Utofauti kati ya watu wa Dar (Mijini) na watu wa Mkoani ndio huu

Utofauti kati ya watu wa Dar (Mijini) na watu wa Mkoani ndio huu

Umeenda semina Njombe, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Ramadhani shukia kwa Sanga. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".

Sure, hata Ulaya naamini hawana huu ujinga wetu wa kuacha mira na desturi, wazungu wanaenzi sana desturi na mila zao, japo zetu na zao hazifanani.
 
Ni kwel wanafanyia wa mikoan tu,niliwah kwenda kwa mama mkubwa kaolewa na baba angu mkubwa ila baba kwa wakat huo hakuwepo,mama alkuwa anajfanya kama mtu ambae yupo busy sana hata sio mzungumzaji,ila nilishangaa wkend moja kuna kijana alkuja pale nyumban mama alkuwa mzungumzaj sana na kucheka mpaka nkashangaa,nikajiuliza kuwa kumbe huwa ni mzungumzaj vile na mchangamfu lakin kwangu mim alkuwa muda wote yupo kimya
Mambo ya kujipendekeza niliacha aisee, kabla ya kusafiri kwenda Dar kwa ishu yoyote unawaza na kuwazua uwapelekee nini,unajikongoja kwa tabu unakipata cha kuwapelekea kuepuka aibu ya kwenda mikono mitupu. Baada ya siku kadhaa unagundua ulichowapelea kimwagwa kwa kuozea ndani.

Hii ilishanitokea,nilikupata kibarua Lushoto sasa mkataba ulipoisha nikasema ngoja niwabebee nyanya na apple zile za Lushoto,Mungu wangu baada ya siku tatu niligundua nyanya zimeoza hazkuwekwa hata kwenye friji zile apple alikula anko kwa kuondoa aibu huku akisifia hizi ndo nzuri huku watoto na mama hakuna aliyegusa. Nilijisikia vibaya sana mpaka mambo ya kicahwi labda lakini niligundua tu ni mambo ya kibaguzi kwakuwa mimi ni mtu wa chini. Umasikini ni mbaya sana.

Kwa uzoefu wangu ni kwamba hao watu wa Dar wanafanya hivyo vituko kwa ndugu zao wanaotoka mikoani ambao ni maskini lakini kwenye uwezo kama wao shughuli zote zinasimama mapaka kwenda kupokelewa hata ingekuwa mtu anafika saa nane usiku.
 
Back
Top Bottom