Utofauti uliopo kati ya mwanaume na mwanamke katika hisia za kimapenzi

Utofauti uliopo kati ya mwanaume na mwanamke katika hisia za kimapenzi

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia inasadikika hakuna kitu ambacho kina nguvu sana kama mahusiano ya mapenzi, hata hivyo kutokana na nguvu hiyo ya mahusino, watu wengi hufikiri mwanaume ndio ambao wanaathiriwa kwa kiwango kikubwa na nguvu hiyo.

Watafiti wa masuala ya mahusiano wanazidi kusema ya kwamba, mwanaume kila baada ya dakika tano ni lazima awaze masuala ya kimapenzi, hii ni kutokana wanaume wengi hupenda zaidi jinsia ya kike kwa kuona kwa macho. Ndio maana ukichunguza kwa makini wanaume huwa wanakuwa wanazingatia zaidi katika kutazama jinsia hii ya kike mahali popote walipo.

Hivi hujawahi ona wanaume wamekaa mahali wanapiga stori ghafla akapite mwanamke mzuri mbele ya macho yao ghafla stori zile zikasimama kwa muda? Bila shaka umewahi kuona. Utawasikia wakisema kwa minong'ono aaah angalia kifaa hicho, wapo wengine utawasikia wakisema mcheki chura huyo. Hii ina maana ya kwamba macho ya mwanaume ndio chanzo kikubwa cha kuingia katika mahusiano kabla ya kumjua tabia aliyonayo mtu huyo.

Lakini ukweli ambao upo nyuma ya pazia ni kwamba wanaume wengi huingia katika matamanio ya kimahusiono kwa kuona kwa macho zaidi tofauti na mwanamke. Hata hivyo mahusiano ya kimapenzi aliyonayo mwanaume ni matokeo ya macho yako. Kwa maneno mengine tunaweza kusema matamanio ya hisia za mwanaume yapo katika kuona zaidi kuliko kitu chochote.

Lakini ukienda upande wa pili wa shilingi, mwanamke huwa yupo tofauti sana ukilinganisha na mwanaume katika suala zima la kuingia katika mahusiano. Hisia za mwanamke huwa zipo zaidi katika maneno na mguso katoka kwa mwanaume. Hisia za mwanamke huwa hazipo katika kuona kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na mwanaume.

Mwanamke huamini sana katika maneno ambayo ataambiwa na mwanaume, kwa mfano mwanamke akiambiwa anapendwa zaidi ya kitu chochote katika dunia hii mwanamke huamini hivyo, hivyo maneno ya mwanaume yana nafasi kubwa katika kuziteka hisia za mwanamke.

Lakini pia kama hiyo haitoshi mwanamke hupata hisia zaidi pale anapoguswa na mwanaume, hivyo ndio maana kama utakutana na msichana kwa mara ya kwanza ataka usimguse katika mwili wake, hii ina maana mguso wa mwanaume una nguvu sana katika kuamsha hisia mwili wa mwanamke.

Hivyo kama ndivyo hivyo basi hii ni utofauti mkubwa ulipo kati ya mwanaume na mwanamke katika kuamsha hisia za kimapenzi. Na kitu kikubwa ambacho huongoza hamasa na kudumu katika mahusiano ya kimapenzi ni "mawasiliano", mawasiliano ndiyo chachu kubwa katika mahusiano yenu. Hivyo kila wakati ili muweze kudumu katika mahusiano yenu hakikisha unakuwa na mawasiliano bora kati yako na mwenzi wako.

FB_IMG_1615625521698.jpg
IMG-20210511-WA0135.jpg
 
Ina maana Bi Mkubwa yale makusanyo ya juzi kati pale uwanjani kayaweka kibindoni!? Sijaelewa kidogo kwenye hizo financial mathematics hapo chini?

Wananchi warudishiwe hela zao na fidia za upotevu na usumbufu wa muda, mali, nguvu, fedha, akili na hisia pia. Bi Mkubwa anza na yule mwanariadha aliyetoka Kigoma, sawa?
 
Ina maana Bi Mkubwa yale makusanyo ya juzi kati pale uwanjani kayaweka kibindoni!? Sijaelewa kidogo kwenye hizo financial mathematics hapo chini?

Wananchi warudishiwe hela zao na fidia za upotevu na usumbufu wa muda, mali, nguvu, fedha, akili na hisia pia. Bi Mkubwa anza na yule mwanariadha aliyetoka Kigoma, sawa?
MSHAPIGWA TAYARI
 
Bado mapenzi yanabaki kuwa ni FreeStyle..

No rules. Japo kwa asilimia chache uliyosema yana ukweli..

Masela tukiona tu tako basi walete
 
Bado mapenzi yanabaki kuwa ni FreeStyle..

No rules. Japo kwa asilimia chache uliyosema yana ukweli..

Masela tukiona tu tako basi walete
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom