DOKEZO Utoaji tenda Arusha DC kuna harufu ya Rushwa na matumizi mabaya ya madaraka, mfumo wa NeST unachezewa

DOKEZO Utoaji tenda Arusha DC kuna harufu ya Rushwa na matumizi mabaya ya madaraka, mfumo wa NeST unachezewa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna changamoto ambayo bila kuifuchua inaweza kuzidi kuwa kubwa na kusababisha ubadhirifu, rushwa na mengine mengi yasiyofaa kwenye jamii yetu.

Uongozi wa Halmashauri ya Arusha DC imekuwa ikifanya michezo michafu kwenye utoaji wa tenda wa kukusanya ushuru wa Halmashauri pamoja na kuchezea mfumo mzima wa ukusanyaji mapato, fedha zinaenda mifukoni mwa watu badala ya kwenda Serikalini

Ipo hivi, Mwaka 2023 kuna mtu alipewa tenda ya kukusanya mapato ya Halmashauri baada ya kushinda Tenda iliyotangazwa, lakini kilichokuja kubainika baadaye ni kuwa hakushinda kihalali.

Kwanza alishinda kwa kuwa Afisa Ugavi wa Halmashauri aliyekuwa akisimamia mchakato na mshindi wa tenda wana ukaribu wa aina fulani.

Hilo tuliliacha likapita, tukasema this time tutajipanga na kufikisha ujumbe kwa usahihi na ikiwezekana kuongeza ushindani katika uombaji wa tenda.

Wakati mchakati ukiendendelea tukagundua kuwa wahusika hasa Afisa Ugavi wa Halmashauri ama na wenzake kadhaa au yeye mwenyewe, wanashiriki kuuchezea Mfumo wa NeST unaotumika kuomba tenda, ambapo wale wanaoomba hasa wa Arusha na wana maslahi hawawezi kuona maombi hayo.

Namaanisha hivi mfano Juma na Bakari wao wamejisajili ndani ya mfumo na wana maslahi na tenda hiyo, hawawezi kuona tenda, kisha wale wengine waliojisajili ambao hawana maslahi wanaweza kuona maombi hayo, ni kama ilivyo kwenye Mfumo wa Status wa WhatsApp, ambapo mtu anaweza kuziba usione alichopost.

Kwa nini wnafanya hivyo, wanafanya hivyo ili watumaji maombi wawe walewale waliolengwa.

Yule aliyeshinda Tenda mwaka jana, safari hii akasajili kampuni sit ana zote zikaomba, hivyo mtu mwingine akiangalia kwenye mfumo anaona maombi yapo na watu wameomba lakini kiuhalisia kuna mambo yanayoendelea na mtu wa karibu na watu hao ndio atajua kinachoendelea, mwingine taona kila kitu kipo sawa.

Mkuu wa Wilaya alijulisha juu ya suala hilo lakini naye kapotezea, aliingilia lakini hakuwa na nia ya kuondoa tatizo sugu linaloendelea.

Kwa ufupi ushindani wa Tenda katika Halmashauri ya Arusha DC haipo fair kwa maana hakuna haki.

Wale wenzetu waliojaribu kufikisha taarifa hii TAKUKURU, ikabainika kuwa pale katika ofisi hiyo Afisa anayesimamia ni mmoja wa watu mbao ana ukaribu na timu ile ya Watu wa Halmashauri.

Hivyo, ukifikisha taarifa TAKUKURU Arusha ili wasaidie Taifa lipate malipo stahiki, taarifa zitawafikia wahusika hata kabla ya Ofisi hiyo kufanya maamuzi.
 
NeST ni takataka kama ufahamu yani tena inatolewa ikipoint mtu .na cha kuchekesha kama hakuna tofauti na zabuni kuzikuta kwa mkurugenzi
 
Hivi ni lini tutaacha hii tabia ya ubinafsi.

Vitu vya maendeleo kwa Uma wengine wanajipigia hesabu wao kwa faida zao. Arusha watendaji mmezidi kila siku mnalalamikiwa kwa kero zenu za kurudisha nyuma maendeleo.

Ikibainika ni kweli bila kuonewa wa husika wachukuliwe hatua kali kama vile kufukuzwa kazi, kutaifishiwa mali zao wanazomiliki na kifungu cha miaka 5.
 
Nakuibia Siri...tenda yote kabla ya i
Kuwekwa NEST jua imeshapata mtu....nimekuona Hilo kupitia industry ya madawa...
 
Hii ndio Tanganyika ya KIZIMKAZI aka CHURA. Wapiga dili wooote ndio watu wake na YY kama Dalali MKUU!!.

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Pole sana mkuu.

Hili swala nimelipigia kelele sana lkn sijawahi kupata msaada.

Mfumo una aina mbili za kutangaza zabuni (1. Advertisement na Invitation). Mfumo wa Invitation unawapa hawa room kubwa sana kumpa kazi mtu wanaemtaka.

Nakushauri usikate tamaa, pambana wakati wako utafika. Ipo siku na wewe utapata pa kutotokea, endelea kujaribu.

Evalution criteria za Nest zinafanana almost nchi nzima. lakini cha kushangaza unaweza kuomba kazi Mtwara ukanyimwa kwa kigezo cha kutokidhi vigezo lakini ukaomba Kigoma ukapata kwa vigezo vile vile.

Nakusihi tena pambana na endelea kujitafuta. Usitegemee kupata msaada kama unatafuta haki kwenye Sector ya manunuzi popote pale Tanzania.
 
Back
Top Bottom