Utofauti kati ya kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye ubongo(Brain) na kumbukumbu zinazohifadhiwa na akili (Mind)

Hii ni comment ya mwisho kwenye huu uzi, Da'Vinci Jifunze kusoma scientific research, books n.k trust me utajifunza mambo mengi, jiweke mbali na fiction stories kama vile spiritual books, mbona mimi nilianza kusoma vitabu vya physics upya, neuroscience, psychology, philosophy, sasa hivi nasoma history.

Haimaanishi kwamba hizo spiritual books sijawahi kuzisoma, nimezisoma sana sana sana ila baada ya kuanza kuchimbua neuroscience hatimaye nikaujua ukweli
 
Fungua uzi mwingine uniulize hilo swali nitakujibu
Huo muda kidogo sina,wewe fungua huo uzi kisha ujibu swali nililo kuuliza nije tujadili.

Kinyume chake utakuwa unakimbia swali kwa uoga.
 
Nilichosema hapo ni kwamba, kama "mind" yenyewe kwa ujumla wake siyo storage facility, maana yake ni kwamba hata hizo aina za "mind" ulizozitaja hapa nazo vilevile kamwe haziwezi kuwa storage facilities.
Tuchukulie mfano mmoja wa sub-consciuous mind namna inavyofanya kazi. Mtoto mchanga ambaye hajui chochote, hajui vile vile kuwa moto ni hatari kwake, lakini ikitokea kwa bahati mbaya akashika kaa la moto, lazima atachomoa mkono wake, tena bila kuhitaji kufikiria kuwa sasa ameshika moto halafu inabidi auchomoe, hapana. Mtoto atashika kaa la moto na atauchomoa mkono wake kutoka kwenye moto huo muda huo huo tena bila kufikiria. Swali linakuja je, mtoto mdogo ambaye bado ni "tabula rasa", wakati huo anakuwa amehifadhi wapi kumbukumbu za kwamba kaa la moto ni hatari? Je, anapochomoa mkono wake kutoka kwenye kaa la moto, unataka kusema kuwa alikuwa ana hifadhi ya kumbukumbu za uhatari wa kaa la moto kwenye "mind" yake; kwamba kaa la moto ni hatari kwake?

Naomba uwe mwangalifu kuwa anavamia mambo mazito namna hii bila kuwa na uelewa sahihi halafu unaanza kulisha watu matango pori humu kwenye mitandao ya jamii, ni kitu kibaya sana. Naomba ukiwa unaeleweshwa, uwe unaelewa. Tafadhali sana
 
Nawewe mbona unataka kupotosha? Unasema vichaa hawana akili?
Wanayo ila iko katika kiwango ambacho hakijafikia threshold ya ile anayotakiwa kuwa nayo mwanadamu wa kawaida. Akili wanayo.

Kwa ujumla tu ni kwamba, hakipo kiumbe ambacho kiko hai ambacho hakina akili. Kiumbe kilicho hai kisichokuwa na akili, ni mtu aliye kwenye comma ambaye hajitambui hata akigusa kaa la moto hawezi kusikia maumivu yoyote, hata ukimkata na kisu hawezi kusikia maumivu.
 
Ili kitu kiweze kufanya kazi kama storage facility (whether for physical or logical storage) l azima kwanza chenyewe kiwe physical, kinashikika au kinapimika kwa dimensions ambazo ni physical. Unapofanya storage kwa mfano ya data tuseme labda "clouds storage", lazima hilo eneo la clouds liwe lipo na linapimika. Kinachofuata sasa ndiyo hapa wewe utanya logical stoage yako huko. Mind ni kitu ambacho hakina physical dimensions na hivyo kinakosa sifa za kuwa storage facility. Kwenye mwili wa binadamu,, ubongo pekee ndiyo storage facility na hivi vingine ndiyo huwa vinafanya kazi kwa ku-coordinate na Ubongo

Kwa mfano hai, nguli wa Fizikia Albert Einstein alipokufa, kuna daktari mmoja alimfanyia upasuaji kwa siri na kuiba ubongo wakena kuuuhifadhi kwa muda na kwa siri akiwa anaufanyia utafiti akiwa anataka kujua kuwa ubongo unawoweza kuhifadhi "mind" ya mtu kama huyo ulikuwa una tofauti gani na bongo za binadamu wengine kama mimi au wewe

Naomba sana watu wasiwe wanavamia topic nzito namna hii pasipokuwa na uelewa stahiki
 
Reactions: SMU
Asante kwa elimu.

Mtu akifa kuna uwezekano wa ku retrieve kumbukumbu zake kutoka kwenye ubongo wake? Or its absolutely impossible?
 
Asante kwa elimu.

Mtu akifa kuna uwezekano wa ku retrieve kumbukumbu zake kutoka kwenye ubongo wake? Or its absolutely impossible?
Inawezekana.
 
Kuna vitu nimejufunza kwenye hii thread

ila kuwa kurekebisha kidogo ni kuwa Brain & mind is the same thing.

Simple proof ni kuwa kuna sehemu ya brain ikipata itirafu binadamu anasahau kila kitu kwenye maisha yake.

MPAKA JINA LAKE
Gud, je mind inaoneka?? Iko sehem ipi kwenye mwili wa binadam??
 
Asante kwa elimu.

Mtu akifa kuna uwezekano wa ku retrieve kumbukumbu zake kutoka kwenye ubongo wake? Or its absolutely impossible?
Hilo sasa ni swali la kitaalamu zaidi, matabibu au madaktari pamoja na watu wa Artificial Intelligence wanaweza kulijibu kwa ufasaha zaidi swali hili. Lakini naweza kusema kuwa as long as memory huwa zinahifadhiwa kwenye ubongo, uwezekano wa kuzi-retreave memory hizo upo. Tatizo linabaki tu kwenye ugunduzi wa kifaa kinachoweza kufanya kazi hiyo
 
Reactions: SMU
Ck sayansi ikifikia hapo, Mungu atakuwa ameweka makazi yake na watu wake, I mean, hii dunia haitakuwepo, Kuna mambo Mungu ameyafumba kwa faida zetu ili mtafaruku usije kutokea, heb fikiria tu tunyonye kumbukumbu za mwalim, au BM, au JPM halafu ziwekwe wazi unajua nn kitatokea??
 
Reactions: SMU
Usifikirie ubaya tu, fikiria na faida.

Imagine unapata maarifa ya Einstein.....

....labda tufike mahali unaweza ku copy (kwa marehemu mmoja kama Einstein) na ku paste wa vijana mia moja hivi. Si "balaa" hilo mpwa?
 
 
Kuna vitu nimejufunza kwenye hii thread

ila kuwa kurekebisha kidogo ni kuwa Brain & mind is the same thing.

Simple proof ni kuwa kuna sehemu ya brain ikipata itirafu binadamu anasahau kila kitu kwenye maisha yake.

MPAKA JINA LAKE
Nifafanulie kidogo how brain na Mind ni kitu kimoja nijifunze mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…