Utitiri wa viongozi serikali una tija gani kwa Taifa?

Labda kama hiyo katiba tutashushiwa toka mbinguni, au tuandikiwe na malaika.
Lakini huyu mama akumbuke yeye alikuwa makamu mwenyekiti wa lile bunge la katiba, akiondoka madarakani bila kutimiza hili hakika atakuwa rais mstaafu alofeli zaidi kwa upande wangu, tena huyu ana fursa nzuri kwa sababu hajapigiwa kura direct.
 
Wewe Mataga hutakiwi hata kukosoa chochote! Nyinyi ndiyo wale wale wafuasi wa chama cha kishetani kama ccm.

Tofauti yako na Mataga wengine ni moja tu, wewe unakufa njaa huko kwenu Mchamba wima! huku wenzako wakipata ulaji.
Aiseee!!! Tulia kabisa, usije kunitafutia ban zingine hapa JF, sawa!??? Usithubutu kabisa kumtaja JPM vibaya. Utabaki unajilaumu the rest of your life 🙂
 
Lakini huyu mama akumbuke yeye alikuwa makamu mwenyekiti wa lile bunge la katiba, akiondoka madarakani bila kutimiza hili hakika atakuwa rais mstaafu alofeli zaidi kwa upande wangu, tena huyu ana fursa nzuri kwa sababu hajapigiwa kura direct.
Hoja yangu ni kwamba hata kama ile draft ya tume ya warioba ingepitishwa kuwa katiba, sijaona unafuu ambao mwananchi wa kawaida angeupata.

Wanafunzi kumi wa kidato cha sita wangeweza kuandika document nzuri sana kuliko ile takataka iliyoligharimu taifa mabilioni ya shilingi
 
Kati ya watu ambao hawana kazi kabisa ni wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, maDAS na maRAS.

Hizi nafasi zifutwe. OCD na RPC, wawe wakuu wa kamati za ulinzi wilayani na mikoani respectively. Tuwe na mkurugenzi wa Wilaya atakaye report kwa gavana wa mkoa. Gavana wa mkoa achaguliwe na wananchi. Mkoani kuwa na baraza la maendeleo la mkoa ambalo wajumbe wake watakuwa wenyeviti wa Halmashauri, mameya na wabunge ndani ya mkoa husika. Nafasi ya ukurugenzi wa wilaya iwe ni nafasi ya kiutalaam, iombwe, ishindanishwe na iwe na vigezo vinavyotambulika.
 
Hoja yangu ni kwamba hata kama ile draft ya tume ya warioba ingepitishwa kuwa katiba, sijaona unafuu ambao mwananchi wa kawaida angeupata.

Wanafunzi kumi wa kidato cha sita wangeweza kuandika document nzuri sana kuliko ile takataka iliyoligharimu taifa mabilioni ya shilingi
Sisi kama nchi au wananchi tuanzie wapi sasa mkuu? Mbona mapichapicha kila kona?
 
Aiseee!!! Tulia kabisa, usije kunitafutia ban zingine hapa JF, sawa!??? Usithubutu kabisa kumtaja JPM vibaya. Utabaki unajilaumu the rest of your life 🙂
Muone huyu Mataga eti ananitishia nyau! 🤭 Kuna sehemu kweli kwenye hayo maelezo yangu nimemtaja huyo JPM wako! Au ndiyo umepaniki kiasi cha kushindwa kuona hata nilicho kiandika!!

By the way, mbona huyu Mama alikuwa ni Msaidizi wake! Imejukuwaje sasa amewaacha yatima!! Eti nitabaki kujilaumu the rest of my life! You are not serious at all!! 😁😁
 
Gavana wa mkoa achaguliwe na wananchi. Mkoani kuwa na baraza la maendeleo la mkoa ambalo wajumbe wake watakuwa wenyeviti wa Halmashauri, mameya na wabunge ndani ya mkoa husika. Nafasi ya ukurugenzi wa wilaya iwe ni nafasi ya kiutalaam, iombwe, ishindanishwe na iwe na vigezo vinavyotambulika.
Ukiondoa huyo mkurugenzi, wengine wote watapatikana kwa kuchaguliwa. Kwa mfumo wetu huu corrupt wa uchaguzi unategemea mabadiliko gani yanayoweza kupatikana!
 
Huu ujinga unatakiwa ukomeshwe haraka iwezekanavyo kupitia Katiba Mpya ya Wananchi.

Cheo kama cha Mkuu wa Mkoa na Wilaya, RAS na DAS, Afisa Tarafa, nk kinainufaisha CCM zaidi kuliko Taifa! Mbaya zaidi kila mwezi mabilioni ya pesa za walipa kodi wa nchi hii hutumika kuwalipa hawa makada wa ccm!

Halafu bado tunaongezewa TOZO kwenye simu!
Toka ni zaliwe sijawahi kusikia mtanzania anasema anatoka kwa afsa tarafa kupata huduma.
 
Lakini huyu mama akumbuke yeye alikuwa makamu mwenyekiti wa lile bunge la katiba, akiondoka madarakani bila kutimiza hili hakika atakuwa rais mstaafu alofeli zaidi kwa upande wangu, tena huyu ana fursa nzuri kwa sababu hajapigiwa kura direct.

Asipoikomboa Zanzibar kutoka kwa mkoloni Tanganyika atalaumiwa sana na waJomba zake.
 
Nimejaribu kufikiri ni kwanini asilimia kubwa ya fedha za serikali znaishia kwenye matumizi ya kawaida, mojawapo ya sababu niliyoona ni uwepo wa utitiri wa viongozi wengi kwenye ngazi za juu hasa kuanzia wilayani na ukizingatia hawa wanahudumiwa siyo tu mishahara mikubwa bali kuna magari/mafuta, nyumba/malazi, posho za hapa na pale plus ubadhirifu huko maofisini n.k

Ukiangalia wilayani kuna wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu tawala, wenyeviti wa halmashauri n.k

Mkoani, kuna wakuu wa mikoa, wakurugenzi wa majiji sijui, makatibu tawala, mameya n.k
Ukiangalia majukumu ya hao viongozi yanafanana fanana sana.

Bungeni ndio vile mipesa mingi isiyoendana na ufanisi wa kazi, mbunge mmoja alipwe 12M kwa mwezi, apewe mkopo wa gari 90M, apewe mafuta lita 1000 kila mwezi, apewe pensheni 250M ndani ya miaka mitano, hapo bado wana kamati mbalimbali huko bungeni, uje uweke wakurugenzi wa mashirika na taasisi mbalimbali za serikali, wenyeviti wa bodi na tume mbalimbali.
Wizarani mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu n.k, hivi kuna haja gani ya kuwa na waziri, naibu waziri na katibu mkuu? Na wizara nyingne zina hadi naibu katibu mkuu[emoji45] kwanini tusiwe na mawazIri wataalam ambao pia watakuwa watendaji?

Kwa utitiri huu wa viongozi kwa nchi maskini km Tanzania tutegemee 90% ya bajeti kuishia kwenye matumizi ya kawaida ya kuendesha serikali. JPM aliwahi kuahidi kupunguza ukubwa wa serikali ila alipofika ikulu kumbukumbu zake zikawa zimeliwa na mchwa, ndo kwanza akaanzisha na wizara mpya ambayo hata waziri muhusika hajui majukumu yake...[emoji15]
Enewei...
Tuliambiwa tukilaumu tutoe na pendekezo, kwangu mimi nafikiri hapa ni Katiba mpya tu, labda itasaidia .
Naunga mkono hoja
 
Mpaka Tanzania na Afrika kuja kulielewa hili na kulichukulia hatua kivitendo, bila shaka tutakuwa tumekula hasara ambayo fidia yake ni infinite compensation.
 
Nimejaribu kufikiri ni kwanini asilimia kubwa ya fedha za serikali znaishia kwenye matumizi ya kawaida, mojawapo ya sababu niliyoona ni uwepo wa utitiri wa viongozi wengi kwenye ngazi za juu hasa kuanzia wilayani na ukizingatia hawa wanahudumiwa siyo tu mishahara mikubwa bali kuna magari/mafuta, nyumba/malazi, posho za hapa na pale plus ubadhirifu huko maofisini n.k

Ukiangalia wilayani kuna wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu tawala, wenyeviti wa halmashauri n.k

Mkoani, kuna wakuu wa mikoa, wakurugenzi wa majiji sijui, makatibu tawala, mameya n.k
Ukiangalia majukumu ya hao viongozi yanafanana fanana sana.

Bungeni ndio vile mipesa mingi isiyoendana na ufanisi wa kazi, mbunge mmoja alipwe 12M kwa mwezi, apewe mkopo wa gari 90M, apewe mafuta lita 1000 kila mwezi, apewe pensheni 250M ndani ya miaka mitano, hapo bado wana kamati mbalimbali huko bungeni, uje uweke wakurugenzi wa mashirika na taasisi mbalimbali za serikali, wenyeviti wa bodi na tume mbalimbali.
Wizarani mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu n.k, hivi kuna haja gani ya kuwa na waziri, naibu waziri na katibu mkuu? Na wizara nyingne zina hadi naibu katibu mkuu[emoji45] kwanini tusiwe na mawazIri wataalam ambao pia watakuwa watendaji?

Kwa utitiri huu wa viongozi kwa nchi maskini km Tanzania tutegemee 90% ya bajeti kuishia kwenye matumizi ya kawaida ya kuendesha serikali. JPM aliwahi kuahidi kupunguza ukubwa wa serikali ila alipofika ikulu kumbukumbu zake zikawa zimeliwa na mchwa, ndo kwanza akaanzisha na wizara mpya ambayo hata waziri muhusika hajui majukumu yake...[emoji15]
Enewei...
Tuliambiwa tukilaumu tutoe na pendekezo, kwangu mimi nafikiri hapa ni Katiba mpya tu, labda itasaidia .
Tanzania ni nchi tajiri sana. Kama hata hawa viongozi wangekuwa waadilifu na walendo tu, hata bila kuondolewa kwa nafasi zao hizi, bado kuna rasilimali za kutosha kabisa kuleta maendeleo hilimivu. But viongozi wamepewa dhamana na marupurupu kibao, lakini ndio ringleaders wa mafisadi, wabadhirifu, wazembe, wahujumu-uchumi, walarushwa na vibaraka wa Amsterdam na genge lake la mabepari na mabeberu.
 
Back
Top Bottom