Utitiri wa maghorofa yanayojengwa Kariakoo siku hizi inaashiria nini?

Utitiri wa maghorofa yanayojengwa Kariakoo siku hizi inaashiria nini?

Ila nilishangaa sana Jiji kupitisha nyumba za chini kujengwa KKOO mtaa wa Kongo karibu na Bigbon kuna nyumba za chini zimejengwa majuzi
Hazijajengwa mkuu, pale ni nyumba za zaman zimekarabatiwa tu ila ukibomoa kabisa lazima ujenge gorofa
 
We jamaa unatembea mjini unahesabu maghorofa waliojenga wenzako! Utachelewa sana![emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Natania tu buana.
Ni kweli mitaa mingi kkoo ukipita utaona ujenzi unaendlea sasa hapo amehesabu vp?

Labda kama hauna harakati za huku mjini
 
Angekuwepo yule wote wanaojenga wangepewa kesi....kisha waambiwe kuacha mpunga kwa Dpp kisha tutaarifiwe Dpp hana nia ya kuendelea na kesi, hihihiii bagosha!!
 
Kama juzi nilikuwa karibu na mtaa wa narung'ombe nikakuta kuna jengo la ghorofa kama sita linadondoshwa,nikashangaa kweli nikasema hapa itakuwa linashuka ghorofa la juu zaidi lenye viwango nyake,ila wacha mji uchangamke
 
Kuna ambalo lilipinda kidogo likapigwa stop ila naona wapangaji wa chini bado wapo. Siku likishuka itakuwaje?
 
Mitaa mingi Kariakoo majengo mengi yanajengwa hii Ina ashiria nini?

Naombeni majibu wale wazee wa kusoma alama za nyakati ndio naowataka.

1. Mtu ana hela.
2. Kapata kiwanja.
3. Kariakoo ni business area.
4. Kapewa vibali.

Nyakati gani zaidi ya uwekezaji? Hii kweli inaitaji rocket science?
 
Wacha Kariakoo ijengwe ili iwe kama Eisleight ya kule Nairobi.
 
Nikiri hapa, mie siyo injinia, mpanga miji, mwanasiasa, mwenyeji au Mwanasayansi wa Kariakoo wala wa Magorofa! Sina ajira yeyote katika Serikali za Mitaa au kitu chechote kinachoanza na Serikali. Maono ni yangu pekee. na Maoni ni yangu .

Hivyo, nianze na kusema

Kuna ashiria ulimbukeni.
Kuna ashiria Maendeleo Uchwara

Kuna ashiria Uhaba wa ardhi na uhaba kwenye mipango ya Mipango miji Kariakoo.

Ina Ashiria Ubunifu hafifu.

Nimalize

Naona kama Dar-es-Salaam ingepaswa kukua kwenda nje na sio kwa mtindo uliopo sasa kama inavyotokea na kuonekana kama hapo Kariakoo.

Kariakoo na vitongoji jirani vingepaswa kubakia kama vilivyokuwa. Sasa ni kubana banan kana kwamba hakuna ardhi.

Hayo magorofa yote yatabidi yahudumiwe na Vikosi vya Zimamoto vyenye kila aina ya kifaa kufika katika eneo na Kupanda juu gorofani bila vikwazo. Sisemi hilo ndilo tatizo kuu, ila laweza kuwa tatizo mbeleni. Kwa sababu imejengwa juu ya mipango ya zamani na miundombinu ya zamani. Kariakoo itaweza kugharamia matrilioni ya pesa, za kuhamia DoDoma kuonekana mtoto!

Lazima kuwe na miundombinu yakuweza kuhimili mshikemshike ya watu kurundikana eneo moja.

Hatahivyo, inaonekana wale wenyeji wenyewe wameamua kuuza ardhi zao ambazo ziilikuwa ni ndogo kimraba kwa pesa nyingi na Kuendeleza maisha yao.
Duh
 
Back
Top Bottom