Utoaji wa tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi wenye Ubunifu yafana

Utoaji wa tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi wenye Ubunifu yafana

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Viongozi mbalimbali nchini na nje ya Tanzania, wamehudhuria hafla ya utoaji tuzo ya taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu.

Hafla hiyo imefanyika leo Alhamisi 13, 2023 katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni Rais Mstaafu wa Msumbiji, Joaquim Chissano, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Rizik Mdoe na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Carolyne Nombo.

Wadau wa uandishi bunifu nao walikuwepo katika hafla hiyo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika nchini

Wahamasishaji wa Uandishi bunifu wakiongoza hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam

Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe.Joaquim Alberto Chissano akiwa pamoja na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akiwa katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo akiwa katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam

Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa akiwa katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba akiwa katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Edward Mpogolo akiwa katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam




Waandishi nguli wa mashairi na riwaya mbalimbali wakiwa katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam


Waandishi nguli wa mashairi na riwaya mbalimbali wakiwa katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam

Mwandishi wa nguli wa vitabu vya Riwaya nchini Richard Mabala akiwa katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam
 
Mwandishi mbona umetubania kujua maudhui ya tuzo hizo na taarifa za wagombania tuzo!
 
Kitenzi chake ni "tuza"

Hivyo tuzo ni sahihi.

Tunza ni kitenzi kingine chenye maana nyingine.
Katika lugha za Kiswahili za Pwani ya Kenya, neno la asili ni "tuzo", na kitenzi chake ni "kutuza"; hakukuwako na neno "tunzo" Hilo nalijua Ila

Huko Pwani ya Kenya kuna kitenzi "kutunza" pia (ambacho kina maana mbili tafauti) - kutegemea na jinsi utakavyoitamka hiyo "t" iliyoko kwenye neno hilo. (Katika lugha hizo, kuna namna nne za kuitamka harufu "t", ambazo hubadilisha maana ya neno). Neno "tunza" ukilitamka kwa "t" laini - kwa kuiweka ncha ya ulimi na kuishikamanisha baina ya meno ya mbele ya juu na ya chini - neno hilo litakuwa na maana ya kuhifadhi au kuhakikisha kwamba hicho ukitunzacho hakifikwi na madhara au uharibifu, kwa mfano. Lakini ukiitamka "t" kavu (kwa mfano, kama iliyoko kwenye neno "pita"), basi neno "tunza" litakuwa na maana ya kidonda, au sehemu ya mwili, kuwa na usaha; yaani kutunza usaha. Kama ujuavyo, kwa maana hii ya pili, neno litumikalo katika Kiswahili Sanifu, (kutokana na lugha za Kiswahili za Pwani ya Tanzania - Zanzibar na Bara), ni "kutunga usaha."

Kwa hivyo, kwa lugha za Kiswahili za Pwani ya Kenya, mtu afanyapo jambo zuri na ukalifurahikia, basi utamtuza mtu huyo; humtunzi.

Katika hizo lugha za Kiswahili za Pwani ya Kenya, hiki kitenzi "kutuza" ni ufupisho wa kitenzi "kutuliza" (kwa mfano, kutuza moyo) - ambavyo vyote viwili viko katika hali ya kusababisha. Vitenzi vya asili ni "kutua" au "kutulia" - kwa maana ya kuwa katika hali ya utulivu baada ya kuwa na wasiwasi, wahaka au jaka la moyo, yaani kumakinika; au baada ya kuhangaikahangaika; au baada ya kulifanya jambo likafanyika kisawasawa na watu wakatosheka nalo.

Kama nilivyoeleza, vitenzi "kutuza" na "kutuliza" viko katika hali ya kusababisha. Na nomino/ jina "tuzo" lawa ni ufupisho wa neno "tulizo" kwa maana ya kitu apawacho mtu ili kumtuliza baada ya kufanya jambo fulani zuri na watu wakalifurahikia. Kwa maoni yangu ya kiwanafunzi, hapa ndipo niionapo sababu ya kwa nini katika baadhi ya lugha
za Kiswahili, kwa muktadha huu, maneno yatumiwayo ni "tuzo" na "kutuza", na wala si "tunzo" na "kutunza".

Au wewe wasemaje?
 
Back
Top Bottom