Utofauti wa viungo wa Simba na Yanga

Utofauti wa viungo wa Simba na Yanga

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Utofauti mkubwa ninaoouna uliopo baina ya timu hizi ni:-

1.Yanga inaviungo ambao si wanyumbufu,hawana ubunifu wa kuutoa mpira eneo la katikati nyuma kwenda mbele.

2 .Hawana umiliki mzuri wa mpira tofauti na viungo wa Simba. Viungo wa Yanga wakiwa na mpira mara nyingi huupoteza kirahisi kabsa kabla hata ya kufika eneo la 18 la mpinzani wakati Simba wakiwa na mpira huumiliki kwa mda mrefu,na ubunifu huongezeka kadri wanavyolikaribia goli.

3.Shishimbi anaongoza kupiga basi za ovyo na kupoteza mipira. Huyu ni mchezaji ambaye huwa anakaba kwa juhudi sn lakini tatizo lake kubwa linaloighalimu timu mara nyingi ni kupoteza mpira kirahisi tena akiwa peke ake na kupiga pasi kipofu (Pasi mkaa) tena sehemu muhimu kabsa.

4.Viungo hawana kasi ni wazito sana tofauti na wa Simba ndio maana mpira wao huwa unakosa raha. Simba kila kiungo ana kasi mfano mzuri ni hizi mechi za kirafiki zimeonesha nini namaanisha.

karibuni kwa nyongeza Mlima Kamgomoli
 
Umeongea kweli, miaka mingi Yanga tunajivunia winga zenye spidi uku Simba ni viungo wazuri.
 
Wamecheza simba na timu ya zambia wewe unaichambua yanga...huu uchambuzi huu,si ukachambue mchele tu
 
Timu za Tanzania yenye best viungo ni Azam Sure Boy Mudathir Yahya
Hao wote wawili wako level ya Mzamiru Yasin
Hapo hujawataja MKUDE, CHAMA, KAHATA, DILUNGA, NDEMLA... Kwa season iliyopita Ya HARUNA, KOTEI.
Azam nawakubali kwenye defender za kati na pembeni sio viungo hawa walioshindwa kuipush timu yao hata kuwa wa 2 kwenye TPL mbele ya Yanga iliyokuwa haiko vzr.
 
Nimeona ubora wa Shomari na Shabalala...kweli.Simba wana majembe ya ukweli.
 
Hao wote wawili wako level ya Mzamiru Yasin
Hapo hujawataja MKUDE, CHAMA, KAHATA, DILUNGA, NDEMLA... Kwa season iliyopita Ya HARUNA, KOTEI.
Azam nawakubali kwenye defender za kati na pembeni sio viungo hawa walioshindwa kuipush timu yao hata kuwa wa 2 kwenye TPL mbele ya Yanga iliyokuwa haiko vzr.
Kumbuka Chama alicheza dk 45 baada ya kuchemsha na mikia kutoka bila ya shot on target..Tatizo la Yanga ilikuwa namba sita..Bui kaja kulifanyia kazi
 
Huu ndo uchambuzi bora na makini wa soka kabla ya msimu wa 2019/2020 kuanza,
 
Kumbuka Chama alicheza dk 45 baada ya kuchemsha na mikia kutoka bila ya shot on target..Tatizo la Yanga ilikuwa namba sita..Bui kaja kulifanyia kazi
Hapo kwenye timu yako kuna kiungo kamzidi Takwimu CHAMA Msimu ulioisha? au unaongelea mechi 1.
 
Wewe utakua ni shabiki wa mbumbumbu fc bila shaka. Wewe tuachie Yanga yetu. Tuonane mzunguko wa ligi utakapo anza.
 
Simba hamna tofauti na anae kwenda kuvuna matikiti kwa shoka wakati hata kisu kingetosha tuuuu mmecheza na wachovu wa kitwe mnajilinganisha na waliocheza na team iliyo suruhu na Everton
 
Back
Top Bottom