Bi Jadda Unajua Unachokiandika Kweli Unaposema Wengi Unajua Unamaanisha Nini?? Unaposema Wengi It's means Sio Wote. Bado Hujajibu.
Yani mimi najibu hoja zako halafu wewe kwa sababu zako binafsi tu unaamua kukataa majibu yangu, kwa kisingizio kwamba sijajibu au unataka nijibu vile unavyotaka wewe, hebu acha huu ujinga kama umeishiwa hoja sema usilazimishe kuandika pumba mradi tu usionekane umeshindwa na huna majibu
Hata Anaezaliwa Kipofu Yeye Hakutaka Iwe Hivyo ila ndo imeshatokea Sasa Kuna Vitu Lazima Atavikosa Kwa Yeye Kuwa Kipofu na Wale Ambao sio Vipofu Watavipata Hiyo Ndio Mipango ya Mungu Au Tuseme Nature Maana ili Uwe Feminist lazima Kwanza Uyakane Maandiko Matukufu.
Sasa ni kanuni gani inayoamua kwamba binadamu mwenye macho mazima ni bora zaidi ya kipofu, na ana mamlaka ya kumtawala kipofu kwa sababu tu ya hizo tofauti za kimaumbile, na hayo unayoyaita maandiko matukufu ni kwa mujibu wa nani
Vigezo Mbona Tulishavitaja Tangu Huko Mwanzo Kwamba ni Nguvu na Uwezo Sasa Tunaposema Nature tunamaanisha Nature Ndio Imeaamua Mwanaume Awe na Nguvu na uwezo mkubwa Kuliko Mwanaume.
Hata Sisi Tunawatawala na Kuwadhibiti Wanyama Kwa Sababu Ya Aidha Nguvu Zetu Au Uwezo Wetu Mkubwa Wa Akili. Ila Sio Kwamba Tunawahudumia.
Sasa ni nature ya aina gani inayoamua kwamba utawala utokane na maumbile ambayo mtawaliwa hana na hakupenda kutokuwa nayo na mbaya zaidi hafurahii huo utawala, hebu acha porojo zenu hao wanyama tuna uwezo wa kuwatawala na kuwadhibiti ikiwa tu tunawafuga na kuwahudumia au wewe nenda kaingie kwenye msitu wa wanyama wakali na silaha zako (ambazo unahisi ndio zitakupa jeuri) halafu uone kama watakutii, kitakachokukuta ndio utajua kwamba hizo propaganda zenu hazifanyi kazi kwenye uhalisia au wewe ulimaanisha hawa wanyama kama paka, mbwa, sijui ng'ombe na mbuzi tu ambao nao lazima uwahudumie au nenda kajaribu kuvamia nyumba yenye mbwa wakali halafu uone kama hao mbwa watakupa utii
Sio kweli kwamba mara Nyingi Anayetawaliwa Anakuwa Hana Furaha. Bibi Zetu Waliishi Maisha ya Furaha Na Babu zetu Na hayo maisha Sisi Tumeyashuhudia(usilete Peculiar cases za Manyanyaso za baadhi ya jamii hakuna Anaekubaliana na Hilo Kwa Sababu kuwa Mtawala haimaanishi uwe mnyanyasaji) Ila Sasa hivi Ndio Hakuna Furaha wala amani katika Ndoa kwa sababu Mnalazimisha Kwenda kinyume na Nature.
Wewe Unaitii Serikali ya Tanzania Jee Huna Furaha ,, unamtii Boss wako jee Huna Furaha unaongea Vitu ambavyo hazipo kabisa.
Manyanyaso ni nini na unayatafsiri vipi, sasa hivi ambao hawana furaha na amani kwenye ndoa ni wanaume kwa sababu hawataki kukubaliana na ukweli kwamba wanawake hawapendi kutawaliwa na ndio maana siku hizi malalamiko mengi kwenye ndoa yanatoka kwa wanaume kuliko wanawake, achilia mbali mimi tu hivi kuna mtu yeyote ambaye anafurahia kuitii serikali yake bila sababu au kuna mtu ambaye anafurahia kumtii boss wake bila sababu sijui hata kama unaelewa ulichouliza au ndio tayari umechanganyikiwa kwa kukosa hoja
Bi Jadda Mbona Tunaliludia hili mara kwa Mara kuwa Ni Nguvu uwezo na Umadhubuti aliokuwa nao Mwanaume Kulinganisha na Mwanamke na pia hilo linakubali katika vitu vingi Vinavyotawaliana Hatusemi Utawala upo tu From no Where Bali Tunaelekezea Hivyo Vigezo kwa Nature sababu Hakuna Alieamua Mwanamke awe Dhaifu na Mwanaume awe Madhubuti. Imetokea tuu Hivyo. Au labda wewe unajua kwa nini??
Sasa kama hakuna aliyeamua mwanaume kuzaliwa madhubuti na mwanamke kuzaliwa dhaifu kwanini ninyi mjiamulie kwamba utawala utokane na hizo sifa za umadhubuti tu na si sifa nyinginezo, mnawashawishije hao mnaotaka kuwatawala ili wakubali kutawaliwa mind you lazima kuwe na sababu ya kumshawishi huyo unayetaka kumtawala akubali kutawaliwa huwezi kumtawala hivi hivi tu bila sababu yoyote, hakuna utawala wa aina hiyo narudia hakuna mtu anayekubali kutawaliwa bila faida yoyote anayopata toka kwa huyo anayemtawala hili ndio nalisikia kwako na mbaya zaidi haujui kulitetea kwa hoja
Mimi Sio Mzungu Wala hapa Hatujadili Weusi na Wazungu Tunajadili Wanaume na wanawake. Hao Wazungu Kama Wanadai Hivyo Inabidi Wathibitishe Ni Nature How?? Usinisukimizie Upande Nisiokuwepo.
Si ndio nilikuambia wazungu walithibitisha hilo kupitia maandiko ya kwenye biblia kuhusu watoto wa Nuhu ambao ni Shem, Ham, na Jafet, kama wewe ni wa dini nyingine basi inabidi tukubaliane kuacha kutumia references toka kwenye vitabu vya dini kwa sababu hatutaelewana, hapo nilikuwa nakuonesha jinsi mifumo ya hii dunia inavyofanya kazi kwa propaganda na si nature kwahiyo huo mfano nilioutoa wa ukoloni ni relevant kabisa hata ukibisha
Naweza kusummarize Kwa Maneno Machache kuwa Feminism and Atheism and Homosexuality Ni Ndugu Wa familia moja Kwa ajili ya Kuharibu Ulimwengu.
Mimi nimekuuliza kuhusu feminism halafu wewe unaniletea habari za atheism na homosexuality hivi unaona kuna uhusiano kati ya swali langu na hilo jibu lako kweli, yani ni sawa mimi nikuambie unifafanulie kuhusu physics halafu wewe uniambie kwamba physics, chemistry na biology ni ndugu wa familia moja kwa sababu tu zote ni science, au ni sawa nikuambie unifafanulie kuhusu mahakama halafu wewe uniambie kwamba mahakama, bunge na utawala ni ndugu wa familia moja kwa sababu tu yote ni mihimili ya serikali hivi unaona kuna uhusiano hapo
Acha kutudanganya Bi jadda hakuna Jibu Umetoa Kama lipo Nenda kalinukuu Ulilete hapa.
Nimekujibu hivi bila kupepesa macho kama mke ndiye anayemhudumia mume basi mume hana budi kumtii huyo mke je sikukujibu hivyo wewe, kama unaona hilo haliwezekani waulize wale wanaume wanaoitwa mamarioo sijui vibenten wanaohudumiwa na wanawake kwamba kati yao ni nani anayemtawala mwenzake, ndio maana mimi tangu mwanzo hoja yangu ni kwamba ili kuepuka hayo yote ni heri kila mmoja ajitawale mwenyewe na kujifanyia maamuzi juu ya maisha yake kusiwe na wa kumtawala mwenzie regardless of majukumu..haya nijibu swali langu je kama mke ni mama wa nyumbani na mume akakwama kiuchumi anafanyaje
Unatuchanganyia Mada Bi Jadda Hapa Hatujadili Wazungu na Waafrika Nishasema hayo madai ya Wazungu wanatakiwa Wathibitishe wao wenyewe mimi sio Mzungu. Mimi Nazungumzia Wanawake na Wanaume na Nimeshasema Ni Nature kwa Sababu zipi.
Ndio wazungu walishathibitisha sasa kwamba huo utawala ni nature na upo kibiblia, kwahiyo hata watu weusi hatukutakiwa kupinga ukoloni wala kudai uhuru tulitakuwa tuwaache wazungu waendelee kututawala kwa sababu kwa mujibu wao hiyo ni nature, wewe mpaka sasa bado hujaelezea msingi wa hiyo nature zaidi ya kuniletea habari zilizo kwenye maandiko na tamaduni huku ukichanganya na hisia zako binafsi..yani kwa kifupi hadi sasa hakuna swali lolote ulilojibu zaidi ya kupuuzia hoja zangu na kutoka nje ya mada
Ili uwe Feminist lazima Uyakane Maandiko Kwanza ndio Maana nikasema kule juu Feminism na Atheism ni Ndugu kwa ajili ya kuharibu Vizazi(ulimwengu) Sisi Tunaamini Maandiko Matakatifu ni Maneno Ya Mungu aliyoyateremsha kwa Mitume Wake. Mungu ndiye Aliyetuumba na kutupangia Mambo na Kanuni. Labda nikuulize Unaamini katika Mungu na Dini na Vitabu vyake??
Ni mungu yupi sasa unayemzungumzia maana kuna miungu zaidi ya 1000 kulingana na dini zilizopo duniani kwa sasa, wewe unao ushahidi gani kwamba hayo maandiko yalishushwa kwa mitume kutoka kwa mungu na ni wapi huyo mungu mwenyewe alisema hivyo, feminism ni matokeo ya watu kuwa open minded na unprejudiced na kukataa kukubaliana na kila porojo wanazo mezeshwa na wanaume na mfumo dume
Maandiko Matukufu sio Maandiko ya Mwanadamu. Mwanadamu ni Messenger Tuu.
Ushahidi wa hili
Uvulana unahusika nini Hapa Bi Jadda??
Wewe probably ni mvulana kwa sababu ungekuwa mwanaume ungekuwa unafikiria kama wanaume, mind you uvulana au uanaume siyo suala la umri bali akili, kitendo cha kupinga uhalisia ambao hata tamaduni zetu zinaufahamu kinadhihirisha hilo
Kwaiyo Unatudhibitishia Kuwa Mwanamke Akianza Kutafuta Mali Hatomtii Mume wake??. Ndio ujue kuwa Huduma sio Kigezo cha Utiifu. Ili kitu kiwe kigezo cha kitu Furani basi kuwepo kwake kutasababisha jambo na kutokuwepo kwake Kutafanya Jambo Lisiwepo.
Hapana wewe ndio ulitakiwa ujue kwamba utii siyo suala la nature na hili nimeshalifafanua, na ndio maana mwanamke ukiwa unamhudumia ndio atakubali umtawale ila ukiwa humhudumii basi usitegemee utamtawala, yani huo ndio uhalisia utii hauji tu hivi hivi huletwa na jambo fulani na mara nyingi huyo anayetii anakuwa anapenda na si kulazimishwa
Sio Kweli Bibi Zetu Waliishi Kwa Amani na Babu Zetu Na Tuliyashuhudia maisha ya Amani katika Ndoa Zao.
Unalinganisha Ndoa za Babu zetu na Hizi Za Siku hizi leo inafungwa kesho Imevunjika. Embu tupe Comparison kuwa Now Ndoa zina Furaha na Amani na Zinadumu Kwa Sababu Feminism imepiga Hatua Ukilinganisha Na Zama hizo. Leta Comparison hapa.
Ndoa za zamani zilikuwa na furaha kwa sababu tu wanawake hawakuwa na sauti wala uhuru wa kujieleza na kusema mabaya yanayowakumba tofauti na sasa hivi ambapo wanawake wana elimu na uhuru wa kujieleza hivyo wakiyasema mabaya yenu mnawaona kama maadui na kuwaita feminists, ni sawa na kuchukulia mfano wa nchi yenye utawala wa dikteta na kusema kwamba wananchi wa hiyo nchi wana furaha sana kwa sababu wanaitii na hawaipingi serikali yao ila kumbe kiuhalisia wameufyata tu kwa sababu hakuna demokrasia wala uhuru wa kujieleza maana wanajua wakifanya hivyo watashughulikiwa na vyombo vya dola, kama kweli unaona wanawake walikuwa na furaha kwa sababu tu ndoa zao zilikuwa zinadumu kwahiyo unataka kusema kwamba hata kukeketwa napo wanawake walikuwa wanapenda (bila shaka unajua mwanamke akikeketwa hakuna raha yoyote anayoipata kwenye tendo) walikuwa wanakeketwa ili tu wasichepuke wawalindie waume zao kwahiyo unataka kusema hili nalo wanawake walilifurahia na kama hawakufurahia kwanini hawakuresist tangu mwanzo kabisa
Usiwasingizie Bibi Zetu. Wao Hawakuwa na Makucha Yoyote. Nyinyi Mmekuwa Manipulated Umejaziwa Fikra mkaona Ndio uhalisia. Nyinyi Mmeuvua Uanamke, mnataka mmvae Uanaume. Hakuna Suala kuwa Rangi halisi sijui vitu gani Hizo ni Propaganda tuu.
Babu zetu Walikuwa wanatekeleza Kile ambacho Kilikuwa kipo katika Uhalisia kwamba Familia Lazima iwe na Kiongozi na kiongozi ni Baba. Basi.
Kama kweli mwanamke anatakiwa kumtii mwanaume bila sababu yoyote ya msingi maana yake hata mwanaume anatakiwa kumpenda mwanamke bila sababu yoyote ya msingi, kwa vile umerejea maandiko basi kumbuka imeandikwa mwanaume anatakiwa ampende mkewe na mwanamke anatakiwa amtii mumewe, kwahiyo nakuuliza ina maana hata kama mwanamke hataki kutimiza majukumu yake mfano kufanya za nyumbani au hataki kuzaa watoto muda mumewe anaotaka unataka kusema huyo mume anatakiwa aendelee kumpenda tu huyo mke regardless of what hebu nijibu hapo bila kujizungusha
Usinibebeshe vitu Mimi Nimejaribu Kukuambia Sio kila kigezo ni Kigezo cha Utawala. Utawala una vigezo vyake ambavyo Ukiwa navyo Automatically unastahili kutiiwa na Kutawala.
Ni nani anayeamua kwamba hivyo vigezo ndio viwe vigezo vya utawala mbona unakwepa kunijibu hapa kwani una shida gani, je huyo unayemtawala naye akili yake automatically inamtuma kukubali kutawaliwa na wewe kiasi cha yeye kufurahia hilo na mambo kuflow smoothly au ndio hadi utumie nguvu kubwa, mimi nataka uniambie vigezo hivyo ni kwa mujibu wa nani na mwanamke anapotawaliwa anapata faida gani kiasi cha kukubali kirahisi
Kila kitu kina kigezo chake Vigezo haviingiliani ili mradi tuu. Mbona jambo hili lipo wazi kabisa.
Huwezi kukataa kuwa Nguvu na Uwezo ni kigezo cha Utawala wakati hii kanuni inakubali katika Maeneo Mengi sana. Boss wako ni mtawala wako kwa sababu ana Nguvu aliyopewa na Taasisi yako Raisi ni Mtawala kwa sababu Ana nguvu ambayo ameitoa kwetu kupitia Kura zetu Sisi Tunawatawala Wanyama Kwa Sababu ya Nguvu zetu na uwezo wa akili. Kwaiyo Hii kanuni ni applicable sehemu Nyingi ila kanuni ya Kutawala kwa sababu ya Huduma Haikubali katika maeneo mengi kama sio yote.
Hapo umezunguka tu ila kiuhalisia sababu kubwa inayofanya mtu amtii boss wake ni kwa sababu tu analipwa mshahara na anaogopa asipotii kibarua kitaota nyasi, hakuna mtu anayekubali kuajiriwa kwenye taasisi fulani halafu akafanye tu kazi na kufuata maelekezo ya maboss bure bure bila maslahi ya kiuchumi narudia hayupo labda wewe peke yako ndio unaweza hilo, na ndio maana taasisi nyingi pale watumishi wanapokosa mishahara yao huweza hata kuandamana na kuwagomea hao maboss wao unaodhani kwamba wanapewa utii kwa sababu tu ya nguvu au mamlaka walizonazo
Hakuna hoja Umejenga hapa.
Umetetea vyema. Ila sio Hoja. Hoja Ni kuwa Katika Familia Lazima kuwe na Kiongozi hamuwezi kuishi two bulls in one House.
Hiyo tafsiri ya two bulls ni yenu na ni subjective, inawezekana kabisa mkaishi bila kutawalana ndani ya nyumba wote mkaishi kwa kushirikiana na kusikilizana, utofauti kwenye maumbile siyo lazima uweke utofauti hadi kwenye haki na wajibu
Dunia haiendeshwi kama Taasisi Usitudanganye kila nchi ina It's own National sovereignty. Kinachofanya Nchi Furani Kuitii nchi Nyengine katika ajenda na Mikakati ni ile Nguvu Na uwezo ambao Unawafanya Wengine wawe wapole wasikilize na watii.
Sasa hiyo nguvu na uwezo inachangiwa na nini, yani from nowhere tu Tanzania tuwatii Iran kwa sababu tu wametuzidi nguvu na uwezo, ilihali hatufaidiki nao kiuchumi
Tunaposema Nature haimaanishi From no Where. Usijifanye Hauelewi.
Hivi ni kwamba hujui maana ya nature au, nature ni kitu chochote ambacho hakijatengenzwa na binadamu bali kilikuwepo kipo na kitaendelea kuwepo, sasa hiyo mifumo yote ya kiutawala siyo nature bali imetengenezwa tu na binadamu
Na ndio maana tunasema Nature kwa Sababu Hakuna Aliemzuia Mwanamke Awe mtawala au apinge wakati Wanaume wanajitangazia utawala. Kama isingekuwa Nature Wanawake Wangepinga na Hadi leo ingekuwepo katika Historia kuwa Wanawake waligoma Utawala wa kimabavu wa wanaume Lakini walishindwa Nguvu hilo halipo.
Una ushahidi gani kuwa Walitawala kimabavu?? Una Ushahidi wa kihistoria kuwa Wanaume wali install Utawala wao kimabavu??
Sasa kama umeshaona mtu amekuzidi nguvu na uwezo kuna haja gani ya kujaribu kumpinga wakati unajua kabisa hata ukifanya hivyo wewe ndio utashindwa, kwahiyo obviously wanaume waliitumia hiyo advantage kujipa mamlaka sababu walijua wanawake hawana uwezo wa kuwapinga, sasa jambo ukishalifanya kwa kulazimisha kaa ukijua siyo watu wote watalikubali lazima watatokea tu ambao watalipinga hata kama itawagharimu maisha yao yote
Maandiko Hayaamuliwi na wanadamu. Usipotoshe watu.
Sasa maandiko yanaamuliwa na nani na ushahidi uko wapi
Kwaiyo Unakataa kuwa Utii hauletwi na Huduma??
Kila kitu tunachokitii Ni kwa sababu tunaogopa Madhara Furani yanayoweza kutokea kama tukienda kinyume hakuna Utii yaani just utii.
Unamtii Boss wako Ukijua Unaweza kufukuzwa kazi tunawatii wazazi kwa kuogopea Laana na vitu kama hivyo Tunawatii Viongozi wa serikali kwa sababu unaogopa Ukienda kinyume Wanaweza wakafanya Kitu furani. Ki ufupi Utii na Uoga Vinaenda sambamba Kwenye Kila Utii kuna aina furani ya Uoga.
Hivi unajua kwamba unavyonasibisha utii na uoga ndivyo unavyozidi kujifunga na kuenda mbali na uhalisia, kama kweli kwenye kila utii kuna aina fulani ya uoga basi ndio unazidi kuthibitisha ile hoja yangu kwamba utii siyo natural bali ni man made, yani hiyo aya yako imebatilisha yale yote uliyokuwa unabisha kule juu na ni kama umeniunga mkono kwamba utii lazima ujengwe na misingi fulani na hiyo misingi isipokuwepo basi hata huo utii nao hauna budi kutokuwepo tena, kama unadai kwamba utii wa mwanamke kwa mwanaume umejengwa katika msingi wa nguvu basi nijibu hili swali langu kwamba je mama au shangazi au dada nao wanatakiwa wawatii ndugu zao wa kiume kwa sababu tu wamewazidi nguvu na wana uwezo wa kuwacharaza makofi, na je unamaanisha mwanamke anatakiwa kutii amri ya mwanaume yeyote yule hata anayekutana naye barabarani kwa sababu tu ni mwanaume na ana nguvu na uwezo wa kumcharaza makofi huyo mwanamke siyo
Sijaona hoja hapa.
Mimi najibu Hoja Sio malalamiko na Sehemu kama Umeivunja vizuri hoja yangu nakuwa Muadilifu nasema Wazi.
Malalamiko gani acha visingizio wewe unajua maana ya malalamiko, we sema tu umeishiwa hoja unatafuta namna ya kukwepa mada, hilo liko wazi wala haihitaji uwe na elimu ya rocket science ili kuliona hilo