sababu walishaaminishwa kwamba mwanamke asiyekeketwa ni malaya na haolewi hivyo kukeketwa ni ufahari ila mioyoni mwao hawakuwa wakifurahia hilo jambo maana lilikuwa ni la maumivu tu,
Aisee Hapa Umetuchanganyia mambo Mno Walikuwa wanaona Fahari Alafu moyoni hawapendi??
Usitumie Neno ufahari na Kutokupenda Sehemu moja Unachekesha. Sema walikuwa Hawapendi ila Tamaduni ziliwalazimisha ila ukisema Wanaona Fahari alafu hawapendi unachekesha.
Sasa mshahara si ndio huduma za kiuchumi, strength ni kile cheo alichonacho acha kupotosha, watu hawawatii maboss wao sababu tu ya vyeo bali kwa sababu za maslahi ya kiuchumi
MSHAHARA SIO HUDUMA ACHA UJINGA. MWANAUME ANAPOTOA HUDUMA NYUMBANI HATOI MSHAHARA KWA MKEWE.
TUMESHAJIBU MAHUSIANO YAO YAPO TOFAUTI. MAHUSIANO YA MTOTO NA MAMA SIO MAHUSIANO YA MKE NA MUME.
Hawakujipa kwa sababu hawakuutaka utawala walitaka usawa in the first place,
NIPE USHAHIDI WA HILI.
kiumbe chochote kinazaliwa na neutral feelings and thoughts hadi pale kitakapofunzwa otherwise, ila wanaume ndio mkalazimisha kujipa utawala kwa kuzingatia vigezo vyenu vinavyowafavour ninyi tu
HAPA UMEONGEA USICHOKIJUA BASI HATA WANAWAKE WANAPOZALIWA NATURALLY WANAKUWA NA UTII HADI WAJE KUMEZESHWA FIKRA MBOVU ZA FEMINISM.
Hili nimeshafafanua tayari

Hapa tusijadiliane kulingana na imani yangu mimi
KWANI WEWE UNA IMANI? AU UPAGANI NI IMANI??
Umezungumza jambo Ambalo lipo Kinyume kabisa na huenda hujui Kitu kinaitwa genetics Usingeandika hizi Porojo zako.
Unazungumia Field ambayo hata huna Knowledge nayo Mtoto hamuogopi nyoka kwa Sababu Akili yake Haijaweza bado kupambanua. Siku akili ikashakuwa Hata kama hajawai kuambiwa wala kuumwa ile Physical appearance ya Nyoka na Genetic information ambayo ako nayo itamfanya tuu aogope hata kama hajawahi kusikia chochote kuhusu nyoka.( Wewe ni mwanafunzi mjuaji)
Sasa si ndio swali langu lilipo kwanini mwanamke yuko obligated kumtii mumewe wa ndoa tu
Utii ni kwa mujibu wa mahusiano yanayoexist kati yenu.
na siyo mwanaume yeyote yule, unaniuliza tena mwanamke amtii mwanaume aliyekutana naye barabarani kwa lipi wakati umesema msingi wa mwanamke kumtii mwanaume ni nguvu na umadhubuti kwani hizo sifa anazo mumewe tu,
Sikukuuliza ni kwa Vigezo gani nimekuuliza ni kwa Kitu gani. Yaani anamtii huyo wa barabarani katika jambo gani??
Ndio.
Ukishazidiwa hoja lazima uone nimepindisha maneno tuende taratibu tu tutaelewana, we si umesema unataka kumwaga elimu unieleweshe basi acha kujilalamisha, tuende kazi mwisho zitajulikana tu mbivu na mbichi
Napenda.
 
Unakichwa kigumu sana. Unaposema Sio wanawake Wote Inamaana Si Wapo Wachache Katika Hao. Ulikosea Kutumia Neno Wanawake Wengi ulitakiwa Useme wanawake wote Tangu kule Mwanzo. Tatizo umekaa kiubishi ubishi Tuu Mdada.
Kutokana na hoja yangu bado nasisitiza kwamba siyo wanawake wote acha kunilisha maneno, hiyo hoja imeshakushinda achana nayo tu kuliko kuikomalia halafu hakuna cha maana unachoandika, na sasa hivi nitakuwa nakujibu zile key points tu maana naona umejificha kwenye minor points ili uonekane una hoja
Mungu Wa Mbinguni Kama na Hiyo Miungu Mengine ipo Mbinguni Jenga Hoja Nyengine.
Kila dini mungu wao yuko mbinguni kwa mujibu wao, ukibisha kwamba wa dini nyingine hayuko mbinguni, basi itabidi uthibitishe bila shaka kwamba wa dini yako pekee ndio yuko mbinguni
Bado unaongelea kuzaa katika muktadha wa physical strength yani wewe hoja zako zimebase kwenye physical strength tu huwezi kufikiria wala kujenga hoja nje ya hapo, nguvu ya kuzaa ninayozungumzia hapa ni ile power ya maamuzi aliyonayo mwanamke yani mwanamke ndiye anaamua azae au asizae, na ndio maana watu huwa wanasema kwamba mwanamke kuwa single mother siyo kosa la mwanaume kwa sababu mwanamke ndiye mwenye maamuzi ya kubeba mimba na kuzaa watoto

Kwahivyo ina maana suala la kuleta uhai na kuongeza population duniani liko mikononi mwa wanawake wakikataa itaaffect population na hakuna kitu mnaweza kuwafanya huko ulaya nilisikia wanawake wameanza kugoma kuzaa mpaka imebidi serikali ziingilie kati kuwabembeleza wanawake wazae, kim jong un rais wa north korea pamoja na udikteta wake wote alihutubia taifa kuwaomba wanawake wazae watoto wengi maana birth rate nchini kwake inapungua wanawake wanagoma kuzaa kutokana na namna anavyowatreat wananchi wake, sasa unawezaje kumu underestimate mtu aliyeshikilia uhai na mwenye uwezo wa kuamua population ya dunia iongezeke au ipungue eti kwa kutumia vigezo vya maumbile ya jinsia moja tu

Kwahivyo narudi kwenye swali langu kwamba hapo napo tuseme wanaume ni dhaifu kwa sababu hawana power ya kuamua kuleta viumbe duniani hata kama wanahitaji watoto kwa wakati fulani, ukisema eti kuzaa siyo faida ya mwanaume tu bali ni ya mwanamke pia (maana najua tu lazima utakuja kusema hivi kutokana na namna unavyojenga hoja zako ni rahisi hata mtu kupredict utajibu vipi hoja zake), basi na mimi nitakuambia hata hiyo nguvu na umadhubuti wa mwanaume kufanya mambo magumu ni faida ya mwanaume mwenyewe zaidi kuliko mwanamke kwa sababu hayo hamuwafanyii wake zenu tu
Hapa mbona unajicontradict mwenyewe sasa mara useme tunawatawala wanyama na wanatutii mara useme ukimuona simba unaogopa sasa mtawala gani anaogopa, okay tukirudi kwenye hoja yako wewe ukienda kutalii na wanyama wakakuacha ndio unakuwa umewatawala na wao wanakuwa wamekutii, hapa nazungumzia unapokutana na mnyama face to face na ukampa amri fulani siyo eti umeenda mbugani umejificha ndani ya gari wanyama wakali hawajakuona halafu unasema eti umewatawala nao wamekutii sijui hata kama umeelewa ulichoandika
Jamii iache kuwasimanga kivipi!!! wakati kila Kitu ni Wanawake siku Hizi Ajira wanawake Mikopo Wanawake Viongozi Wanawake Na Tawala zinawapa Kipaumbele na Sauti wanawake Sasa Jamii gani Inayowasimanga Wanawake washindwe Kufanya Mambo Yao??
Tofautisha kati ya jamii na serikali inayowapambania wanawake siku hizi ni serikali ila huku chini kwenye ngazi ya jamii bado wanawake wanakumbana na masimango mengi sana, yani mwanaume na mwanamke wakiachana anayetukanwa ni mwanamke, mwanamke aliyechelewa kuolewa anatukanwa zaidi kuliko mwanaume aliyechelewa kuoa, single mother anatukanwa zaidi kuliko single father, bila kujali nani ndio chanzo na hiyo ni mifano michache tu
Nani Anamtesa Mwanaume katika Jamii?? Mbona Unatunga Mambo. Unachekesha mno . Eti Single Mothers ni kwa Sababu Wanawake wanasimangwa ,,, Mikopo kausha Damu Kisa wanasimangwa Wadangani na Makahaba Kisa wanasimangwa.( Unasikitisha)
Sasa kama wanaume hamteseki kwanini malalamiko mengi kwenye ndoa siku hizi yanatoka kwa wanaume kuliko kwa wanawake, kwanini kwenye mahusiano wanaume ndio wanaongoza kulalamika kuhusu tabia mbovu za wanawake kuliko wanawake wanavyolalamikia tabia mbovu za wanaume, ofcourse kinachowafanya wanawake wawe na pressure ni kwa sababu jamii ndio inawapa hiyo pressure na si kwamba hiyo pressure inatoka ndani yao, na ndio maana kwenye jamii za wazungu ambako wanawake hawapewi hiyo pressure utakuta wanaolewa hadi na miaka 50 bila kujali wana watoto au la, ila huku kwenye jamii za kiafrika mwanamke akifika miaka 30 tu hajaolewa tena akiwa single mother atauona moto wake
Bibi zetu walikuwa na furaha kwa mujibu wa nani kwa uelewa wako ni nini maana ya furaha na ni lini wanawake walikiri wenyewe kwamba wanasikia fahari kuwatii wanaume, halafu ulisema mwenyewe kwamba hakuna mwanaume anayezaliwa na mentality ya kutaka kutawaliwa na mwanamke na kila mwanamke anazaliwa na mentality ya kutaka kumtii mwanaume, halafu sasa hivi unasema eti kuna pure women na manipulated women sasa hao wanawake waliokuwa manipulated walikuwa manipulated na nani in the first place na kwa faida ya nani mbona hoja zako zinakinzana tena
Waliwajibishwa kwa makosa gani usije ukawa unaongelea makosa kama kuiba mke wa mtu yani yale makosa ambayo mwanaume anakuwa kamkosea mwanaume mwenzie zaidi, hakuna mtu aliyekuwa anawawajibisha wanaume kwa kuwakosea wake zao acha kupotosha hapa yani zamani mwanaume awajibishwe kisa kachepuka au kampiga mkewe hebu acha kuandika hisia zako, ndio zamani wanawake walikuwa wanafungiwa ndani kwa maana kwamba majukumu yao yalikuwa ni kazi za nyumbani na shambani tu hawakuruhusiwa kufanya mengine sasa kufungiwa ndani wewe kwa akili yako ndogo umetafsiri kana kwamba mtu hatoki kabisa nje ni nani kasema hayo
Hivi hapo unaona umejibu swali langu kweli yani mimi nimekuuliza kwanini utii wa mwanamke kwa mwanaume uwe ni katika taasisi ya ndoa tu halafu wewe unarudia hicho hicho nilichouliza kisha unasema umejibu, hivi huoni kwamba vigezo ulivyovielezea (nguvu na umadhubuti) vinakinzana na hilo jibu lako la kwamba utii wa mwanamke kwa mwanaume ni katika taasisi ya ndoa tu kwani mwanaume hizo nguvu na umadhubuti anavipata akiwa kwenye ndoa tu, obviously jibu ni hapana sasa kama ni hapana kwanini hizo nguvu na umadhubuti azioneshe kwa mkewe tu kwanini asizioneshe na kwa mama yake na ndugu na jamaa zake wa kike kwani hao siyo wanawake kwanini hizo kazi ngumu anazofanya mwanaume (ambazo hafanyi kwa faida ya mkewe pekee) zisimfanye apewe utii na wanawake wote ambao wanafaidika kutokana na hayo majukumu kwanini apewe utii na mkewe tu
Hili narudia linakinzana na hoja yako ya awali maana ulisema mwenyewe kwamba kila mwanamke anazaliwa na mentality ya kutaka kutawaliwa na mwanaume na hakuna mwanaume anayezaliwa na mentality ya kutaka kutawaliwa na mwanamke sasa hizo fikira chafu zilitoka wapi ni nani alizianzisha na kwa faida ya nani, feminism huwezi kuifananisha na homosexuality kwa sababu homosexuality inalazimishwa ila feminism hailazimishwi huwezi kulinganisha idadi ya feminists na idadi ya homosexuals duniani kote au wewe unadhani idadi ya mashoga duniani ni ipi kulinganisha na wanaume rijali halafu linganisha idadi ya feminists wanawake na wale wanawake ambao bado wanasupport mfumo dume, na nakuhakikishia hao wanawake ambao bado wanasupport mfumo dume ni either hawajaelimika au hawana ajira hivyo wanaona njia pekee ya kupunguza makali ya maisha ni kukubali kuwa chini ya wanaume ili wapate financial security ila ni ngumu kukuta mwanamke aliyeelimika na ana ajira halafu akakubali kuwa chini ya mwanaume na wengi ndio hao wakiingia kwenye mahusiano au ndoa wanaume wanawalalamikia kuwa siyo wife material
Hakuna Utawala uliotambulishwa kimabavu Maisha Yalikuwa yanaenda Smoothly Zamani. Unachanganya kati ya Manipulated women (kama wewe) na Wale pure women (Bibi zetu)
Nimesema hivi na nasisitiza tena kwamba zamani maisha yalikuwa yanaonekana yanaenda smoothly kwa sababu wanawake hawakuwa na sauti ya kujitetea wala uhuru wa kujiamulia mambo, na ndio maana walipopata hivyo vitu na kuanza kusema uhalisia ulioko akilini na mioyoni mwao ndio mnaanza kuona kama wamekengeuka kumbe hizo zilikuwa fikira zao toka zamani ila walikosa tu pa kusemea, wewe sidhani hata kama unaendaga kijijini kwenu kupiga story na bibi zako (kama wapo) ila mimi hadi nyanya zangu walikuwepo (wa mwisho ndio alifariki mwaka juzi), tulikuwa tukienda vijijini kuwasalimia na katika story tulipowauliza walikiri kwamba zamani waliokuwa wanafurahia ndoa ni wanaume, mwanamke aliolewa ili kuenda kumfurahisha mume na siyo kwa ajili ya furaha yake mwenyewe ndio maana ndoa zao zilidumu

Sababu jamii ilimjenga mwanaume kwamba hatakiwi kuvumilia makosa ya mke ila ilimjenga mwanamke kwamba ndio anatakiwa kuvumilia makosa ya mume ndio maana hadi leo kwenye jamii zetu za kiafrika bado kuna kale kaimani kwamba mwanaume akikosea ndoa bado itadumu ila mwanamke akikosea hiyo ndoa haina maisha marefu, kwahiyo ndoa za zamani kudumu haina maana kwamba wote walikuwa na furaha ila wao waliamini kwamba hata mwanaume tu akiwa na furaha (ambayo itasababishwa na tabia njema za mkewe) basi hiyo ni sababu tosha ya ndoa kudumu bila kujali mwanamke naye ana furaha au hana, sababu hata kama mume ana makosa (mfano ulevi, uasherati, ubabe, unyanyasaji, nk) mke atalazimika kuvumilia tu apende asipende kwahiyo mwisho wa siku ndoa itadumu tu

Na zamani suala la mwanamke kuachika lilikuwa linachukuliwa serious sana yani kuachika ilionekana ni fedheha kubwa kwa huyo binti pamoja na familia yake na hata baba wa binti akiwepo na akasikia eti binti yake anarudi nyumbani kisa kaachika atamtimua kama mbwa mwizi, tena baba anasema kabisa kwamba "haiwezekani mimi nile mahari ya watu halafu wewe urudi hapa uniambie umeachika" sasa katika hali kama hiyo, unadhani kuna mwanamke ambaye angethubutu kukubali kuachika kirahisi hata kama haifurahii hiyo ndoa hapo obviously ndoa lazima idumu tu ila huwezi kusema eti hiyo ndoa imedumu kwa sababu mwanamke ana furaha utakuwa mwendawazimu
Inabidi ujue Nature na Scriptures Ni vitu viwili tofauti. Ila vinaweza kutumika Kujengea hoja Moja Ila Haimaanishi Vinafanana Usichanganye vitu.
Mimi naongelea holy scriptures not just any scriptures, watu wengi wananasibisha maandiko ya dini na nature sababu wanaamini hayo maandiko yanatoka kwa mungu mwenyewe, na wanaamini chochote kilichoagizwa na mungu ni nature
Historia inavielezea vitu hivyo hivyo vitatu katika paragraph moja. Ila sijui kama Historia inaelezea Utawala wa wanaume kwa wanawake na Ukoloni katika Paragraph moja. (UNARUKA RUKA MNO)
Ni historia gani inaelezea hivyo vitu katika paragraph moja, hebu ilete hapa na uoneshe uhusiano baina ya hivyo vitu, siyo unaleta porojo zako
Huijui Familia wewe Binti Unaongea Nadharia na Pumba.

Tumeshataja mbona ni ile Nguvu yake Uwezo wake na Umadhubuti wake Sasa unaposema kitu gani cha ziada Unamaanisha huoni kwamba Wanaume wana Nguvu kuliko Wanawake??. (Unafikiri kwa kutumia nini??)
Hili tayari nimeshafafanua
Upo so negative always kwanini usingeegemea katika Sababu zenye Mashiko kama Kuangalia watoto. Kwanini Umerukia sababu zisizo na mashiko kujengea hoja. (Una Matatizo makubwa)
Sasa kama kuangalia watoto ingekuwa ni sababu mbona wanawake wanafanya kazi, basi wasingekuwa wanatoka kabisa kuenda kutafuta pesa ili wakae tu nyumbani kuangalia watoto, yani mwanamke akitoka kuenda kazini hiyo sababu ya kuangalia watoto inakuwa haipo ila akitaka kuenda sehemu nyingine hiyo sababu ndio inaibuka
Ndio Maana nikasema Maisha ya Kifamilia lazima Awepo kiongozi. Na Bibi Zetu waliwatii Babu zetu Na Hakukuwa na Kitu walipungukiwa kwa kuwatii. Ninyi mnaona Tabu Sababu Nyie sio pure women ni Manipulated Women.
Mnajuaje kama bibi zetu hawakupungukiwa na kitu walipokuwa wanawatii babu zetu, yani mtu anashindwa kujiamualia kuhusu maisha yake na kushindwa kufanya baadhi ya mambo hadi apate ruhusa ya mumewe halafu unasema hapungukiwi na kitu, kwanini wanaume mnalazimisha kuwasemea wanawake na kujifanya mnajua kipi kizuri na kipi kibaya kwao kwani wao hawana utashi
Sasa kumbe unajua kwamba baba akiyumba anaweza kupata msaada kama ulivyosema hapo, hivyo basi baba akikwama hakuna haja ya kumtegemea mkewe mwenye kipato kuendesha familia bali atatafuta huo msaada kama ulivyosema kwahiyo hatakuwa na haja ya kumtii mkewe, hiyo ndio hoja yangu au ndio umechanganyikiwa hadi umesahau hii hoja ilianzia wapi
Kuzaa na Kubeba Mimba nishafafanua Ni katika Vitu vinavyohusiana na Physical Weakness ya Mwanamke sasa vipi uvihusishe na Umadhubuti wa mwanaume??(Hoja kituko).
Hili nimeshafafanua tayari
Wewe Ulishapinga maandiko wazi wazi Sasa unalalamika nini?? Wewe umeshakana Imani kwa Mungu ili utete Feminism kama una Imani basi ni Huo u Feminism.
Wewe imani yangu haikuhusu tujadili mada iliyoko hapa nimeshakuambia mimi ukinileta kwenye dini nipo na ukinileta nje ya dini pia nipo, hakuna sehemu ambako nitakwepa hoja yako wewe ndiye ambaye hueleweki unahamahama, unanileta nje ya dini halafu ukiona hoja zimekushinda unaanza kunisingizia kwamba nimeikana dini sasa hilo linahusiana nini
Mimi hakuna sehemu nimekataa mwanaume awe kiongozi ila hoja yangu ni kwamba mwanaume siyo kiongozi kwa vigezo hivyo unavyovisema wewe, bali ni kwa kigezo cha kuhudumia familia yake kiuchumi tu basi nje ya hapo wote wanakuwa sawa, kama lipo hilo andiko kutoka kwenye kitabu cha dini yoyote ile unayoijua wewe linalosema kwamba mwanaume ni kiongozi kwa vigezo vya nguvu na umadhubuti basi liweke hapa

Lakini yapo maandiko kadhaa yanayosisitiza mwanaume kuhudumia familia yake, ila hakuna andiko linalomsisitiza mwanamke hilo jukumu unadhani ni kwanini, tena mwanaume aliambiwa kabisa atakula kwa jasho lake ila hakuna mahali mwanamke ameambiwa atakula kwa jasho lake

Kwahivyo katika mantiki hiyo mnaopinga dini ni ninyi na siyo feminists kwa sababu wanaume mnachagua maandiko, yale mnayoona yanawafavour ninyi ndio mnayafuata ila yale mnayoona hayawafavour mnajifanya kama hamyaoni, lakini cha ajabu mnataka wanawake wafuate maandiko yote na wakijaribu kujitune kulingana na ninyi mlivyo mnaanza kusema wamekana dini what kind of logic is this
Hapa kwanza utuambie hao Wanaume ni kina nani na walikuwa na mchango gani ni lipi lilikuwa jukumu lao??
Hebu nijibu kwanza swali langu kule juu kuhusu hii hoja acha kudandia na kuchomekea maswali yako kwa juu wakati yangu hujanijibu, yani ni kama vile wewe umeshindwa kujibu kwahiyo unajifanya kunigeuzia kuniuliza mimi ili mimi ndio nikupe jibu, hapana safari hii hebu nijibu kwanza mimi maswali niliyotangulia kukuuliza halafu nami ndio nitakujibu yako na kama huna majibu sema kisha ndio uniulize na mimi
Sasa kumbe nilishakudai ushahidi Sasa mbona hujauleta bali umezua lengine. Niletee mimi kwanza ushahidi alafu kisha mimi nije nikufundishe.
Hadi sasa hakuna chochote ulichonifundisha zaidi ya kuona unanipotezea time tu kwa sababu matokeo yake ni mimi sasa ndiye ninayekufundisha, nakuuliza maswali badala ya kunijibu nawe unaniuliza tena na mengine unarudia kunijibu yale yale ambayo nimeshakuambia kwamba siyo majibu sahihi kwa sababu hayana uhalisia ila wewe unalazimisha tujadili hisia zako, siyo siri katika watu wote niliowahi kujadiliana nao humu jf kuhusiana na mada kama hizi wewe ni kati ya watu wenye hoja shallow sana yani hata kutetea hoja zako tu hujui halafu unadai eti unanifundisha wakati mimi naona unanimalizia energy tu kurudiarudia kukuelewesha vitu vile vile
Si anamtii kwa kigezo cha nguvu na umadhubuti, au mwenye hivyo vigezo ni mume wake tu hao wa barabarani ndio hawajamzidi hizo nguvu na umadhubuti, hoja zako ni mufilisi
Kwa mujibu Wetu sisi tuliozikuta Mimi nimeshuhudia ndoa za zamani nyingi zilikuwa na Furaha.
Vigezo ni kuwa hakukuwa na Mashindano na Magomvi Hakukuwa na Talaka mwendokasi hakukuwa na single mothers kama Hivi Sasa Hakukuwa na Mikopo kausha Damu.
Hili tayari nimeshafafanua
Sasaivi ndoa hazina Furaha kama tunavyoshuhudia Talaka mwendokasi,, Single Mom wa kutosha ,, Magomvi na kutunishiana misuli kuliko zidi. Au wewe unapinga haya??
Sasa hivi ndoa zinazokosa furaha ni matokeo ya wanaume kushindwa kukubaliana na hali halisi
Oohh kwahiyo wewe unadhani wanawake wangeweza kukubaliana, na jambo ambalo linawaumiza wao wenyewe maisha yao yote, hivi hilo wewe linakuingia akilini kweli au mwenzetu unatumia nini kufikiri
Faida au hasara ni kwa Mujibu wa Jamii husika wewe unaona ina hasara kwa kuangalia upande wako lakini wao waliona una faida kwa kuangalia Vipengele vyao.
Ndio maana nikasema faida waliyoiangalia ni ya mwanaume ila hawakuangalia upande wa mwanamke hakuna mwanamke aliyekuwa anafurahia kukeketwa, hilo siyo suala mtambuka bali ni suala la uhalisia mwanamke akikeketwa hapati faida yoyote zaidi ya kushindwa kuenjoy tendo la ndoa maisha yake yote, ila wanaume hawakujali hilo wao walichojali ni kwamba mwanamke akikeketwa hachepuki atatulia na mume wake basi
Wanawake kama wewe mliomezeshwa fikra za Ajabu ajabu ndio Ma feminist kwani wapo Wanawake waliosoma na wanawatii waume zao wapo wenye Mamlaka makubwa lakini wanawatii waume zao usi generalize mambo.
Ukiona mwanamke ana hivyo vyote na bado anamtii mume wake basi ujue huyo mwanaume anasimamia majukumu yake yote kama baba, bila kuhitaji msaada wa mke yani mke kusaidia ni aamue mwenyewe tu, vinginevyo hakuna mwanamke atakubali kumtii mwanaume ambaye wanagawana majukumu narudia huyo mwanamke HAYUPO
Hapo mwanzo Hakukuwa na Elimu both kwa wanaume na wanawake ila Wanaume Waliwatawala Wanawake Ila unakuja hapa unatuambia ninyi akili zimefunguka baada ya kusoma Kwaiyo Wanaume wao akili zao zilishafunguka hata bila ya kusoma???
Sasa kumbe hata historia yenyewe huijui vizuri halafu uko hapa unabishana na mimi kuhusu masuala ya historia na unadai eti nikuletee na ushahidi kabisa sasa kwa akili kama hizi hata nikikuletea huo ushahidi utaelewa kweli, si utaendelea tu kubisha mradi usionekane umeshindwa kwahiyo wewe kwa akili yako unadhani elimu ni ile ya kukaa darasani tu na kushika kalamu na vitabu kisha baadaye unakuja kufanya mitihani si ndio, anyway ngoja nikusaidie ewe ngumbaru kuna aina mbili za elimu formal education hiyo niliyoongelea hapo juu na informal education zamani kulikuwa na hiyo informal education pekee, ambayo watu walikuwa wanapewa ujuzi na maarifa mbalimbali ya kuendesha maisha yao ya kila siku au wewe unadhani zamani watu walikuwa wanatibiwaje au bidhaa zilikuwa zinatengenezwaje nk, sasa hiyo hiyo informal education ndio ambayo wanawake walikuwa wananyimwa wao walifundishwa kazi za nyumbani na shambani tu ilihali ujuzi na maarifa mengine ya muhimu wanaume walikuwa wakifundishana wenyewe kwa wenyewe tu
Unachekesha sisi tunaelezea kinachoendelea Haimaanishi kuna kitu Kinatozonga kichwani. Matatizo mengi mnayapata ninyi wanawake. Mwanaume ni Constant na Mwanamke ni dependent Variable utake usitake.
Mnaeleza kinachoendelea wakati kutwa mnalialia na mnalalamika kwamba siku hizi wanawake hawana zile sifa za wife material hivyo mnakosa furaha kwenye ndoa kwa sababu wanawavuruga, unaweza ukaniambia ni wanawake wangapi siku hizi wanalalamika kuhusu tabia zenu mbovu kama kweli wanawake ndio wanaumia mbona mnaoongoza kulalamika ni ninyi sasa, nashindwa hata nianzie wapi kukuelezea hili maana hapa nahisi ndio nitashusha kitabu kabisa nitakuchanganya na utanichosha bure tu kwa sababu naona kama haya masuala wewe yamekuzidi upeo yani wewe bado ni mweupe sana
Bibi zetu walidhibitisha hili. Acha porojo.
Walithibitishaje
Kukeketwa Kuna madhara ambayo yanayoweza kuulezewa kibailogia na Kitabibu naomba nipe madhara atakayoyapata mwanamke akiimtii Mumewe????
Wewe ina maana hujui madhara ya kupangiwa maisha na binadamu kama wewe ilihali wewe mwenyewe una utashi wako au kwako madhara ni yale yanayoonekana kimwili tu, yani huwezi kujiamulia baadhi ya mambo hadi uombe ruhusa kwa mtu mwingine na huyo mtu akikataa basi tena huwezi kulifanya hilo jambo hata kama wewe ulikuwa unaona ni la muhimu kwako, ni sawa hata mtu anapokuwa ameajiriwa kuna baadhi ya mambo hawezi kujiamulia bila ruhusa ya boss wake na kinachofanya akubali hilo ni ule mshahara anaopokea tu na si kingine chochote siku akiukosa huo mshahara hatasikiliza amri yoyote ya boss na kuna uwezekano akaacha kazi
Kwa Sababu Mahusiano yaliyopo baina ya Mke na Mume Sio Sawa na mahusiano na hao watu uliowataja.
Sasa kama hayo mahusiano ni tofauti basi automatically hicho kigezo cha nguvu na umadhubuti kinakataa hapo maana kigezo cha nguvu na umadhubuti hakichagui aina ya mahusiano, kwa sababu mwanaume hawi na hizo nguvu pale anapokuwa kwenye ndoa tu bali siku zote mwanaume yeyote huwa ana nguvu kuliko mwanamke yeyote bila kujali ni nani yake, kwahiyo kwa kuzingatia hicho kigezo chako maana yake ni kwamba mwanamke yeyote yule anatakiwa amtii mwanaume yeyote yule bila kujali ni nani yake wala mahusiano waliyonayo
KIDINI Tunajadili nini wakati wewe ni Mpagani!!!

Tangu ulipoyakataa maandiko sikujengea Hoja tena Maandiko Kwaiyo Kuwa mpole. (Usilalamike)
Sasa kama umeacha kujenga hoja kutimia maandiko mbona bado naona masuala ya sijui feminism ni mpango wa shetani, sijui ili uikubali feminism lazima ukane maandiko sasa hayo yanatokana na nini kama siyo dini, yani wewe bado huelewi unaposimamia unatapatapa tu ukiona huku kumekushinda unahamia huku baadaye unarudi tena hii ni ishara ya kuishiwa hoja
Regardless of what ndo nini!!!! kwani VIGEZO tulivyovizungumza huvioni mbona unaturudisha nyuma kila mara.
Okay nakuuliza hivi, na mwanaume alipoambiwa ampende mkewe aliambiwa ampende kwa kuzingatia vigezo gani, na kwanini aliyeambiwa ampende mwenzie ni mwanaume tu na si mwanamke
Duuh wewe kweli umeishiwa sasa kumbe hoja umeshaielewa ila unabaki kucheza na uandishi wangu na namna nilivyotumia maneno yani hiyo ndio mbinu pekee uliyobaki nayo, unajaza magazeti ili uonekane una hoja kumbe unajificha kwenye minor points huku ukiacha zile key points au ukizitolea majibu ya uwongo yasiyo na uhalisia, by the way kuhusu hiyo hoja nilikuwa nanukuu kulingana na kile kinachoonekana au kinachoaminiwa na si kwamba nilikuwa naunga mkono kuwa ni kweli wanawake walikuwa wanaona ufahari kufuata hizo tamaduni
MSHAHARA SIO HUDUMA ACHA UJINGA. MWANAUME ANAPOTOA HUDUMA NYUMBANI HATOI MSHAHARA KWA MKEWE.
Mshahara ni wajibu na jukumu la muajiri kwa muajiriwa kama ambavyo kulisha familia ni wajibu na jukumu la mume kwa mke, ishu siyo lugha au jina lililotumika kuita aina ya huo wajibu au hilo jukumu, bali ishu ni kwamba hilo ni jambo la lazima halihitaji mjadala wala mashindano
TUMESHAJIBU MAHUSIANO YAO YAPO TOFAUTI. MAHUSIANO YA MTOTO NA MAMA SIO MAHUSIANO YA MKE NA MUME.
Sasa kwani utofauti wa hayo mahusiano, ndio unaondoa nguvu na umadhubuti wa mwanaume, hapa kubali umechemka tu
NIPE USHAHIDI WA HILI.

HAPA UMEONGEA USICHOKIJUA BASI HATA WANAWAKE WANAPOZALIWA NATURALLY WANAKUWA NA UTII HADI WAJE KUMEZESHWA FIKRA MBOVU ZA FEMINISM.
Sasa kama wanawake wote naturally wanazaliwa na utii ni kina nani wanaowamezesha hizo fikira mbovu za feminism
KWANI WEWE UNA IMANI? AU UPAGANI NI IMANI??
Yani kumbe hata hujui maana ya imani, mimi siyo mpagani ila hata upagani nao ni imani, kwa taarifa yako ambacho siyo imani ni atheism tu
Sasa hapa ndio umetetea nini mbona hata huelewi unachokisimamia, umeshasema atamuogopa kwa sababu ya physical appearance kwa maana kwamba kama nyoka asingekuwa anatisha basi asingemuogopa kwahiyo bado uoga wa aina hiyo siyo nature, yani hapo ndio umekuja kuprove sasa point yangu kwamba mwanamke anamuogopa mwanaume kwa sababu tu ya physical appearance yake kwamba anamzidi nguvu na uoga wa aina hiyo siyo nature
Utii ni kwa mujibu wa mahusiano yanayoexist kati yenu.
Hapa pamekushinda kujibu
Sikukuuliza ni kwa Vigezo gani nimekuuliza ni kwa Kitu gani. Yaani anamtii huyo wa barabarani katika jambo gani??
Si katika jambo lolote tu ambalo anaweza akamtuma alifanye au akamkataza asilifanye
Hapa naona umeamua kujitoa ufahamu na kujiropokea hili jibu ili mradi tu utetee uongo wako, wewe umeona wapi wanawake wanaowatii workmates wao wa kiume ambao kivyeo wako sawa, yani wewe unajadili mambo kinadharia na siyo kiuhalisia halafu unanilazimisha nikubaliane na mawazo yako
Ungeacha tu kujisifia kwamba eti unataka kunielimisha maana ndio unazidi kunionesha jinsi gani ulivyo mweupe kichwani, sababu hadi sasa sijaona chochote ulichonifundisha zaidi ya mimi ndio kugeuka mwalimu wako (wewe mwalimu gani muongo hivyo), yani unazidi kudhihirisha uwezo wako mdogo wa kufikiri na kujadili hoja..pathetic!!
 
Hoja imenishinda kivipi!! Wewe Unachanganya Maneno unatoa Hoja alafu unakuja kuvikataa Mwenyewe. Unasikitisha.
Kila dini mungu wao yuko mbinguni kwa mujibu wao, ukibisha kwamba wa dini nyingine hayuko mbinguni, basi itabidi uthibitishe bila shaka kwamba wa dini yako pekee ndio yuko mbinguni
Wahindu Wanamiungu Yao (Ng'ombe) na Wengine (masanamu) kwenye Temples, Wapo Wanaoabudia Moto(Sijui Moto nao upo mbinguni!!),, Wapo Wale Buddha Miungu yao pia ni mfano wa Wahindu,, waafrika tulikuwa na tunaabudia Miti mikubwa na Mizimu kama miungu sijui nayo ipo Mbinguni??.

(Kwanini Unazungumza mambo Usiyoyajua??) .
Sio Kweli Unatudanganya Kuzaa Ni Maamuzi Ya Mwanaume Na Mwanamke Hakuna Anayeweza kulifanikisha Hilo Pekee yake.
na ndio maana watu huwa wanasema kwamba mwanamke kuwa single mother siyo kosa la mwanaume kwa sababu mwanamke ndiye mwenye maamuzi ya kubeba mimba na kuzaa watoto
Mwanamke hawezi kujitungisha Mimba. Unachekesha.
Kwahivyo ina maana suala la kuleta uhai na kuongeza population duniani liko mikononi mwa wanawake wakikataa itaaffect population na hakuna kitu mnaweza kuwafanya
Aisee Unajua unachokiandika kweli?? Wanaume Wasipotoa Mbegu Zao(Sperms) Wasipokubali Kufanya Sexual intercourse na Ninyi Hizo Mimba Mtazitoa wapi??
Mwanzo kabisa Nilikufundisha Kuhusu Maana ya Majukumu ya Kimaumbile kwa Sababu ulikuwa Unachanganya. Sasa Majukumu ya Kimaumbile kila Jinsia Ina Ya Kwake. Ambayo hayawezi kufanywa na Upande wa Pili..
unapozungumzia kuzaa ujue Kuwa hilo Ni Jambo Shirikishi Hakuna Anaweza kulifanikisha Bila Mwengine.
Kwahivyo narudi kwenye swali langu kwamba hapo napo tuseme wanaume ni dhaifu kwa sababu hawana power ya kuamua kuleta viumbe duniani
Unasikitisha Kwani Sperms, Erection ,, Copulation Nani Anahusika??
Mimi Sijafikilia Kujibu Hivi kwa sababu akili Yangu Ni Pana zaidi na Timamu.
basi na mimi nitakuambia hata hiyo nguvu na umadhubuti wa mwanaume kufanya mambo magumu ni faida ya mwanaume mwenyewe zaidi kuliko mwanamke kwa sababu hayo hamuwafanyii wake zenu tu
Sijajua ulikuwa Unajenga Hoja gani hapa. Anyways Nguvu na Umadhubuti na uwezo wa Mwanaume Vinamuwezesha Mwanaume kutekeleza Majukumu yake na Wajibu wake katika Familia kama Kiongozi wa Familia. Bila Shaka Majukumu ya Baba Yanaathari kwa Mama na Kwa Familia kwa ujumla Sasa sijajua Uliposema "ni kwa Faida ya mwanaume mwenyewe zaidi" ulikuwa unamaanisha nini??
Unatetea hoja kinadharia mno. Utawala naozungumzia ni Sisi Kuweza Kuyaendesha(Kuyabadili) maisha yao tukiamua ila wao hawawezi kuja huku na kuyabadilisha maisha yetu katika chochote. Namaanisha Sisi Tunaweza tukaamua Tukawachukue hai Simba na chui nk tukawaweke Zoo ila Simba hawezi kuamua aje akuchukue wewe uende Serengeti. (Legeza nati)
Tofautisha kati ya jamii na serikali inayowapambania wanawake siku hizi ni serikali ila huku chini kwenye ngazi ya jamii bado wanawake wanakumbana na masimango mengi sana
Nani anawasimanga Wanawake na katika lipi??
Naomba kujua Nani anawatukana Hao uliowataja??
Huenda Hawalalamiki ila wanaelezea Situation wanazokumbana nazo kwa waliopata Bahati mbaya kuoa Feminist au Ambae ana Idea za kifeminist.
ofcourse kinachowafanya wanawake wawe na pressure ni kwa sababu jamii ndio inawapa hiyo pressure
Huo ni udhaifu Mwengine,,, utakuwaje na pressure katika Jambo ambalo kwa mtazamo wako Sio Sahihi??
Acha Uongo WAZUNGU siku hizi hawaooani Wanaume Wanaogopa Kuoa Wanaogopa Matatizo ya Talaka.
Bibi zetu walikuwa na furaha kwa mujibu wa nani kwa uelewa wako ni nini maana ya furaha
Furaha ni Hali ya msawazo wa Nafsi na Mwili. Bibi zetu Walikuwa na Furaha kwa namna walivyokuwa wanaishi na Babu zetu na Vile walivyokuwa Wanatulea Sisi pamoja na yale waliyokuwa wanatufundisha.

Kama unakataa hili Njoo na Ushahidi kudhibitisha kinyume( hawakuwa na furaha)
na ni lini wanawake walikiri wenyewe kwamba wanasikia fahari kuwatii wanaume,
Bibi zetu walithibitisha kimatendo na katika mafundisho yao kwa Mabinti Zao (Unyago).
Kama umeona mkinzano wowote hapo nina mashaka na Akili yako.

Manipulated women ni wale mfano wako waliomezeshwa Fikra Za Kwamba You can be better or at least equal to man and Your first enemy is man. Lakini Wapo Wanawake wasio na fikra hizi wao kuwatii Wanaume na Kukubali Kuwa chini ya Mwanaume kwao sio Jambo la Kufanya mjadala kama Huu.
Una ushahidi wa Haya au unaandika tuu kwa Nadharia (Tatizo lako zile Jamii chache ndizo unazozikazania Na unafikiri Jamii ya Mababu zetu walikuwa na Negative things pekee)
ndio zamani wanawake walikuwa wanafungiwa ndani kwa maana kwamba majukumu yao yalikuwa ni kazi za nyumbani na shambani tu
Sio kweli Hii Jamii haikuwepo unatunga Jamii yako. Kulikuwa na Sherehe mbalimbali za kitamaduni Wanawake Walikuwa Wanashiriki Pia Events mbalimbali za kitamaduni. Sasa wewe unaposema "kazi za nyumbani na shambani tuu" Unamaanisha hadi Unyago walikuwa wanafundisha Wanaume au unajua Unyago ni katika kazi za Nyumbani??
hawakuruhusiwa kufanya mengine sasa kufungiwa ndani wewe kwa akili yako ndogo umetafsiri kana kwamba mtu hatoki kabisa nje ni nani kasema hayo
Wewe ndio Mawazo yako hayo Unasikitisha.
Nilishatangulia kusema kuwa Utawala unatokana na Mahusiano yaliyo baina ya pande mbili Mwanaume Hawezi kuwa Kiongozi kwa Dada sijui Mama na Ndugu wa kike Sababu kuna Kiongozi wa Juu Yake Baba wa Familia hiyo ambayo hata na yeye anatakiwa kumtii huyo Kiongozi. Kama Tukiangalia Katika ngazi ya Familia Basi Baba ndio Kiongozi. Katika ngazi ya Jamii nzima mwanaume anastahili kuwa Mtawala kama ilivyokuwa kwa Watemi na Machifu.

Ukiona Jibu langu Halitoshelezi Basi tukuulize wewe kama utii ni kwa sababu ya Huduma Jee Mtoto akiwahudumia Wazazi wake Basi Wazazi wamtii Huyo Mtoto na Mtoto awatawale Wazazi wake??
Kwanza nilekebishe Ufahamu wako. Mwanamke Anazaliwa na Hali ya utegemezi na kutaka kusaidiwa na kusimamiwa Mambo yake lakini Mwanaume anazaliwa akiwa na ile hali ya kujitegemea zaidi na kupenda kusaidia na kuongoza mambo. Na hili ni kutokana na uwezo wake alionao. Hili linamfanya Awe kiongozi katika ngazi yoyote ya Jamii...
feminism huwezi kuifananisha na homosexuality kwa sababu homosexuality inalazimishwa ila feminism hailazimishwi
Feminism hailazimishwi kweli?? Kwani Wanaume wangapi wanapinga Huu Mfumo?? Au ndoa nyingi za wanawake wajuaji kama wewe zinavunjika kwa sababu ya nini?? (Unatudanganya.)
huwezi kulinganisha idadi ya feminists na idadi ya homosexuals duniani kote au wewe unadhani idadi ya mashoga duniani ni ipi kulinganisha na wanaume rijali halafu linganisha idadi ya feminists
Idadi zinafanana na zote zinakua kwa rate moja zikitetewa na kufadhiliwa na Wazungu.
Usitudanganye.. kuna Wanawake wengi tuu wamesoma lakini wanatumia vizuri elimu zao kujenga familia zao bora na sio kuingia vitani na wanaume. Sijui kama wewe una ajira au elimu kumshinda Rais Samia ambae anasema wazi yeye ni mtiifu kwa mwandani wake. (Tofautisha kati ya Manipulated na Educated)
Tangu zamani ya wapi?? Wewe ulishawahi kukaa na Bibi mmoja wa zamani ukamuuliza kuwa alikuwa na Fikra chafu kama zako au Unaaandika Nadharia???
Haya sio ya kweli Hata kidogo. Labda Bibi yako Hayo ni mawazo yake binafsi au kwamba bibi zetu walitofautiana katika kuielezea Ndoa.

Na kama ingekuwa hivyo basi ndoa ingekuwa ni jambo la Kulazimishana na Mabinti wakisikia wanataka kuolewa basi awe anahisi kama anaenda kuzimu lakini hili halikuwepo bali Kila Binti ilikuwa Hamu yake ni Kuolewa na ndio maana nashawishika kuwa maisha ya ndoa za zamani yalikuwa Na furaha.

Ni ngumu kuniaminisha kuwa Binti anakua anaona kwa Jirani Mke anapigwa kila siku sijui manyanyaso alafu atamani kuingia kwenye ndoa (Ajabu)
Hii ni kanuni ya kawaida ya kiutawala Hata Sheria imewekwa kuwa Rais hashitakiwi. Na wewe Ukikosea Rais anaweza kukuhukumu ila wewe huwezi kwenda ikulu ukamuwajibishe Rais. (Labda nikuulize kwanini??)
Solution ni kutatua hizo changamoto za ulevi nk ila sio Kumpamba Mwanamke amuasi Mumewe. Sio uamuzi wa Busara.
Embu Jaribu Kujadili pia Familia Ambazo zilikuwa na Furaha baina ya pande mbili au hazikuwepo??
Mimi naongelea holy scriptures not just any scriptures, watu wengi wananasibisha maandiko ya dini na nature sababu wanaamini hayo maandiko yanatoka kwa mungu mwenyewe, na wanaamini chochote kilichoagizwa na mungu ni nature
Maandiko sio nature Acha kutudanganya hiyo imani umeitoa wapi??

Wewe ulishasema maandiko yameandikwa na watu kama sisi alafu Unajenga hoja kuwa ni nature!!! (Ajabu)
Ni historia gani inaelezea hivyo vitu katika paragraph moja, hebu ilete hapa na uoneshe uhusiano baina ya hivyo vitu, siyo unaleta porojo zako
Nitaeleza.
Kwani Hoja ilikuwa ni nini??? maana naona umehama kabisa (umepata Kauchocholo)
Mnajuaje kama bibi zetu hawakupungukiwa na kitu walipokuwa wanawatii babu zetu, yani mtu anashindwa kujiamualia kuhusu maisha yake na kushindwa kufanya baadhi ya mambo hadi apate ruhusa ya mumewe halafu unasema hapungukiwi na kitu,
Kama anapungukiwa na kitu kitaje.

Alafu kama una mambo yako unataka ujiaamulie Mwenyewe endelea kukaa Single usiolewe,,, ukishaingia kwenye ndoa hiyo ni Taasisi vigezo na masharti kuzingatiwa.
kwanini wanaume mnalazimisha kuwasemea wanawake na kujifanya mnajua kipi kizuri na kipi kibaya kwao kwani wao hawana utashi
Sisi tunasema uhalisia.
Katika wale wa kumpa msaada nilimuweka mkewe pia sijui ulimuona??
Mbona mimi nilishasema kuwa Tangu ulipoyakana maandiko nikaacha kuyatumia au uliona tena natumia Maandiko kujengea hoja??
Mimi hakuna sehemu nimekataa mwanaume awe kiongozi
Hongera. Umeanza kuelewa.
ila hoja yangu ni kwamba mwanaume siyo kiongozi kwa vigezo hivyo unavyovisema wewe, bali ni kwa kigezo cha kuhudumia familia yake kiuchumi tu basi nje ya hapo wote wanakuwa sawa,
Mwanaume na Mwanamke hawawezi kuwa Sawa Hata iweje.

Pili Kigezo chako Kinalazimisha Mwanaume amtii mkewe kama ikitokea Mwanamke ndio anahudumia Familia na Sisi ndio tunakataa hili.
kama lipo hilo andiko kutoka kwenye kitabu cha dini yoyote ile unayoijua wewe linalosema kwamba mwanaume ni kiongozi kwa vigezo vya nguvu na umadhubuti basi liweke hapa
Sitaki kutumia Maandiko tena wewe ulishayakana maandiko unanilazimisha mbona!!!!.
Kwani wewe unayaamini maandiko!!! sasa mbona unayajengea hoja???
Kwani wewe si ndio ulisema maandiko yameandikwa na binadamu kama sisi tuu Sasa Wewe si ndio ulikana Dini?? Unatubadilika tena??

Mind you sisi hatukatai uwajibu wa mwanaume kuhudumia Familia yake Na tunahimiza hilo ila Utiifu wa Mwanamke kwa Mumewe Haujajengwa katika huduma Hili ndio Hatulitaki sisi.
Aliyeanza kumuuliza mwenzie nani??
Malalamiko.
Si anamtii kwa kigezo cha nguvu na umadhubuti, au mwenye hivyo vigezo ni mume wake tu hao wa barabarani ndio hawajamzidi hizo nguvu na umadhubuti, hoja zako ni mufilisi
Hahaha malalamiko makubwa.
Hili tayari nimeshafafanua

Sasa hivi ndoa zinazokosa furaha ni matokeo ya wanaume kushindwa kukubaliana na hali halisi
Hata huko ulaya ulipoanza huu ufeminism ndoa hazina furaha na Pia talaka ni nyingi na In short msingi wa Familia umeshapolomoka unalizungumziaje hili??
Oohh kwahiyo wewe unadhani wanawake wangeweza kukubaliana, na jambo ambalo linawaumiza wao wenyewe maisha yao yote, hivi hilo wewe linakuingia akilini kweli au mwenzetu unatumia nini kufikiri
Jenga hoja.
Kwanza tukuulize kama hekima ni mwanamke kutochepuka jee Hilo ni manufaa kwa mwanaume pekee. Jee Kuchepuka kwa mwanamke ni sahihi au ndio kuna manufaa na mwanamke??

Pili hata tohara ya wanaume nayo inapunguza Radha ya tendo pia ni jambo lenye maumivu unalizungumziaje hili??

Mind you kuna kampeni ndogo Ndogo zimeanza kupinga Tohara ya wanaume kama ilivyo kwa wanawake.
Wapo Wengi mno Bi Jadda nahisi umezungukwa na Feminist wenzako pekee hujawahi Kuyaona maisha kinyume na Ya Ki Feminism.
Unatudanganya Mi nachojua ukizungumza Informal Education ni Jando(Kwa wanaume )na Unyago(kwa wanawake)

(Umefirisika)
Malalamiko.

Sasa mbona unauliza swali alafu unajibu mwenyewe. Kwani Boss wako akiwa anakupangia cha kufanya na kutofanya wewe unapata madhara gani??. U Feminism ni Ujinga.
Nasisitiza Katika ngazi ya Familia Baba ndio kiongozi na katika ngazi ya Jamii basi mwanaume ndio kiongozi (mtawala) Sasa sisi Wanaume sio vichaa kwamba nikukute barabarani nianze kuonesha umwamba sijui nikuamrishe. Yaani unazungumza mambo hayapo kabisa.
Wewe uiniuliza Uhusiano uliopo mimi nimejibu unalalamika tena!!!
Okay nakuuliza hivi, na mwanaume alipoambiwa ampende mkewe aliambiwa ampende kwa kuzingatia vigezo gani, na kwanini aliyeambiwa ampende mwenzie ni mwanaume tu na si mwanamke
Ampende kwa Sababu Yeye ni ubavu wake.
Unakimbia kimbia tuu Siku nyengine usitumie Kuchukia na kuona fahari Sehemu moja Sawa??
Sawa ila Siku nyengine usirudie kusema Mshahara ni Huduma sawa??
Sasa kwani utofauti wa hayo mahusiano, ndio unaondoa nguvu na umadhubuti wa mwanaume, hapa kubali umechemka tu
Nimejibu huko juu.
Sasa kama wanawake wote naturally wanazaliwa na utii ni kina nani wanaowamezesha hizo fikira mbovu za feminism
Walioanzisha u Feminism.
Yani kumbe hata hujui maana ya imani, mimi siyo mpagani ila hata upagani nao ni imani, kwa taarifa yako ambacho siyo imani ni atheism tu
Kwani Atheism ni nini na UPAGANI ni nini??
Sasa hapa ndio umetetea nini mbona hata huelewi unachokisimamia, umeshasema atamuogopa kwa sababu ya physical appearance kwa maana kwamba kama nyoka asingekuwa anatisha basi asingemuogopa kwahiyo bado uoga wa aina hiyo siyo nature,
Physical appearance sio nature??
yani hapo ndio umekuja kuprove sasa point yangu kwamba mwanamke anamuogopa mwanaume kwa sababu tu ya physical appearance yake kwamba anamzidi nguvu na uoga wa aina hiyo siyo nature
Kwani Physical appearance sio Nature??? Naomba jibu.
Hapa pamekushinda kujibu

Si katika jambo lolote tu ambalo anaweza akamtuma alifanye au akamkataza asilifanye
Sasa huo si ukichaa umkute mtu barabara umuamlishe au umkataze vitu!!!!. Nadharia zako zinachekesha.
Jambo ni Gumu kwa Feminist ila ni Jepesi kwa wanawake(pure)
Malalamiko.
 
Hoja imenishinda kivipi!! Wewe Unachanganya Maneno unatoa Hoja alafu unakuja kuvikataa Mwenyewe. Unasikitisha.
Yani wewe unashindwa kuelewa hoja kwa sababu akili yako ni ndogo halafu unakuja kusema eti mimi ndio nimechanganya maneno, hebu kuwa serious acha kujaza magazeti for nothing halafu kabla hujajibu comment fulani soma kwanza aya nzima uielewe ndio ujibu acha kusoma na kujibu vipande vipande, maana naona unakuwa unakimbilia kujibu hoja ambayo nimeshaifafanua chini yake yani unauliza kitu ambacho jibu lake liko chini yake halafu unanipa kazi ya kujibu tena
Oohh kwahiyo maana yake kila dini inayoabudu sanamu basi mungu wao hayuko mbinguni, kwamba hata waroma mungu wao hayuko mbinguni kwa sababu wanaabudu sanamu la yesu, wewe ndio unazungumza usiyoyajua nimekuambia thibitisha kwamba mungu wa dini yako pekee ndiye ambaye yuko mbinguni
Hivi hebu nikuulize generally kati ya mwanaume na mwanamke ni nani anayependa kuwa na watoto wengi zaidi, najua hapa utajifanya kuzunguka sababu unajua ukitoa jibu sahihi utajifunga lakini ukweli unajulikana jibu ni mwanaume siyo rahisi mwanamke kutamani kuzaa watoto wengi, hakuna mwanaume ambaye hataki watoto haijalishi hali yake ya kiuchumi (ndio maana hata masikini wana watoto) ila mwanamke kuzaa ni hadi ajione yupo tayari kwa wakati husika

Kwenye ndoa mfano mwanaume anaweza kuhitaji watoto watano ila mke anahitaji watatu tu je unadhani mwanaume atamlazimisha huyo mwanamke kuzaa watoto watano, hawezi sana sana ataenda kutafuta mwanamke mwingine (mchepuko) amuombe amzalie hao wengine ndio nakuuliza sasa je ina maana hapo mwanaume anakuwa dhaifu kwa sababu mwanamke ndio kaamua idadi ya watoto, ndio maana nikakupa huo mfano kuwa hata leo hii population inavyokuwa kwa kasi ndogo wanaobebembelezwa kuzaa ni wanawake kwanini hao viongozi huko ulaya wasingebembeleza na wanaume kwanini wanawabembeleza wanawake tu

Ni kwa sababu wanajua mwanaume hawezi kukataa kuzaa na wala hawezi kukataa sexual intercourse yani mwanaume hata akiwa kataa ndoa bado atatafuta walau mwanamke wa kumzalia watoto ili aendeleze kizazi chake, kwahiyo bado hoja yangu iko pale pale kwamba hata kama mwanaume anataka watoto ila mwanamke akikataa kuzaa kwa wakati huo basi huyo mwanaume hatapata hao watoto kwa wakati anaoutaka, ila mwanamke yeye muda wowote akitaka watoto ila mwanaume hataki anaweza hata akajitegesha akapata mimba akazaa kwahiyo maamuzi ya kuzaa yapo mikononi mwa mwanamke
Yani unafananisha kuchangia mbegu na kubeba mimba, kuzaa na kunyonyesha, kama hayo yangekuwa yanafanana unadhani ni kwanini watoto wanaambiwa wawapende zaidi mama zao, kwanini wasiambiwe wawapende na baba zao sababu wamechangia mbegu, mambo mengine mbona yako wazi tu hata hayahitaji mtu apoteze muda wake kuyafafanua ndio maana nasema wewe una upeo mdogo sana
Oohh kwahiyo mwanamke anapozaa haina athari au faida kwa mwanaume na familia kwa ujumla, yani majukumu ya mwanaume tu ndio yenye faida ila ya mwanamke hayana faida, nilimaanisha hayo majukumu anayofanya mwanaume hayamfaidishi mke pekee bali yeye mwenyewe kwanza
Hivi unaelewa hata unachotetea kweli sasa ukishamuweka mnyama zoo si maana yake atakutii kwa sababu unamhudumia na yuko chini ya uangalizi wako lakini si kwamba umemzidi nguvu, wewe ndio ulegeze nati mimi naongelea generally katika mazingira ambayo kila mtu yuko kivyake yani huyo mnyama hakujui wala hakutegemei kwa chochote unadhani atakutii, halafu naona unakuwa too specific unaongelea wale wanyama ambao wanaweza kufugwa kwanini usiongelee in general maana kuna wanyama huwezi kuwaweka kwenye zoo mfano kifaru, kiboko, tembo, mbwa mwitu, nk
Nani anawasimanga Wanawake na katika lipi??

Naomba kujua Nani anawatukana Hao uliowataja??
Sasa si nimeshafafanua kwamba ni wanaume, halafu unaniuliza tena ni kina nani, aloo we jamaa mbona una kichwa kigumu sana
Huenda Hawalalamiki ila wanaelezea Situation wanazokumbana nazo kwa waliopata Bahati mbaya kuoa Feminist au Ambae ana Idea za kifeminist.
Hoja siyo kulalamika bali hoja ni kwamba hawana furaha kwenye hizo ndoa, sasa kuelezea situations wanazokumbana nazo ndio inawafanya wasiwe wanalalamika au, kitendo cha kuvoice out hizo situations ndio malalamiko yenyewe hayo kitu ambacho miaka hii wanawake wamekipunguza sana
Huo ni udhaifu Mwengine,,, utakuwaje na pressure katika Jambo ambalo kwa mtazamo wako Sio Sahihi??
Hivi wewe unaijua hata saikolojia ya binadamu inavyofanya kazi kweli mbona unaongea nadharia sana, unajua namna masimango kwa mtu juu ya jambo fulani yanavyoweza kupelekea hata huyo mtu kujiua kwa kujiona hafai katika jamii hata kama si kweli, hao wanawake wangekuwa kweli wanazipenda hizo ndoa kutoka mioyoni mwao si wangezipigania ili zidumu mbona sasa nyingi zinavunjika huku wanaume wakidai kwamba wanawake ndio chanzo
Acha Uongo WAZUNGU siku hizi hawaooani Wanaume Wanaogopa Kuoa Wanaogopa Matatizo ya Talaka.
Wewe ndio uache uongo una takwimu zozote zinazoonesha kwamba siku hizi wazungu hawaoani kabisa, again unaongea nadharia na mawazo yako tu duniani kote kila siku ndoa zinafungwa na hazitaacha kufungwa, usipende kufanya hasty generalizations siyo wote wanaoogopa hayo matatizo ya talaka
Furaha ni Hali ya msawazo wa Nafsi na Mwili. Bibi zetu Walikuwa na Furaha kwa namna walivyokuwa wanaishi na Babu zetu na Vile walivyokuwa Wanatulea Sisi pamoja na yale waliyokuwa wanatufundisha.
Hili halithibitishi furaha ya bibi zetu, sana sana unataka tu nirudie kueleza kile kile nilichotoka kueleza, hili silirudii tena mpaka utakapokuja na hoja ya maana iliyojitosheleza
Kama unakataa hili Njoo na Ushahidi kudhibitisha kinyume( hawakuwa na furaha)
Niliishathibitisha
Bibi zetu walithibitisha kimatendo na katika mafundisho yao kwa Mabinti Zao (Unyago).
Hizo tamaduni hawakuzitunga wao wanawake
Hapo hujajibu swali langu nimekuuliza hivi waliowamanipulate hao wanawake ni kina nani na waliwamanipulate kwa faida ya nani, maana ulisema kwamba wanawake wote wanazaliwa na fikira za kutaka kutawaliwa na wanaume na hakuna mwanaume anayezaliwa na fikira za kutaka kutawaliwa na mwanamke, sasa kwa mujibu wako feminism ilitoka wapi ilianzishwa na nani na kwa faida ya nani jibu hili
Una ushahidi wa Haya au unaandika tuu kwa Nadharia (Tatizo lako zile Jamii chache ndizo unazozikazania Na unafikiri Jamii ya Mababu zetu walikuwa na Negative things pekee)
Nani kakudanganya kwamba ni jamii chache ndio zilikuwa na negative things huo ndio ulikuwa utamaduni wa karibu jamii zote, by the way hata kwenye dunia ya leo iliyojaa feminism bado kuna ndoa nyingi tu zina furaha sasa wewe kwanini unaongelea zile zenye migogoro tu, ukipata jibu basi utaelewa kwanini na mimi naongelea jamii za kizamani katika negativities tu
Sasa kwani unyago na hizo sherehe nyingine zilikuwa zinawafundisha nini cha maana wanawake zaidi ya namna ya kuwa watumwa kwa waume zao, yani hoja ni kwamba tukio lolote walilokuwa wanashiriki wanawake kwa asilimia kubwa lazima liwe linahusu mambo ya nyumbani tu hawakucheza mbali na hapo, hakuna mwanamke aliyekuwa anaruhusiwa kufanya shughuli ambazo hazihusiani na mambo ya nyumbani hebu acha kukaza hilo fuvu
Sasa hapo ndio umetetea nini kwani baba akiwa kiongozi ndio inamuondolea kaka uanaume wake, kwani ndio inamuondolea kaka hicho kigezo cha nguvu na umadhubuti ambacho unasema ndio kigezo cha mwanaume kumtawala mwanamke haya vipi baba akifariki je, kwahiyo wewe unadhani hao viongozi walikuwa wanapewa utii kwa sababu tu ni wanaume haya vipi kama kiongozi ni mwanamke huwa wanamtii kwa sababu gani
Ukiona Jibu langu Halitoshelezi Basi tukuulize wewe kama utii ni kwa sababu ya Huduma Jee Mtoto akiwahudumia Wazazi wake Basi Wazazi wamtii Huyo Mtoto na Mtoto awatawale Wazazi wake??
Nilishakuambia utii wa mtoto kwa mzazi umejengwa katika msingi wa mzazi kumzaa na kumlea huyo mtoto hicho kigezo cha kuzaa ndio chenye nguvu kisha ndio vinafuata hivyo vingine, sasa kwani mtoto akijitegemea na anapowahudumia wazazi wake ndio anakuwa amewazaa kwanini umetupilia mbali hicho kigezo cha kumzaa, ndio maana nikakuuliza ukitoa huduma za kiuchumi msingi wa mwanaume kumtawala mwanamke ni upi wewe unaniletea habari za nguvu na umadhubuti kana kwamba mwenye hivyo vigezo ni mume wa ndoa tu
Mwanamke anazaliwa na hali ya utegemezi na kutaka kusaidiwa katika yale majukumu ya kimaumbile, yani wewe bado unaongelea majukumu ya kimaumbile ambayo mwanamke hawezi kuyafanya lakini unasahau kwamba, hata mwanaume kuna majukumu hawezi kufanya mfano kazi za nyumbani pamoja na malezi ya watoto kwahiyo hapo napo tuseme mwanaume anasaidiwa na mwanamke
Feminism hailazimishwi kweli?? Kwani Wanaume wangapi wanapinga Huu Mfumo?? Au ndoa nyingi za wanawake wajuaji kama wewe zinavunjika kwa sababu ya nini?? (Unatudanganya.)
Sasa kwani hapa tunaongelea supporters wa hizo agenda au tunaongelea wahusika, yani kitendo cha wanawake wengi kuikubali feminism na kuwa feminists ni jibu tosha kwamba hailazimishwi, wanaume wengi lazima waipinge kwa sababu haiko upande wao mind you hapa tunaongelea suala la wanawake kuzaliwa na utii kwa wanaume ni nature au siyo nature
Idadi zinafanana na zote zinakua kwa rate moja zikitetewa na kufadhiliwa na Wazungu.
Yani kwahiyo agenda ikitetewa na wazungu basi ukuaji wake ndio unakuwa wa rate moja hivi we jamaa unaelewa unachoandika kweli, kwa taarifa yako idadi ya mashoga haifikii hata nusu ya idadi ya wanaume rijali duniani kote uwe unafanya research kabla ya kuropoka, mnajazana ujinga eti oo wanaume tumeisha sijui nini wakati population ratio duniani inawaumbua na hizo propaganda zenu
Duuh kwahiyo kwa akili yako wewe ulitaka mama Samia awaambie mabinti wawe wajeuri kwa waume zao hata kama yeye yuko hivyo, by the way kwani yeye ndio kielelezo cha namna wanawake wote duniani wanavyotakiwa kuwa, halafu usilolijua ni sawa na usiku wa giza ngoja nikuache kwa sababu unaweza kuwa hufahamu vitu ambavyo mimi navifahamu kwahiyo huo mfano wako kwangu mimi ni UONGO..tuishie hapa!!
Hakuna cha mawazo yake binafsi yeye alielezea hali halisi iliyokuwepo kwa wanawake wengi wa enzi zao kwani unadhani bibi zetu walikuwa hawakutani kusimuliana baadhi ya mambo yao, na aliyeongea hayo siyo bibi yangu tu nina marafiki pia ambao wameshawahi kuambiwa hayo na bibi zao ndio maana nilikuuliza wewe huwa unaongea na bibi zako kweli (najua hapa unaweza kutunga lolote mradi tu utetee uongo wako), anyway pengine huwa wanashindwa kuwaeleza wajukuu zao wa kiume sababu wanahisi wanaume wote lenu moja hivyo hamtawaelewa kwahiyo labda wanaamua kuwaeleza wajukuu zao wa kike tu
Hivi kwanini unanilazimisha nikae narudiarudia kuelezea yale yale kila wakati hilo si nimeshalielezea kwamba zamani mwanamke kutokuolewa au kuachika ilichukuliwa kama ni laana na fedheha kubwa kwake na kwa wazazi wake sasa kwa hali hiyo kuna mwanamke angekataa kuolewa, vipigo na manyanyaso haikuwahi kuwa sababu ya kumfanya mwanamke asiolewe maana waliambiwa wavumilie sasa kama miaka hii tu kuna wanawake wengi wanafanyiwa hayo na wanavumilia sembuse zamani na ukizingatia wengi walivumilia kwa sababu tu mwanamke akiachika hana pa kwenda na mara nyingi huachwa na watoto hivyo wanawake walivumilia ili kuepuka hili, okay labda nikuulize na wewe si ulisema kwamba ndoa za siku hizi hazina furaha kwa sababu ya feminism kutake over sasa mbona bado wanaume wanaendelea kuoa kila kukicha pamoja na kuzijua tabia za wanawake wa siku hizi ina maana wanaume hawapendi kupata furaha
Hii ni kanuni ya kawaida ya kiutawala Hata Sheria imewekwa kuwa Rais hashitakiwi. Na wewe Ukikosea Rais anaweza kukuhukumu ila wewe huwezi kwenda ikulu ukamuwajibishe Rais. (Labda nikuulize kwanini??)
Okay kwahiyo unataka kusema watu wanafurahia hicho kitendo cha kushindwa kumshitaki rais akikosea, maana hapa hoja ni kwamba je huyo mtawaliwa anafurahia huo utawala au la, hizo ni sheria walizojiwekea wenyewe hao viongozi hawakukubaliana na wananchi wote hivyo huwezi kusema wananchi wanafurahia hilo
Solution ni kutatua hizo changamoto za ulevi nk ila sio Kumpamba Mwanamke amuasi Mumewe. Sio uamuzi wa Busara.
Sasa wa kutafuta hiyo solution alikuwa nani yani mwanamke ndio atafute solution ya tabia mbovu za mwanaume, au wanaume ambao karibu wote walikuwa na tabia hizo hizo ndio wangetafuta solution ya hizo tabia zao, unachekesha kweli hivi mbona umejaza nadharia nyingi sana humo kwenye kichwa chako kuhusu maisha ya zamani, watu tunaongea uhalisia wewe unaleta nadharia, ujue hapa tunaongelea maisha halisi yaliyokuwepo hatuchambui riwaya wala mashairi
Embu Jaribu Kujadili pia Familia Ambazo zilikuwa na Furaha baina ya pande mbili au hazikuwepo??
Wewe mbona haujadili ndoa zilizo na furaha katika era hii ya feminism unajadili kama kwamba zote zina migogoro tu, by the way mimi hapa naongelea in general ila haimaanishi kwamba hakukuwa na few exceptions za ndoa zenye furaha, ila zile zisizo na furaha ndio zilikuwa nyingi kwa sababu wanaume wengi walikuwa na tabia zinazofanana ambazo wao waliona ndio uanaume ilihali kwa wanawake zilikuwa ni mateso
Maandiko sio nature Acha kutudanganya hiyo imani umeitoa wapi??

Wewe ulishasema maandiko yameandikwa na watu kama sisi alafu Unajenga hoja kuwa ni nature!!! (Ajabu)
Dooh wewe nashindwa hata nikuelezeeje maana your level of dumbness is out of proportion, nimesema kwamba watu wa dini wanaamini kuwa maandiko ya kwenye vitabu vya dini zao ni nature kwa sababu yametoka kwa miungu yao, sasa wewe unanishutumu mimi kana kwamba mimi ndio naamini hivyo wakati mimi napinga imani ya aina hiyo
Nitaeleza.
Nasubiri
Kwani Hoja ilikuwa ni nini??? maana naona umehama kabisa (umepata Kauchocholo)

Kama anapungukiwa na kitu kitaje.
Anapungukiwa na uhuru wa kufanya baadhi ya vitu
Alafu kama una mambo yako unataka ujiaamulie Mwenyewe endelea kukaa Single usiolewe,,, ukishaingia kwenye ndoa hiyo ni Taasisi vigezo na masharti kuzingatiwa.
Vigezo na masharti vinatakiwa viwe ni kwa makubaliano na maslahi ya pande zote mbili, na siyo upande mmoja unajiamulia vigezo na masharti vinavyompendelea yeye kisha unataka upande wa pili ukubali tu bila kuhoji, hiyo ni taasisi ya kihuni hakuna taasisi ya namna hiyo
Sisi tunasema uhalisia.

Katika wale wa kumpa msaada nilimuweka mkewe pia sijui ulimuona??
Sasa ndio asimtegemee mkewe kwa asilimia mia akatafute msaada na huko kwingine ulikosema, mwanaume kukwama au kufilisika siyo excuse ya kuyaacha majukumu yake, vinginevyo awe tayari kukabidhi na nafasi yake maana ni wazi imemshinda
Mbona mimi nilishasema kuwa Tangu ulipoyakana maandiko nikaacha kuyatumia au uliona tena natumia Maandiko kujengea hoja??

Hongera. Umeanza kuelewa.

Mwanaume na Mwanamke hawawezi kuwa Sawa Hata iweje.
Kwenye majukumu ya kimaumbile ndio hawawezi kuwa sawa, ila kwenye mambo mengine imekuwa proven kuwa wanaweza, na utofauti wa kimaumbile siyo justification ya kuweka utofauti kwenye kila kitu
Pili Kigezo chako Kinalazimisha Mwanaume amtii mkewe kama ikitokea Mwanamke ndio anahudumia Familia na Sisi ndio tunakataa hili.
Sasa kama hamtaki kuwatii wanawake si ndio mhakikishe mnatafuta kwa nguvu na bidii zote ili isifikie hatua ya wanawake kuwasaidia majukumu yenu
Ni wapi nilipokana dini hebu nioneshe nasisitiza nioneshe usiniletee mawazo yako
Mind you sisi hatukatai uwajibu wa mwanaume kuhudumia Familia yake Na tunahimiza hilo ila Utiifu wa Mwanamke kwa Mumewe Haujajengwa katika huduma Hili ndio Hatulitaki sisi.
Sasa tofauti na hilo umejengwa katika nini nimeshakuambia kigezo cha nguvu na umadhubuti kinakataa hapo hivyo usikilazimishe, kwa sababu itabidi kila mwanaume awe na uwezo wa kumtawala kila mwanamke bila kujali ni nani yake, na vivyo hivyo kila mwanamke awe na wajibu wa kumtii kila mwanaume bila kujali ni nani yake sijui kwanini huoni hili tatizo kwenye hiyo hoja yako
Aliyeanza kumuuliza mwenzie nani??
Jibu maswali wacha kurukaruka
Malalamiko.

Hahaha malalamiko makubwa.
Sababu huwezi kujibu
Hata huko ulaya ulipoanza huu ufeminism ndoa hazina furaha na Pia talaka ni nyingi na In short msingi wa Familia umeshapolomoka unalizungumziaje hili??
Sasa kama kweli hali ingekuwa mbaya kiasi hicho mbona wanaume bado wanaendelea kuoa, ina maana wanaume hawapendi kupata furaha si waache kuoa basi ili tujue kwamba kweli hawazipendi hizi tabia za wanawake, kwanini kila siku bado wanaendelea kujiingiza kwenye jambo ambalo wanajua litaenda kuwanyima furaha
Jenga hoja.

Kwanza tukuulize kama hekima ni mwanamke kutochepuka jee Hilo ni manufaa kwa mwanaume pekee. Jee Kuchepuka kwa mwanamke ni sahihi au ndio kuna manufaa na mwanamke??
Sasa kama wanaume hawakutaka wake zao wachepuke si wangeoa wake wachache wanaoweza kuwamudu kuna haja gani ya kuoa wake wengi ambao unajua huwezi kuwatosheleza, na badala yake unaenda kuwatesa kwa kuwakeketa sasa hapo ujinga ni wa nani, yani hoja ni kwamba kwanini umtese mtu mwingine kwa sababu tu ya ubinafsi wako halafu uje useme eti anafurahia hayo mateso
Pili hata tohara ya wanaume nayo inapunguza Radha ya tendo pia ni jambo lenye maumivu unalizungumziaje hili??
Hili ndio kwanza nalisikia kwao naona umeamua kuwa daktari uchwara sasa
Mind you kuna kampeni ndogo Ndogo zimeanza kupinga Tohara ya wanaume kama ilivyo kwa wanawake.
Hizo kampeni zimeanzishwa na kina nani na je kwani tohara kwa wanaume ilianzishwa na wanawake si walianzisha wanaume wenyewe, kwamba wanaume walianzisha tohara kwa faida ya wanawake ndicho unachotaka kusema, hiyo ni tofauti na ukeketaji kwa sababu ukeketaji haukuanzishwa na wanawake bali ni tamaduni zilizowekwa na wanaume kisha wanawake wakalazimika kuzifuata tu
Wapo Wengi mno Bi Jadda nahisi umezungukwa na Feminist wenzako pekee hujawahi Kuyaona maisha kinyume na Ya Ki Feminism.
Mimi siishi ulaya niko hapa hapa afrika ambako bado kuna masalia ya wanawake wanaounga mkono mfumo dume na wengi ni either hawana elimu au ajira narudia hakuna mwanamke mwenye hivyo vyote atakubali kuwa chini ya mwanaume kubali ukatae, ukitaka kuendelea kukaza kichwa na kujifariji sawa maana hiki ndicho wanaume mlichobaki kufanya kwa sasa mnajifariji na mnadanganyana kwamba wanawake wazuri na wema bado wapo wengi sana, kumbe huku kwa ground mambo ni tofauti matokeo yake mnaoa chui waliojificha kwenye ngozi za kondoo halafu baadaye mnakuja kutupigia makelele humu oo kataa ndoa ni utapeli mara oo wanawake hivi wanawake vile kumbe mnajenga matarajio makubwa halafu mkija kukutana na hali halisi mnachanganyikiwa
Unatudanganya Mi nachojua ukizungumza Informal Education ni Jando(Kwa wanaume )na Unyago(kwa wanawake)

(Umefirisika)
Dooh kwahiyo na jamii ambazo hazikuwa na jando na unyago maana yake hazikuwa na informal education, asee hebu vitu vingine jaribu hata kuenda google basi ikusaidie ili usiwe unaumbuka kama hivi, halafu unakazia kabisa eti "mi nachojua" sasa hapa hatujadili wewe unachojua bali tunajadili uhalisia kwa sababu kwanza haujui na kwa bahati mbaya hautaki kukubali kwamba haujui
Malalamiko.


Sasa mbona unauliza swali alafu unajibu mwenyewe. Kwani Boss wako akiwa anakupangia cha kufanya na kutofanya wewe unapata madhara gani??. U Feminism ni Ujinga.
Ndio maana nikakuambia kitakachokufanya ukubali boss wako akupangie ni mshahara na siyo kile cheo chake, ndio maana boss asipokulipa mshahara unaanza kuona ugumu na uzito kumtii tena na unaweza hata ukaacha hiyo kazi, feminism siyo ujinga bali ni matokeo ya wanawake waliokataa utumwa uliojificha kwenye mwamvuli wa mfumo dume
Ndio kwani mwanaume akimkuta mwanamke barabarani hawezi kumuagiza mahali mfano dukani na hiyo ya barabarani ni mfano tu ila hoja yangu ni kwamba kwa kuzingatia kigezo cha nguvu na umadhubuti basi mwanaume yeyote anaweza kumtawala mwanamke yeyote akiamua bila kujali ni nani yake
Wewe uiniuliza Uhusiano uliopo mimi nimejibu unalalamika tena!!!
Sasa ulishindwa kuleta uhusiano uliopo kwa kujenga hoja nje ya dini, na ndio maana nikakuambia wewe unahamahama ukiona huku huna hoja unahamia upande mwingine, haya kwa vile umesema hutahusianisha tena na dini basi lete uhusiano uliopo nje ya dini
Ampende kwa Sababu Yeye ni ubavu wake.
Okay kwahiyo hata kama huyo mwanamke hatimizi majukumu yake na ni mjeuri bado mumewe ataendelea kumpenda tu siyo
Unakimbia kimbia tuu Siku nyengine usitumie Kuchukia na kuona fahari Sehemu moja Sawa??
Hoja zinakupiga chenga unatafuta visingizio, hadi sasa wewe ndio uliyekimbia hoja zangu nyingi yani umeziacha tu juu kwa juu, sasa naona umejishitukia unaamua kutumia mbinu nyingine ya kujifanya kwamba mimi natumia maneno yasiyo sahihi ili uzipotezee hoja zangu kiujanja
Sawa ila Siku nyengine usirudie kusema Mshahara ni Huduma sawa??
Hapo napo unafanya kile kile
Nimejibu huko juu.

Walioanzisha u Feminism.
Kina nani jibu
Kwani Atheism ni nini na UPAGANI ni nini??
Si unaona sasa kumbe hata hujui kutofautisha kati ya atheism na paganism kazi kuropoka na kubwabwaja tu, atheism ni kuikana miungu yani unakuwa huamini kama kuna any supernatural being aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ila paganism ni kutokuamini dini yoyote yani unakuwa unaamini kwamba kuna supernatural being aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo ila unaamini hayuko kama dini zinavyomuongelea
Physical appearance sio nature??

Kwani Physical appearance sio Nature??? Naomba jibu.
Hivi unaelewa hata ulichouliza kweli sasa kumuogopa mnyama kwa sababu ya physical appearance maana yake hiyo physical appearance ndio inakuwa siyo nature, mimi nimesema uoga wa aina hiyo siyo nature kwa sababu hujamuogopa yule mnyama kwa kuwa unajua ni hatari bali umemuogopa kwa sababu ya muonekano wake, kwa maana kwamba ukikutana na mnyama hatari mwenye muonekano mzuri hutamuogopa kwa sababu hujajua kama ni hatari na muonekano wake haukutishi
Sasa huo si ukichaa umkute mtu barabara umuamlishe au umkataze vitu!!!!. Nadharia zako zinachekesha.
Ndio unaweza kumtuma mahali fulani
Jambo ni Gumu kwa Feminist ila ni Jepesi kwa wanawake(pure)
Haya katika scenario kama hiyo mwanamke anatakiwa amtii mwanaume kwa kigezo gani, hapa ulikurupuka kujibu ila hujajua kama umejifunga, nasubiri jibu la hapa ili sasa nizidi kuthibitisha na kupigilia msumari hoja zangu za juu kule
Malalamiko.
Wewe ndio bingwa wa malalamiko mimi naendeleza kile ulichoanza tu, naona sasa umeshika adabu umeacha kujisifia eti oo namwaga elimu, ndugu mwalimu hiyo elimu yako inatia mashaka sana yani waalimu wote wangekuwa waongo na wapotoshaji kama wewe hii dunia sijui ingekuwa wapi asee
 
Mbona Unanisingizia yale unayoyafanya wewe. Uzuri hapa kila Mtu anaona Kwamba nani Anatoa Hoja Na Nani Anatunga Maneno.
Nithibitishe Kwa Namna Gani Tena Nimekwambia Wahindu Ng'ombe kwao ni Mungu Jee Ng'ombe Yupo Mbinguni?? Kuna watu Mungu wao ni Moto Je Moto uko mbinguni?? Hao Waroma Unawazushia Maneno na Wanakushangaa Wao wenyewe. (Aibu)
Hakuna Hoja Hapa.
Kwenye ndoa mfano mwanaume anaweza kuhitaji watoto watano ila mke anahitaji watatu tu je unadhani mwanaume atamlazimisha huyo mwanamke kuzaa watoto watano, hawezi sana sana ataenda kutafuta mwanamke mwingine (mchepuko)
kama mwanamke Akitaka Watoto watatu alafu Mume akataka wawili itakuaje??
Nasisitiza Suala la kuzaa ni Jukumu Shirikishi. Hakuna anaeweza kulifanikisha Pekee yake.
Ni kwa sababu wanajua mwanaume hawezi kukataa kuzaa na wala hawezi kukataa sexual intercourse
Nadharia.
yani mwanaume hata akiwa kataa ndoa bado atatafuta walau mwanamke wa kumzalia watoto ili aendeleze kizazi chake,
Nadharia.
Hahahaha kwaiyo ukijitegesha Alafu nikiondoka Utapata Mimba??
Tatizo lako wewe ulilisema jambo la kuzaa kana kwamba Mwanaume Hausiki kabisa. Sisi hatukatai kuwa Mama ana Play role kubwa katika Suala la Kuzaliwa Watoto. Na ndio maana Tangu mwanzo tulishasema Jambo Hili linafanya Kina Mama wapendwe zaidi na watoto wao ila sio kigezo cha kuwa kiongozi.
Oohh kwahiyo mwanamke anapozaa haina athari au faida kwa mwanaume na familia kwa ujumla,
Kwani nani amesema haina athari??
yani majukumu ya mwanaume tu ndio yenye faida ila ya mwanamke hayana faida, nilimaanisha hayo majukumu anayofanya mwanaume hayamfaidishi mke pekee bali yeye mwenyewe kwanza
Unageuka tena wewe si ulisema Majukumu ya mwanaume yanamnufaisha zaidi yeye mwenyewe??
Hivi unaelewa hata unachotetea kweli sasa ukishamuweka mnyama zoo si maana yake atakutii kwa sababu unamhudumia na yuko chini ya uangalizi wako lakini si kwamba umemzidi nguvu,
Aisee kazi ipo.
Hapa tunazungumzia kitendo cha wewe kuwa na uwezo wa kumtoa polini na kumuweka Zoo. Bila yeye kufanya lolote. Masuala ya huduma yamekujaje?? Kwani hao wanyama Usipowapa hizo huduma Hapo zoo watafanyaje??? Watakupiga?? Unachekesha.
Hakuna mnyama ambae hawezi kuwekwa zoo.. kwanza hapa hatuongelei masuala ya wanyama mana naona umehama kabisa. Mind you Zoo sio yale mabanda ya kufungia tumbili pekee acha ujuha.
Sasa si nimeshafafanua kwamba ni wanaume, halafu unaniuliza tena ni kina nani, aloo we jamaa mbona una kichwa kigumu sana
Wanaowasakama wanawake wasipoolewa ni Wanaume? Wanaowasakama wanawake wakiachika ni Wanaume?? Hivi unatujua Sisi wanaume.!!! (Sisi huwa hatuna muda na mambo ya kipuuzi)
Mi nachojua kesi nyingi katika madawati ya kijinsia ni za wanawake alafu unatuambia mmeacha malalamiko. Ajabu.
Hivi wewe unaijua hata saikolojia ya binadamu inavyofanya kazi kweli mbona unaongea nadharia sana, unajua namna masimango kwa mtu juu ya jambo fulani yanavyoweza kupelekea hata huyo mtu kujiua kwa kujiona hafai katika jamii hata kama si kweli
Huu ni udhaifu na sio jambo la kawaida.
, hao wanawake wangekuwa kweli wanazipenda hizo ndoa kutoka mioyoni mwao si wangezipigania ili zidumu mbona sasa nyingi zinavunjika huku wanaume wakidai kwamba wanawake ndio chanzo
Ndoa za Mafeminist ndio zinavunjika kwa wingi(mfano ulaya).
Huo ndio ukweli siku hizi wanawake wajuaji kama wewe mnazalishwa tuu.

Mind you ndoa zitaendelea kufungwa kwa sababu sio wanawake wote ni Wajuaji kama wewe pia hata Watu wajuaji kama wewe wakifika Umri wa jioni akili zinawaingia. (Kwaiyo hata wewe Tunakupa muda)
Hili halithibitishi furaha ya bibi zetu, sana sana unataka tu nirudie kueleza kile kile nilichotoka kueleza, hili silirudii tena mpaka utakapokuja na hoja ya maana iliyojitosheleza
Sasa furaha ni kitu gani?? Bibi zetu tumeshuhudia maisha yao wakiwa na Furaha na kulidhika wewe unasema hiyo sio furaha sasa furaha kwako ni kitu gani??
Niliishathibitisha
Sio kweli.
Hizo tamaduni hawakuzitunga wao wanawake
Tamaduni za Masuala ya mwanamke Pia walitunga Wanaume!!! au unahisi yale Wanayofundisha Kwenye unyago ni Vitabu vilitungwa na Wanaume?? (Tatizo hujapita kwenye Unyago ndio maana umekuwa Mjuaji)
Hapo hujajibu swali langu nimekuuliza hivi waliowamanipulate hao wanawake ni kina nani na waliwamanipulate kwa faida ya nani,
Swali lako hili na mengine kama hilo nitajibu.
Subiri.
Nani kakudanganya kwamba ni jamii chache ndio zilikuwa na negative things huo ndio ulikuwa utamaduni wa karibu jamii zote,
Kwaiyo Jamii zote zilikuwa na mambo mabaya??
by the way hata kwenye dunia ya leo iliyojaa feminism bado kuna ndoa nyingi tu zina furaha sasa wewe kwanini unaongelea zile zenye migogoro tu, ukipata jibu basi utaelewa kwanini na mimi naongelea jamii za kizamani katika negativities tu
Ndoa zenye Furaha ni zile Za Pure women. Au zile za Mafeminist waliowaoa wanaume wao (yaani mwanaume analelewa) ila Ndoa ya feminist na Mwanaume Rijali Haiwezi kutoboa. Labda utupe mfano wa ndoa yako ( kwanza uitoe wapi!!!)
Sasa kwani unyago na hizo sherehe nyingine zilikuwa zinawafundisha nini cha maana wanawake zaidi ya namna ya kuwa watumwa kwa waume zao,
Aisee kazi ipo. So negative mdada.

Mabinti walikuwa wanafunzwa malezi,, wanafunzwa kupika,, wanafunzwa Tendo la Ndoa kwa umahili,,, wanafunzwa Usafi wao kiujumla na wafunzwa nafasi zao katika familia. (Ndo maana siku hizi hamjui kupika) ,,,,Huo utumwa Walifunzwa vipi??
Sasa ulitaka mwanamke afanye Shughuli gani zaidi?? Embu nitajie mfano wa shughuli ambayo angeweza mwanamke wa zamani kuifanya out ya kazi za nyumbani?? Ulitaka aende vitani?? U feminism Mzigo.
Sasa hapo ndio umetetea nini kwani baba akiwa kiongozi ndio inamuondolea kaka uanaume wake, kwani ndio inamuondolea kaka hicho kigezo cha nguvu na umadhubuti ambacho unasema ndio kigezo cha mwanaume kumtawala mwanamke
Hakuna mafahali wawili katika zizi moja.
haya vipi baba akifariki je, kwahiyo wewe unadhani hao viongozi walikuwa wanapewa utii kwa sababu tu ni wanaume haya vipi kama kiongozi ni mwanamke huwa wanamtii kwa sababu gani
Baba akifariki Kiongozi wa familia Anakuwa Kaka mkubwa hili lipo wazi. (Zingatia Familia gani unayokusudia maana Mashangazi wao ni wa familia nyengine na wanakaka zao wakubwa)
Sasa hili si ndio jibu kuwa Mtoto hawezi Kutaka utiifu kwa Mama ake kwa Sababu Uhusiano wao sio sawa na Mahusiano ya mke na Mume. Nashukuru kwa kuelewa.
ndio maana nikakuuliza ukitoa huduma za kiuchumi msingi wa mwanaume kumtawala mwanamke ni upi wewe unaniletea habari za nguvu na umadhubuti kana kwamba mwenye hivyo vigezo ni mume wa ndoa tu
Unajibu kisha unauliza tena swali hilo hilo.
Mwanamke anazaliwa na hali ya utegemezi na kutaka kusaidiwa katika yale majukumu ya kimaumbile,
Unachanganya tena Wakati nilishakufundisha Kwenda vitani,, Kuchimba Visima,, sio Majukumu ya Kimaumbile. (Elewa)
Moja, Majukumu ya kimaumbile ya mwanamke ni Kutengeneza mayai, kubeba mimba,kuzaa,kunyonyesha, na majukumu ya kimaumbile ya mwanaume ni Kutengeneza mbegu ku erect kupeleka mbegu kwenye njia ya uzazi.

Hayo majukumu Mengine sio Majukumu ya Kimaumbile usichanganye vitu.

Kuna majukumu ya kimaumbile(Biological mfano kuzaa ku erect ),,majukumu ya kitabia mf kutongoza,,, majukumu ya kiuwezo (Ability related Roles ambazo ni Naturally selected mf kwenda vitani),,, Na Majukumu ya Kimakubaliano mf. Majukumu ya Rais.
(Usichanganye vitu.)

Pili kazi za nyumbani wanaume wanafanya hakuna kazi ya nyumbani ambayo mwanaume hawezi kufanya. (Kama ipo nitajie.)
Sasa kwani hapa tunaongelea supporters wa hizo agenda au tunaongelea wahusika, yani kitendo cha wanawake wengi kuikubali feminism na kuwa feminists ni jibu tosha kwamba hailazimishwi,
Feminist mko wengi kwa data ipi?? Maana hata mashoga na wasagaji(LGPTQ+ Members) nao Watakwambia wapo wengi.
wanaume wengi lazima waipinge kwa sababu haiko upande wao mind you hapa tunaongelea suala la wanawake kuzaliwa na utii kwa wanaume ni nature au siyo nature
Nasisitiza sio kila kinachopata wafuasi ni kitu Sahihi. Nchi kama Ujerumani ushoga ni jambo la kawaida mno na ukionekana unapinga ushoga Ujerumani utakuwa na wakati mgumu mno jee Mashoga waseme ushoga ni jambo zuri kwa sababu haulazimishwi??
Mimi sizungumzii usawa katika Idadi nazungumzia Ukuaji na uungwaji mkono.
Pia wewe unaposema haifiki nusu una Data umeegemea au na wewe ni mlopokaji??
Duuh kwahiyo kwa akili yako wewe ulitaka mama Samia awaambie mabinti wawe wajeuri kwa waume zao hata kama yeye yuko hivyo,
Sisi tunasikiliza maneno yake kama wewe unamjua kiundani Rais Hongera.
Aisee Hongera kumbe kuna za chinichini za Rais Unazijua!!! ,,, unayajua maisha ya Ndani ya Rais!!! Hongera.
Wewe ndio unatunga maneno hadi unajistukia. Una akili za kitoto mno.
anyway pengine huwa wanashindwa kuwaeleza wajukuu zao wa kiume sababu wanahisi wanaume wote lenu moja hivyo hamtawaelewa kwahiyo labda wanaamua kuwaeleza wajukuu zao wa kike tu
Hhahaahaha aiseee!!!!
Hivi kwanini unanilazimisha nikae narudiarudia kuelezea yale yale kila wakati hilo si nimeshalielezea kwamba zamani mwanamke kutokuolewa au kuachika ilichukuliwa kama ni laana
Ni laana?? Aisee we unazungumia Jamii gani??
na fedheha kubwa kwake na kwa wazazi wake sasa kwa hali hiyo kuna mwanamke angekataa kuolewa, vipigo na manyanyaso haikuwahi kuwa sababu ya kumfanya mwanamke asiolewe maana waliambiwa wavumilie
Mabinti walikuwa wanataka Wenyewe waolewe kwa faida za ndoa walizokuwa wanaziona haya unayoyafunga yanastaajabisha. Labda kama unazungumzia zile Jamii chache ambazo huwezi ku conclude kwa jamii nzima.
sasa kama miaka hii tu kuna wanawake wengi wanafanyiwa hayo na wanavumilia sembuse zamani na ukizingatia wengi walivumilia kwa sababu tu mwanamke akiachika hana pa kwenda na mara nyingi huachwa na watoto hivyo wanawake walivumilia ili kuepuka hili,
Suala la Kuvumiliana hilo jambo la kimaisha Sababu kila mmoja ana mapungufu yake usidhani ninyi Wanawake ni malaika na nyinyi mna Vituko vyenu ambavyo Wanaume wanavumilia.
As long as Sio wanawake wote ni ma Feminist basi ndoa zitaendelea kufungwa lakini Idadi ya Talaka inazidi kuwa juu kwa Wale wanaojidai wajuaji.
Naona unapinga katiba sasa. Kwaiyo huko ulaya Rais anashitakiwa?? Maana ninyi Ulaya ndio role model.

Kwaiyo wewe unahuzuni hapo sababu Katiba imesema Rais hashitakiwi. U Feminism ni uwendawazimu.
Sasa wa kutafuta hiyo solution alikuwa nani yani mwanamke ndio atafute solution ya tabia mbovu za mwanaume, au wanaume ambao karibu wote walikuwa na tabia hizo hizo ndio wangetafuta solution ya hizo tabia zao,
Aisee mbona unatutukania Babu zetu!!!!
kwamba Babu zetu wote walikuwa Wanyanyasaji Mbona sisi tumeishi Nao Hatujayaona hayo unayoyasema. Labda nikuulize Babu yako alikuwa anampiga na kumnyanyasa Bibi yako???
unachekesha kweli hivi mbona umejaza nadharia nyingi sana humo kwenye kichwa chako kuhusu maisha ya zamani, watu tunaongea uhalisia wewe unaleta nadharia, ujue hapa tunaongelea maisha halisi yaliyokuwepo hatuchambui riwaya wala mashairi
Uzuri Wanaofatilia huu Mjadala watakuwa wanajua Nani anatunga Maneno na nani anajenga Hoja.
Wewe mbona haujadili ndoa zilizo na furaha katika era hii ya feminism unajadili kama kwamba zote zina migogoro tu, by the way mimi hapa naongelea in general ila haimaanishi kwamba hakukuwa na few exceptions za ndoa zenye furaha,
Hizo few exceptions Zimekuwaje na furaha!!! Wakati wewe unasema Bibi yako amekuambia Ndoa zao zilikuwa hazina furaha.!!!!
ila zile zisizo na furaha ndio zilikuwa nyingi kwa sababu wanaume wengi walikuwa na tabia zinazofanana ambazo wao waliona ndio uanaume ilihali kwa wanawake zilikuwa ni mateso
Mind you Wanawake ndani ya Nyumba Huwa wana vituko vingi mno Na wanaume huwa Wanavumilia vitu vingi Sana. ( Kama mimi navyo vumilia Utoto wako unaouandika hapa). So Tabia mbovu zilikuwapo kwa wote.
Watu wa Dini Wanaamini maandiko ni Nature kwa ushahidi upi maana na Mimi ni Mtu wa Dini Sasa Nashangaa unachokisema.
Nasubiri

Anapungukiwa na uhuru wa kufanya baadhi ya vitu
Umeshaolewa unataka Uhuru wa kufanya nini??
Kwani watu huwa wanalazimishwa kuolewa?? Si huwa wanatia saini wenyewe kwenye kile cheti. Sasa umeolewa unataka uruke viwanja kama Wanawake wengine. Cha msingi Usiolewe.
Sasa ndio asimtegemee mkewe kwa asilimia mia akatafute msaada na huko kwingine ulikosema, mwanaume kukwama au kufilisika siyo excuse ya kuyaacha majukumu yake, vinginevyo awe tayari kukabidhi na nafasi yake maana ni wazi imemshinda
Aisee Umefirisika kumbe ulikuwa hujasoma vizuri majibu yangu!!.(Uwe unasoma vizuri)
Kwenye majukumu ya kimaumbile ndio hawawezi kuwa sawa, ila kwenye mambo mengine imekuwa proven kuwa wanaweza, na utofauti wa kimaumbile siyo justification ya kuweka utofauti kwenye kila kitu
Majukumu ya kimaumbile unayoyakusudia ni yapi?? Na huko kwingine unakokusema ni kupi??
Sasa kama hamtaki kuwatii wanawake si ndio mhakikishe mnatafuta kwa nguvu na bidii zote ili isifikie hatua ya wanawake kuwasaidia majukumu yenu
Kwenye maisha kuna Kuanguka Mdada. Tatizo wanawake kama ninyi mnawaza pesa na Maisha ya Ulaya yaani mumeo akianguka kidogo Huwezi kumfariji katika kipindi hicho ila utaanza kumsimanga. (Hovyo kabisa)
Ni wapi nilipokana dini hebu nioneshe nasisitiza nioneshe usiniletee mawazo yako
Wewe hukusema Maandiko ni Maneno tuu ya watu??. Nikakuuliza Unaamini katika mungu ukaniuliza Mungu yupi??

Tuachane na Hayo Kama utanithibitishia kuwa wewe unayaamini maandiko basi nitaanza tena kuyatumia..
Hilo "bila kujali" umeitoa wapi!! Kwani huu mjadala haukulenga Mume na Mke??.

Anyway kwani si nimesema hata katika ngazi ya jamii Mwanaume ndio kiongozi.

Nasisitiza utii unazingatia mahusiano yaliyopo baina yenu. Kama ni kaka na dada basi kaka ni Kiongozi kama ni shangazi na mjomba basi mjomba ni kiongozi kama ni baba na Mama basi Baba ni kiongozi kama ni babu na bibi basi babu ni Kiongozi.

Sasa usihamishe ukaniuliza Bibi na Kaka?? wakati unajua Mahusiano ya kaka na dada sio sawa na ya Kaka na Bibi.
Jibu maswali wacha kurukaruka
Ukijibu langu nitajibu lako kwa sababu swali langu ndio la kwanza.
As long as sio wanawake wote ni Wajuaji kama wewe basi ndoa zitaendelea kufungwa.
Aisee Sasa Suala la kuoa wake wengi limetoka wapi tena?? Hujajibu swali unaanzisha Mada nyengine.
Hili ndio kwanza nalisikia kwao naona umeamua kuwa daktari uchwara sasa
Hujui na hutaki kujifunza kabla ya kuniita daktari uchwara ungefanya research kwanza. (Yaani usilopoke)
Ukeketaji Ulianzishwa na wanaume kwa ushahidi upi?? U feminism Takataka.
Mimi siishi ulaya niko hapa hapa afrika ambako bado kuna masalia ya wanawake wanaounga mkono mfumo dume na wengi ni either hawana elimu au ajira narudia hakuna mwanamke mwenye hivyo vyote atakubali kuwa chini ya mwanaume kubali ukatae,
Wapo Wenye akili sio wanawake wote wasomi Hawana akili kama wewe. Nimekutolea mfano tuu Rais Samia.

Pili ikiwa Mwanamke msomi mwenye ajira hawezi kuwa chini ya Mwanaume inamaanisha hata ukimuhudumia hawezi kukutii kisa ni msomi ana ajira??
ukitaka kuendelea kukaza kichwa na kujifariji sawa maana hiki ndicho wanaume mlichobaki kufanya kwa sasa mnajifariji na mnadanganyana kwamba wanawake wazuri na wema bado wapo wengi sana,
Kwaiyo wanawake wema hawapo mmebaki ninyi Majike dume???
Unatudhibitishia kuwa ninyi ni chui Sio Wanawake. Nakumbuka nilikuwa namsikia Feminist mmoja akisema Yeye yupo na financial independence ndio mana Ameweza kutoka nyumbani bila kumuaga mumewe namnukuu akasema" unajua jeuri hii nimeitoa wapi?? Ni kwa sababu ya financial independence". Nikawa najiuliza kama suala la kutoka nyumbani bila kuaga ni jambo zuri kwa nini amesema "jeuri hii" mbona kama inaashiria hilo jambo hata kwake sio zuri ila Kwa Sababu ya mashindano amelazimisha ku prove umwamba.
Informal Education ni jando na unyago full stop na hakukuwa na jamii usiyokuwa na Jando na Unyago kama unapinga njoo na ushahidi hapa.
Ndio maana nikakuambia kitakachokufanya ukubali boss wako akupangie ni mshahara na siyo kile cheo chake, ndio maana boss asipokulipa mshahara unaanza kuona ugumu na uzito kumtii tena na unaweza hata ukaacha hiyo kazi,
Mimi sizungumzii haya nimekuuliza unapokuwa unamtii Boss wako unakuwa Huna furaha??? Jibu hili.
feminism siyo ujinga bali ni matokeo ya wanawake waliokataa utumwa uliojificha kwenye mwamvuli wa mfumo dume
Feminism hii ya leo (third wave) ni upumbavu.
Kwaiyo umkute mtu Mtaa wa kongo kariakoo umuagize dukani. Aisee una umri gani wewe???
Sasa ulishindwa kuleta uhusiano uliopo kwa kujenga hoja nje ya dini, na ndio maana nikakuambia wewe unahamahama ukiona huku huna hoja unahamia upande mwingine, haya kwa vile umesema hutahusianisha tena na dini basi lete uhusiano uliopo nje ya dini
Unachekesha mimi nilihusianisha baina ya Feminism na Atheism Alafu unataka nikupe uhusianao njee ya dini. Ajabu..
Okay kwahiyo hata kama huyo mwanamke hatimizi majukumu yake na ni mjeuri bado mumewe ataendelea kumpenda tu siyo
Wanawake jeuri Walikuwa wanaadhibiwa na waume zao. Imeisha.
Kwani si ni kweli kwamba umetumia maneno yasiyo sahihi sasa unalalamika nini??
Hapo napo unafanya kile kile
Tatizo ujuaji mwingi.
Umetetea vyema. Sasa katika suala la kuamini Mungu huyu tunaemuamini Sisi (sijui kama na wewe unamuamini) Hao wote wako sawa.
Hivi unaelewa hata ulichouliza kweli sasa kumuogopa mnyama kwa sababu ya physical appearance maana yake hiyo physical appearance ndio inakuwa siyo nature,
Unatudanganya mdada. Miili yetu ni nature sasa sijui wewe Physical appearance unajua ni kitu gani??
mimi nimesema uoga wa aina hiyo siyo nature kwa sababu hujamuogopa yule mnyama kwa kuwa unajua ni hatari bali umemuogopa kwa sababu ya muonekano wake,
Aisee umeandika Ujinga.
kwa maana kwamba ukikutana na mnyama hatari mwenye muonekano mzuri hutamuogopa kwa sababu hujajua kama ni hatari na muonekano wake haukutishi
Eeee kuna mnyama hatari mwenye muonekano mzuri(ambao hauwezi kukutisha) embu tutajie!!!!
Ndio unaweza kumtuma mahali fulani
Nadharia.
Haya katika scenario kama hiyo mwanamke anatakiwa amtii mwanaume kwa kigezo gani, hapa ulikurupuka kujibu ila hujajua kama umejifunga, nasubiri jibu la hapa ili sasa nizidi kuthibitisha na kupigilia msumari hoja zangu za juu kule
Embu subili Jadda kwanza kwani Rais akikukuta Barabarani akakutuma. Utamtii kwa vigezo gani?? Japo naamini si Rahisi kiongozi akukute tuu barabarani alafu akutume hhahahahha aisee kazi ipo.
Nataka uniambie kama unayakubali maandiko ya kikristo (bible) au ya kiislamu (Quran) au ya kiyahud niambie nianze kuyatumia maana huko juu uliniambia nikuletee maandiko.
 
Poa tusiongelee ndoa mwanamke unayemuongelea wewe the so called hahitaji ndoa anakwenda kwa muongozo gani?

1. Anapataje mahitaji yake ya kifedha
2. Analala na nani bila kushiriki ngono na uzinifu?
3. Anaishi kwa misingi ya kitabu gani cha kiimani?
4. So hatambui kuwa kuna MUNGU, maana maisha nje ya ndoa ni maisha nje ya MUNGU so anajilinda mwenyewe si ndio?

5. Watoto atawapataje nje ya ndoa? Na kama akiwapata anawakuza katika malezi ya namna gani?

6. Mtu wa namna hii unategemea awe na influence au mchango gani wa kijamii?
7. Wewe unaishi kwa imani gani hadi usapoti mwanamke mwenzako kuishi kwa mfumo kama huo wa nje ya ndoa?
 
Na huu ndo ukweli wanaume hawataki kusikia[emoji419][emoji625]
Hakuna ukweli hapo, hata wewe unajua kuwa mwenzako anachoongea ni hoja zinazofanania fikra zake tu na sio uhalisia.
 
Aliyekwambia heshima ni matokeo ya size ya mwili au kipato ni nani?

Heshima ni matokeo ya mamlaka. Wanawake hawa hawa wasiokubali kujishusha mbele za wanaume wanakwenda madhabahuni kujinyenyekesha mbele za MUNGU ili iweje, MUNGU ambaye una kaidi maagizo yake unakwenda kwenye nyumba ya ibada kumuomba kitu gani, si uende huko kwa mafreemason wenzako mkamsujudie shetani mkuu wenu ng'ombe kabisa.
 
Joyce kiria kawakalilisha kwamba utiifu ni utumwa.
Halafu kaishia kwenda kuforce ndoa na yule jamaa wake wa sasa hata haeleweki ni mwanaume au mwanamke yupo yupo tu mradi wamekutana wote vituko.

Mwanamke akishakuwa mpumbavu ni ngumu sana kumrekebisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…