Nikiri hapa, mie siyo injinia, mpanga miji, mwanasiasa, mwenyeji au Mwanasayansi wa Kariakoo wala wa Magorofa! Sina ajira yeyote katika Serikali za Mitaa au kitu chechote kinachoanza na Serikali. Maono ni yangu pekee. na Maoni ni yangu .
Hivyo, nianze na kusema
Kuna ashiria ulimbukeni.
Kuna ashiria Maendeleo Uchwara
Kuna ashiria Uhaba wa ardhi na uhaba kwenye mipango ya Mipango miji Kariakoo.
Ina Ashiria Ubunifu hafifu.
Nimalize
Naona kama Dar-es-Salaam ingepaswa kukua kwenda nje na sio kwa mtindo uliopo sasa kama inavyotokea na kuonekana kama hapo Kariakoo.
Kariakoo na vitongoji jirani vingepaswa kubakia kama vilivyokuwa. Sasa ni kubana banan kana kwamba hakuna ardhi.
Hayo magorofa yote yatabidi yahudumiwe na Vikosi vya Zimamoto vyenye kila aina ya kifaa kufika katika eneo na Kupanda juu gorofani bila vikwazo. Sisemi hilo ndilo tatizo kuu, ila laweza kuwa tatizo mbeleni. Kwa sababu imejengwa juu ya mipango ya zamani na miundombinu ya zamani. Kariakoo itaweza kugharamia matrilioni ya pesa, za kuhamia DoDoma kuonekana mtoto!
Lazima kuwe na miundombinu yakuweza kuhimili mshikemshike ya watu kurundikana eneo moja.
Hatahivyo, inaonekana wale wenyeji wenyewe wameamua kuuza ardhi zao ambazo ziilikuwa ni ndogo kimraba kwa pesa nyingi na Kuendeleza maisha yao.