Utii wa wanawake wa kisasa

Utii wa wanawake wa kisasa

Muktadha wa hoja yako umejikita kwenye UTII Vs HUDUMA.

Kipi kinatakiwa kuanza kati ya hivyo viwili?

-Kaveli-
Mkuu sidhani kama hilo ni suala la kipi kinatakiwa kuanza, mkishaingia tu ndoani kila mmoja anatakiwa aanze kutekeleza majukumu yake papo hapo, wala si suala la kusubiri fulani aanze au kushindana
 
Hiki ni kisingizio tu kuhalalisha ujeuri wako, utiifu upo ndani ya mtu naturaly tu. Utiifu wala hautolewi kwa masharti.
Wewe unachanganya utii ule tunaouonyesha kwa wazazi, unataka kuuleta kwa mpenzi/mume.
Wazazi tunawaheshimu sababu wanatuhudumia bila manung’uniko, ila nyie wanaume huduma sifuri, mmejaa viburi na mitabia ya hovyo.!!
Sasa mtu km huyo nimtii wa kazi gani??
 
Sasa. Anatokea punda anakomaa kabisa anasema haijalishi. Mwanaume lazima aheshimiwe!!! No thank you:
Hapa ndipo wanapotuonaga sisi wabaya, yani mtu hatimizi majukumu yake anataka msaidiane 50/50 halafu hapo hapo anataka heshima, ndio kina Natafuta Ajira hao eti asili sijui ni asili gani hiyo inayochagua upande
 
Mkuu sidhani kama hilo ni suala la kipi kinatakiwa kuanza, mkishaingia tu ndoani kila mmoja anatakiwa aanze kutekeleza majukumu yake papo hapo, wala si suala la kusubiri fulani aanze au kushindana
Vipi kuhusu wapenzi ambao bado hamjaingia ndani ya ndoa. Kila mmoja anaishi kwake, hapa mwanaume anawajibika kutoa izo huduma vinginevyo hakuna utiifu? na vipi kuhusu wanandoa ambao wote mna kipato hapa mwanaume atawajibika kutoa izo huduma vinginevyo hakuna utiifu?
 
Wewe unachanganya utii ule tunaouonyesha kwa wazazi, unataka kuuleta kwa mpenzi/mume.
Wazazi tunawaheshimu sababu wanatuhudumia bila manung’uniko, ila nyie wanaume huduma sifuri, mmejaa viburi na mitabia ya hovyo.!!
Sasa mtu km huyo nimtii wa kazi gani??
Wala sijachanganya chochote. Nimeongelea utiifu kama tabia ambayo ipo ndani ya mtu kiasili kama tabia zingine mfano wizi, unyanyasaji, ulevi n.k.. yaani ni tabia ambazo mtu anajikuta anazi-practice tu automatically. Kama wewe sio mnyanyasaji mtu akikunyanyasa utaachana nae tu ila ukilipiza kumnyanyasa wote mnakua wanyanyasaji hauwezi kusema nimemnyanyasa kwa sababu na yeye alininyanyasa. Hauwezi kutumia kosa kuhalalisha kosa.
Ukishaweka kigezo cha pesa ili nawe uwe mtiifu hapa uta-practice utiifu kwa kuigiza tu mirija ya pesa ikikata automatically na utiifu utakata.
 
Sasa alichoandika hapo kina shida gani, hiyo asili ya mwanamke kumtii mwanaume inaendana na asili ya mwanaume kumhudumia mwanamke na mimi wala sipingi hilo, mimi napingana na wanaotaka mwanaume na mwanamke wasaidiane majukumu halafu bado wanataka utii
hapo nimekuelewa.
 
Hapa ndipo wanapotuonaga sisi wabaya, yani mtu hatimizi majukumu yake anataka msaidiane 50/50 halafu hapo hapo anataka heshima, ndio kina Natafuta Ajira hao eti asili sijui ni asili gani hiyo inayochagua upande
Mkuu naomba nionyeshe wapi nilishakubaliana na wanaume ambao hawatimizi majukumu yao kama mume. Kwa kifupi ni kwamba sikubaliani na 50/50, sikubaliani na unyanyasaji wa wanawake, sikubaliani na wanaume wote ambao hawatimizi majukumu yao kama mume(naomba nieleweke hapa nimesema mume sio boyfriend), sikubaliani na wanaume wanaozalisha wanawake na kuwaacha single mother(labda kama uyo mwanamke mwemyewe alikua ndie chanzo cha yeye kuachwa)
 
Back
Top Bottom