Bado Hujajibu Bi Jadda Nani Aliwanyima Hiyo Fursa Wanawake na Akawapa Wanaume,,, Wanaume Walipewa Hiyo Fursa Ya kuwazuia Wanawake Kujitetea na Nani?
Hivi kwanini unaandika maelezo marefu halafu unarudia vitu vile vile ambavyo nimeshafafanua yani ni kama unakuwa unanirudisha nyuma, nimeshakuambia wanaume ndio walijipa hayo mamlaka kupitia maandiko na tamaduni mbalimbali ambavyo walivitunga wao wenyewe bila kuwashirikisha wanawake, kwahiyo wanaume walitumia maumbile yao kujipa utawala wa mabavu dhidi ya wanawake na kudai kwamba ni nature ndio imeamua hivyo eti kwa sababu za kimaumbile tu
Sasa ndio Tukuulize Wewe bi Jadda Kabla ya mimi kutoa maelezo malefu Juu ya Hili Tumbie Hao Wazungu Waliwatawala Mababu zetu kama wakoloni Kwa Kuwa walikuwa wanatoa Huduma??
Sasa wewe unadhani wazungu walikuwa wanakalia ardhi ya waafrika hivi hivi tu, wao si ndio walioleta maendeleo kwa kujenga miundombinu mbalimbali, ambayo hata waafrika walikuwa wakifaidika nayo
Hujawa Muadilifu katika Hili Kwamba Wanawake Wamejikomboa Wenyewe kwa Kuona Wanauwezo wa Kutafuta Pesa?? Unahisi Bibi Zetu Walikuwa Hawajui Kwamba Wanaweza Kutafuta pesa?? Labda utakuwa Hujui Historia ya Feminism.
Bibi zetu walikuwa wameshaaminishwa kwamba mwanamke hatakiwi kutoka kuenda kutafuta pesa anatakiwa afanye kazi za nyumbani na shambani, feminism ilipoanzishwa ndipo wanawake wakaanza kuona kwamba kumbe wana uwezo wa kutafuta pesa na maisha mengine yakaendelea, ndio wanawake wamejikomboa kwa sababu kwa kiasi fulani imewafanya nao wawe ni sehemu ya ushauri na maamuzi ndani ya familia tofauti na zamani ambapo walikuwa wanahudumiwa hawakupewa hiyo nafasi
Haya Maelezo yako Yanasikitisha Kwa Sababu mimi Sijasema Mume Kashindwa kutafuta shughuli yoyote (Mbona unayachukulia mambo in negative way always!!) Wewe unayajua Maisha kwamba kuna kupanda na kushuka kuna kufukuzwa kazi kuna kukwama kila jambo unalolifanya Unayajua haya. Sasa haya hutokea katika Familia na Mama anaweza kumsaidia Baba katika kipindi hicho Ndio nikauliza Jee Sasa Kuanzia Hapo Kichwa cha Familia atakuwa Mama (Pia inabidi ujue Kichwa cha Familia Kinakuwa na Majukumu Gani alafu hayo majukumu Mpe Mama Wakati Baba Yupo alafu Pima Kama Inawezekana..)
Sasa labda nikuulize vipi kwa wale wake ambao ni wamama wa nyumbani halafu mume akafukuzwa kazi na shughuli nyingine zote zikakwama inakuwaje hapo
In Short Ulitakiwa useme Wanawake wameumbwa Dhaifu (Weak) kuliko wanaume. Alafu sasa Litumbukize hili Katika ile Law ya Survival of fittest.( Sijui kama utakuwa umegundua kitu?)
Ndio maana nikasema kuumbwa dhaifu siyo hoja bali inatakiwa kuspecify je wameumbwa dhaifu katika angle gani, ninyi mmejitangazia utawala kwa kuzingatia angle moja tu ya nguvu za mwili, ndio mnatakiwa mseme sasa ni kanuni gani inayoamua kwamba nguvu za mwili ndio ziwe kigezo cha kutawala na si sifa nyingine
Aisee Bi Jadda Unasikitisha Sana Yaani Kigezo cha Nguvu na Maumbile sio Kigezo cha Kuwa Mtawala!! Aisee Mbona kama Upo Nyuma Sana Katika hili. Ule mfano wangu Wa Mke akimtawala Mumewe alafu Muwe Siku Akiaamua kumchalaza Makofi Hujauzingatia kabisa.
Kuwa na uwezo wa kumcharaza mtu makofi siyo kigezo cha yeye kukutii labda kukuogopa tu, vinginevyo uelezee hii ni kanuni ya wapi yani unatakiwa uelezee msingi wa hizi kanuni zako, siyo unalazimisha tujadili kwa kutumia mitazamo yako binafsi au kwa kutumia doctrines ambazo ziliwekwa na binadamu kama sisi na kudai ni nature
Bi Jadda Ni kweli kwamba Haya mambo huyaelewi au Unalazimisha Kutoyaelewa Yaani Unahusisha Utawala na Kuzaa?? Hivi unajua maana ya kutawala??
Umesahau Kuanzia kule Juu tulishasema Nature ndio Imeamua Mwanaume Awe Mtawala wa Mwanamke Kama Vile Kipofu hawezi kuwa Fundi saa Tayari Nature imeamua hivyo Pia Kiwete Hawezi kwenda Shamba kulima Iyo ndiyo nature Na pia Wanawake hawawezi kuwatawala Wanaume Kwa Sababu Huwezi kukitawala kitu ambacho wewe ni Dhaifu kuliko hiko kitu.
Haya maelezo yako yanadhihirisha kwamba hujanielewa ila unaandika mradi tu ubishe, ndio maana unajaza risala na unanipa kazi ya kuelezea yale yale kila wakati, mimi hoja yangu tangu mwanzo ni kwamba kila mmoja ajitawale mwenyewe yani kusiwe na ulazima wowote wa mmoja kumtawala mwenzake
Kwahivyo mimi kupinga mfumo dume haimaanishi kwamba nataka mfumo jike eti mwanamke ndio amtawale mwanaume hapana, yani kusiwe na kujipa mamlaka kwa kutumia vigezo vya kimaumbile ambavyo mwenzako hana na hakupenda kutokuwa navyo, yani kwanini umlazimishe mtu fulani kufuata mfumo fulani (ambao yeye kwa utashi wake anaona haumfavour yeye) kwa kigezo cha kwamba alizaliwa na jinsia fulani kana kwamba alichagua kuzaliwa nayo
Ndio maana nikakuambia wanaume kujipa mamlaka kwa kigezo cha nguvu ni sawa na wanawake nao waseme wanataka mamlaka kwa kigezo cha kuzaa kitu ambacho siyo sawa, kwahiyo mimi hoja yangu ni kwamba kila mtu afanye majukumu yake kulingana na maumbile yake na yale majukumu yasiyo ya kimaumbile wasaidiane na wote waheshimiane na kusikilizana, bila mmoja kulazimisha kumtawala mwenzie kwa kudhani yeye ni bora kwa sababu za majukumu ya kimaumbile ilihali mwenzie naye ana majukumu ya kimaumbile ambayo huyo anayejiita mtawala hawezi kutekeleza
Ngoja Sasa Nikupe Faida Bi Jadda.
Moja,, Utiifu Umejengwa Katika Nguvu na Uwezo Wa Yule anayetakiwa kutiiwa na Asilimia kubwa Duniani Utiifu Baina ya Watu,, jumuiya,, Taasisi au Hata Mataifa unaangukia katika kigezo hiki.
Sasa hapo ndipo tunapopishana yani wewe unataka tujadili matokeo ilihali mimi nataka tujadili chanzo, mimi nataka kujua kwanini utiifu umejengwa katika nguvu na uwezo tu yani imekuwa hivyo kwa misingi gani, wewe unataka nikubali hiyo doctrine kwa sababu tu ndio imeshakuwa hivyo toka zamani
Pili Kuna utiifu Unaotokana na kuhitaji Social Security and Considerations (Nashindwa kuliweka hili katika kiswahili) ila huu ni Utiifu Tunaowapa Viongozi Wetu wa Dini au Watu Muhimu wenye kuheshimiwa katika Jamii.
Utiifu wa aina hiyo siyo nature
Tatu Utiifu wa Watoto Kwa Wazazi wao Ni Utiifu ambao inajitegemea na Unamaelezo yake Marefu.(Sio Muhimu kwa Hapa)
Ukitumia Hivyo Vigezo Utaona Kila Kinachotiiwa Kuheshimiwa Na Kutawala Kinadondokea katika Vigezo Hivyo aidha Kimojawapo au Kimekusanya.
Hoja siyo tu vigezo vya kupewa utii, bali hoja ni msingi wa hivyo vigezo vya kupewa utii, je ni nature au ni social constructs tu
Katika Nchi nyingi Kuna Watu Wanatii Serikali zao Kwa Sababu Zina majeshi yenye Nguvu Na sio kwa Sababu Hizo Serikali zinawahudumia wao Na siku Serikali Ikikosa Nguvu Hawatoitii Kuanzia Hapo Na Ndio Maana Unasikia Mapinduzi Katika Nchi Nyingi za Afrika.
Nafikiri unashindwa kutofautisha kati ya utii na uoga ukiweza kutofautisha hayo basi hoja zako ndio zitakuwa na mantiki, vinginevyo kwa kutumia huo mfano wako unataka kuniambia hata wanawake wanachofanya kwa waume zao ni kuwaogopa na siyo kuwatii (kitu ambacho siyo natural), by the way kinachowafanya wananchi watii serikali zao ni huduma za kiuchumi ila nguvu za kijeshi zinawafanya wananchi waogope tu
Pili Nchi Nyingi za Afrika zinaonyesha Utiifu Na Heshima Kwa Mataifa Ya kimagharibi (Wazungu) kwa sababu Hayo Mataifa Yana Nguvu za Kijeshi na Uwezo Wa Kiuchumi (Sio Huduma).
Hapa tena narudia kukuambia tofautisha kati ya utii na uoga, kinachofanya nchi masikini kutii nchi tajiri ni kwa sababu ya faida za kiuchumi wanazopata kupitia mikopo misaada na uwekezaji (utii wa aina hii nao pia siyo nature), hizo nguvu za kijeshi zinafanya nchi masikini ziogope tu nchi tajiri na siku zote kumuogopa mtu siyo natural trait bali ni instilled mentality baina ya watu
Sasa Nikwambie Bi Jadda HUDUMA kama ulivyong'ang'ania Ni "ZAWADI" anayotoa yule Mtawala kwa wale anaowatala yaani Wanaomtii. Sasa Zawadi Haifanyi lile Kusudi La Utiifu Kuondoka Au Kuingia Kwa Sababu Sio Kigezo cha Utiifu.
Sasa Mababu Zetu Walikuwa Wanatoa Huduma Kwa Wake zao waliokuwa Wakiwatii Kama Zawadi Kwa namna Mbalimbali Mfano Kuwalinda Kutokana na Hatari ,, Kuwapambania Vitani na kukubali wao wauawe lakini Wake zao na Watoto wao Wapone. (Japo mara kwa mara mmekuwa mkiwashutumu Mababu zetu Bila kusahau vita zote walikuwa wanaenda wao kufa kwa ajili ya wake zao na watoto Wao).
Pia Huduma Katika Kufanya Zile kazi Ambazo zinahitaji Nguvu Nyingi Kama Kujenga,, Kuchimba visima Hizi zote ni Huduma Na Ni Zawadi Walikuwa Wanatoa.
Na Kama Mtawala asipotoa Zawadi hii Jamii itamshangaa na Wazee lazima Wakae nae Huyo Mwanaume kwanini Hatoi Huduma Ambayo ni Zawadi Ya Kutiiwa kwake?? (Na ndio maana kulikuwa na kitu kinaitwa JANDO mwanaume anafundishwa Wajibu wake katika Familia).
Hii Ni Kanuni Ya Asili kwamba Mtawala hutoa Zawadi ya Huduma Lakini Haimaanishi Ni lazima Mtawala atoe Huduma ndio Atawale HAPANA.
HIvi unaelewa hata ulichokiandika kweli jambo likishakuwa wajibu linakuwaje zawadi tena hivi unajua tofauti kati ya wajibu na zawadi, wajibu ni jambo ambalo mtu lazima alifanye ila zawadi ni hisani au hiyari tu ni kitu ambacho mtu anaamua yeye akupe au asikupe na siku zote zawadi hailazimishwi kutolewa ukiona zawadi inalazimishwa ujue hiyo siyo zawadi tena bali ni wajibu, sasa wewe unataka kudanganya hapa kwamba mwanaume kumhudumia mkewe ni hisani au hiyari wakati kwa tamaduni zetu ni wajibu
Kuhusu masuala ya wanaume kupigana vita sijui kupambana na majambazi sijui kwanini huwa mnapenda kutolea hiyo mifano kana kwamba vita au ujambazi ni sehemu ya maisha ya kila mtu, kwani ni wanaume wangapi kuanzia wanazaliwa hadi wanakufa uzeeni hawajawahi kuexperience hayo mazingira, kwanini mnatolea mifano ambayo siyo daily activities kama yalivyo majukumu ya wanawake ya kila siku
Na hata kama tukichukulia hao wanaume ambao wameexperience hayo mazingira au tukichukua hayo majukumu ya ujenzi sijui uchimbaji visima bado tunarudi pale pale kwamba hayo ni majukumu ya kimaumbile, huwezi kutegemea mwanamke akapigane vita ambavyo huanzishwa na wanaume na huhusisha wanaume tupu au apambane na majambazi (ambao wengi huwa ni wanaume) wakati maumbile yao hayafanani, hapo obviously mwanamke atashindwa kwahiyo ili iwe fair battle ni lazima wapambane watu wenye maumbile yanayofanana na si vinginevyo
Ndio maana hata kwenye mchezo wa boxing ili pambano liwe fair lazima wanaopigana wawe na uzito unaokaribiana ndio maana kuna featherweight sijui heavyweight nk, huwezi kumuweka mtu mwenye kilo 90 apambane na mtu mwenye kilo 50 pamoja na kwamba wote ni wanaume wewe unadhani ni kwanini yani kwanini wasiwapambanishe kwa kuzingatia jinsia zao na siyo kilo zao, halafu futa hiyo kauli kwamba wanaume wanapoenda vitani wanawapigania wake zao na watoto wao tu bali wanapigania taifa lao au jamii yao kwa ujumla kwa sababu humo kuna wazazi wao, walezi wao, ndugu zao na jamaa zao nk (ambao hawalazimiki kukutii kwa sababu eti umeenda kuwapigania vitani sasa iweje mkeo ndio alazimike kukutii kwa sababu hiyo) au unataka kusema kila mwanaume anayeenda kupigana vita ana mke na watoto hakuna ambao wako single kabisa
Anyway kwahiyo wewe unaona ni sawa kumtambia mwenzio kwa kuweza kufanya jukumu ambalo mwenzio hawezi kufanya kwa sababu hana maumbile kama yako, na ndio maana nikatolea mfano wa mwanamke kuzaa je wewe unaona ni sawa mwanamke kumtambia mwanaume kwa kuweza kubeba mimba na kuzaa, (jukumu ambalo mwanaume hawezi kufanya kwa sababu hana maumbile kama ya mwanamke) au wewe unadhani kuzaa ni jukumu jepesi, hata mwanamke anapoamua kuzaa anarisk maisha yake pia lile ni suala la kufa na kupona ndio maana nikasema bora wanaume mngejitangazia utawala kwa kuzingatia jukumu la huduma za kiuchumi kidogo mngeeleweka, kwa sababu hata wanawake wanaweza kujihudumia kiuchumi ila wakiamua wenyewe kukubali kukaa nyumbani na kuhudumiwa basi hawana budi kuwatii wale wanaowahudumia
LEO HII HATA KAMA WAZUNGU HAWATALETA MSAADA WOWOTE AFRIKA,, MATAIFA YA AFRIKA HAYAWEZI KWENDA KINYUME NA AGENDA NA AMRI ZA MATAIFA MAKUBWA WEWE UNAHISI NI KWANINI?? JIBU NI KWA SABABU WANAJUA UWEZO WAO NA NGUVU YAO WALIYONAYO.
Hili sikubaliani na wewe kwa sababu ni uongo hata leo hii kuna nchi nyingi tu zimetuzidi kiuchumi na kimedani na zina uwezo wa kutufanya chochote zikiamua lakini hatuzitii kwa sababu hakuna zinachotusaidia, ukweli ni kwamba hayo mataifa ya magharibi tunayatii kwa sababu tunafaidika nayo kiuchumi hakuna sababu nyingine na hata wao wenyewe wanajua hilo siku wakiacha kutupa misaada kiuchumi basi huu utii wetu (ambao na wenyewe siyo nature) utakufa, kitakachobaki kitakuwa ni ule uoga tu kwamba wametuzidi kimedani hivyo tukizingua wanaweza kutufanya chochote muda wowote and mind you uoga siyo nature ndio maana nikakuambia unatakiwa kutofautisha kati ya utii na uoga