Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Wakati watu wanahimizwa kusoma tangu utotoni na kujiendeleza hata wakiwa makazini, ila ukweli ni kwamba, kusoma sana na kupata ma-degree mengi, sometimes huwa hakuna maana sana na hii ni kutokana na ulipaji wa mishahara serikalini kutegemea mtu anafanya kazi katika taasisi au shirika gani la umma.
Unaweza kuwa na masters ila kama uko wizarani au katika Halmshauri, unawezakuta unazidiwa mshahara na mtu mwenye Bachelor au hata Diploma anaefanya kazi katika taasisi (mara nyingi hizi Authority) za serikali. Hapo bado marupurupu.
Kwa mfano, dereva mwenye form iv anaeanza kazi pale BOT au TRA, sijui kama anazidiwa mshahara na mtumishi anaenza kazi akiwa na Diploma au Bachelor katika Halmshauri zetu.
Haya mambo ya kila taasisi kuwa na scale zake za mishahara, sometimes kunaondoa kabisa maana nzima ya kukaa darasa moja na kusotea degree ile ile wakati mkija kuajiriwa mmoja anakuwa yuko mawingumi na mwingine ardhini.
Kuna umuhimu wa serikali kutazama upya jambo hili na kufanya harmonisation ya mishahara serikalini ili kuondoa hali hii.Mambo ya kusema kuna taasisi zinazalisha au zinaingiza fedha serikalini hakutoia uhalali wa huu upendeleo kwani elimu waliyonayo wangeipata wapi bila mwalimu au wakiuguwa bila daktari au nesi watakuwa na afya ya kukusanya hizo hela na kuzipeleka serikalini au kutoa gawio kwa serikali?
Kama huu utofauti ni lazima uwepo (haukwepeki!), basi uwe reasonable na sio kuwa na ma- gape makubwa na ya kukatisha tamaa kwani ukweli wote tunategemeana. Wewe unaelipwa mshahara wa mamilioni, bila Polisi usalama wa mali zako ungetoka wapi?
Siku tukipata mtawala ataeamua kuweka wazi/hadharani scale za mishahara kwa watumishi wa umma, nadhani siku hiyo mitandao ya kijamii itashindwa kuhimili mijadala itayoibuka baada ya hapo, na huyo Raisi atajizolea sifa nyingi iwapo atahakikisha kunawakuwa na harmonisation ya mishahara serikalini.
Kama mnasema kila mtu na bahati yake, basi hata wakati wa ukoloni wazungu na wahindi ilikuwa sahihi kulipwa mishahara minono kutokana na bahati yao ya kuwa na ngozi nyeupe.