Utitiri wa maghorofa yanayojengwa Kariakoo siku hizi inaashiria nini?

Utitiri wa maghorofa yanayojengwa Kariakoo siku hizi inaashiria nini?

Mamujay

Senior Member
Joined
Dec 24, 2022
Posts
149
Reaction score
345
Mitaa mingi Kariakoo majengo mengi yanajengwa hii Ina ashiria nini?

Naombeni majibu wale wazee wa kusoma alama za nyakati ndio naowataka.
 
Nikiri hapa, mie siyo injinia, mpanga miji, mwanasiasa, mwenyeji au Mwanasayansi wa Kariakoo wala wa Magorofa! Sina ajira yeyote katika Serikali za Mitaa au kitu chechote kinachoanza na Serikali. Maono ni yangu pekee. na Maoni ni yangu .

Hivyo, nianze na kusema

Kuna ashiria ulimbukeni.
Kuna ashiria Maendeleo Uchwara

Kuna ashiria Uhaba wa ardhi na uhaba kwenye mipango ya Mipango miji Kariakoo.

Ina Ashiria Ubunifu hafifu.

Nimalize

Naona kama Dar-es-Salaam ingepaswa kukua kwenda nje na sio kwa mtindo uliopo sasa kama inavyotokea na kuonekana kama hapo Kariakoo.

Kariakoo na vitongoji jirani vingepaswa kubakia kama vilivyokuwa. Sasa ni kubana banan kana kwamba hakuna ardhi.

Hayo magorofa yote yatabidi yahudumiwe na Vikosi vya Zimamoto vyenye kila aina ya kifaa kufika katika eneo na Kupanda juu gorofani bila vikwazo. Sisemi hilo ndilo tatizo kuu, ila laweza kuwa tatizo mbeleni. Kwa sababu imejengwa juu ya mipango ya zamani na miundombinu ya zamani. Kariakoo itaweza kugharamia matrilioni ya pesa, za kuhamia DoDoma kuonekana mtoto!

Lazima kuwe na miundombinu yakuweza kuhimili mshikemshike ya watu kurundikana eneo moja.

Hatahivyo, inaonekana wale wenyeji wenyewe wameamua kuuza ardhi zao ambazo ziilikuwa ni ndogo kimraba kwa pesa nyingi na Kuendeleza maisha yao.
 
Mitaa mingi kaliakoo majengo mengi yanajengwa hii Ina ashiria Nini?
Naombeni majibu wale wazee was kusoma alama za nyakati ndio naowataka.
we mgeni mbona tangu zilipo pigwa marufuku mbavu za mbwa wenye hela wakaanza kuwekeza magorofa
 
Ukijenga gorofa kariakoo unawahi kupata wapangaji kwa bei nzuri vyumba vingine huwa ni godown za kuhifadhi mizigo kutoka bandarini hasa magendo ya kwenda mikoani kwa hiyo miaka michache unaanza kula faida.
 
Kujenga magorofa k.koo ni dalili kwamba makao makuu ya nchi yanarudi pale magogoni!!!!
Ruksa pia kujenga Dodoma, ni vile tu utashi utakavyokutuma! Calculation on how you can payback! ::Most Important!
Si serekali inayojenga, bali ni watu binafsi na utashi wao!
 
Hakuna ujinga na kosa kubwa kama kuacha mpango wa KIGAMBONI CITY...

Ulikuwa ni mpango wa maono.....lakini ni kipimo.cha uwezo wetu kufikiri
 
Back
Top Bottom