Utii wa wanawake wa kisasa

Utii wa wanawake wa kisasa

Mimi huwa sibishani jambo ambalo silijui au sijalifanyia utafiti wengine huwa hatubishani ili mradi tu kutafuta ushindi humu, ila tunabisha pale tunapoona kuna watu wanajaribu kupindisha ukweli kwa malengo yao au maslahi binafsi bila kuwa na hoja za msingi, shukrani kama umeliona hilo mkuu
Kitu kimoja ambacho wanaume wengi hawaoni ni kuwa each gender ina nguvu sawa, am not speaking of physicality! Ambacho wanahisi ni nguzo ya utawala sjui kuumbwa na nguvu, hio yote imeletwa na misingi ya nature, mwanaume ni Provider and protector meaning atakwenda kutafta ndo maana yupo physically strong, mwanamke ni nuturure and reciever, meaning kazi yake ni kuongeza uzao by giving birth na kuhakikisha wanae wana thrive. Hizi roles ndo basis za masculine and feminine. Ila kutokana na mifumo ya kibinadamu, na manipulations ambazo zimeletwa through generations ndo yamesababisha yote haya.

Kingine hizo roles lazima zina nguvu sawa, sema indoctrination na man-made beliefs ndo zinasababisha watu waone tofauti. Kikubwa ni watu kuishi uhalisia, ukiishi kwa uhalisia hauta mwona mmoja mkubwa kuliko mwingine. Hizo roles ndo msingi, ila kutokana na mabadiliko haziwezi ku apply ktk maisha ya siku hizi, both men and women need to work and cooperate together na kusaidina majukumu. Kila mtu anapower na uwezo sawa sema tu in terms of application ndo tunatofautiana.
 
Bi Jadda Wewe sio Mwadilifu Nanukuu Maneno Yako "Lakini mfumo dume siyo kanuni ya asili kwa sababu haiko applicable kwa wanawake 'wote' dunia nzima maana kuna wanawake 'wengi' hawazaliwi na ule msukumo wa ndani wa kuona kwamba wanatakiwa kuwa chini ya wanaume, yani wao wanazaliwa wanajikuta tu kwamba hawana fikira za aina hiyo sasa kama mfumo dume ungekuwa wa asili basi wanawake wote duniani wangekuwa wanazaliwa na uniform mentality, kwamba no matter the circumstances wao wanatakiwa kuwa chini ya wanaume but that is not the case"

Katika Maneno Yako Haya ulikua unamaanisha Nini??
Sasa ambacho hujaelewa hapo ni nini nimemaanisha wengi hawazaliwi na ule msukumo wa ndani wa kukubaliana na maandiko na tamaduni walizozikuta yani wanajikuta tu haviwaingii akilini, ila wengine wanakubaliana tu na maandiko na tamaduni walizozikuta bila kuhoji kwa sababu tu wameambiwa wafanye hivyo ila si kwamba wanapenda kwa utashi wao, mfumo dume ni mentality iliyopandikizwa kwenye vichwa vya watu kupitia malezi na majukumu sasa katika hao watu siyo wote walikubali hilo ndio maana walikuwepo waliopinga kwahiyo hakuna mtu anazaliwa na msukumo wa kutaka kutawaliwa
Umetetea Vyema.

Hatupo Hapa Kujadili Uhalali Au Ubatili wa Ukoloni Hapa Tunajadili Misingi na Vigezo Vya Mmoja kumtawala mwenzake. Usichanganye mambo Bi Jadda.
Sasa wewe ndio unapindisha mada na kunipelekea unakotaka wewe ila mimi hoja yangu tangu mwanzo ni kwamba hakuna utawala wa aina yoyote ambao ni nature lazima kuwe na msingi au sababu za mtu kutawala na mwingine kukubali kutawaliwa, na mara nyingi huyo mtawaliwa anakuwa hafurahii kutawaliwa bali anatii kwa sababu tu sheria au tamaduni zinataka au kuna vitu anafaidika navyo ila ninyi mnang'ang'ania kwamba utawala wa mwanaume na mwanamke ni nature na haujabase kwenye msingi wowote wala sababu yoyote yani wenyewe upo tu na ndio unavyotakiwa kuwa, kwahiyo ofcourse lazima tujadili uhalali au ubatili wa utawala kwa sababu ndipo msingi wa mada ulipo maana hata watu weupe wanadai kwamba wao kuwatawala watu weusi ni nature kama ninyi mnavyodai kwamba wanaume kutawala wanawake ni nature jambo ambalo halina ukweli wowote
Umetetea vyema.ila Kuna kitu unakijua au hukijui kuhusu Historia ya kuanzishwa Kwa Feminism na Waliohusika katika hilo.
Historia ya feminism ni gani na ni nani aliyeanzisha kama unajua hebu elezea
Swali langu Ambalo Hukulijibu Lilikuwa Linahoji Baba atakaposhindwa Kuhudumia Familia kwa Muda Furani kwa Sababu zilizo njee ya Uwezo Wake na ikabidi Mama amsaidie.. Jee Kwa wakati Huo Mama Ameyabeba Majukumu Ya Baba Itabidi Baba Amtii Mama?? Na Mama Ndiye Awe Kichwa cha Familia Kwa Muda huo. Ukijibu hili nitajibu Hilo Swali Lako.
Jibu nimeshakupa hebu uwe unasoma comments zangu uzielewe usisome tu mradi uje kubisha, nimeshakupa jibu hivyo na mimi naomba unijibu vinginevyo sema tu kwamba huna jibu, acha kujizunguzungusha hapa ilihali unaonekana kabisa huna hoja yoyote
Tukianza na Kanuni ya Kuwa Chenye Nguvu Ndio kitakitawala Kilicho Dhaifu Hii Ni Kanuni Inaingii kwenye kila Nyanja ya Maisha ya mwanadamu na viumbe Wengine na ndio maana Tukaenda mbali kukutolea mifano ya sababu ya sisi waafrika kutawaliwa na Wazungu.
Hoja ni kwamba je hizo aina za utawala ni nature au siyo nature, na kama ni nature kwahiyo ina maana sisi weusi hatukutakiwa kuhoji wala kupinga ukoloni kwa sababu kwa mujibu wao wanadai tunapingana na nature, maana wanawake wakipinga utawala wa wanaume mnadai kwamba wanapingana na nature si ndivyo
Pili Vitabu Vitakatifu Vimeashiria kuwa Baba(Mwanaume) ni kichwa cha Familia. Hakuna Maandiko yanayoashiria Mke Akimuhudumia Mume Basi Mume Amtii Mke wake. Na Ndio Maana tunakataa kuwa Utiifu Katika familia Haujajengwa katika Huduma kwa Sababu Vice versa haiwezekani.
Duuh kwani hivyo vitabu vilishushwa si viliandikwa na binadamu kama sisi tena wanaume wewe unajuaje kama walichoandika ni nature au ni mawazo yao tu kwa ajili ya maslahi yao binafsi, ndio maana nikakuambia unapojadili huo msingi wa utawala wa mwanaume dhidi ya mwanamke usiniletee maandiko na tamaduni zilizowekwa na wazee wetu na kupandikizwa vichwani mwa watu vizazi hadi vizazi kisha wakaiita nature hakuna nature ya namna hiyo, wanaume ndio wanaolazimisha utiifu ujengwe katika huduma (ndio maana nakushangaa wewe hapa unabisha wakati wanaume wenzio wanalifahamu hilo au yawezekana hapa najadiliana na mvulana) ndio maana walikuwa hawataki wanawake nao watoke kuenda kutafuta pesa na mali maana walijua wakianza hivyo hakutakuwa na utii tena wewe unadhani ni kwa sababu gani
Hapa Sijaelewa ulikua unajenga Hoja Gani. Umeelezea tuu maisha Mazuuri yaliyokuwepo zama hizo za Mababu zetu Siku hizi Hayapo tena ni Matatizo na mitifuano tuu (mashindano).
Hayo matatizo yametokana na ninyi wanaume kushindwa kukubaliana na ukweli kwamba wanawake hawafurahii kutawaliwa na wala hawajawahi kufurahia kutawaliwa, yani hawa wanawake wa leo ndio wamewadhihirishia rangi halisi ya mwanamke wale bibi zetu walikuwa wanaficha tu makucha yao na kuigiza sababu babu zetu waliwazidi uwezo na nguvu na waliwabana na kuwanyima uhuru, kwahiyo hivi sasa wanawake ndio wanawaonesha jinsi gani mwanamke anavyoweza kuwa akipewa uhuru ndio maana babu zetu walikuwa hawataki mwanamke apewe uhuru maana walilijua hili ndio maana nasema utii wa mwanamke kwa mwanaume siyo suala la nature
Hueleweki Bi Jadda. Wewe ulitoa hoja kuwa Mwanamke kuzaa iwe kigezo cha kuwa mtawala Mimi nikakwambia Kigezo cha Kuwazaa watoto kinakufanya uwe wa Muhimu zaidi kwa Watoto wako Ila hiko Sio Kigezo Cha kuwa Kiongozi wa Familia na kama ingekuwa Hivyo Naturally Tangu zama Hizo Wanawake wangekuwa Viongozi tena bila malumbano yoyote.

Kila kitu kina Vigezo na Sababu zake Na Hazichangamani. Na Ndio Maana Tumekuta tuu Kuwa Watoto mara nyingi wanawapenda zaidi Mama Zao hii ni Natural hakuna alielazimisha au kupanga iwe hivyo Na Tumekuta Wanaume ni Watawala wa Wanawake Katika Familia Hiyo ndio Nature Bi Jadda.
Aise unaonesha una kichwa kigumu na uwezo mdogo sana wa kuelewa mambo na kujadili hoja, yani pamoja na kufafanua kote huko ila bado unarudia yale yale hivi unasoma kweli ninachoandika au napoteza tu muda wangu hapa, mimi sijasema kwamba mwanamke kuzaa iwe kigezo cha kumtawala mwanaume hebu elewa hilo

Nilikuwa najaribu tu kukuonesha kwamba huwezi kujipa utawala kwa kuzingatia majukumu ya kimaumbile ambayo mwenzako hawezi kuyafanya kwa sababu hana maumbile kama yako, ndio nikatolea huo mfano wa kuzaa kwamba ninyi mnaposema mnatakiwa kuwatawala wanawake kwa sababu mna nguvu, ni sawa na wanawake waseme wanatakiwa kuwatawala kwa sababu wanaleta uhai duniani kitu ambacho siyo sawa kabisa

Hayo majukumu yote hapo ni kwa sababu za kimaumbile tu na siyo kigezo cha kuwa mtawala, sasa suala la kupendwa na watoto linahusiana nini na kuweza au kushindwa kuwa mtawala kwani mwanamke hao watoto kajizalia mwenyewe, tena watoto si wanachukua majina ya baba na kuendeleza ukoo wa baba kwahiyo unataka kusema baba hafaidiki na watoto wake kisa tu watoto humpenda zaidi mama si ndio
Bi Jadda Unamaanisha Concept ya Leadership Huna?? Uongozi katika Taasisi Au Jumuiya yoyote ni Jambo Lipo Wazi Sidhani ni Jambo la kujadili.

Taasisi Yoyote lazima Iwe na Kiongozi Na ni kiongozi Mmoja Hakuna Taasisi ina Viongozi Wawili alafu wote Wakawa Wapo Sawa Kimamlaka. Ndoa (Familia) pia Ni Taasisi lazima iwe na Kiongozi mmoja.
Ni nani kakudanganya kwamba kila taasisi lazima iwe na kiongozi mmoja mbona kuna taasisi nyingi tu unakuta zina shareholders kadhaa wenye mamlaka sawa ambao kati yao hakuna anayeweza kufanya maamuzi yahusuyo taasisi peke yake bila kuwashirikisha wenzake, taasisi ambazo kiongozi ni mmoja ni either huyo kiongozi ndio ana shares nyingi na jukumu kubwa au huyo kiongozi ana vigezo fulani au amepitia mchakato fulani wa kumfanya afike hapo na tena kinamchofanya awe kiongozi ni uwezo wake wa kuwajibika kwa faida ya walioko chini yake, (ikiwemo kujali maslahi yao ya kiuchumi) hayuko pale ilimradi tu (ndio maana akishindwa huo wajibu anavuliwa uongozi) na hapo ndipo unapokuja ule msemo "with great authority comes great responsibility" hakuna mamlaka bila wajibu
Swala la Nchi Au mataifa.. Nchi Za Dunia Hii Hazipo katika Taasisi Moja Yaani Kila Mmoja Anaendesha Mambo Yake. Hapo Sio Sawa Mmoja Kulazimisha Kumtawala Mwengine. Ila Ndani Ya Taasisi Moja Lazima Kuwe na Kiongozi. (Hii mbona Ni Concept Nyepesi mno.)
Nchi hazipo katika taasisi moja ila kiuchumi kwa asilimia kubwa zinategemeana kuna vyombo vinavyosimamia sheria za kimataifa ambazo ziko applicable dunia nzima na zinatakiwa kufuatwa na nchi zote duniani, na nchi yoyote ikikiuka inaweza kushitakiwa kwenye mahakama ya kimataifa na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na wanafanya hivyo kwa maslahi ya dunia hivyo hata hii dunia inaendeshwa kama taasisi tu, kwahiyo huo mfano wangu bado ni relevant kama ambavyo kuna watu mnaona haiwezekani taasisi kuwa na kiongozi zaidi ya mmoja (kama marekani inavyoamini) ndivyo pia kuna watu wanaona kwamba hilo linawezekana kabisa (kama russia and co wanavyoamini) kwahiyo suala la utawala ni mtambuka yani nsubjective na siyo nature
Mimi Nilichokuwa Nataka Ugundue Ni Kuwa Tangu Huko ilitokea tuu Mwanaume ndio Kiongozi katika Jamii na Serikali. Na Wanawake Walikuwa ni Watiifu kwa Wanaume. Ni part ya Nature kwa Sababu Hakuna Aliemsaidia Mwanaume kufanikiwa Kumtawala Mwanamke Pia Hakuna Aliemzuia Mwanamke Kumtawala Mwanaume ilitokea Naturally kwa Mujibu wa Uwezo na Nguvu Mwanaume Aka simama kama Mtawala na Automatically Mwanamke Akatii kama Mtawaliwa Hakuna Vita Ilipiganwa Kati Ya wanaume na wanawake kisha Ndio wanaume wakashinda.
Sasa ulitaka mwanaume asaidiwe na nani kuwa mtawala wakati wao ndio waliojipa hayo mamlaka bila kusikiliza upande wa wanawake, unadhani wanawake wangewezaje kubisha wakati wanaume waliwazidi uwezo na nguvu hivyo wakajipa utawala wa mabavu kwa sababu tu ya hayo maumbile yao, mimi nilitegemea mniambie kwamba zamani wanawake nao walipewa au walijipa sauti na uhuru wa kusema wao wanataka maandiko na tamaduni ziweje wakasema wanataka kutawaliwa na wanaume tu hapo ndio ningeamini kweli utawala wa wanaume ni nature kwa sababu wanawake walipewa nafasi wakakataa na wakashindwa wao wenyewe tu basi
Aisee Mbona Unajichanganya Bi Jadda wewe si Ndio unang'ang'ania mwanamke Amtii Mwanaume kwa sababu ya Huduma (kufaidika) kwaiyo Wanawake Sio Watiifu ila ni Waoga. Nahisi Hujajua Ulichokiandika.
Mimi sijataka iwe hivyo ila wanaume wengi ndio wanataka hivyo (of which nawaelewa ila siku mambo yakienda kinyume basi nao wakubali kutawaliwa maana huo msingi waliuweka wenyewe), mimi nataka kusiwe na wa kumtawala mwenzie regardless of what ndio maana nikakuambia, ukishaona mtu anakubali kuwa chini yako kwa sababu tu anafaidika na jambo fulani kutoka kwako basi huo siyo utii bali ni uoga maana siku akiacha kufaidika basi anaweza asikutii tena

Na kingine ndio kama ulivyosema kwamba mwanaume anaweza kumcharaza makofi mwanamke na asimfanye chochote hiyo nayo ni moja ya sababu wanawake wanaonekana wanawatii wanaume ila kiuhalisia wanawaogopa tu, yani kuna ile mtu anakubali kitu kwa sababu tu anajua akigoma unaweza ukamdhuru kwa vile una nguvu zaidi yake sasa huo ni uoga, (hujawahi kusikia haya maneno "nidhamu ya uoga") japo binadamu tunalazimisha kuutafsiri kama utii na tunaenda mbali zaidi na kuuita eti ni nature ilihali sivyo ilivyo

Na hilo suala la mwanaume kuwa na uwezo wa kumcharaza mwanamke makofi halitakiwi kuwa kigezo cha utawala, kwa sababu hata mtoto wa kiume akishakuwa mtu mzima anao uwezo wa kumcharaza mama yake au hata shangazi yake makofi vizuri tu, lakini hilo halifanya mama au shangazi wamtii huyo mtoto wao kwa sababu tu eti ni mwanaume na ana nguvu zaidi yao so kuwa makini na hoja zako
Bi Jadda Unajua Unachokiandika kweli
Sasa Mbona kama Unaniunga mkono mimi. Japo Mimi Sisemi Mwanaume Asihudumie Familia yake Afanye Hivyo na ni Wajibu wake Ila Kuhudumia Familia Sio kigezo Cha Utii wa Mke kwa Mumewe Hilo Ndio Mimi Nalikataa.
Sasa kwani wewe ukilikataa hilo ndio inabadili ukweli kwamba hicho ni kigezo cha mwanaume kumtawala mwanamke, ndio maana nasema wewe unataka tuache kujadili uhalisia tujadili maoni yako binafsi yani unataka ukilikataa jambo basi na sisi tulikatae halafu tukae tunajadili mawazo yako, hebu kuwa serious jaribu kujadili hoja kwa kuzingatia uhalisia uliopo jambo kama hulijui basi usijiandikie tu kwa kutumia hisia zako na mihemko yako bila hoja zozote
Umechanganya Mambo Weka Hoja Zako Vizuri.

Inasikitisha kusoma hiki ulichokiandika.

Hapa Umechemka.

Umetumia Hisia kujadili hili jambo na sio Uhalisia.

Haya pia ni malalamiko.
Hizo aya za mwisho nilijua tu huwezi kujibu chochote cha maana sababu huna hoja ulikurupuka tu kuandika yale uliyoandika, unajifanya kuzipuuzia hoja za muhimu kwa visingizio vya kijinga halafu unashikilia zile ambazo unaona angalau ndio una point, kumbe hata huko kwenyewe nako hakuna chochote cha maana umepuyanga tu
 
Hapo mfano wa ukoloni uliongea kinyume, hawakutoa huduma yoyote ya maana na hatukuwatii bali tuliwaogopa, na nguvu yao ilitushinda hadi wakaweza kututawala.
Sasa ndio uone hii mifumo ya utawala ilivyo batili wao wanajua kabisa kwamba walitutawala kimabavu na hatukuwatii bali tuliwaogopa, lakini wanadai kwamba hiyo utawala wao nature na weusi hawakutakiwa kupinga wao kuwatawala, kama ambavyo wanaume wanadai kwamba utawala wao ni nature hivyo wanawake hawatakiwi kupinga wao kuwatawala huoni uhusiano hapo
Kwa upande wa huduma, ni jukumu la mwanaume, japo kuna mahala inaweza ikitokea shida, mwanaume akafukuzwa kazi au akaumwa akashindwa kutimiza majukumu, mke akiwa na kahenge kake, akawa anapata elfu kumi kumi kwaajili ya kuhudumia familia yake ya watoto wawili, mpaka pale mume atapopona na kurudi kwenye utafutaji, je huyo mke asitishe utiifu wake kwa mume kisa mume hawezi kutafuta kwaajili ya kuumwa, mpaka pale atapopona?
Na ndio maana nikauliza vipi kama huyo mke akiwa mama wa nyumbani, mimi nilitaka tukubaliane kwanza kwamba msingi wa mwanaume kumtawala mwanamke siyo nature bali umejengwa katika misingi fulani, vinginevyo basi mwanamke yeyote yule angekuwa anatakiwa kumtii mwanaume yeyote yule hata anayekutana naye barabarani kwa sababu tu ni mwanaume

Halafu ndio tuje sasa kwenye hoja kwamba utii ukishajengwa kwa sababu fulani huo unakuwa siyo utii tena bali ni uoga japo sisi binadamu ndio tunalazimisha kuutafsiri kama utii, kwa mfano mke anapomtii mumewe kwa sababu tu anapata financial security, huo siyo utii kwa sababu siku akiikosa hiyo financial security kuna uwezekano huo unaoitwa utii usiwepo tena

Na pia kuna hilo suala la mwanaume kumzidi nguvu mwanamke hiyo nayo ni sababu nyingine inayofanya wanawake waonekane wanawatii waume zao ila in real sense ni wanawaogopa, yani kuna ile mtu anakubali kitu kwa sababu tu anajua akigoma unaweza ukampiga naye akashindwa kukufanya chochote maana anajua una nguvu zaidi yake, sasa huo siyo utii bali ni uoga na uoga siyo nature kwahiyo hizo sababu hazitakiwi kuwa msingi wa wanaume kuwatawala wanawake
Swali la nyongeza, tusisomeshe watoto wa kike au tuwazuie kufanya kazi ili wawe wamama wa nyumbani wa kuletewa tu ili watutii? Maana tukiwasomesha na kuwatafutia kazi, watajitafutia na kusaidia familia, mwisho wake wakose kutii waume zao.
Hapana tatizo wala siyo kusomesha watoto wa kike ila tatizo ni wanaume kushindwa kukubali ukweli kwamba wanawake hawafurahii na wala hawajawahi kufurahia kutawaliwa toka zamani, ukweli ni kwamba bibi zetu walilazimika kuwatii wanaume kwa sababu tu ya huduma za kiuchumi na kuogopa kudhuriwa ila si kwa sababu walikuwa wanapenda kwa utashi wao, kwahiyo solution hapa ni wanaume kukubali kuwa sawa na wanawake linapokuja kwenye suala la haki na majukumu utofauti ubaki kwenye maumbile tu ila siyo kwenye mambo mengine wote washirikiane na wasikilizane kusiwe na ulazima wa mmoja kumtawala mwingine au mmoja kumtii mwingine
 
Kabla ya Kukanusha kuwa Huo mfumo Uliouita Mfumo Dume kuwa Sio mfumo wa asili ulitakiwa Ujiuulize ILIKUWAJE HADI IKATOKEA HUKO TANGU KWA ANCESTORS WETU MWANAUME ALIKUWA NI MTAWALA NA MSIMAMIZI WA MWANAMKE??
Je ilishawahi kujiuliza Ilikuwaje hadi wanaume Waka"win" kuwatawala wanawake Huko nyuma Na bila resistance yoyote inayojulikana leo hii.

Pia Tukuulize Bi Jadda imekuaje Hadi imetokea kuna wanawake wao wanakubali kuwa chini ya Mwanaume Kwa msukumo wa ndani lakini pia kuna ambao wapo kinyume na hilo kama ulivyodai (Japo sio kweli). Lakini hakuna mwanaume anaezaliwa na msukumo wa ndani wa kutawaliwa na Mwanamke( kama wapo pia tuambie).

Bado Swali linakuja Hayo yote yanatokea kwa nini?? Kwanini Wanawake walikubali hili Jee Kuna Nguvu Ya Nje walipewa wanaume Kulifanikisha hili??

Umetetea vyema. Ila Unatakiwa Utuambie Ni Nani Aliyewapa Nguvu Wanawake Hadi wakajiona Sasa Wanavifua na ilikuaje jee Hawakusaidiwa?

Ukisema kwa Sababu Za Kiuchumi tuu Utakuwa Hujayazingatia maisha ya Kifamilia labda maisha ya Kimahusiano tuu nje ya Familia kwa sababu Kwa Hoja yako hii Inamaanisha Baba atatiiwa na Mama akiwa na pesa na siku Baba akiishiwa Pesa ,, Na ikabidi mke ahudumie Familia Basi Sasa Baba atatakiwa kutiii mke. Na mke atakuwa ndio kichwa cha Familia. (Hii ni ajabu kabisa)

Mimi mbona nimetoa Sababu yangu moja wapo kuwa ni kwa Sababu Madume yana Nguvu kuliko Majike Jee wewe unalikataa hili??

Pili Hayo maumbile unayoyakataa ndio Hoja ambayo ni Ngumu kuivunja Sababu Maumbile ya mwanamke Yanamfanya Automatically kuwa Weak ukilinganisha na Mwanaume Sasa Kanuni za kiasili zinamfaidisha Mwanaume kumtawala Mwanamke kwa yale maumbile yake.
Ndio maana nikakutolea Mfano kwamba Unaweza ukawa unamuhudia huyo mwanaume Ambae kwa Hoja yako Sasa utakuwa unamtawala Alafu siku ikitokea ugomvi atakuchalaza makofi na hutakuwa na la kumfanya Huo ni Utawala Gani Sasa.!!!
Umeongea ukweli mkuu. Msingi wa utawala ni nguvu na hapo ndipo panapompa mwanaume advantage ya kuwa juu ya mwanamke, sasa umtawale mtu aliekuzidi nguvu hivi asipofanya kile unachotaka utamuwajibishaje. Maelezo yako yanapita mule mule kwenye kanuni za asili tatizo uyo ulienzisha nae ligi ni mbishi sana
 
Kama msingi wa mwanaume kumtawala mwanamke ni nguvu pekee kwanini mwanaume anatakiwa kumtawala mkewe tu na si wanawake wote wanaomzunguka, na kwanini mwanamke naye anatakiwa amtii mumewe tu kwanini asimtii mwanaume yeyote tu hata yule anayekutana naye barabarani kwa sababu tu ni mwanaume, kwahiyo unataka kusema mwanaume anatakiwa kuwatawala hadi mama yake, shangazi zake na dada zake wakubwa kwa sababu tu yeye ni mwanaume na hao ni wanawake, kupinga utawala wa mwanaume haimaanishi kwamba tunataka mwanamke ndio awe mtawala bali kila mmoja ajitawale mwenyewe na awe na maamuzi juu ya maisha yake kusiwe na wa kumtawala mwenzie regardless of majukumu
 
Kitu kimoja ambacho wanaume wengi hawaoni ni kuwa each gender ina nguvu sawa, am not speaking of physicality! Ambacho wanahisi ni nguzo ya utawala sjui kuumbwa na nguvu, hio yote imeletwa na misingi ya nature, mwanaume ni Provider and protector meaning atakwenda kutafta ndo maana yupo physically strong, mwanamke ni nuturure and reciever, meaning kazi yake ni kuongeza uzao by giving birth na kuhakikisha wanae wana thrive. Hizi roles ndo basis za masculine and feminine. Ila kutokana na mifumo ya kibinadamu, na manipulations ambazo zimeletwa through generations ndo yamesababisha yote haya.

Kingine hizo roles lazima zina nguvu sawa, sema indoctrination na man-made beliefs ndo zinasababisha watu waone tofauti. Kikubwa ni watu kuishi uhalisia, ukiishi kwa uhalisia hauta mwona mmoja mkubwa kuliko mwingine. Hizo roles ndo msingi, ila kutokana na mabadiliko haziwezi ku apply ktk maisha ya siku hizi, both men and women need to work and cooperate together na kusaidina majukumu. Kila mtu anapower na uwezo sawa sema tu in terms of application ndo tunatofautiana.
Aise umemaliza kila kitu mkuu sina tena la kuongezea hapo, nashukuru kwa kunielewa wanaobisha acha waendelee kubisha nasi tutaendelea kuwaelewesha tu, pamoja na kwamba wanajitutumua kubisha humu ila somo wanakuwa wamelipata vizuri tu
 
Sasa ambacho hujaelewa hapo ni nini nimemaanisha wengi hawazaliwi na ule msukumo wa ndani wa kukubaliana na maandiko na tamaduni walizozikuta
Bi Jadda Unajua Unachokiandika Kweli Unaposema Wengi Unajua Unamaanisha Nini?? Unaposema Wengi It's means Sio Wote. Bado Hujajibu.
yani wanajikuta tu haviwaingii akilini, ila wengine wanakubaliana tu na maandiko na tamaduni walizozikuta bila kuhoji kwa sababu tu wameambiwa wafanye hivyo ila si kwamba wanapenda kwa utashi wao, mfumo dume ni mentality iliyopandikizwa kwenye vichwa vya watu kupitia malezi na majukumu sasa katika hao watu siyo wote walikubali hilo ndio maana walikuwepo waliopinga kwahiyo hakuna mtu anazaliwa na msukumo wa kutaka kutawaliwa
Hata Anaezaliwa Kipofu Yeye Hakutaka Iwe Hivyo ila ndo imeshatokea Sasa Kuna Vitu Lazima Atavikosa Kwa Yeye Kuwa Kipofu na Wale Ambao sio Vipofu Watavipata Hiyo Ndio Mipango ya Mungu Au Tuseme Nature Maana ili Uwe Feminist lazima Kwanza Uyakane Maandiko Matukufu.
Sasa wewe ndio unapindisha mada na kunipelekea unakotaka wewe ila mimi hoja yangu tangu mwanzo ni kwamba hakuna utawala wa aina yoyote ambao ni nature lazima kuwe na msingi au sababu za mtu kutawala na mwingine kukubali kutawaliwa,
Vigezo Mbona Tulishavitaja Tangu Huko Mwanzo Kwamba ni Nguvu na Uwezo Sasa Tunaposema Nature tunamaanisha Nature Ndio Imeaamua Mwanaume Awe na Nguvu na uwezo mkubwa Kuliko Mwanaume.
Hata Sisi Tunawatawala na Kuwadhibiti Wanyama Kwa Sababu Ya Aidha Nguvu Zetu Au Uwezo Wetu Mkubwa Wa Akili. Ila Sio Kwamba Tunawahudumia.
na mara nyingi huyo mtawaliwa anakuwa hafurahii kutawaliwa bali anatii kwa sababu tu sheria au tamaduni zinataka au kuna vitu anafaidika navyo
Sio kweli kwamba mara Nyingi Anayetawaliwa Anakuwa Hana Furaha. Bibi Zetu Waliishi Maisha ya Furaha Na Babu zetu Na hayo maisha Sisi Tumeyashuhudia(usilete Peculiar cases za Manyanyaso za baadhi ya jamii hakuna Anaekubaliana na Hilo Kwa Sababu kuwa Mtawala haimaanishi uwe mnyanyasaji) Ila Sasa hivi Ndio Hakuna Furaha wala amani katika Ndoa kwa sababu Mnalazimisha Kwenda kinyume na Nature.
Wewe Unaitii Serikali ya Tanzania Jee Huna Furaha ,, unamtii Boss wako jee Huna Furaha unaongea Vitu ambavyo hazipo kabisa.
ila ninyi mnang'ang'ania kwamba utawala wa mwanaume na mwanamke ni nature na haujabase kwenye msingi wowote wala sababu yoyote yani wenyewe upo tu na ndio unavyotakiwa kuwa,
Bi Jadda Mbona Tunaliludia hili mara kwa Mara kuwa Ni Nguvu uwezo na Umadhubuti aliokuwa nao Mwanaume Kulinganisha na Mwanamke na pia hilo linakubali katika vitu vingi Vinavyotawaliana Hatusemi Utawala upo tu From no Where Bali Tunaelekezea Hivyo Vigezo kwa Nature sababu Hakuna Alieamua Mwanamke awe Dhaifu na Mwanaume awe Madhubuti. Imetokea tuu Hivyo. Au labda wewe unajua kwa nini??
kwahiyo ofcourse lazima tujadili uhalali au ubatili wa utawala kwa sababu ndipo msingi wa mada ulipo maana hata watu weupe wanadai kwamba wao kuwatawala watu weusi ni nature kama ninyi mnavyodai kwamba wanaume kutawala wanawake ni nature jambo ambalo halina ukweli wowote
Mimi Sio Mzungu Wala hapa Hatujadili Weusi na Wazungu Tunajadili Wanaume na wanawake. Hao Wazungu Kama Wanadai Hivyo Inabidi Wathibitishe Ni Nature How?? Usinisukimizie Upande Nisiokuwepo.
Historia ya feminism ni gani na ni nani aliyeanzisha kama unajua hebu elezea
Naweza kusummarize Kwa Maneno Machache kuwa Feminism and Atheism and Homosexuality Ni Ndugu Wa familia moja Kwa ajili ya Kuharibu Ulimwengu.
Jibu nimeshakupa hebu uwe unasoma comments zangu uzielewe usisome tu mradi uje kubisha, nimeshakupa jibu hivyo na mimi naomba unijibu vinginevyo sema tu kwamba huna jibu, acha kujizunguzungusha hapa ilihali unaonekana kabisa huna hoja yoyote
Acha kutudanganya Bi jadda hakuna Jibu Umetoa Kama lipo Nenda kalinukuu Ulilete hapa.
Hoja ni kwamba je hizo aina za utawala ni nature au siyo nature, na kama ni nature kwahiyo ina maana sisi weusi hatukutakiwa kuhoji wala kupinga ukoloni kwa sababu kwa mujibu wao wanadai tunapingana na nature, maana wanawake wakipinga utawala wa wanaume mnadai kwamba wanapingana na nature si ndivyo
Unatuchanganyia Mada Bi Jadda Hapa Hatujadili Wazungu na Waafrika Nishasema hayo madai ya Wazungu wanatakiwa Wathibitishe wao wenyewe mimi sio Mzungu. Mimi Nazungumzia Wanawake na Wanaume na Nimeshasema Ni Nature kwa Sababu zipi.
Duuh kwani hivyo vitabu vilishushwa si viliandikwa na binadamu kama sisi tena wanaume wewe unajuaje kama walichoandika ni nature au ni mawazo yao tu kwa ajili ya maslahi yao binafsi,
Ili uwe Feminist lazima Uyakane Maandiko Kwanza ndio Maana nikasema kule juu Feminism na Atheism ni Ndugu kwa ajili ya kuharibu Vizazi(ulimwengu) Sisi Tunaamini Maandiko Matakatifu ni Maneno Ya Mungu aliyoyateremsha kwa Mitume Wake. Mungu ndiye Aliyetuumba na kutupangia Mambo na Kanuni. Labda nikuulize Unaamini katika Mungu na Dini na Vitabu vyake??
ndio maana nikakuambia unapojadili huo msingi wa utawala wa mwanaume dhidi ya mwanamke usiniletee maandiko na tamaduni zilizowekwa na wazee wetu na kupandikizwa vichwani mwa watu vizazi hadi vizazi kisha wakaiita nature
Maandiko Matukufu sio Maandiko ya Mwanadamu. Mwanadamu ni Messenger Tuu.
hakuna nature ya namna hiyo, wanaume ndio wanaolazimisha utiifu ujengwe katika huduma (ndio maana nakushangaa wewe hapa unabisha wakati wanaume wenzio wanalifahamu hilo au yawezekana hapa najadiliana na mvulana)
Uvulana unahusika nini Hapa Bi Jadda??
ndio maana walikuwa hawataki wanawake nao watoke kuenda kutafuta pesa na mali maana walijua wakianza hivyo hakutakuwa na utii tena wewe unadhani ni kwa sababu gani
Kwaiyo Unatudhibitishia Kuwa Mwanamke Akianza Kutafuta Mali Hatomtii Mume wake??. Ndio ujue kuwa Huduma sio Kigezo cha Utiifu. Ili kitu kiwe kigezo cha kitu Furani basi kuwepo kwake kutasababisha jambo na kutokuwepo kwake Kutafanya Jambo Lisiwepo.
Hayo matatizo yametokana na ninyi wanaume kushindwa kukubaliana na ukweli kwamba wanawake hawafurahii kutawaliwa na wala hawajawahi kufurahia kutawaliwa,
Sio Kweli Bibi Zetu Waliishi Kwa Amani na Babu Zetu Na Tuliyashuhudia maisha ya Amani katika Ndoa Zao.
Unalinganisha Ndoa za Babu zetu na Hizi Za Siku hizi leo inafungwa kesho Imevunjika. Embu tupe Comparison kuwa Now Ndoa zina Furaha na Amani na Zinadumu Kwa Sababu Feminism imepiga Hatua Ukilinganisha Na Zama hizo. Leta Comparison hapa.
yani hawa wanawake wa leo ndio wamewadhihirishia rangi halisi ya mwanamke wale bibi zetu walikuwa wanaficha tu makucha yao na kuigiza sababu babu zetu waliwazidi uwezo na nguvu na waliwabana na kuwanyima uhuru,
Usiwasingizie Bibi Zetu. Wao Hawakuwa na Makucha Yoyote. Nyinyi Mmekuwa Manipulated Umejaziwa Fikra mkaona Ndio uhalisia. Nyinyi Mmeuvua Uanamke, mnataka mmvae Uanaume. Hakuna Suala kuwa Rangi halisi sijui vitu gani Hizo ni Propaganda tuu.
kwahiyo hivi sasa wanawake ndio wanawaonesha jinsi gani mwanamke anavyoweza kuwa akipewa uhuru ndio maana babu zetu walikuwa hawataki mwanamke apewe uhuru maana walilijua hili ndio maana nasema utii wa mwanamke kwa mwanaume siyo suala la nature
Babu zetu Walikuwa wanatekeleza Kile ambacho Kilikuwa kipo katika Uhalisia kwamba Familia Lazima iwe na Kiongozi na kiongozi ni Baba. Basi.
Aise unaonesha una kichwa kigumu na uwezo mdogo sana wa kuelewa mambo na kujadili hoja, yani pamoja na kufafanua kote huko ila bado unarudia yale yale hivi unasoma kweli ninachoandika au napoteza tu muda wangu hapa, mimi sijasema kwamba mwanamke kuzaa iwe kigezo cha kumtawala mwanaume hebu elewa hilo
Usinibebeshe vitu Mimi Nimejaribu Kukuambia Sio kila kigezo ni Kigezo cha Utawala. Utawala una vigezo vyake ambavyo Ukiwa navyo Automatically unastahili kutiiwa na Kutawala.
Nilikuwa najaribu tu kukuonesha kwamba huwezi kujipa utawala kwa kuzingatia majukumu ya kimaumbile ambayo mwenzako hawezi kuyafanya kwa sababu hana maumbile kama yako, ndio nikatolea huo mfano wa kuzaa kwamba ninyi mnaposema mnatakiwa kuwatawala wanawake kwa sababu mna nguvu, ni sawa na wanawake waseme wanatakiwa kuwatawala kwa sababu wanaleta uhai duniani kitu ambacho siyo sawa kabisa
Kila kitu kina kigezo chake Vigezo haviingiliani ili mradi tuu. Mbona jambo hili lipo wazi kabisa.

Huwezi kukataa kuwa Nguvu na Uwezo ni kigezo cha Utawala wakati hii kanuni inakubali katika Maeneo Mengi sana. Boss wako ni mtawala wako kwa sababu ana Nguvu aliyopewa na Taasisi yako Raisi ni Mtawala kwa sababu Ana nguvu ambayo ameitoa kwetu kupitia Kura zetu Sisi Tunawatawala Wanyama Kwa Sababu ya Nguvu zetu na uwezo wa akili. Kwaiyo Hii kanuni ni applicable sehemu Nyingi ila kanuni ya Kutawala kwa sababu ya Huduma Haikubali katika maeneo mengi kama sio yote.
Hayo majukumu yote hapo ni kwa sababu za kimaumbile tu na siyo kigezo cha kuwa mtawala, sasa suala la kupendwa na watoto linahusiana nini na kuweza au kushindwa kuwa mtawala kwani mwanamke hao watoto kajizalia mwenyewe, tena watoto si wanachukua majina ya baba na kuendeleza ukoo wa baba kwahiyo unataka kusema baba hafaidiki na watoto wake kisa tu watoto humpenda zaidi mama si ndio
Hakuna hoja Umejenga hapa.
Ni nani kakudanganya kwamba kila taasisi lazima iwe na kiongozi mmoja mbona kuna taasisi nyingi tu unakuta zina shareholders kadhaa wenye mamlaka sawa ambao kati yao hakuna anayeweza kufanya maamuzi yahusuyo taasisi peke yake bila kuwashirikisha wenzake, taasisi ambazo kiongozi ni mmoja ni either huyo kiongozi ndio ana shares nyingi na jukumu kubwa au huyo kiongozi ana vigezo fulani au amepitia mchakato fulani wa kumfanya afike hapo na tena kinamchofanya awe kiongozi ni uwezo wake wa kuwajibika kwa faida ya walioko chini yake, (ikiwemo kujali maslahi yao ya kiuchumi) hayuko pale ilimradi tu (ndio maana akishindwa huo wajibu anavuliwa uongozi) na hapo ndipo unapokuja ule msemo "with great authority comes great responsibility" hakuna mamlaka bila wajibu
Umetetea vyema. Ila sio Hoja. Hoja Ni kuwa Katika Familia Lazima kuwe na Kiongozi hamuwezi kuishi two bulls in one House.
Nchi hazipo katika taasisi moja ila kiuchumi kwa asilimia kubwa zinategemeana kuna vyombo vinavyosimamia sheria za kimataifa ambazo ziko applicable dunia nzima na zinatakiwa kufuatwa na nchi zote duniani, na nchi yoyote ikikiuka inaweza kushitakiwa kwenye mahakama ya kimataifa na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na wanafanya hivyo kwa maslahi ya dunia hivyo hata hii dunia inaendeshwa kama taasisi tu,
Dunia haiendeshwi kama Taasisi Usitudanganye kila nchi ina It's own National sovereignty. Kinachofanya Nchi Furani Kuitii nchi Nyengine katika ajenda na Mikakati ni ile Nguvu Na uwezo ambao Unawafanya Wengine wawe wapole wasikilize na watii.
kwahiyo huo mfano wangu bado ni relevant kama ambavyo kuna watu mnaona haiwezekani taasisi kuwa na kiongozi zaidi ya mmoja (kama marekani inavyoamini) ndivyo pia kuna watu wanaona kwamba hilo linawezekana kabisa (kama russia and co wanavyoamini) kwahiyo suala la utawala ni mtambuka yani nsubjective na siyo nature.
Tunaposema Nature haimaanishi From no Where. Usijifanye Hauelewi.
Sasa ulitaka mwanaume asaidiwe na nani kuwa mtawala
Na ndio maana tunasema Nature kwa Sababu Hakuna Aliemzuia Mwanamke Awe mtawala au apinge wakati Wanaume wanajitangazia utawala. Kama isingekuwa Nature Wanawake Wangepinga na Hadi leo ingekuwepo katika Historia kuwa Wanawake waligoma Utawala wa kimabavu wa wanaume Lakini walishindwa Nguvu hilo halipo.
wakati wao ndio waliojipa hayo mamlaka bila kusikiliza upande wa wanawake, unadhani wanawake wangewezaje kubisha wakati wanaume waliwazidi uwezo na nguvu hivyo wakajipa utawala wa mabavu
Una ushahidi gani kuwa Walitawala kimabavu?? Una Ushahidi wa kihistoria kuwa Wanaume wali install Utawala wao kimabavu??
kwa sababu tu ya hayo maumbile yao, mimi nilitegemea mniambie kwamba zamani wanawake nao walipewa au walijipa sauti na uhuru wa kusema wao wanataka maandiko na tamaduni ziweje wakasema wanataka kutawaliwa na wanaume tu hapo ndio ningeamini kweli utawala wa wanaume ni nature kwa sababu wanawake walipewa nafasi wakakataa na wakashindwa wao wenyewe tu basi
Maandiko Hayaamuliwi na wanadamu. Usipotoshe watu.
Mimi sijataka iwe hivyo ila wanaume wengi ndio wanataka hivyo (of which nawaelewa ila siku mambo yakienda kinyume basi nao wakubali kutawaliwa maana huo msingi waliuweka wenyewe) mimi nataka kusiwe na wa kumtawala mwenzie regardless of what, ndio maana nikakuambia ukishaona mtu anakubali kuwa chini yako kwa sababu tu anafaidika na jambo fulani kutoka kwako basi huo siyo utii
Kwaiyo Unakataa kuwa Utii hauletwi na Huduma??
maana siku akiacha kufaidika basi anaweza asikutii tena, na kingine ndio kama ulivyosema kwamba mwanaume anaweza kumcharaza makofi mwanamke na asimfanye chochote hiyo nayo ni moja ya sababu wanawake wanaonekana wanawatii wanaume ila kiuhalisia wanawaogopa tu yani kuna ile mtu anakubali kitu kwa sababu tu anajua akigoma unaweza ukamdhuru kwa vile una nguvu zaidi yake sasa huo ni uoga (hujawahi kusikia haya maneno "nidhamu ya uoga") japo binadamu tunalazimisha kuutafsiri kama utii na tunaenda mbali zaidi na kuuita eti ni nature kumbe ni implanted mentality tu
Kila kitu tunachokitii Ni kwa sababu tunaogopa Madhara Furani yanayoweza kutokea kama tukienda kinyume hakuna Utii yaani just utii.
Unamtii Boss wako Ukijua Unaweza kufukuzwa kazi tunawatii wazazi kwa kuogopea Laana na vitu kama hivyo Tunawatii Viongozi wa serikali kwa sababu unaogopa Ukienda kinyume Wanaweza wakafanya Kitu furani. Ki ufupi Utii na Uoga Vinaenda sambamba Kwenye Kila Utii kuna aina furani ya Uoga.
Sasa kwani wewe ukilikataa hilo ndio inabadili ukweli kwamba hicho ni kigezo cha mwanaume kumtawala mwanamke, ndio maana nasema wewe unataka tuache kujadili uhalisia tujadili maoni yako binafsi yani unataka ukilikataa jambo basi na sisi tulikatae halafu tukae tunajadili mawazo yako, hebu kuwa serious jaribu kujadili hoja kwa kuzingatia uhalisia uliopo jambo kama hulijui basi usijiandikie tu kwa kutumia hisia zako na mihemko yako bila hoja zozote
Sijaona hoja hapa.
Hizo aya za mwisho nilijua tu huwezi kujibu chochote cha maana sababu huna hoja ulikurupuka tu kuandika yale uliyoandika, unajifanya kuzipuuzia hoja za muhimu kwa visingizio vya kijinga halafu unashikilia zile ambazo unaona angalau ndio una point, kumbe hata huko kwenyewe nako hakuna chochote cha maana umepuyanga tu
Mimi najibu Hoja Sio malalamiko na Sehemu kama Umeivunja vizuri hoja yangu nakuwa Muadilifu nasema Wazi.
 
Kama msingi wa mwanaume kumtawala mwanamke ni nguvu pekee kwanini mwanaume anatakiwa kumtawala mkewe tu na si wanawake wote wanaomzunguka, na kwanini mwanamke naye anatakiwa amtii mumewe tu kwanini asimtii mwanaume yeyote tu hata yule anayekutana naye barabarani kwa sababu tu ni mwanaume,
Mkuu unachanganya utawala na unyanyasaji, utiifu na uoga/utumwa.. Utawala tunaoongelea hapa sio kumpigisha mkeo pushups au kumchalaza bakora au kujenga mazingira ya kuogopwa kwamba popote mwanaume utakapotokea tu basi mwanamke aanze kutetemeka kwa uoga. Utawala unaoongelewa na ule wa nani anaeweka kanuni na anatakiwa kuzisimamia pale mambo yanapoenda nje ya mstari, hapo ndipo mwanaume anapata advantage kwa sababu kiasili ana nguvu kushinda mwanamke ivyo basi ataweza kuchukua hatua za kinidhamu endapo mwanamke akitoka nje ya mstari. Sasa nimepishana na mwanamke njiani unataka nionyeshe utawala kwa namna gani, kwamba nimkamate nimtandike makofi bila sababu kwa sababu mimi ni mwanaume namzidi nguvu? Nimepishana na mwanamke njiani unataka mwanamke anionyeshe utiifu gani kwamba anipigie magoti na kuniamkia?
kwahiyo unataka kusema mwanaume anatakiwa kuwatawala hadi mama yake, shangazi zake na dada zake wakubwa kwa sababu tu yeye ni mwanaume na hao ni wanawake,
Kama unaona mama, shangazi au dada anafanya maamuzi ya ajabu ajabu mwanaume lazima uingilie kati kusimamia shoo.
kupinga utawala wa mwanaume haimaanishi kwamba tunataka mwanamke ndio awe mtawala bali kila mmoja ajitawale mwenyewe na awe na maamuzi juu ya maisha yake kusiwe na wa kumtawala mwenzie regardless of majukumu
Mkuu ilo suala haliwezekani ni against nature. Mafahali wawili hawaishi zizi moja nimeona uko juu umepewa mfano wa wanyama ambao hawazijui hizi ideologies za 50/50 angalia mfumo wao wa maisha kati ya jike na dume ni nani mtawala? Ili mahusiano yaende lazima mmoja awe chini ndipo hapa mwenye nguvu anakua juu kwa sababu naturally dhaifu hawezi kumtawala au kulinga madaraka na mwenye nguvu.
 
Umeongea ukweli mkuu. Msingi wa utawala ni nguvu na hapo ndipo panapompa mwanaume advantage ya kuwa juu ya mwanamke, sasa umtawale mtu aliekuzidi nguvu hivi asipofanya kile unachotaka utamuwajibishaje. Maelezo yako yanapita mule mule kwenye kanuni za asili tatizo uyo ulienzisha nae ligi ni mbishi sana
Naupenda Ubishi Wake Mkuu Sababu ananifanya Nimwage Elimu Nyingi Sana Kwa wengine. Ili wale Wengine ambao Wanaweza kuelewa waelewe.
Sikusudii Bi Jadda Aseme Umenishinda Kama akiwa na Time zaidi itapendeza tuendelee Nizidi kutoa elimu.
 
Mkuu unachanganya utawala na unyanyasaji, utiifu na uoga/utumwa.. Utawala tunaoongelea hapa sio kumpigisha mkeo pushups au kumchalaza bakora au kujenga mazingira ya kuogopwa kwamba popote mwanaume utakapotokea tu basi mwanamke aanze kutetemeka kwa uoga. Utawala unaoongelewa na ule wa nani anaeweka kanuni na anatakiwa kuzisimamia pale mambo yanapoenda nje ya mstari, hapo ndipo mwanaume anapata advantage kwa sababu kiasili ana nguvu kushinda mwanamke ivyo basi ataweza kuchukua hatua za kinidhamu endapo mwanamke akitoka nje ya mstari. Sasa nimepishana na mwanamke njiani unataka nionyeshe utawala kwa namna gani, kwamba nimkamate nimtandike makofi bila sababu kwa sababu mimi ni mwanaume namzidi nguvu? Nimepishana na mwanamke njiani unataka mwanamke anionyeshe utiifu gani kwamba anipigie magoti na kuniamkia?
Mkuu Umemaliza kila kitu.
Kama unaona mama, shangazi au dada anafanya maamuzi ya ajabu ajabu mwanaume lazima uingilie kati kusimamia shoo.

Mkuu ilo suala haliwezekani ni against nature. Mafahali wawili hawaishi zizi moja nimeona uko juu umepewa mfano wa wanyama ambao hawazijui hizi ideologies za 50/50 angalia mfumo wao wa maisha kati ya jike na dume ni nani mtawala? Ili mahusiano yaende lazima mmoja awe chini ndipo hapa mwenye nguvu anakua juu kwa sababu naturally dhaifu hawezi kumtawala mwenye nguvu.
 
Aise umemaliza kila kitu mkuu sina tena la kuongezea hapo, nashukuru kwa kunielewa wanaobisha acha waendelee kubisha nasi tutaendelea kuwaelewesha tu, pamoja na kwamba wanajitutumua kubisha humu ila somo wanakuwa wamelipata vizuri tu
Tatizo watu wanaliangalia hilo swala with logical mind ambayo imekua instilled with alot of false knowledge. It requires understanding both sides of the coin, bila hivyo mtaongelea ma dhana na ma ideologies mengi mpk mtachoka bure. Hiyo viscious cycle inachekesha sana🤣
 
Bi Jadda Unajua Unachokiandika Kweli Unaposema Wengi Unajua Unamaanisha Nini?? Unaposema Wengi It's means Sio Wote. Bado Hujajibu.
Yani mimi najibu hoja zako halafu wewe kwa sababu zako binafsi tu unaamua kukataa majibu yangu, kwa kisingizio kwamba sijajibu au unataka nijibu vile unavyotaka wewe, hebu acha huu ujinga kama umeishiwa hoja sema usilazimishe kuandika pumba mradi tu usionekane umeshindwa na huna majibu
Hata Anaezaliwa Kipofu Yeye Hakutaka Iwe Hivyo ila ndo imeshatokea Sasa Kuna Vitu Lazima Atavikosa Kwa Yeye Kuwa Kipofu na Wale Ambao sio Vipofu Watavipata Hiyo Ndio Mipango ya Mungu Au Tuseme Nature Maana ili Uwe Feminist lazima Kwanza Uyakane Maandiko Matukufu.
Sasa ni kanuni gani inayoamua kwamba binadamu mwenye macho mazima ni bora zaidi ya kipofu, na ana mamlaka ya kumtawala kipofu kwa sababu tu ya hizo tofauti za kimaumbile, na hayo unayoyaita maandiko matukufu ni kwa mujibu wa nani
Vigezo Mbona Tulishavitaja Tangu Huko Mwanzo Kwamba ni Nguvu na Uwezo Sasa Tunaposema Nature tunamaanisha Nature Ndio Imeaamua Mwanaume Awe na Nguvu na uwezo mkubwa Kuliko Mwanaume.
Hata Sisi Tunawatawala na Kuwadhibiti Wanyama Kwa Sababu Ya Aidha Nguvu Zetu Au Uwezo Wetu Mkubwa Wa Akili. Ila Sio Kwamba Tunawahudumia.
Sasa ni nature ya aina gani inayoamua kwamba utawala utokane na maumbile ambayo mtawaliwa hana na hakupenda kutokuwa nayo na mbaya zaidi hafurahii huo utawala, hebu acha porojo zenu hao wanyama tuna uwezo wa kuwatawala na kuwadhibiti ikiwa tu tunawafuga na kuwahudumia au wewe nenda kaingie kwenye msitu wa wanyama wakali na silaha zako (ambazo unahisi ndio zitakupa jeuri) halafu uone kama watakutii, kitakachokukuta ndio utajua kwamba hizo propaganda zenu hazifanyi kazi kwenye uhalisia au wewe ulimaanisha hawa wanyama kama paka, mbwa, sijui ng'ombe na mbuzi tu ambao nao lazima uwahudumie au nenda kajaribu kuvamia nyumba yenye mbwa wakali halafu uone kama hao mbwa watakupa utii
Sio kweli kwamba mara Nyingi Anayetawaliwa Anakuwa Hana Furaha. Bibi Zetu Waliishi Maisha ya Furaha Na Babu zetu Na hayo maisha Sisi Tumeyashuhudia(usilete Peculiar cases za Manyanyaso za baadhi ya jamii hakuna Anaekubaliana na Hilo Kwa Sababu kuwa Mtawala haimaanishi uwe mnyanyasaji) Ila Sasa hivi Ndio Hakuna Furaha wala amani katika Ndoa kwa sababu Mnalazimisha Kwenda kinyume na Nature.
Wewe Unaitii Serikali ya Tanzania Jee Huna Furaha ,, unamtii Boss wako jee Huna Furaha unaongea Vitu ambavyo hazipo kabisa.
Manyanyaso ni nini na unayatafsiri vipi, sasa hivi ambao hawana furaha na amani kwenye ndoa ni wanaume kwa sababu hawataki kukubaliana na ukweli kwamba wanawake hawapendi kutawaliwa na ndio maana siku hizi malalamiko mengi kwenye ndoa yanatoka kwa wanaume kuliko wanawake, achilia mbali mimi tu hivi kuna mtu yeyote ambaye anafurahia kuitii serikali yake bila sababu au kuna mtu ambaye anafurahia kumtii boss wake bila sababu sijui hata kama unaelewa ulichouliza au ndio tayari umechanganyikiwa kwa kukosa hoja
Bi Jadda Mbona Tunaliludia hili mara kwa Mara kuwa Ni Nguvu uwezo na Umadhubuti aliokuwa nao Mwanaume Kulinganisha na Mwanamke na pia hilo linakubali katika vitu vingi Vinavyotawaliana Hatusemi Utawala upo tu From no Where Bali Tunaelekezea Hivyo Vigezo kwa Nature sababu Hakuna Alieamua Mwanamke awe Dhaifu na Mwanaume awe Madhubuti. Imetokea tuu Hivyo. Au labda wewe unajua kwa nini??
Sasa kama hakuna aliyeamua mwanaume kuzaliwa madhubuti na mwanamke kuzaliwa dhaifu kwanini ninyi mjiamulie kwamba utawala utokane na hizo sifa za umadhubuti tu na si sifa nyinginezo, mnawashawishije hao mnaotaka kuwatawala ili wakubali kutawaliwa mind you lazima kuwe na sababu ya kumshawishi huyo unayetaka kumtawala akubali kutawaliwa huwezi kumtawala hivi hivi tu bila sababu yoyote, hakuna utawala wa aina hiyo narudia hakuna mtu anayekubali kutawaliwa bila faida yoyote anayopata toka kwa huyo anayemtawala hili ndio nalisikia kwako na mbaya zaidi haujui kulitetea kwa hoja
Mimi Sio Mzungu Wala hapa Hatujadili Weusi na Wazungu Tunajadili Wanaume na wanawake. Hao Wazungu Kama Wanadai Hivyo Inabidi Wathibitishe Ni Nature How?? Usinisukimizie Upande Nisiokuwepo.
Si ndio nilikuambia wazungu walithibitisha hilo kupitia maandiko ya kwenye biblia kuhusu watoto wa Nuhu ambao ni Shem, Ham, na Jafet, kama wewe ni wa dini nyingine basi inabidi tukubaliane kuacha kutumia references toka kwenye vitabu vya dini kwa sababu hatutaelewana, hapo nilikuwa nakuonesha jinsi mifumo ya hii dunia inavyofanya kazi kwa propaganda na si nature kwahiyo huo mfano nilioutoa wa ukoloni ni relevant kabisa hata ukibisha
Naweza kusummarize Kwa Maneno Machache kuwa Feminism and Atheism and Homosexuality Ni Ndugu Wa familia moja Kwa ajili ya Kuharibu Ulimwengu.
Mimi nimekuuliza kuhusu feminism halafu wewe unaniletea habari za atheism na homosexuality hivi unaona kuna uhusiano kati ya swali langu na hilo jibu lako kweli, yani ni sawa mimi nikuambie unifafanulie kuhusu physics halafu wewe uniambie kwamba physics, chemistry na biology ni ndugu wa familia moja kwa sababu tu zote ni science, au ni sawa nikuambie unifafanulie kuhusu mahakama halafu wewe uniambie kwamba mahakama, bunge na utawala ni ndugu wa familia moja kwa sababu tu yote ni mihimili ya serikali hivi unaona kuna uhusiano hapo
Acha kutudanganya Bi jadda hakuna Jibu Umetoa Kama lipo Nenda kalinukuu Ulilete hapa.
Nimekujibu hivi bila kupepesa macho kama mke ndiye anayemhudumia mume basi mume hana budi kumtii huyo mke je sikukujibu hivyo wewe, kama unaona hilo haliwezekani waulize wale wanaume wanaoitwa mamarioo sijui vibenten wanaohudumiwa na wanawake kwamba kati yao ni nani anayemtawala mwenzake, ndio maana mimi tangu mwanzo hoja yangu ni kwamba ili kuepuka hayo yote ni heri kila mmoja ajitawale mwenyewe na kujifanyia maamuzi juu ya maisha yake kusiwe na wa kumtawala mwenzie regardless of majukumu..haya nijibu swali langu je kama mke ni mama wa nyumbani na mume akakwama kiuchumi anafanyaje
Unatuchanganyia Mada Bi Jadda Hapa Hatujadili Wazungu na Waafrika Nishasema hayo madai ya Wazungu wanatakiwa Wathibitishe wao wenyewe mimi sio Mzungu. Mimi Nazungumzia Wanawake na Wanaume na Nimeshasema Ni Nature kwa Sababu zipi.
Ndio wazungu walishathibitisha sasa kwamba huo utawala ni nature na upo kibiblia, kwahiyo hata watu weusi hatukutakiwa kupinga ukoloni wala kudai uhuru tulitakuwa tuwaache wazungu waendelee kututawala kwa sababu kwa mujibu wao hiyo ni nature, wewe mpaka sasa bado hujaelezea msingi wa hiyo nature zaidi ya kuniletea habari zilizo kwenye maandiko na tamaduni huku ukichanganya na hisia zako binafsi..yani kwa kifupi hadi sasa hakuna swali lolote ulilojibu zaidi ya kupuuzia hoja zangu na kutoka nje ya mada
Ili uwe Feminist lazima Uyakane Maandiko Kwanza ndio Maana nikasema kule juu Feminism na Atheism ni Ndugu kwa ajili ya kuharibu Vizazi(ulimwengu) Sisi Tunaamini Maandiko Matakatifu ni Maneno Ya Mungu aliyoyateremsha kwa Mitume Wake. Mungu ndiye Aliyetuumba na kutupangia Mambo na Kanuni. Labda nikuulize Unaamini katika Mungu na Dini na Vitabu vyake??
Ni mungu yupi sasa unayemzungumzia maana kuna miungu zaidi ya 1000 kulingana na dini zilizopo duniani kwa sasa, wewe unao ushahidi gani kwamba hayo maandiko yalishushwa kwa mitume kutoka kwa mungu na ni wapi huyo mungu mwenyewe alisema hivyo, feminism ni matokeo ya watu kuwa open minded na unprejudiced na kukataa kukubaliana na kila porojo wanazo mezeshwa na wanaume na mfumo dume
Maandiko Matukufu sio Maandiko ya Mwanadamu. Mwanadamu ni Messenger Tuu.
Ushahidi wa hili
Uvulana unahusika nini Hapa Bi Jadda??
Wewe probably ni mvulana kwa sababu ungekuwa mwanaume ungekuwa unafikiria kama wanaume, mind you uvulana au uanaume siyo suala la umri bali akili, kitendo cha kupinga uhalisia ambao hata tamaduni zetu zinaufahamu kinadhihirisha hilo
Kwaiyo Unatudhibitishia Kuwa Mwanamke Akianza Kutafuta Mali Hatomtii Mume wake??. Ndio ujue kuwa Huduma sio Kigezo cha Utiifu. Ili kitu kiwe kigezo cha kitu Furani basi kuwepo kwake kutasababisha jambo na kutokuwepo kwake Kutafanya Jambo Lisiwepo.
Hapana wewe ndio ulitakiwa ujue kwamba utii siyo suala la nature na hili nimeshalifafanua, na ndio maana mwanamke ukiwa unamhudumia ndio atakubali umtawale ila ukiwa humhudumii basi usitegemee utamtawala, yani huo ndio uhalisia utii hauji tu hivi hivi huletwa na jambo fulani na mara nyingi huyo anayetii anakuwa anapenda na si kulazimishwa
Sio Kweli Bibi Zetu Waliishi Kwa Amani na Babu Zetu Na Tuliyashuhudia maisha ya Amani katika Ndoa Zao.
Unalinganisha Ndoa za Babu zetu na Hizi Za Siku hizi leo inafungwa kesho Imevunjika. Embu tupe Comparison kuwa Now Ndoa zina Furaha na Amani na Zinadumu Kwa Sababu Feminism imepiga Hatua Ukilinganisha Na Zama hizo. Leta Comparison hapa.
Ndoa za zamani zilikuwa na furaha kwa sababu tu wanawake hawakuwa na sauti wala uhuru wa kujieleza na kusema mabaya yanayowakumba tofauti na sasa hivi ambapo wanawake wana elimu na uhuru wa kujieleza hivyo wakiyasema mabaya yenu mnawaona kama maadui na kuwaita feminists, ni sawa na kuchukulia mfano wa nchi yenye utawala wa dikteta na kusema kwamba wananchi wa hiyo nchi wana furaha sana kwa sababu wanaitii na hawaipingi serikali yao ila kumbe kiuhalisia wameufyata tu kwa sababu hakuna demokrasia wala uhuru wa kujieleza maana wanajua wakifanya hivyo watashughulikiwa na vyombo vya dola, kama kweli unaona wanawake walikuwa na furaha kwa sababu tu ndoa zao zilikuwa zinadumu kwahiyo unataka kusema kwamba hata kukeketwa napo wanawake walikuwa wanapenda (bila shaka unajua mwanamke akikeketwa hakuna raha yoyote anayoipata kwenye tendo) walikuwa wanakeketwa ili tu wasichepuke wawalindie waume zao kwahiyo unataka kusema hili nalo wanawake walilifurahia na kama hawakufurahia kwanini hawakuresist tangu mwanzo kabisa
Usiwasingizie Bibi Zetu. Wao Hawakuwa na Makucha Yoyote. Nyinyi Mmekuwa Manipulated Umejaziwa Fikra mkaona Ndio uhalisia. Nyinyi Mmeuvua Uanamke, mnataka mmvae Uanaume. Hakuna Suala kuwa Rangi halisi sijui vitu gani Hizo ni Propaganda tuu.

Babu zetu Walikuwa wanatekeleza Kile ambacho Kilikuwa kipo katika Uhalisia kwamba Familia Lazima iwe na Kiongozi na kiongozi ni Baba. Basi.
Kama kweli mwanamke anatakiwa kumtii mwanaume bila sababu yoyote ya msingi maana yake hata mwanaume anatakiwa kumpenda mwanamke bila sababu yoyote ya msingi, kwa vile umerejea maandiko basi kumbuka imeandikwa mwanaume anatakiwa ampende mkewe na mwanamke anatakiwa amtii mumewe, kwahiyo nakuuliza ina maana hata kama mwanamke hataki kutimiza majukumu yake mfano kufanya za nyumbani au hataki kuzaa watoto muda mumewe anaotaka unataka kusema huyo mume anatakiwa aendelee kumpenda tu huyo mke regardless of what hebu nijibu hapo bila kujizungusha
Usinibebeshe vitu Mimi Nimejaribu Kukuambia Sio kila kigezo ni Kigezo cha Utawala. Utawala una vigezo vyake ambavyo Ukiwa navyo Automatically unastahili kutiiwa na Kutawala.
Ni nani anayeamua kwamba hivyo vigezo ndio viwe vigezo vya utawala mbona unakwepa kunijibu hapa kwani una shida gani, je huyo unayemtawala naye akili yake automatically inamtuma kukubali kutawaliwa na wewe kiasi cha yeye kufurahia hilo na mambo kuflow smoothly au ndio hadi utumie nguvu kubwa, mimi nataka uniambie vigezo hivyo ni kwa mujibu wa nani na mwanamke anapotawaliwa anapata faida gani kiasi cha kukubali kirahisi
Kila kitu kina kigezo chake Vigezo haviingiliani ili mradi tuu. Mbona jambo hili lipo wazi kabisa.

Huwezi kukataa kuwa Nguvu na Uwezo ni kigezo cha Utawala wakati hii kanuni inakubali katika Maeneo Mengi sana. Boss wako ni mtawala wako kwa sababu ana Nguvu aliyopewa na Taasisi yako Raisi ni Mtawala kwa sababu Ana nguvu ambayo ameitoa kwetu kupitia Kura zetu Sisi Tunawatawala Wanyama Kwa Sababu ya Nguvu zetu na uwezo wa akili. Kwaiyo Hii kanuni ni applicable sehemu Nyingi ila kanuni ya Kutawala kwa sababu ya Huduma Haikubali katika maeneo mengi kama sio yote.
Hapo umezunguka tu ila kiuhalisia sababu kubwa inayofanya mtu amtii boss wake ni kwa sababu tu analipwa mshahara na anaogopa asipotii kibarua kitaota nyasi, hakuna mtu anayekubali kuajiriwa kwenye taasisi fulani halafu akafanye tu kazi na kufuata maelekezo ya maboss bure bure bila maslahi ya kiuchumi narudia hayupo labda wewe peke yako ndio unaweza hilo, na ndio maana taasisi nyingi pale watumishi wanapokosa mishahara yao huweza hata kuandamana na kuwagomea hao maboss wao unaodhani kwamba wanapewa utii kwa sababu tu ya nguvu au mamlaka walizonazo
Hakuna hoja Umejenga hapa.

Umetetea vyema. Ila sio Hoja. Hoja Ni kuwa Katika Familia Lazima kuwe na Kiongozi hamuwezi kuishi two bulls in one House.
Hiyo tafsiri ya two bulls ni yenu na ni subjective, inawezekana kabisa mkaishi bila kutawalana ndani ya nyumba wote mkaishi kwa kushirikiana na kusikilizana, utofauti kwenye maumbile siyo lazima uweke utofauti hadi kwenye haki na wajibu
Dunia haiendeshwi kama Taasisi Usitudanganye kila nchi ina It's own National sovereignty. Kinachofanya Nchi Furani Kuitii nchi Nyengine katika ajenda na Mikakati ni ile Nguvu Na uwezo ambao Unawafanya Wengine wawe wapole wasikilize na watii.
Sasa hiyo nguvu na uwezo inachangiwa na nini, yani from nowhere tu Tanzania tuwatii Iran kwa sababu tu wametuzidi nguvu na uwezo, ilihali hatufaidiki nao kiuchumi
Tunaposema Nature haimaanishi From no Where. Usijifanye Hauelewi.
Hivi ni kwamba hujui maana ya nature au, nature ni kitu chochote ambacho hakijatengenzwa na binadamu bali kilikuwepo kipo na kitaendelea kuwepo, sasa hiyo mifumo yote ya kiutawala siyo nature bali imetengenezwa tu na binadamu
Na ndio maana tunasema Nature kwa Sababu Hakuna Aliemzuia Mwanamke Awe mtawala au apinge wakati Wanaume wanajitangazia utawala. Kama isingekuwa Nature Wanawake Wangepinga na Hadi leo ingekuwepo katika Historia kuwa Wanawake waligoma Utawala wa kimabavu wa wanaume Lakini walishindwa Nguvu hilo halipo.

Una ushahidi gani kuwa Walitawala kimabavu?? Una Ushahidi wa kihistoria kuwa Wanaume wali install Utawala wao kimabavu??
Sasa kama umeshaona mtu amekuzidi nguvu na uwezo kuna haja gani ya kujaribu kumpinga wakati unajua kabisa hata ukifanya hivyo wewe ndio utashindwa, kwahiyo obviously wanaume waliitumia hiyo advantage kujipa mamlaka sababu walijua wanawake hawana uwezo wa kuwapinga, sasa jambo ukishalifanya kwa kulazimisha kaa ukijua siyo watu wote watalikubali lazima watatokea tu ambao watalipinga hata kama itawagharimu maisha yao yote
Maandiko Hayaamuliwi na wanadamu. Usipotoshe watu.
Sasa maandiko yanaamuliwa na nani na ushahidi uko wapi
Kwaiyo Unakataa kuwa Utii hauletwi na Huduma??

Kila kitu tunachokitii Ni kwa sababu tunaogopa Madhara Furani yanayoweza kutokea kama tukienda kinyume hakuna Utii yaani just utii.
Unamtii Boss wako Ukijua Unaweza kufukuzwa kazi tunawatii wazazi kwa kuogopea Laana na vitu kama hivyo Tunawatii Viongozi wa serikali kwa sababu unaogopa Ukienda kinyume Wanaweza wakafanya Kitu furani. Ki ufupi Utii na Uoga Vinaenda sambamba Kwenye Kila Utii kuna aina furani ya Uoga.
Hivi unajua kwamba unavyonasibisha utii na uoga ndivyo unavyozidi kujifunga na kuenda mbali na uhalisia, kama kweli kwenye kila utii kuna aina fulani ya uoga basi ndio unazidi kuthibitisha ile hoja yangu kwamba utii siyo natural bali ni man made, yani hiyo aya yako imebatilisha yale yote uliyokuwa unabisha kule juu na ni kama umeniunga mkono kwamba utii lazima ujengwe na misingi fulani na hiyo misingi isipokuwepo basi hata huo utii nao hauna budi kutokuwepo tena, kama unadai kwamba utii wa mwanamke kwa mwanaume umejengwa katika msingi wa nguvu basi nijibu hili swali langu kwamba je mama au shangazi au dada nao wanatakiwa wawatii ndugu zao wa kiume kwa sababu tu wamewazidi nguvu na wana uwezo wa kuwacharaza makofi, na je unamaanisha mwanamke anatakiwa kutii amri ya mwanaume yeyote yule hata anayekutana naye barabarani kwa sababu tu ni mwanaume na ana nguvu na uwezo wa kumcharaza makofi huyo mwanamke siyo
Sijaona hoja hapa.

Mimi najibu Hoja Sio malalamiko na Sehemu kama Umeivunja vizuri hoja yangu nakuwa Muadilifu nasema Wazi.
Malalamiko gani acha visingizio wewe unajua maana ya malalamiko, we sema tu umeishiwa hoja unatafuta namna ya kukwepa mada, hilo liko wazi wala haihitaji uwe na elimu ya rocket science ili kuliona hilo
 
Mkuu unachanganya utawala na unyanyasaji, utiifu na uoga/utumwa.. Utawala tunaoongelea hapa sio kumpigisha mkeo pushups au kumchalaza bakora au kujenga mazingira ya kuogopwa kwamba popote mwanaume utakapotokea tu basi mwanamke aanze kutetemeka kwa uoga. Utawala unaoongelewa na ule wa nani anaeweka kanuni na anatakiwa kuzisimamia pale mambo yanapoenda nje ya mstari, hapo ndipo mwanaume anapata advantage kwa sababu kiasili ana nguvu kushinda mwanamke ivyo basi ataweza kuchukua hatua za kinidhamu endapo mwanamke akitoka nje ya mstari. Sasa nimepishana na mwanamke njiani unataka nionyeshe utawala kwa namna gani, kwamba nimkamate nimtandike makofi bila sababu kwa sababu mimi ni mwanaume namzidi nguvu? Nimepishana na mwanamke njiani unataka mwanamke anionyeshe utiifu gani kwamba anipigie magoti na kuniamkia?
Oohh vipi na mwanaume naye akienda nje ya mstari na kanuni anatakiwa awajibishwe na nani, au umeambiwa mwanamke ni kiumbe asiye na utashi kwamba hajui kuwa anachofanya ni kizuri au kibaya, kwa kuzingatia kauli yenu ya kwamba msingi wa utawala wa mwanaume kwa mwanamke ni nguvu maana yake hata ukikutana na mwanamke barabarani ukamtuma afanye jambo fulani basi anatakiwa akutii sababu tu wewe ni mwanaume una nguvu zaidi yake
Kama unaona mama, shangazi au dada anafanya maamuzi ya ajabu ajabu mwanaume lazima uingilie kati kusimamia shoo.
Hivi unaelewa maana ya utawala na utii, sasa wewe ukiingilia kati na kusimamia shoo ndio maana yake unakuwa unawatawala, na wao ndio wanakuwa wanakutii au
Mkuu ilo suala haliwezekani ni against nature. Mafahali wawili hawaishi zizi moja nimeona uko juu umepewa mfano wa wanyama ambao hawazijui hizi ideologies za 50/50 angalia mfumo wao wa maisha kati ya jike na dume ni nani mtawala? Ili mahusiano yaende lazima mmoja awe chini ndipo hapa mwenye nguvu anakua juu kwa sababu naturally dhaifu hawezi kumtawala au kulinga madaraka na mwenye nguvu.
Hivi ni lini wanyama walikaa na binadamu wakawaambia kwamba kwao madume ndio hutawala kwa sababu hizi na hizi (japo kuna species nyingine majike ndio hutawala do your research), labda nikusaidie tu suala la madume kutawala majike kwa wanyama ni sisi binadamu ndio tunaliona hivyo kulingana na tafsiri yetu tuliyojiwekea ya neno utawala na si kulingana na instincts zao wao wanyama, hizo kauli za mafahali wawili sijui upuuzi gani ni mawazo yenu tu ila mwanaume na mwanamke kuwa sawa haimaanishi kwamba wanafanana maumbile na huo utofauti wa maumbile siyo justification ya kuweka utofauti kwenye kila kitu hadi kwenye haki na wajibu
 
Tatizo watu wanaliangalia hilo swala with logical mind ambayo imekua instilled with alot of false knowledge. It requires understanding both sides of the coin, bila hivyo mtaongelea ma dhana na ma ideologies mengi mpk mtachoka bure. Hiyo viscious cycle inachekesha sana🤣
Sure mkuu watu wamelishwa false knowledge ya kutosha, halafu mbaya zaidi wanajiona wako sahihi, na wanalazimisha kuwa eti ni nature hivyo hatutakiwi kuhoji
 
Acheni hizi porojo zenu msingi wa mwanamke kumtii mwanaume uko katika mwanaume kumhudumia mwanamke huwezi kukitawala kiumbe usichokihudumia, kinachofanya wanawake wengi wa dunia ya leo kutokuwatii wanaume wao ni kile kitendo cha wao nao kuanza kujitafutia pesa na mali zao bila kuwategemea wanaume, hata mimi huwa nasema humu kama mwanaume anamhudumia mwanamke basi shurti huyo mwanamke amtii hiyo siyo hiyari bali lazima, ila kama mwanaume hawajibiki kwa lolote kwa mwanamke wake halafu anataka utii basi mtaendelea kulalamika na kutukana hadi mwisho wa dahari, huku mkisubiri mwanamke awe 'reject' ndio awe na utii
Ni vipi kama huyo mwanamke anataka nimhudumie kwa standards ambazo ni unrealistic. Mfano mimi uwezo wangu ni kumnunulia Samsung A05 halafu yeye anataka iPhone 15 pro max. Na kwa hilo kushindwa kulitekeleza ananiletea dharau na kutonitii na kusema simhudumii, hiyo imekaaje kwako? [emoji848]
 
Kama kuwa na tabia njema ni kuwapa maua wazazi au walezi wako, kwanini wanaume msiwe na hizo tabia njema, au ninyi hamtaki wazazi au walezi wenu wapate hayo maua
Jibu hoja upande wako usihamishe hoja na maswali kwa wanaume. Yeye ameongelea kuwa binti/mwanamke kuwa na utii na tabia njema ya mke ni fahari ya wazazi wake. Je ni uongo ama ni ukweli?

Sasa ukija kuleta deflections maana yake ni hautaki kukubaliana na ukweli.
 
Huyo Jadda uliyemtaja nadhani ndo mwanamke jeuri JF nzima, ngoja nature ifanye kazi yake kisawasawa.
Nature huwa ni mwendo wa K.O haicheki na kiumbe yeyote yule.
 
Back
Top Bottom