Utofauti wa Bunge, mkutano na kikao kwa mujibu wa sheria

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
678
Na Elius Ndabila

0768239284

Leo nikiwa kwenye daladala zinazoenda Mwenge nimekuta kuna mtu anamsimulia mwenzake utofauti uliopo kati ya kikao na mkutano kwenye masuala ya Kibunge. Lakini aliyekuwa akizungumza niligundua naye hanaufahamu wa kutosha juu ya dhana hizi. Hata hivyo nikiwa nasubiri kuungana nao kwenye mazungumzo yao iliniweze kuwapa kidogo ufahamu wangu juu ya haya wakawa wameshuka kwenye gari.

Mjadala huu umenifanya nije nitoe elimu fupi juu yaa dhana hizi tatu yaani Bunge la…, Mkutano na Kikao. Nimefanya hivyo nikiamini kuwa wapo wanaojua na wapo ambao hawajui tofauti hizi. Hivyo ninataka nitoe elimu kwa wale ambao hawajui ili tuweze kuwa na uelewa wa pamoja. Ukisoma katiba sura yote ya tatu inayozungumzia Bunge haijatoa maelekezo yoyote juu ya dhani hizi ila imetoa miongozo mbalimbali ya Kibunge.

Kwa ufupi tunapozungumzia Bunge la…..huwa tunahesabu miaka mitano ya uhai wa Bunge. Tunapo sema mkutano wa…..tunakuwa tunahesabu mikutano ya Bunge ndani ya miaka mitano. Na tunaposema kikao cha….. basi tunaakua tunahesabu vikao ndani ya mkutano wa….Inawezekana bado hujaelewa. Ngoja nifafanue kwa mikutadha ya mifano.

1- Mkutano wa Bunge tunahesabu miaka mitano ya uhai wa Bunge. Kwa mfano Bunge lililoanza mwaka 2015 ambalo litamalizika mwaka huu 2020 linaitwa Bunge la kumi na moja (11). Miaka mitano inahesabika kama ni Bunge moja. Kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu Bunge la kwanza lilikuwa ni Bunge la 1965-1970, Bunge la pili ni 1970-1980, Bunge la tatu 1980-1985 na Bunge la 2015-2020 ni Bunge la 11 ukihesabu kwa mfululizo nilioanza nao. Hivyo Mh Ndugai ni Spika wa Bunge la 11, na Bunge la 2020-2025 litakuwa Bunge la 12. Ibara ya 65 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa maisha ya ya kila Bunge ni muda wa miaka mitano. Hivyo uhai wa Bunge huanza pale ambapo RAIS ameita Bunge kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi na hukoma siku ya kulivunja. Ninadhani sasa umeanza kuelewa.

2 - Mkutano wa…, Mkutano ni tofauti na Bunge la…Kwa mujibu wa Katiba na kanuni za Bunge kila mwaka kunatakiwa kuwe na Mikutano ya Bunge minne. Mkutano wa Bunge ni mfululizo wa vikao vya Bunge, kuanzia kikao cha kwanza hadi cha mwisho. Kuna mikutano 20 katika Bunge moja. Maana yake ni kwamba kila miaka mitano inakuwa na mikutano 20. Kwa mfano Mkutano unaoendelea sasa Dodoma ni Mkutano wa 18 bado mikutano miwili tu kumalizika kwa Bunge naa kuitishwa kwa Uchaguzi. Kwa utaratibu wa Kibunge Mkutano wa kwanza unakuwa kati ya mwezi October hadi November, MMkutaano wa pili ni kaati ya January hadi February , Mkutano wa tatu ni kati ya AApril hadi Juni na Mkutano wan ne ni kati ya Augost hadi Septemba. Hivyo mikutano inahesaabiwa ndani ya miaaka mitano.

3 - Kikao cha…Kwa mujibu wa sheria na kanuni za kudumu za Bunge vikao vinahesabiwaa ndani ya mkutano mmoja. Kikao cha Bunge ni kile kinachoanza kwa kusomaa Dua na baadae mchana au jioni kuahirishwa hadi siku inayofuata au inayotajwa. Na kanuni ya 29(2) ya kanuni za kudumu za Bunge imempa nguvu Waaziri mkuu ambaye ndiye kiongozi wa shughuli zaserikali Bungeni kutoa hoja ya kuahilisha Bunge kwa kutaja siku, mahali na saa ambapo ambapo mkutano unaofuata utaanza. Kwa mfano jana siku ya Jumanne vikao vya Bunge vimeanza Dodoma. Hivyo jana kilikuwa kikao cha kwanza, leo cha pili na kesho cha Tatu.

Kwa msingi huo nikitaka kutumia vikao vinavyoendelea Dodoma ambavyo vimeanza janaa ninaweza kutamka hivi,… BUNGE LA 11, MKUTANO WA 18 NA KIKAO CHA 2(kwa leo). Kesho kitakuwa kikao cha tatu ila Bunge litaendelea kuwa la 11 na mkutano wa 18.Huu ndio ufahamu wangu kwenye suala la Constitutional Law, na ninaaamini nimejaribu kukutoa wingu zito ulilokuwa nalo juu ya utofauti wa BUNGE, MKUTANO NA KIKAO.
 
Asante sana kwa hii elimu

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Asiyeelewa huo uafafanuzi wako hatakaa aelewe tena hata akifafanuliwa na mbunge, spika au katibu wa bunge
Pia anayejifanya ameelewa kila kitu kana kwamba maelezo hayo ni mwisho basi hatataka kusoma, kutafiti na kusikiliza maelezo zaidi ya hayo, kimsingi atakuwa mwelevu finyu wa kujifanya anajua kila kitu na mjinga wa kujitakia.
 
Back
Top Bottom