Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Habari zenu wakuu. Natumaini mko salama humu jukwaani. Bila kupoteza muda, naomba niende moja kwa moja kwenye mada.
Jana nilikutana na mjadala mtandaoni kuhusu uzinduzi wa kadi mpya za mwendokasi, ambapo sasa bila kadi hii huwezi kufanya safari kwenye usafiri wa mwendokasi. Hii imenifikirisha kuhusu utitiri wa kadi mbalimbali tunazotumia kwa huduma tofauti, kama N-Card kwa ununuzi wa tiketi za michezo na kadi mpya za mwendokasi kwa usafiri. Changamoto hii ya kuwa na kadi nyingi inaleta usumbufu na hatari ya kupoteza kadi hizo.
Nadhani ni wakati wa serikali na taasisi husika kuangalia uwezekano wa kuwa na kadi moja inayoweza kutumika kwa huduma zote kwani itapunguza mzigo wa kubeba kadi nyingi na itarahisisha maisha kwa kuongeza usalama na urahisi wa matumizi kwa wananchi.
Nawakaribisha kwa michango yenu kwenye mjadala huu muhimu!
Pia soma: