Utofauti ambao niliuona Kati ya Tanazania na Kenya katika Maisha ni huu hapa

Utofauti ambao niliuona Kati ya Tanazania na Kenya katika Maisha ni huu hapa

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
32,386
Reaction score
83,431
Kwanza nchi za EA .au nchi za jangwa la Sahara ni Kama viongozi wao walizaliwa na Mama mmoja .

Ila zipo tofauti ndogo ,ndogo ambazo niliziona Tz

Wakenya wapo Mbele ya muda kwenye Upande wa teknolojia ,kuliko kenya.

Nidhamu ya muda , wakenya wanajali Sana muda , hata ukitokea msiba wanaweza wakapeleka maiti mortuary hata miezi miwili na baadae ndo wakaja wakazika , wanafanya hivi kujipanga kiuchumi na kutoruhusu msiba kuvuruga ratiba zao za uzalishaji.

Katika shughuli za kiuchumi , wakenya kwao kila kitu kipo professionalism.

Ukiingia katika migahawa ya kenya unaona kabisa hawa wanajua wanachofanya .

Kujitambua -Wakenya wanajitambua Sana kujua haki zao za kijamii , kisiasa n.k.

Kuhusu kiwango cha ujinga , sio kikubwa ukilinganisha na ile nchi jirani.

Hitimisho

Ili utoboe Kenya lazima akili iwe vizuri Sana .
 
Yani hapa ndugu yangu umetuchamba weeee 😂😂😂😂
 
Ukabila sisi wakenya tunaongoza
Ubinafsi tuko number 1
Ukatili hapa sisi ni Barbarians
Life kenya ni expensive sana tuna import junky food na GMO
Rushwa ...daah kenya hatuna soni
Ardhi ..Kenyatta ,MOI na akina kibaki walishagawana kitambo...we are settlers in our our land.
Ustaarabu bongo wametuzidi
 
Kuna siku nikikaa na dada mmoja kwenye daladala,Sasa kila muda akawa anasonya sana na makasiriko mengi.

Ilibidi nimuulize shida Nini?
Kumbe amechukizwa na kauli za konda kufokea abiria yaani Ile "dada,bimkubwa,dingi,Shem,bro vuta nyuma,bana upande huo kama hutaki shuka" na maneno mengi tu.

Ile ongea yake nikagundua ni mkenya,Sasa Mimi nikamwambia pole,ndyo tunaishi hivi.

Akaniambia unajua watanzania ni wavivu hata kujua tu haki zao ukiachana na kupambania haki zenyewe.

Nikamuuliza 'kwahyo na Mimi ni mvivu?'😀😀😀 hakuendelea Tena kuongea maana nilishaanda ngumi angejibu chochote
 
Back
Top Bottom