Hoja imenishinda kivipi!! Wewe Unachanganya Maneno unatoa Hoja alafu unakuja kuvikataa Mwenyewe. Unasikitisha.
Yani wewe unashindwa kuelewa hoja kwa sababu akili yako ni ndogo halafu unakuja kusema eti mimi ndio nimechanganya maneno, hebu kuwa serious acha kujaza magazeti for nothing halafu kabla hujajibu comment fulani soma kwanza aya nzima uielewe ndio ujibu acha kusoma na kujibu vipande vipande, maana naona unakuwa unakimbilia kujibu hoja ambayo nimeshaifafanua chini yake yani unauliza kitu ambacho jibu lake liko chini yake halafu unanipa kazi ya kujibu tena
Wahindu Wanamiungu Yao (Ng'ombe) na Wengine (masanamu) kwenye Temples, Wapo Wanaoabudia Moto(Sijui Moto nao upo mbinguni!!),, Wapo Wale Buddha Miungu yao pia ni mfano wa Wahindu,, waafrika tulikuwa na tunaabudia Miti mikubwa na Mizimu kama miungu sijui nayo ipo Mbinguni??.
(Kwanini Unazungumza mambo Usiyoyajua??) .
Oohh kwahiyo maana yake kila dini inayoabudu sanamu basi mungu wao hayuko mbinguni, kwamba hata waroma mungu wao hayuko mbinguni kwa sababu wanaabudu sanamu la yesu, wewe ndio unazungumza usiyoyajua nimekuambia thibitisha kwamba mungu wa dini yako pekee ndiye ambaye yuko mbinguni
Sio Kweli Unatudanganya Kuzaa Ni Maamuzi Ya Mwanaume Na Mwanamke Hakuna Anayeweza kulifanikisha Hilo Pekee yake.
Mwanamke hawezi kujitungisha Mimba. Unachekesha.
Aisee Unajua unachokiandika kweli?? Wanaume Wasipotoa Mbegu Zao(Sperms) Wasipokubali Kufanya Sexual intercourse na Ninyi Hizo Mimba Mtazitoa wapi??
Hivi hebu nikuulize generally kati ya mwanaume na mwanamke ni nani anayependa kuwa na watoto wengi zaidi, najua hapa utajifanya kuzunguka sababu unajua ukitoa jibu sahihi utajifunga lakini ukweli unajulikana jibu ni mwanaume siyo rahisi mwanamke kutamani kuzaa watoto wengi, hakuna mwanaume ambaye hataki watoto haijalishi hali yake ya kiuchumi (ndio maana hata masikini wana watoto) ila mwanamke kuzaa ni hadi ajione yupo tayari kwa wakati husika
Kwenye ndoa mfano mwanaume anaweza kuhitaji watoto watano ila mke anahitaji watatu tu je unadhani mwanaume atamlazimisha huyo mwanamke kuzaa watoto watano, hawezi sana sana ataenda kutafuta mwanamke mwingine (mchepuko) amuombe amzalie hao wengine ndio nakuuliza sasa je ina maana hapo mwanaume anakuwa dhaifu kwa sababu mwanamke ndio kaamua idadi ya watoto, ndio maana nikakupa huo mfano kuwa hata leo hii population inavyokuwa kwa kasi ndogo wanaobebembelezwa kuzaa ni wanawake kwanini hao viongozi huko ulaya wasingebembeleza na wanaume kwanini wanawabembeleza wanawake tu
Ni kwa sababu wanajua mwanaume hawezi kukataa kuzaa na wala hawezi kukataa sexual intercourse yani mwanaume hata akiwa kataa ndoa bado atatafuta walau mwanamke wa kumzalia watoto ili aendeleze kizazi chake, kwahiyo bado hoja yangu iko pale pale kwamba hata kama mwanaume anataka watoto ila mwanamke akikataa kuzaa kwa wakati huo basi huyo mwanaume hatapata hao watoto kwa wakati anaoutaka, ila mwanamke yeye muda wowote akitaka watoto ila mwanaume hataki anaweza hata akajitegesha akapata mimba akazaa kwahiyo maamuzi ya kuzaa yapo mikononi mwa mwanamke
Mwanzo kabisa Nilikufundisha Kuhusu Maana ya Majukumu ya Kimaumbile kwa Sababu ulikuwa Unachanganya. Sasa Majukumu ya Kimaumbile kila Jinsia Ina Ya Kwake. Ambayo hayawezi kufanywa na Upande wa Pili..
unapozungumzia kuzaa ujue Kuwa hilo Ni Jambo Shirikishi Hakuna Anaweza kulifanikisha Bila Mwengine.
Unasikitisha Kwani Sperms, Erection ,, Copulation Nani Anahusika??
Yani unafananisha kuchangia mbegu na kubeba mimba, kuzaa na kunyonyesha, kama hayo yangekuwa yanafanana unadhani ni kwanini watoto wanaambiwa wawapende zaidi mama zao, kwanini wasiambiwe wawapende na baba zao sababu wamechangia mbegu, mambo mengine mbona yako wazi tu hata hayahitaji mtu apoteze muda wake kuyafafanua ndio maana nasema wewe una upeo mdogo sana
Mimi Sijafikilia Kujibu Hivi kwa sababu akili Yangu Ni Pana zaidi na Timamu.
Sijajua ulikuwa Unajenga Hoja gani hapa. Anyways Nguvu na Umadhubuti na uwezo wa Mwanaume Vinamuwezesha Mwanaume kutekeleza Majukumu yake na Wajibu wake katika Familia kama Kiongozi wa Familia. Bila Shaka Majukumu ya Baba Yanaathari kwa Mama na Kwa Familia kwa ujumla Sasa sijajua Uliposema "ni kwa Faida ya mwanaume mwenyewe zaidi" ulikuwa unamaanisha nini??
Oohh kwahiyo mwanamke anapozaa haina athari au faida kwa mwanaume na familia kwa ujumla, yani majukumu ya mwanaume tu ndio yenye faida ila ya mwanamke hayana faida, nilimaanisha hayo majukumu anayofanya mwanaume hayamfaidishi mke pekee bali yeye mwenyewe kwanza
Unatetea hoja kinadharia mno. Utawala naozungumzia ni Sisi Kuweza Kuyaendesha(Kuyabadili) maisha yao tukiamua ila wao hawawezi kuja huku na kuyabadilisha maisha yetu katika chochote. Namaanisha Sisi Tunaweza tukaamua Tukawachukue hai Simba na chui nk tukawaweke Zoo ila Simba hawezi kuamua aje akuchukue wewe uende Serengeti. (Legeza nati)
Hivi unaelewa hata unachotetea kweli sasa ukishamuweka mnyama zoo si maana yake atakutii kwa sababu unamhudumia na yuko chini ya uangalizi wako lakini si kwamba umemzidi nguvu, wewe ndio ulegeze nati mimi naongelea generally katika mazingira ambayo kila mtu yuko kivyake yani huyo mnyama hakujui wala hakutegemei kwa chochote unadhani atakutii, halafu naona unakuwa too specific unaongelea wale wanyama ambao wanaweza kufugwa kwanini usiongelee in general maana kuna wanyama huwezi kuwaweka kwenye zoo mfano kifaru, kiboko, tembo, mbwa mwitu, nk
Nani anawasimanga Wanawake na katika lipi??
Naomba kujua Nani anawatukana Hao uliowataja??
Sasa si nimeshafafanua kwamba ni wanaume, halafu unaniuliza tena ni kina nani, aloo we jamaa mbona una kichwa kigumu sana
Huenda Hawalalamiki ila wanaelezea Situation wanazokumbana nazo kwa waliopata Bahati mbaya kuoa Feminist au Ambae ana Idea za kifeminist.
Hoja siyo kulalamika bali hoja ni kwamba hawana furaha kwenye hizo ndoa, sasa kuelezea situations wanazokumbana nazo ndio inawafanya wasiwe wanalalamika au, kitendo cha kuvoice out hizo situations ndio malalamiko yenyewe hayo kitu ambacho miaka hii wanawake wamekipunguza sana
Huo ni udhaifu Mwengine,,, utakuwaje na pressure katika Jambo ambalo kwa mtazamo wako Sio Sahihi??
Hivi wewe unaijua hata saikolojia ya binadamu inavyofanya kazi kweli mbona unaongea nadharia sana, unajua namna masimango kwa mtu juu ya jambo fulani yanavyoweza kupelekea hata huyo mtu kujiua kwa kujiona hafai katika jamii hata kama si kweli, hao wanawake wangekuwa kweli wanazipenda hizo ndoa kutoka mioyoni mwao si wangezipigania ili zidumu mbona sasa nyingi zinavunjika huku wanaume wakidai kwamba wanawake ndio chanzo
Acha Uongo WAZUNGU siku hizi hawaooani Wanaume Wanaogopa Kuoa Wanaogopa Matatizo ya Talaka.
Wewe ndio uache uongo una takwimu zozote zinazoonesha kwamba siku hizi wazungu hawaoani kabisa, again unaongea nadharia na mawazo yako tu duniani kote kila siku ndoa zinafungwa na hazitaacha kufungwa, usipende kufanya hasty generalizations siyo wote wanaoogopa hayo matatizo ya talaka
Furaha ni Hali ya msawazo wa Nafsi na Mwili. Bibi zetu Walikuwa na Furaha kwa namna walivyokuwa wanaishi na Babu zetu na Vile walivyokuwa Wanatulea Sisi pamoja na yale waliyokuwa wanatufundisha.
Hili halithibitishi furaha ya bibi zetu, sana sana unataka tu nirudie kueleza kile kile nilichotoka kueleza, hili silirudii tena mpaka utakapokuja na hoja ya maana iliyojitosheleza
Kama unakataa hili Njoo na Ushahidi kudhibitisha kinyume( hawakuwa na furaha)
Niliishathibitisha
Bibi zetu walithibitisha kimatendo na katika mafundisho yao kwa Mabinti Zao (Unyago).
Hizo tamaduni hawakuzitunga wao wanawake
Kama umeona mkinzano wowote hapo nina mashaka na Akili yako.
Manipulated women ni wale mfano wako waliomezeshwa Fikra Za Kwamba You can be better or at least equal to man and Your first enemy is man. Lakini Wapo Wanawake wasio na fikra hizi wao kuwatii Wanaume na Kukubali Kuwa chini ya Mwanaume kwao sio Jambo la Kufanya mjadala kama Huu.
Hapo hujajibu swali langu nimekuuliza hivi waliowamanipulate hao wanawake ni kina nani na waliwamanipulate kwa faida ya nani, maana ulisema kwamba wanawake wote wanazaliwa na fikira za kutaka kutawaliwa na wanaume na hakuna mwanaume anayezaliwa na fikira za kutaka kutawaliwa na mwanamke, sasa kwa mujibu wako feminism ilitoka wapi ilianzishwa na nani na kwa faida ya nani jibu hili
Una ushahidi wa Haya au unaandika tuu kwa Nadharia (Tatizo lako zile Jamii chache ndizo unazozikazania Na unafikiri Jamii ya Mababu zetu walikuwa na Negative things pekee)
Nani kakudanganya kwamba ni jamii chache ndio zilikuwa na negative things huo ndio ulikuwa utamaduni wa karibu jamii zote, by the way hata kwenye dunia ya leo iliyojaa feminism bado kuna ndoa nyingi tu zina furaha sasa wewe kwanini unaongelea zile zenye migogoro tu, ukipata jibu basi utaelewa kwanini na mimi naongelea jamii za kizamani katika negativities tu
Sio kweli Hii Jamii haikuwepo unatunga Jamii yako. Kulikuwa na Sherehe mbalimbali za kitamaduni Wanawake Walikuwa Wanashiriki Pia Events mbalimbali za kitamaduni. Sasa wewe unaposema "kazi za nyumbani na shambani tuu" Unamaanisha hadi Unyago walikuwa wanafundisha Wanaume au unajua Unyago ni katika kazi za Nyumbani??
Sasa kwani unyago na hizo sherehe nyingine zilikuwa zinawafundisha nini cha maana wanawake zaidi ya namna ya kuwa watumwa kwa waume zao, yani hoja ni kwamba tukio lolote walilokuwa wanashiriki wanawake kwa asilimia kubwa lazima liwe linahusu mambo ya nyumbani tu hawakucheza mbali na hapo, hakuna mwanamke aliyekuwa anaruhusiwa kufanya shughuli ambazo hazihusiani na mambo ya nyumbani hebu acha kukaza hilo fuvu
Wewe ndio Mawazo yako hayo Unasikitisha.
Nilishatangulia kusema kuwa Utawala unatokana na Mahusiano yaliyo baina ya pande mbili Mwanaume Hawezi kuwa Kiongozi kwa Dada sijui Mama na Ndugu wa kike Sababu kuna Kiongozi wa Juu Yake Baba wa Familia hiyo ambayo hata na yeye anatakiwa kumtii huyo Kiongozi. Kama Tukiangalia Katika ngazi ya Familia Basi Baba ndio Kiongozi. Katika ngazi ya Jamii nzima mwanaume anastahili kuwa Mtawala kama ilivyokuwa kwa Watemi na Machifu.
Sasa hapo ndio umetetea nini kwani baba akiwa kiongozi ndio inamuondolea kaka uanaume wake, kwani ndio inamuondolea kaka hicho kigezo cha nguvu na umadhubuti ambacho unasema ndio kigezo cha mwanaume kumtawala mwanamke haya vipi baba akifariki je, kwahiyo wewe unadhani hao viongozi walikuwa wanapewa utii kwa sababu tu ni wanaume haya vipi kama kiongozi ni mwanamke huwa wanamtii kwa sababu gani
Ukiona Jibu langu Halitoshelezi Basi tukuulize wewe kama utii ni kwa sababu ya Huduma Jee Mtoto akiwahudumia Wazazi wake Basi Wazazi wamtii Huyo Mtoto na Mtoto awatawale Wazazi wake??
Nilishakuambia utii wa mtoto kwa mzazi umejengwa katika msingi wa mzazi kumzaa na kumlea huyo mtoto hicho kigezo cha kuzaa ndio chenye nguvu kisha ndio vinafuata hivyo vingine, sasa kwani mtoto akijitegemea na anapowahudumia wazazi wake ndio anakuwa amewazaa kwanini umetupilia mbali hicho kigezo cha kumzaa, ndio maana nikakuuliza ukitoa huduma za kiuchumi msingi wa mwanaume kumtawala mwanamke ni upi wewe unaniletea habari za nguvu na umadhubuti kana kwamba mwenye hivyo vigezo ni mume wa ndoa tu
Kwanza nilekebishe Ufahamu wako. Mwanamke Anazaliwa na Hali ya utegemezi na kutaka kusaidiwa na kusimamiwa Mambo yake lakini Mwanaume anazaliwa akiwa na ile hali ya kujitegemea zaidi na kupenda kusaidia na kuongoza mambo. Na hili ni kutokana na uwezo wake alionao. Hili linamfanya Awe kiongozi katika ngazi yoyote ya Jamii...
Mwanamke anazaliwa na hali ya utegemezi na kutaka kusaidiwa katika yale majukumu ya kimaumbile, yani wewe bado unaongelea majukumu ya kimaumbile ambayo mwanamke hawezi kuyafanya lakini unasahau kwamba, hata mwanaume kuna majukumu hawezi kufanya mfano kazi za nyumbani pamoja na malezi ya watoto kwahiyo hapo napo tuseme mwanaume anasaidiwa na mwanamke
Feminism hailazimishwi kweli?? Kwani Wanaume wangapi wanapinga Huu Mfumo?? Au ndoa nyingi za wanawake wajuaji kama wewe zinavunjika kwa sababu ya nini?? (Unatudanganya.)
Sasa kwani hapa tunaongelea supporters wa hizo agenda au tunaongelea wahusika, yani kitendo cha wanawake wengi kuikubali feminism na kuwa feminists ni jibu tosha kwamba hailazimishwi, wanaume wengi lazima waipinge kwa sababu haiko upande wao mind you hapa tunaongelea suala la wanawake kuzaliwa na utii kwa wanaume ni nature au siyo nature
Idadi zinafanana na zote zinakua kwa rate moja zikitetewa na kufadhiliwa na Wazungu.
Yani kwahiyo agenda ikitetewa na wazungu basi ukuaji wake ndio unakuwa wa rate moja hivi we jamaa unaelewa unachoandika kweli, kwa taarifa yako idadi ya mashoga haifikii hata nusu ya idadi ya wanaume rijali duniani kote uwe unafanya research kabla ya kuropoka, mnajazana ujinga eti oo wanaume tumeisha sijui nini wakati population ratio duniani inawaumbua na hizo propaganda zenu
Usitudanganye.. kuna Wanawake wengi tuu wamesoma lakini wanatumia vizuri elimu zao kujenga familia zao bora na sio kuingia vitani na wanaume. Sijui kama wewe una ajira au elimu kumshinda Rais Samia ambae anasema wazi yeye ni mtiifu kwa mwandani wake. (Tofautisha kati ya Manipulated na Educated)
Duuh kwahiyo kwa akili yako wewe ulitaka mama Samia awaambie mabinti wawe wajeuri kwa waume zao hata kama yeye yuko hivyo, by the way kwani yeye ndio kielelezo cha namna wanawake wote duniani wanavyotakiwa kuwa, halafu usilolijua ni sawa na usiku wa giza ngoja nikuache kwa sababu unaweza kuwa hufahamu vitu ambavyo mimi navifahamu kwahiyo huo mfano wako kwangu mimi ni UONGO..tuishie hapa!!
Tangu zamani ya wapi?? Wewe ulishawahi kukaa na Bibi mmoja wa zamani ukamuuliza kuwa alikuwa na Fikra chafu kama zako au Unaaandika Nadharia???
Haya sio ya kweli Hata kidogo. Labda Bibi yako Hayo ni mawazo yake binafsi au kwamba bibi zetu walitofautiana katika kuielezea Ndoa.
Hakuna cha mawazo yake binafsi yeye alielezea hali halisi iliyokuwepo kwa wanawake wengi wa enzi zao kwani unadhani bibi zetu walikuwa hawakutani kusimuliana baadhi ya mambo yao, na aliyeongea hayo siyo bibi yangu tu nina marafiki pia ambao wameshawahi kuambiwa hayo na bibi zao ndio maana nilikuuliza wewe huwa unaongea na bibi zako kweli (najua hapa unaweza kutunga lolote mradi tu utetee uongo wako), anyway pengine huwa wanashindwa kuwaeleza wajukuu zao wa kiume sababu wanahisi wanaume wote lenu moja hivyo hamtawaelewa kwahiyo labda wanaamua kuwaeleza wajukuu zao wa kike tu
Na kama ingekuwa hivyo basi ndoa ingekuwa ni jambo la Kulazimishana na Mabinti wakisikia wanataka kuolewa basi awe anahisi kama anaenda kuzimu lakini hili halikuwepo bali Kila Binti ilikuwa Hamu yake ni Kuolewa na ndio maana nashawishika kuwa maisha ya ndoa za zamani yalikuwa Na furaha.
Ni ngumu kuniaminisha kuwa Binti anakua anaona kwa Jirani Mke anapigwa kila siku sijui manyanyaso alafu atamani kuingia kwenye ndoa (Ajabu)
Hivi kwanini unanilazimisha nikae narudiarudia kuelezea yale yale kila wakati hilo si nimeshalielezea kwamba zamani mwanamke kutokuolewa au kuachika ilichukuliwa kama ni laana na fedheha kubwa kwake na kwa wazazi wake sasa kwa hali hiyo kuna mwanamke angekataa kuolewa, vipigo na manyanyaso haikuwahi kuwa sababu ya kumfanya mwanamke asiolewe maana waliambiwa wavumilie sasa kama miaka hii tu kuna wanawake wengi wanafanyiwa hayo na wanavumilia sembuse zamani na ukizingatia wengi walivumilia kwa sababu tu mwanamke akiachika hana pa kwenda na mara nyingi huachwa na watoto hivyo wanawake walivumilia ili kuepuka hili, okay labda nikuulize na wewe si ulisema kwamba ndoa za siku hizi hazina furaha kwa sababu ya feminism kutake over sasa mbona bado wanaume wanaendelea kuoa kila kukicha pamoja na kuzijua tabia za wanawake wa siku hizi ina maana wanaume hawapendi kupata furaha
Hii ni kanuni ya kawaida ya kiutawala Hata Sheria imewekwa kuwa Rais hashitakiwi. Na wewe Ukikosea Rais anaweza kukuhukumu ila wewe huwezi kwenda ikulu ukamuwajibishe Rais. (Labda nikuulize kwanini??)
Okay kwahiyo unataka kusema watu wanafurahia hicho kitendo cha kushindwa kumshitaki rais akikosea, maana hapa hoja ni kwamba je huyo mtawaliwa anafurahia huo utawala au la, hizo ni sheria walizojiwekea wenyewe hao viongozi hawakukubaliana na wananchi wote hivyo huwezi kusema wananchi wanafurahia hilo
Solution ni kutatua hizo changamoto za ulevi nk ila sio Kumpamba Mwanamke amuasi Mumewe. Sio uamuzi wa Busara.
Sasa wa kutafuta hiyo solution alikuwa nani yani mwanamke ndio atafute solution ya tabia mbovu za mwanaume, au wanaume ambao karibu wote walikuwa na tabia hizo hizo ndio wangetafuta solution ya hizo tabia zao, unachekesha kweli hivi mbona umejaza nadharia nyingi sana humo kwenye kichwa chako kuhusu maisha ya zamani, watu tunaongea uhalisia wewe unaleta nadharia, ujue hapa tunaongelea maisha halisi yaliyokuwepo hatuchambui riwaya wala mashairi
Embu Jaribu Kujadili pia Familia Ambazo zilikuwa na Furaha baina ya pande mbili au hazikuwepo??
Wewe mbona haujadili ndoa zilizo na furaha katika era hii ya feminism unajadili kama kwamba zote zina migogoro tu, by the way mimi hapa naongelea in general ila haimaanishi kwamba hakukuwa na few exceptions za ndoa zenye furaha, ila zile zisizo na furaha ndio zilikuwa nyingi kwa sababu wanaume wengi walikuwa na tabia zinazofanana ambazo wao waliona ndio uanaume ilihali kwa wanawake zilikuwa ni mateso
Maandiko sio nature Acha kutudanganya hiyo imani umeitoa wapi??
Wewe ulishasema maandiko yameandikwa na watu kama sisi alafu Unajenga hoja kuwa ni nature!!! (Ajabu)
Dooh wewe nashindwa hata nikuelezeeje maana your level of dumbness is out of proportion, nimesema kwamba watu wa dini wanaamini kuwa maandiko ya kwenye vitabu vya dini zao ni nature kwa sababu yametoka kwa miungu yao, sasa wewe unanishutumu mimi kana kwamba mimi ndio naamini hivyo wakati mimi napinga imani ya aina hiyo
Nasubiri
Kwani Hoja ilikuwa ni nini??? maana naona umehama kabisa (umepata Kauchocholo)
Kama anapungukiwa na kitu kitaje.
Anapungukiwa na uhuru wa kufanya baadhi ya vitu
Alafu kama una mambo yako unataka ujiaamulie Mwenyewe endelea kukaa Single usiolewe,,, ukishaingia kwenye ndoa hiyo ni Taasisi vigezo na masharti kuzingatiwa.
Vigezo na masharti vinatakiwa viwe ni kwa makubaliano na maslahi ya pande zote mbili, na siyo upande mmoja unajiamulia vigezo na masharti vinavyompendelea yeye kisha unataka upande wa pili ukubali tu bila kuhoji, hiyo ni taasisi ya kihuni hakuna taasisi ya namna hiyo
Sisi tunasema uhalisia.
Katika wale wa kumpa msaada nilimuweka mkewe pia sijui ulimuona??
Sasa ndio asimtegemee mkewe kwa asilimia mia akatafute msaada na huko kwingine ulikosema, mwanaume kukwama au kufilisika siyo excuse ya kuyaacha majukumu yake, vinginevyo awe tayari kukabidhi na nafasi yake maana ni wazi imemshinda
Mbona mimi nilishasema kuwa Tangu ulipoyakana maandiko nikaacha kuyatumia au uliona tena natumia Maandiko kujengea hoja??
Hongera. Umeanza kuelewa.
Mwanaume na Mwanamke hawawezi kuwa Sawa Hata iweje.
Kwenye majukumu ya kimaumbile ndio hawawezi kuwa sawa, ila kwenye mambo mengine imekuwa proven kuwa wanaweza, na utofauti wa kimaumbile siyo justification ya kuweka utofauti kwenye kila kitu
Pili Kigezo chako Kinalazimisha Mwanaume amtii mkewe kama ikitokea Mwanamke ndio anahudumia Familia na Sisi ndio tunakataa hili.
Sasa kama hamtaki kuwatii wanawake si ndio mhakikishe mnatafuta kwa nguvu na bidii zote ili isifikie hatua ya wanawake kuwasaidia majukumu yenu
Sitaki kutumia Maandiko tena wewe ulishayakana maandiko unanilazimisha mbona!!!!.
Kwani wewe unayaamini maandiko!!! sasa mbona unayajengea hoja???
Kwani wewe si ndio ulisema maandiko yameandikwa na binadamu kama sisi tuu Sasa Wewe si ndio ulikana Dini?? Unatubadilika tena??
Ni wapi nilipokana dini hebu nioneshe nasisitiza nioneshe usiniletee mawazo yako
Mind you sisi hatukatai uwajibu wa mwanaume kuhudumia Familia yake Na tunahimiza hilo ila Utiifu wa Mwanamke kwa Mumewe Haujajengwa katika huduma Hili ndio Hatulitaki sisi.
Sasa tofauti na hilo umejengwa katika nini nimeshakuambia kigezo cha nguvu na umadhubuti kinakataa hapo hivyo usikilazimishe, kwa sababu itabidi kila mwanaume awe na uwezo wa kumtawala kila mwanamke bila kujali ni nani yake, na vivyo hivyo kila mwanamke awe na wajibu wa kumtii kila mwanaume bila kujali ni nani yake sijui kwanini huoni hili tatizo kwenye hiyo hoja yako
Aliyeanza kumuuliza mwenzie nani??
Jibu maswali wacha kurukaruka
Malalamiko.
Hahaha malalamiko makubwa.
Sababu huwezi kujibu
Hata huko ulaya ulipoanza huu ufeminism ndoa hazina furaha na Pia talaka ni nyingi na In short msingi wa Familia umeshapolomoka unalizungumziaje hili??
Sasa kama kweli hali ingekuwa mbaya kiasi hicho mbona wanaume bado wanaendelea kuoa, ina maana wanaume hawapendi kupata furaha si waache kuoa basi ili tujue kwamba kweli hawazipendi hizi tabia za wanawake, kwanini kila siku bado wanaendelea kujiingiza kwenye jambo ambalo wanajua litaenda kuwanyima furaha
Jenga hoja.
Kwanza tukuulize kama hekima ni mwanamke kutochepuka jee Hilo ni manufaa kwa mwanaume pekee. Jee Kuchepuka kwa mwanamke ni sahihi au ndio kuna manufaa na mwanamke??
Sasa kama wanaume hawakutaka wake zao wachepuke si wangeoa wake wachache wanaoweza kuwamudu kuna haja gani ya kuoa wake wengi ambao unajua huwezi kuwatosheleza, na badala yake unaenda kuwatesa kwa kuwakeketa sasa hapo ujinga ni wa nani, yani hoja ni kwamba kwanini umtese mtu mwingine kwa sababu tu ya ubinafsi wako halafu uje useme eti anafurahia hayo mateso
Pili hata tohara ya wanaume nayo inapunguza Radha ya tendo pia ni jambo lenye maumivu unalizungumziaje hili??
Hili ndio kwanza nalisikia kwao naona umeamua kuwa daktari uchwara sasa
Mind you kuna kampeni ndogo Ndogo zimeanza kupinga Tohara ya wanaume kama ilivyo kwa wanawake.
Hizo kampeni zimeanzishwa na kina nani na je kwani tohara kwa wanaume ilianzishwa na wanawake si walianzisha wanaume wenyewe, kwamba wanaume walianzisha tohara kwa faida ya wanawake ndicho unachotaka kusema, hiyo ni tofauti na ukeketaji kwa sababu ukeketaji haukuanzishwa na wanawake bali ni tamaduni zilizowekwa na wanaume kisha wanawake wakalazimika kuzifuata tu
Wapo Wengi mno Bi Jadda nahisi umezungukwa na Feminist wenzako pekee hujawahi Kuyaona maisha kinyume na Ya Ki Feminism.
Mimi siishi ulaya niko hapa hapa afrika ambako bado kuna masalia ya wanawake wanaounga mkono mfumo dume na wengi ni either hawana elimu au ajira narudia hakuna mwanamke mwenye hivyo vyote atakubali kuwa chini ya mwanaume kubali ukatae, ukitaka kuendelea kukaza kichwa na kujifariji sawa maana hiki ndicho wanaume mlichobaki kufanya kwa sasa mnajifariji na mnadanganyana kwamba wanawake wazuri na wema bado wapo wengi sana, kumbe huku kwa ground mambo ni tofauti matokeo yake mnaoa chui waliojificha kwenye ngozi za kondoo halafu baadaye mnakuja kutupigia makelele humu oo kataa ndoa ni utapeli mara oo wanawake hivi wanawake vile kumbe mnajenga matarajio makubwa halafu mkija kukutana na hali halisi mnachanganyikiwa
Unatudanganya Mi nachojua ukizungumza Informal Education ni Jando(Kwa wanaume )na Unyago(kwa wanawake)
(Umefirisika)
Dooh kwahiyo na jamii ambazo hazikuwa na jando na unyago maana yake hazikuwa na informal education, asee hebu vitu vingine jaribu hata kuenda google basi ikusaidie ili usiwe unaumbuka kama hivi, halafu unakazia kabisa eti "mi nachojua" sasa hapa hatujadili wewe unachojua bali tunajadili uhalisia kwa sababu kwanza haujui na kwa bahati mbaya hautaki kukubali kwamba haujui
Malalamiko.
Sasa mbona unauliza swali alafu unajibu mwenyewe. Kwani Boss wako akiwa anakupangia cha kufanya na kutofanya wewe unapata madhara gani??. U Feminism ni Ujinga.
Ndio maana nikakuambia kitakachokufanya ukubali boss wako akupangie ni mshahara na siyo kile cheo chake, ndio maana boss asipokulipa mshahara unaanza kuona ugumu na uzito kumtii tena na unaweza hata ukaacha hiyo kazi, feminism siyo ujinga bali ni matokeo ya wanawake waliokataa utumwa uliojificha kwenye mwamvuli wa mfumo dume
Nasisitiza Katika ngazi ya Familia Baba ndio kiongozi na katika ngazi ya Jamii basi mwanaume ndio kiongozi (mtawala) Sasa sisi Wanaume sio vichaa kwamba nikukute barabarani nianze kuonesha umwamba sijui nikuamrishe. Yaani unazungumza mambo hayapo kabisa.
Ndio kwani mwanaume akimkuta mwanamke barabarani hawezi kumuagiza mahali mfano dukani na hiyo ya barabarani ni mfano tu ila hoja yangu ni kwamba kwa kuzingatia kigezo cha nguvu na umadhubuti basi mwanaume yeyote anaweza kumtawala mwanamke yeyote akiamua bila kujali ni nani yake
Wewe uiniuliza Uhusiano uliopo mimi nimejibu unalalamika tena!!!
Sasa ulishindwa kuleta uhusiano uliopo kwa kujenga hoja nje ya dini, na ndio maana nikakuambia wewe unahamahama ukiona huku huna hoja unahamia upande mwingine, haya kwa vile umesema hutahusianisha tena na dini basi lete uhusiano uliopo nje ya dini
Ampende kwa Sababu Yeye ni ubavu wake.
Okay kwahiyo hata kama huyo mwanamke hatimizi majukumu yake na ni mjeuri bado mumewe ataendelea kumpenda tu siyo
Unakimbia kimbia tuu Siku nyengine usitumie Kuchukia na kuona fahari Sehemu moja Sawa??
Hoja zinakupiga chenga unatafuta visingizio, hadi sasa wewe ndio uliyekimbia hoja zangu nyingi yani umeziacha tu juu kwa juu, sasa naona umejishitukia unaamua kutumia mbinu nyingine ya kujifanya kwamba mimi natumia maneno yasiyo sahihi ili uzipotezee hoja zangu kiujanja
Sawa ila Siku nyengine usirudie kusema Mshahara ni Huduma sawa??
Hapo napo unafanya kile kile
Nimejibu huko juu.
Walioanzisha u Feminism.
Kina nani jibu
Kwani Atheism ni nini na UPAGANI ni nini??
Si unaona sasa kumbe hata hujui kutofautisha kati ya atheism na paganism kazi kuropoka na kubwabwaja tu, atheism ni kuikana miungu yani unakuwa huamini kama kuna any supernatural being aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ila paganism ni kutokuamini dini yoyote yani unakuwa unaamini kwamba kuna supernatural being aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo ila unaamini hayuko kama dini zinavyomuongelea
Physical appearance sio nature??
Kwani Physical appearance sio Nature??? Naomba jibu.
Hivi unaelewa hata ulichouliza kweli sasa kumuogopa mnyama kwa sababu ya physical appearance maana yake hiyo physical appearance ndio inakuwa siyo nature, mimi nimesema uoga wa aina hiyo siyo nature kwa sababu hujamuogopa yule mnyama kwa kuwa unajua ni hatari bali umemuogopa kwa sababu ya muonekano wake, kwa maana kwamba ukikutana na mnyama hatari mwenye muonekano mzuri hutamuogopa kwa sababu hujajua kama ni hatari na muonekano wake haukutishi
Sasa huo si ukichaa umkute mtu barabara umuamlishe au umkataze vitu!!!!. Nadharia zako zinachekesha.
Ndio unaweza kumtuma mahali fulani
Jambo ni Gumu kwa Feminist ila ni Jepesi kwa wanawake(pure)
Haya katika scenario kama hiyo mwanamke anatakiwa amtii mwanaume kwa kigezo gani, hapa ulikurupuka kujibu ila hujajua kama umejifunga, nasubiri jibu la hapa ili sasa nizidi kuthibitisha na kupigilia msumari hoja zangu za juu kule
Wewe ndio bingwa wa malalamiko mimi naendeleza kile ulichoanza tu, naona sasa umeshika adabu umeacha kujisifia eti oo namwaga elimu, ndugu mwalimu hiyo elimu yako inatia mashaka sana yani waalimu wote wangekuwa waongo na wapotoshaji kama wewe hii dunia sijui ingekuwa wapi asee