Utofauti wa mishahara katika Utumishi wa umma, kunavunja moyo na kusababisha watu kubeza kusoma sana

Kati ya NIDA na ILALA/KINONDONI manispaa nani anaingiza mapato mengi serikalini kwa mwaka?
Safi Sana kwa kuelewa. Sasa anzisha mada ya mbuga kunyang'anywa Tanapa na kupewa halmashauri ili mishahara yenu ipande au siyo?
 
Kwamba halmashauri Hawana umuhimu na Kazi zao ni ndogo sanaa?

Halmashauri ya ilala kwa robo ya pili ya mwaka imekusanya Bil 18.8.
Nao si wanazalisha?

#YNWA
Inawatumishi wangapi na hizo taasisi tunazozisema zinaingiza pesa nyingi mbona hujaweka takwimu zake hapa kwa hiyo robo ya mwaka?

Pia hiyo ni halmashauri moja Tena ya mjini, Sasa niambie halmashauri ya nanyamba au namtumbo Kama zimefikia hata 1 b
 
Hilo swala kifupi halipo kama upo chini na unapata pesa kidogo still una nafasi ya kuomba watu wapo kwa matasisi wanafanya kazi mpaka saa moja usiku kutokana na unyeti wa kazi mtu anaingia saa 2 mpaka saa. 12 au moja usiku usijfananishe na wa mazoea masaa saa 2 mpaka saa nane

Kingine magap tapo daim milele msanii wa wcb akipiga show analipwa tofauti na mwingine haijalishi wote ni wanamuziki japo jamaa aa juzi juzi

Hata fiest wale wasanii wakiwachukua despite wamepangiwa labda nusu saa kuperfom kwa kila mmoja ila mwisho wa siku kila mtu anapewa amount kivyake kutokana na brand yake ndo ivyo brand za TRA ni kubwa huwezi linganisha na mwasibu wa halmashauri hat wawe na elimu sawa
 
Naomba hilo swala la kuharmonize lisitokee milele na milele dunia hii haina haki sawa since kuna maskini na matajiri basi mtoa uzi lalamika kwa mungu kwa hilo kama unajua sana kikubwa elewa mungu ameweka utofauti wa kipato ,maisha, afya,elimu vyeo na mambo kibao ili tuweke kuheshimiana na kusaidia

Assume mtu yupo TRA una kuta anakula pesa na pia ni msaada mkubwa kwa famila yake kwa ujumla hizo nfasi zipo tu ikiwa rizki yako tu unakula kila mtu apambanane uache kujifananisha na watu ,kuangalia salary slip ya mtu ni umbea ona umeona pesa ndefu unaleta husda
 
Hiyo harmonization hata ikifanyika bado haiwezi kuleta equality. Mfano: kuna professions ni rare kwenye nchi kama madaktari bingwa huwezi kusema mishahara iendane na daktari wa kawaida.
Wewe hujaelewa hiyo maana ya salaries hamonization kwa watumishi wa umma iliyokuwa inafanywa na SCOPO. Haimaanishi watumishi wa umma walingane mishahara, yaani kwa mfano wako wa medical clinicians kwamba Clinical Officer, Assistant Medical Officer, Medical Officer na Medical Specialist wote walingane mshahara! Hamonization inayoongelewa ni ulinganisho wa mishahara ya watumishi wa umma wanaolingana kwa qualification na experience. Kwa mfano sasa hivi Medical Specialist grade II anayeajiriwa Muhimbili NH anapata mshahara wa tsh 2.5 million kwa mwezi wakati specialist wa grade hiyo hiyo aliyeajiriwa TRA au BoT anapata mshahara wa tsh 15 million kwa mwezi. Na tasisi zote hizi ni za serikali na mishahara yao ni ya serikali (inayotokana na kodi zetu wote). Kwa nini hawa wapishane mishahara kwa kiwango kikubwa kama hichi?
 
Wewe ni mjinga. Kabisa unauliza eti dereva wa raisi Ana nini special??
Ungekuwa karibu ningekukata kibao

We Kilaza sana alaf unaamini unajua wakati huna argument yenye mashiko umekomaa dereva wa rais dereva wa rais.
Ukilaza wako unaamini unaweza kumzaba makofi mtu mzima mwenzio? Alaf nakutazama tu unanizaba kibao?
 

Hakuna swali hapo Chief unauliza utopolo tu
 
Hahahah hawa jamaa wa NSSF wanalipana vizuri sana pamoja na wale wa PSPF! Hizi taasisi mtu ukiingia umeuaga umaskini. As you grow na kisomo shavu linaongezeka maradufu.
Nina sista wangu flani alikuwaga hapo enzi za J.K yeye alikuwa senior level Liaison Officer anakunja 7M kwa mwezi. Sahizi yuko WCF huko! Mchawi ni Ajira portal tu ila zama za vimemo ungekuta tuko vitengo muda sana hata kwa kujitolea.
 
Ni ushetani tu, hakuna justification. Na huu ushetani uliasisiwa na Mkapa.
Mtu anayekuingizia mamilioni unataka alingane na mtu ambaye kazi yake kutumia hela tu

Dunia mzima income generators hulipwa mishahara mikubwa Mno ndio maana makampuni kama ya mafuta kumkuta meneja mkuu analipwa mshahara shilingi milioni 100 kwa mwezi wala sio ajabu

Mfano chukulia dereva wa halmashauri na dereva wa Benki wa halmashauri kazi yake kubeba takataka za halmashauri wa Benki anabeba pesa risk kubwa na dhamana aliyopewa kubwa Mon wa halmashauri akikimbia na takataka sio kitu kikubwa wa Benki akikimbia na pesa kitu kikubwa
 
Mkuu bonge la CONTENT....
 
Tuko nyuma sana ndugu zangu
Tumechezewa sana ndugu zangu
Tumedanganywa sana ndugu zangu.
Harmonisation of salary ni sasa awamu hii.
 
Ukisikia utopolo ndo huu sasa au nasema uongo
ndugu zangu. Eti anabeba takataka eti mwingine anabeba vitu vikubwa aiseee wewe jamaa usamehewe bure akili yako ndo imeishia hapo
 
Ofisi gani wanafanya kazi kuanzia asubuhi hadi saa moja usiku bila kulipwa overtime?
 
Now, what's the problem with her kulipwa 7m?
Sasa mimi wa Mshahara wa laki 8 kwa nini nisikaze ili na mimi siku moja niwe kwenye hilo shirika la sister ako na mimi nikunje 7m?

Kwa nini mimi niombee sister ako ashushwe ili apokee laki 8 ili tulingane? Akishushwa tukalingana, inakuwa imenisaidia vipi mimi?

Huoni kwamba the best thing ni yeye kuendelea kulipwa hiyo 7m na mimi nikaze ili siku moja na mimi niwe kwenye shirika hilo lao na mimi nikunje hiyo 7m?

Nakuuliza wewe.
 
Kati ya mkurugenzi wa NIDA na mkurugenzi wa halmashauri nani ana majukumu mengi?
Halmashauri inashughulikia elimu, afya,kilimo, michezo, ardhi, takwimu na mengine mengi mbona salary yake kisoda ukilinganisha na huyo wa NIDA
 
Tatizo lako unadhani wote wanaopinga wapo halmashauri. Mi nipo private sector na nalipwa vizuri tu. Kama kuna mapungufu lazima yasemwe for the good of the country. Wewe unabeza kwa sababu unafaidika na system mbovu
 
Tatizo lako unadhani wote wanaopinga wapo halmashauri. Mi nipo private sector na nalipwa vizuri tu. Kama kuna mapungufu lazima yasemwe for the good of the country. Wewe unabeza kwa sababu unafaidika na system mbovu
Maneno mengi ya nini? Usijaze servers mzee... JIBU swali nililouliza ambalo wewe na wenzako wote mnalikimbia .
 
Yah ishu sio kupunguza mishahara, ni kustandardize ofcourse sio kila mtu atalipwa 7M! Ila complain ya watu atleast huyu wa laki 8 apewe 3M
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…